Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,249
Reaction score
5,743
Wakuu, leo, Disemba 14, 2014 Watanzania wanapiga kura kuchagua viongozi wao wa Serikali za Mitaa, Tanzania Bara (Tanganyika).

Viongozi wanaochaguliwa leo ni katika nafasi za Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Wenyeviti wa Vitongoji, Wajumbe 6 wa Serikali ya Mtaa (Halmashauri) na wajumbe wa Viti Maalum wa Mtaa/Kijiji.

Kama ilivyo ada JamiiForums itakuwa ikikujuza yanayojiri, katika uzi huu utapata/utaleta updates zinazohusiana na uchaguzi huu.

Karibuni sana

========
UPDATES MUHIMU:



Hapa ni Mtaa wa Kijitonyama
- Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana
Huku Dodoma, CCM wanadaiwa kumteka na kumsihi mgombea wa CHADEMA atangaze kujitoa... Hadi sasa amepatikana na amekana kujitoa kabisa..

Wananchi wamegoma kupiga kura hadi mgombea huyo awe huru na aje kupiga kura yake..
- Mgombea wa CHADEMA Kijiji cha Darajani huko Liwale, M. Manakwa amepigwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo, amelazwa hospitali


-Mkuu wa Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Suleiman Liwowa ametangaza kuwa katika vitongoji 613 vya Wilaya hiyo vyama vya Upinzani vimeshindwa kusimamisha wagombea.
Hapa Mbagala Saku, Kituo Mfenesini karatasi za kupigia kura zipo 300 tu na watu walio jiandikisha kupiga kura ni 1512 ,kwa hiyo mpaka sasa upigaji kura bado haujaanza

Mkuzo, Songea:

Baada ya watu kuwa wengi; Uamuzi uliotolewa ni kuingia watu wanne wanne kupiga kura.

Atayebainika kurudia atabakizwa ndani au wapiga kura wataamua nini atendewe.

 

Attachments

  • p1.jpg
    50 KB · Views: 4,686
Hapa mtaani kwetu nasikia sauti za swalaa swalaa ndio tunajiandaa kwa swala halafu tunarudi kufungua ofisi ya chama kwa uratibu wa zoezi la leo.
Delete ccm imekuwa ni operesheni ya kimya kimya!
 
wazirii ? Wapi huko ? Nani huyo ? Weka picha video si wote tutaona mkuu

TUFANYE UCHAGUZI WA AMANI
 
mtaa wa Migungani , sokon one, arusha mjini sisi tunasubiria kusherekea ushindi tu kisha wiki inayofuata tuwaburuze mahakamani mwenyekiti wa ccm aliyepita na wajumbe wake kwa kutowai kusoma mapato na matumizi ya mtaa na pia kujivutia bomba la mtaa kwake na kuuza maji pasipo serikali ya mtaa kupata mapato
 
Hivi unawezaje kuupload video? Kuna Waziri alitaitiwa jana usiku akitoa hongo ..

mkuu kama unatumia whatsapp ni-pm namba yako unitumie video nitaiweka hapa.
 
Hivi unawezaje kuupload video? Kuna Waziri alitaitiwa jana usiku akitoa hongo ..

Na nyie RAIA mmekuwa dhaifu sana, mtu anatoa rushwa mnamwangalia tu? Huyo alikuwa Wa kuchoma moto kabisa, hana tofauti na vibaka mnaowatia kiberiti mkidai nyie ni raia wenye hasira kali au kama ni m-mama mngemgegeda hadharani!! Mkuu mmeonesha udhaifu mkubwa kabisa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…