Yaliyojiri katika Clubhouse session ya Jamiiforums 15/02/2022: Safari ya matibabu kwa Mtoto mwenye Saratani

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1644936445687.png
Jamii Forums kwa kushirikiana na MUHAS, MNH, TLM wameandaa Mjadala utakaofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums ili kuongeza uelewa juu ya Saratani kwa Watoto Nchini Tanzania. Kujua zaidi soma: Una swali lolote kuhusu ugonjwa wa saratani kwa watoto?

Mjadala huu unatarajiwa kufanyika leo Jumanne, Februari 15, 2022 kuanzia saa 12:00 jioni mpaka saa 1:30 usiku ambapo Wataalamu mbalimbali wa Afya wataeleza kwa kina kuhusu Saratani ya Watoto na namna ya kukabiliana nayo.

Ili kujiunga na mjadala huu bonyeza link hii hapa chini:

UPDATES


Baadi ya hoja zinazotolewa na wataalamu katika mjadala
Dkt. Anzibert Rugakingira: Saratani ni ugonjwa ambao unaathiri watu wa rika na jinsia zote; watoto, watu wazima, wanawake na wanaume. Takwimu za Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (International Atomic Research on Cancer-IARC) na Shirika la Afya Duniani (WHO), 2018 zinaeleza kwamba kila mwaka duniani kote kunatokea wagonjwa wapya wanaokadiriwa kufikia milioni 18.1, na kati ya hao, zaidi ya wagonjwa milioni 9.6 hufariki kutokana na ugonjwa wa saratani kila mwaka ambao ni sawa na takribani asilimia 50.

Aidha, zaidi ya watu ya millioni 43.8 wanaishi na saratani duniani. Kama hatua madhubuti za kinga, uchunguzi wa mapema na tiba stahiki hazitachukuliwa haraka, tatizo la saratani linakadiriwa kuongezeka na idadi ya wagonjwa wapya kufikia milioni 24 ifikapo mwaka 2035, huku ongezeko kubwa likiwa katika ukanda wa nchi zinazoendelea kama Tanzania.

Dkt. Anzibert Rugakingira: Serikali kupitia Wizara ya Afya sasa hivi imetoa kipaumbele kikubwa kwenye Magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Saratani.

Magonjwa haya mpaka sasa yanasababisha 33% ya Vifo. Wagonjwa 42,000 kila mwaka wanagundulika na Saratani na kati yao 4,000 ni Watoto.

Dkt. Anzibert Rugakingira: Katika safari ya kumuhudumia Mtoto mwenye Saratani, changamoto zipo nyingi. Tunazitambua!

Kwa upande wa Matibabu, Hospitali za Kanda zinaboreshwa Huduma. Mgonjwa akiwa Kigoma hatakiwi kuja Muhimbili kupata huduma.

Ruchius Philbert (Muuguzi - Tumaini la Maisha): Saratani kwa Watoto ipo, ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo na ulemavu duniani. Ni miongoni mwa vipaumbele vya Shirika la Afya Duniani (WHO)

Familia inaweza kumuwahisha au kumchelewesha Mtoto kupata Matibabu.

Ruchius Philbert: Takriban Watoto 300,000 hugundulika na Saratani duniani 80% ya Watoto wanaopatikana na Saratani hutokea katika nchi za Uchumi wa Chini na Uchumi wa Kati.

Ruchius Philbert: Dalili za Awali za Saratani kwa Watoto ni homa za mara kwa mara, kupungukiwa damu, kutokwa na damu puani, kwenye fizi au sehemu inayozunguka jicho. Dalili nyingine ni mtoto kukonda na kudhoofika, maumivu ya kichwa, hali ya kutapika nyakati za asubuhi dalili nyingine ni jicho kutoka uchafu

Ruchius Philbert: Ruchius Philbert: Mzazi anapoona dalili zinazoelkeana na zilizotajwa awahi hospitali kwa kuwa kadiri mtoto anavyochelewa ndivyo Saratani inavyosambaa na kuwa ngumu kutibika. Saratani inaposambaa huwa ni gharama sana kutibika lakini hutibika kirahisi ikiwa katika hatua za awali.

Ruchius Philbert: Ushauri wangu ni Jamii ijenge mazoea ya kuwa inawachunguza Watoto wao mfano Mama awe anamchungunza Mtoto kuanzia kichwa hadi miguu.

Saratani inatibika, jambo la msingi ni Jamii kutambua dalili mapema

Dokta Lulu Chirande - Daktari Bingwa: Dalili za saratani zinafanana na magonjwa mengine ya kawaida. Wazazi wakiona dalili hizo wampleke mtoto kituo cha afya. Badhi ya saratani huwa hazioneshi uvimbe kama saratani ya damu na ubongo.

Dokta Lulu Chirande: Mzazi anaweza kumpeleka mtoto mwenye dalili hospitali yoyote ambapo wataalamu wakitambua dalili ataweza kumshauri aende hatua ya mbele. Vipimo vinapatikana Hospitali mbalimbali kwa hiyo haina haja ya mtu wa mkoani kusafiri kutafuta hospitali.

