Yaliyojiri katika mahafali ya CHASO mbele ya Edward Lowassa - Karimjee Hall, Dar

Subiri n'jiandae kuelekea kunako tukio. Hawa ndo wakombozi wetu wa siku za usoni ambao wanaenda kupambana dhidi ya USIGINAJI wa DEMOKRASIA unaofanywa na serikali ya awamu ya tano. Hongereni sana wasomi wetu kwa kuhitimisha masomo yenu.
 
Naona leo mawingu fm watakosa msikilizaji wao maarufu
 
Watapewa ajira serikalini kweli kama wanajitanabaishe wako mrengo gani live?!
 
WanaJF

Ni asubuhi tulivu ya Jumamosi.Jiji la Dar es Salaam lina pilikapilika kama kawaida huku kukiwa na hali nzuri kabisa ya hewa huku jua likiwa linawaka katika kona zote za jiji.

Katika ukumbi huu wa Karimjee tayari kumepambwa kwa mapambo ya rangi nyekundu,bluu,nyeusi na nyekundu kuashiria tukio kuu la Chama cha Chadema.

Ni katika ukumbi huu yatafanyika mahafali ya vijana wanavyuo wa Chadema wanaohitimu katika vyuo kadhaa DSM

Mgeni rasmi katika tukio hili ni Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.Tayari ukumbi umefurika idadi kubwa ya waandishi wa habari huku kukiwa na ulinzi imara wa Red Brigades.

Tuko hapa ukumbini kuwaletea kila kitakachojiri...Karibuni sana..

sio waziri mkuu mstaafu, sema fisadi lowasa
 
Waandishi wamesikia kua Rais wa mioyo ya watanzania ikawa tabu, wamejaa wao humo. Viva chaso
 
Hamjazingirwa kweli maana wazee wa intelijensia kama kawaida yao mikusanyiko ya watu hawa hutafsiriwa kama uchochezi.
 
Impact gani unazungumzia? Yasingekuwa na impact mngemzuia asifanye mikutano? acheni utani aisee!
bhas hayana positive impact .m.yana negative impact kwa taifa hili ....kwa kuwa hana jipya kwanza anaongea dakika tano kachoka
 
WanaJF

Ni asubuhi tulivu ya Jumamosi.Jiji la Dar es Salaam lina pilikapilika kama kawaida huku kukiwa na hali nzuri kabisa ya hewa huku jua likiwa linawaka katika kona zote za jiji.

Katika ukumbi huu wa Karimjee tayari kumepambwa kwa mapambo ya rangi nyekundu,bluu,nyeusi na nyekundu kuashiria tukio kuu la Chama cha Chadema.

Ni katika ukumbi huu yatafanyika mahafali ya vijana wanavyuo wa Chadema wanaohitimu katika vyuo kadhaa DSM

Mgeni rasmi katika tukio hili ni Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.Tayari ukumbi umefurika idadi kubwa ya waandishi wa habari huku kukiwa na ulinzi imara wa Red Brigades.

Tuko hapa ukumbini kuwaletea kila kitakachojiri...Karibuni sana..
Mnakibali cha polisi?
Hivi Fisadi Lowasa atakwenda lini kuchunga ng'ombe kama alivyo ahidi? Mbona ana ng'ang'ania mjini?
 
Naona umekurupuka tu kitandani na kutupia hii post hata chai hujaipata
 
Back
Top Bottom