Yaliyojiri katika mahafali ya CHASO mbele ya Edward Lowassa - Karimjee Hall, Dar

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,228
WanaJF

Ni asubuhi tulivu ya Jumamosi.Jiji la Dar es Salaam lina pilikapilika kama kawaida huku kukiwa na hali nzuri kabisa ya hewa huku jua likiwa linawaka katika kona zote za jiji.

Katika ukumbi huu wa Karimjee tayari kumepambwa kwa mapambo ya rangi nyekundu,bluu,nyeusi na nyekundu kuashiria tukio kuu la Chama cha Chadema.

Ni katika ukumbi huu yatafanyika mahafali ya vijana wanavyuo wa Chadema wanaohitimu katika vyuo kadhaa DSM

Mgeni rasmi katika tukio hili ni Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.Tayari ukumbi umefurika idadi kubwa ya waandishi wa habari huku kukiwa na ulinzi imara wa Red Brigades.

Tuko hapa ukumbini kuwaletea kila kitakachojiri...Karibuni sana..

Updates 1
Tayari ukumbi umefurika vijana wa CHASO kutoka vyuo mbalimbali vya mkoa wa DSM.Vijana hao wamejipamba na mavazi maalum ya Chadema yakiwemo mavazi ya kombati nyeusi na za kaki huku wengine wakivalia Tshirts za chama hicho.Kwa sasa wanasubiriwa viongozi mbalimbali kuwasili akiwemo mgeni Rasmi shujaa mpambanaji Edward Lowassa.

Tayari mgeni rasmi Rais wa mioyo ya watanzania Edward Lowassa smeshaingia ukumbini akiwa na Meya wa Jiji la DSM Mstahiki Issaya Mwita.Pia wapo viongozi wengine kadhaa wa mkoa na Taifa.

Mratibu wa CHASO mkoa wa DSM Yuda Guti ndiyo anatoa utambulisho sasa mbele ya mgeni rasmi.Baada ya utambulisho amewapongeza na kuwashukuru wanachama wa CHASO kwa uvumilivu wao pamoja na vikwazo mbalimbali wanavyopata wakiwa vyuoni kutokana na itikadi yao ya kuipenda Chadema.Amewataka huko wanakokwenda baada ya kumaliza vyuo wajue kwamba ndiyo wanatakiwa wakajipambanue zaidi kuipigania Chadema na Taifa

Sasa anazungumza Meya wa jiji la DSM Mstahiki Isaya Mwita ambapo anaanza kwa kuwapongeza vijana wa Chadema waliopigana kuhakikisha chama kinapata ushindi mkubwa DSM na kumtoa Meya na Naibu wake kutoka mshirika wetu wa Ukawa.Meya anasema hata kuwepo ndani ya ukumbi wa Karimjee ulioko chini yake ni matunda ya kazi yao.

Meya Issaya anawaasa vijana wasiogope kuingia kwenye soko la ushindani.Anasema yeye alipomaliza chuo alikataa kuajiriwa na akahakikisha anapambana mpaka akafanikiwa.Amewataka vijana wafanye kazi kwa bidii na wabadilishe mentality ya watu huko wanakokwenda kuhusu kufanya kazi kwa bidii.

Lowassa anazungumza
Sasa anakaribishwa mgeni Rasmi waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye anaanzs kuwashukuru vijana kwa kumwamini na kumwalika katika mahafali hayo.

Lowassa anasema akiona umati huo wa wanafunzi wenye bashasha unamkumbusha mbali sana katika mapambano ya uchaguzi mkuu mwaka jana.

Anasema hakuna asiyejua kwamba alishinda na kutokana na sababu hiyo wakawakamata vijana wa Chadema na kuwafunga ili wafute ushahidi.

Huku akishangiliwa Rais...Rais.Rais kiongozi huyo amewataka watanzania kupigania Tume huru ya uchaguzi kama Kenya wanavyofanya kwani tume iliyopo ni kama kitengo cha CCM.

Pia Lowassa amewataka wahitimu hao kuhakikisha kwamba wanaongoza watanzania kudai katiba mpya vinginevyo itakuwa vigumu sana kupambana na watu wanaotumia katiba mbovu kama kichaka cha kuminya demokrasia.

Lowassa amesema kwa hali yoyote ni lazima tume hii ya uchaguzi yenye mafungamano na CCM iondoke.Amesema haiwezekani tume inayoshindwa kutangaza mtu aliyeshinda uchaguzi.

Waziri mkuu huyo mstaafu amesema kamwe hawezi kukubali matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana hata kama itabidi kufa.