Dokta Lulu Chirande: Dalili za saratani zinafanana na magonjwa mengine ya kawaida. Wazazi wakiona dalili hizo wampleke mtoto kituo cha afya. Badhi ya saratani huwa hazioneshi uvimbe kama saratani ya damu na ubongo.

Dokta Lulu Chirande: Mambo yanayochangia kuchelewa ni pamoja na imani ambapo watu huambiana waanze kwa Waganga wa Kienyeji, wengine huchelewa kutokana na majukumu.

Pia, usafiri huwa ni changamoto lakini tumejitahidi kusaidia kutatua changamoto ya usafiri.

Dokta Lulu Chirande: Kwa asilimia kubwa Saratani za Watoto hazisababishwi na mambo aliyofanya. Kuna asilimia ndogo ya Saratani zinatokea kutokana na Urithi. Mfano ni Saratani ya Jicho.

Kuna baadhi ya Magonjwa yanaweza kuongeza uwezekano wa Saratani mfano Upungufu wa Kinga Mwilini.

Dokta Lulu Chirande: Katila kupambana na Saratani kwa Watoto tunasisitiza tuigundue haraka. Mtoto anapoonesha dalili tugundue haraka na aanze matibabu anayostahili. Watoto wanapona.

Familia ni muhimu zishikamane, kumuomba Mungu na kufuatilia matibabu kadiri ya maelekezo.

Dkt. Lulu Chirande: Tunaisihi Jamii wasiwe Wataalamu sana, wapo hata Viongozi wa Dini wanaoshauri Watoto waende kuombewa. Sisi tunasema waombewe huku wanapata Matibabu.

Dkt. Lulu Chirande: Tunategemea tukiwa na kila kitu kinachohitajika, asilimia 90% ya Watoto wenye Saratani watapona na kujenga Taifa hili

Dkt. Hadija Mwamtemi (MNH): Katika kipindi cha miaka 10 tumepiga hatua kubwa katika kutoa huduma kwa Watoto wenye Saratani. Watu wengi wana dhana kwamba Saratani haitibiki, wanauliza "Hivi kweli wale watoto wanapona?"

Jambo la msingi ni kuwahi matibabu.

Dkt. Hadija Mwamtemi (MNH): Matibabu ya mtoto wa saratani hayamhusu daktari wa saratani peke yake. Tunashirikiana na madaktari wengine kama wa upasuaji, ubongo, wafamasia. Waatalu wa lishe na wanasihi.

Dkt. Hadija Mwamtemi (MNH): Muitikio wa watu kwenye utoaji damu ni changamoto ktk kufanikisha matibabu ya saratani kwa mtoto. Kuna baadhi ya saratani huhitaji damu nyingi, mathalani mtoto akitakiwa kufanyiwa chemotherapy.

Dkt. Hadija Mwamtemi (MNH): Wataalamu waliopo hawatoshelezi ndio sababu ya kuwa na ucheleweshaji wa upimaji. Juhudi zinafanyika ili kuongeza wataalamu lakini nyingine ziko nje ya uwezo wetu.

Dkt. Hadija Mwamtemi (MNH): Matibabu ya saratani yako ya aina mbalimbali kama utoaji dawa pia kuna uchomaji wa mionzi

Uchomaji wa mionzi huwa na changamoto kwa kuwa wazazi wanaamini ukichoma mionzi wanapunguza uhai wa watoto hivyo mara nyingine hutoroka.

Dkt. Hadija Mwamtemi (MNH): Matibabu huchukua muda mrefu, miaka 3 hadi 6 ambapo mtu huweza kuwa anapatiwa tiba kwa wiki ambapo ni vigumu mzazi kurudi mkoani na kuja tena kufuata tiba.

Hivyo tumejenga hosteli za watoto, lakini vyumba vilivyopo havitoshi.

Dkt. Hadija Mwamtemi (MNH): Serikali imejitahidi kuchangia huduma. Na sisi wananchi tunaweza kuchangia huduma ili kupunguza changamoto zilizopo.

Pia nitoe wito kwa wananchi wachangie damu kwa kuwa damu inahitajika sana kwa matibabu ya watoto.

Dkt. Hadija Mwamtemi: Mungu anawapenda Watoto, hapendi wapoteze maisha. Kinachotakiwa ni tushirikiane kwa pamoja kufanikisha Mapambano dhidi ya Saratani kwa Watoto

Dkt. Moses Karashani: Uwekezaji unatakiwa ufanyike ili kupunguza changamoto zilizopo katika matibabu ya Saratani.

Mara nyingine watu hutoka hospitali moja kwenda nyingine kwa sababu tu hospitali aliyopo wamekosa kipimo kimoja, mathalani cha 'Full Blood Picture'.

Dkt. Moses Karashani: Bado tuna shida kidogo kwenye Hospitali za ngazi za chini licha za jitihada kadhaa za Serikali ikiwemo kuongeza Wataalamu na kufanya Uwekezaji.

