Taasisi ya Saratani ya Ocean Road yatoa mafunzo ya matibabu ya Teknolojia ya Nyuklia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Nguvu za Atomic, International Atomic Energy Agency (IAEA), imetoa mafunzo ya matibabu ya Teknolojia ya Nyuklia kwa wataalamu 18 kutoka mataifa 15 ya Afrika.

Mafunzo hayo yamezinduliwa Septemba 4, 2023 katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam, ambapo yanatarajiwa kuchukua muda wa wiki moja.

09ee731e-d329-47d6-90fd-e5606488b5d3.jpg

2300f0bd-79ac-4de0-85d9-57ac8d80278b.jpg

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Omari Ubuguyu amesema Serikali imeanza kuongeza uwezo katika kuimarisha Teknolojia za kisasa kutibu magonjwa ya saratani nchini.

"Rais Dk.Samia kupitia Wizara ya Afya chini ya Waziri Ummy Mwalimu, amekuwa ukifanya jitihada kubwa za kuimarisha huduma za matibabu ya mionzi kupitia Taasisi hii ya Ocean Road, jambo ambalo limesaidia kuboresha huduma hizo nchini,” alisema.

Alieleza kuwa, katika jitihada hizo, Tanzania ipo katika maandalizi ya kujenga kituo cha bora cha umahiri wa matibabu ya saratani nchini ambacho kitakuwa bora kuliko vyote Afrika.

375a0cf1-fd3a-4000-b2ad-7264a0926dca.jpg

38144590-e4ae-411b-b885-91be28b56aa5.jpg
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage amemshukuru Rais Dk. Samia kwa kuweka kipaumbele suala la kuboresha matibabu ya kansa kupitia Taasisi hiyo kwa kutoa fedha za kujenga miundombinu mbalimbali na kununua mashine mbalimbali za matibabu na vifaa tiba.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Nyuklia wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Tausi Maftah, alisema kupitia Teknolojia hiyo wanafanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo Figo, Moyo na magonjwa ya njia ya chakula kwa kutumia Nyuklia isiyo na athari kwa binadamu kwa makundi mbalimbali wakiwemo watoto.

ca99721f-42c2-4d10-8ba7-4e3398ce6605.jpg

5487feab-86e6-46d6-8c11-1b1288f00cdb.jpg
Alisema kuwa huduma hiyo ya Nyuklia bado changamoto nchini ambapo mafunzo kama hayo ya Nyuklia ufanyika katika mataifa yaliyoendelea hivyo wamefurahi kwa hatua hiyo ya mafunzo hayo ambayo yatasaidia kuwajengea uwezo wataalamu ndani na nje ya Afrika.
 
Back
Top Bottom