Lowassa amesema baada ya uchaguzi mkuu walimleta Nabii Joshua ili amshawishi akubali matokeo lakini alimjibu Nabii huyo kama atakubaliana na matokeo yale basi ajue heshima yake itashuka.Lowassa amesema Nabii Joshua aliondoka kwenye hoteli aliyopangiwa na alikataa kushiriki kuapishwa kwa Rais mpya

Kwa mara ya kwanza Lowassa amezungumzia kuhusu Bunge kutokuwa Live na kusema kuzuiwa matangazo ya moja kwa moja ni aibu kubwa kwa watawala na heshima yao imeshuka kupitiliza.

Lowassa ameendelea kusema vijana wengi hawana ajira na ni bomu linalosubiri kulipuka wakati wowote kuanzia sasa.

Kuhusu elimu Lowassa amesema haoni mpango wowote madhubuti wa kukwamua elimu yetu.Amesema inatakiwa kuwe na mpango madhubuti wa muda mfupi na mrefu kuhusu elimu kama ilivyo katika ilani ya uchaguzi ya Chadema.

Lowassa anesema watawala hawana raha kwa sababu Chadema na Ukawa wameshinda maeneo mengi sana kote nchini.Amewataka wote walioshinda kuhakikisha wanafanya kazi kubwa na nzuri kuwatumikia watu ili uchaguzi wa 2020 washinde kwa urahisi.Lowassa ameapa mwamko anaoona sasa wa watanzania na mateso makubwa wanayopata chini ya CCM basi ni dhahiri mwaka 2020 Chadema na Ukawa watapata ushindi mkubwa sana.Anasema watanzania wamekata tamaa chini ya utawala huu na hawana matumaini tena

Lowassa amemaliza kuhutubia na kuwashukuru tena vijana wa Chaso kwa jinsi wanavyopigania Chadema.Lowassa anashangiliwa sana kwa shangwe kuu huku mamia ya vijana hawa wakiimba...Rais...Rais...Rais.Kwa hali inayojionyesha hapa ukumbini ni wazi Edward Lowassa ndiye mwanasiasa maarufu zaidi Tanzania na anayependwa kupitiliza.

Sasa inafuatia kula kiapo kwa viongozi wapya wa matawi na kisha utafuatia ugawaji wa vyeti kwa wahotimu......

Asanteni sana kwa kunifuatilia.
IMG-20160618-WA0033.jpg

IMG-20160618-WA0017.jpg
IMG-20160618-WA0015.jpg
IMG-20160618-WA0013.jpg
IMG-20160618-WA0011.jpg
IMG-20160618-WA0038.jpg
 

Attachments

  • VID-20160618-WA0023.mp4
    4.3 MB · Views: 75
Ni siku ya pekee iliyokuwa inasubiriwa na watanzania walio wengi ambapo Mh Edward Lowasa ataongea na watanzania kwenye sherehe maalumu kutoa vyeti kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali ambao ni wanachama wa CHADEMA mnakaribishwa ukumbi wa Karimjee asante sana kamanda Molemo kwa kutuwekea update live
 
Ni siku ya pekee iliyokuwa inasubiriwa na watanzania walio wengi ambapo Mh Edward Lowasa ataongea na watanzania kwenye sherehe maalumu kutoa vyeti kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali ambao ni wanachama wa CHADEMA mnakaribishwa ukumbi wa Karimjee asante sana kamanda Molemo kwa kutuwekea update live

Tundu Lissu angefaa zaidi huyo mfugaji anawapunguzia wanachama na wapenzi.
 
WanaJF

Ni asubuhi tulivu ya Jumamosi.Jiji la Dar es Salaam lina pilikapilika kama kawaida huku kukiwa na hali nzuri kabisa ya hewa huku jua likiwa linawaka katika kona zote za jiji.

Katika ukumbi huu wa Karimjee tayari kumepambwa kwa mapambo ya rangi nyekundu,bluu,nyeusi na nyekundu kuashiria tukio kuu la Chama cha Chadema.

Ni katika ukumbi huu yatafanyika mahafali ya vijana wanavyuo wa Chadema wanaohitimu katika vyuo kadhaa DSM

Mgeni rasmi katika tukio hili ni Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.Tayari ukumbi umefurika idadi kubwa ya waandishi wa habari huku kukiwa na ulinzi imara wa Red Brigades.

Tuko hapa ukumbini kuwaletea kila kitakachojiri...Karibuni sana..
Kill them , edward Lowassa ...polisiem hawachelewi kusingizia intel ...wakati amboni hata hawakugundua.

Kazi yao n kugundua intel kwa watu hata wasiojua kurusha ngumi.
 
Haya mambo yalikuwa na maana enzi za chama kushika hatamu na si zama hizi. CCM wameshindwa kubadilika baada ya kuanza vyama vingi na kuendeleza siasa vyuoni hadi sehemu zingine zisizofaa. Upinzani wamejikuta wakifata mkumbo huu ambao hauna afya. Tufike mahali tuchore vyema mstari wa wapi uvyama vyama ukome.
 
Back
Top Bottom