Dkt Moses Karashani: Dkt. Moses Karashani: Saratani za watoto hazina zile sababu za kitabia ambazo unaweza kuzibadilisha kama kwa Saratani za watu wazima.

Kwa takwimu zilizopo na 'tulivyozi-forecast' mifumo yetu inaweza kuelemewa kwa kuwa Wagonjwa wataongezeka kwa kasi.

Germana (Mzazi wa mtoto mwenye saratani): Mwanangu aligunduliwa na saratani na nilikumbana na changamoto kadhaa

Baadhi ya changamoto moja, nilifuatwa na watu wakaniambia mtoto hawezi kupona hivyo nimpeleke 'sehemu fulani' lakini mimi niliamua kutilia mkazo tiba za hospitali.

Germana (Mzazi): Safari ya kumuhudumia Mtoto mwenye Saratani ina mambo mengi. Wazazi tunaposhauriwa Mtoto apate Huduma hospitali basi tukubali.

Familia ina sehemu kubwa katika kumuhudumia Mtoto, tukisimama pamoja safari ya kumuhudumia Mtoto inakuwa nyepesi.

Dkt. Jerry Ndumbalo: Kwenye Matibabu ya Saratani kwa Tanzania sasa hivi miundombinu kwa kiasi kikubwa imewekwa kwenye Tiba

Sisi Ocean Road tiba ambayo ungeweza kuifauata India sasa hivi unaweza kuyapata hapa Tanzania. Mtoto asipocheleweshwa, matibabu yanapatikana.

Dkt. Moses Karashani: Tunapoadhimisha Siku ya Watoto wenye Saratani Duniani leo Februari 15, Jamii ya Kitanzania tuamke kwamba hili janga ni letu sote

Unapokuwa na Mtoto mmoja kwenye Familia mwenye Saratani, ni kama Familia nzima imeathirika. Jamii tuje pamoja.

Germana (Mzazi): Safari ya kumuhudumia Mtoto mwenye Saratani ina mambo mengi. Wazazi tunaposhauriwa Mtoto apate Huduma hospitali basi tukubali.

Familia ina sehemu kubwa katika kumuhudumia Mtoto, tukisimama pamoja safari ya kumuhudumia Mtoto inakuwa nyepesi.
 
Shukran..nadhani Kuna haja serikali ikaharakisha uwepo wa bima za afya kwa wote kwa Bei nafuu Ili angalua wazazi na jamii imudu gharama za awali za kufanya uchunguzi kuhusu saratani na magonjwa mengine yenye hatua za ukuaji
 
Hapa jirani yupo mtoto ana umri kama miaka mitano sasa.

Alipozaliwa jicho moja lilionekana lina tatizo.

Baada ya vipimo ilionekana ni saratani. Jicho liliondolewa, halijawekwa lingine hivyo kufanya lile tundu la jicho kuziba.

Tabu inayomkuta mtoto japo yupo chekechea sasa ni wenzie kumwita kijicho.

Hapo ikiwezekana elimu pia ifike mashuleni.

Kitu nimeona siku za karibuni eneo linalozunguka jicho limetoa vijipu.

Kwa hali hiyo mzazi wa mtoto anatakiwa afanye nini maana nimeona wakikamua majipu bila kwenda hospital.

Nimeona niseme tu hapa pengine majibu yatasaidia wengine.

Nawasilisha.
 
Je ni Nini kifanyike ili kuokoa watoto waliopo vijijin ndani ili kuokoa maisha ya Hawa watoto

Je hiyo chemotherapy Hain madhara yoyote kwa watoto. Na side effect za madawa wanayopewa

Je mtoto anazaliwa akiwa na hiyo saratani. Au anaipataje hizo saratani

Njia gan za kujikinga na saratani kwa watoto

Kwann gharama ni kubwa San katik kutib ugojwa wa saratani

Je kama mtot akicheleweshwa ni madhara gani yanatokea?

Je saratani ya damu inatibika

Je, saratani inaambukiza. Eg blood transfution
 
Naomba niseme tena kidogo

Hapa mtaani pana mtoto tuseme hajafikisha miaka miwili.

Ninachoona kwa huyu mtoto ambaye ni wa kike, kwenye mguu wake wa kushoto kidole kidogo cha mwisho pana kakidole kengine kapo pembeni, tokea anazaliwa kipo, na haka kadole kadogo pia kana ukucha.

Anavyokua kile kidole ambacho kimeshika kidole kidogo kinazidi kujaa, yaani kama kanavimba.

Nilipouliza jibu ni kwamba hata bibi yake alikuwa hivyo na sasa mguu umekatwa.

Ninachotamani kujua kutoka kwa madaktari wetu humu, ni je haiwezekani mtoto anapozaliwa na kiotea kama hicho kidole kikawahiwa kuondolewa kuliko kukua nacho?

Mtanisamehe pale ambapo sijaeleweka vizuri.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom