Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Chato: Mkutano wa mgombea Urais Dkt. Magufuli (CCM) - Septemba 14, 2020

Huyu mgombea wa ccm mbona abadilishi Kanda mwezi Sasa yupo Kanda hio hio lini atafika Arusha, mtwara, Lindi, Mbeya, Iringa awanadi wabongea wa ccm
 
Ni CCM ndio ilimtengeneza Magufuli na pia Magufuli hailaumu CCM may be mtu mmoja mmoja lakini sio Chama. CCM hainaga sera yeyote kandamizi au inayoelekea kuharibu maliasili za taifa Kama Chadema wanvyosema kwenye ilani yao kuweka rehani madini yetu na kuchungia kwenye hifadhi zetu
Kuweka rehani ni sawa tu bora pesa inalipwa. Kuweka rehani ni kuwa unalipwa pesa in advance halafu wao ndiyo wanajijua cha kufanya mbele. Uganda wamekalia mafuta yao kwa miaka 14 wakipigania wasidhulumiwe sasa leo wanakubali wakati hata bei ya mafuta ishaanguka. Faida wailipoteza hiyo miaka 14 leo wangekuwa wapi .... Kupanga ni kuchagua.
 
Mi nachoweza kumwambia JPM ni kwamba anapozidi kuwafanyia figisu wapinzani ili yeye apewe coverage peke yake hapo ndipo anapozidi kujipunguzia kura. Hiwezi kuhubiri usawa na amani jukwaani wakati watu wanaona kabisa unadanganya!
Hoja hiyo ni HOJA au KIOJA maana zaidi ya 90% ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umiliki wake ni watu binafsi vikiendeshwa kibiashara. Ili upate "coverage" lazima ulipie. Je, hao wamelipia wakakataliwa?
 
Just muongo balaa et anawadanganya alichaguliwa uenyekiti wa SADC kwa kua ana mahusiano mazuri wakati uenyekiti huo ni wa kupokezana hata Kama hupendwi lazma upewe
 
Just muongo balaa et anawadanganya alichaguliwa uenyekiti wa SADC kwa kua ana mahusiano mazuri wakati uenyekiti huo ni wa kupokezana hata Kama hupendwi lazma upewe

Acha kuposha wewe,Mbali na kupokezana lazima wajiridhishe na utendaji kazi,Uwajibikaji na mahusiano na mataifa Mengine.
Sasa unachokisema sijui umekitolea wap ndugu yangu?
 
Mgombea Urais kupitia CCM leo akiwa chato kule alikozaliwa amefika shehemu sasa amechoka kukaa na nyongo tumboni hivyo ameitema kama ilivyo alipokuwa jukwaani. Nyongo hiyo ambayo ni chungu sana ambayo yeye amekaanayo sana na sasa kuamua kutemea wenzake waionje, Amesema wapinzani wote amewaangalia na kuona kuwa wote ni wachovu wamechoka hakuna kiongozi hata mmoja anayeweza kulisogeza taifa hili mbele hata robo ya kazi aliyoifanya, na zaidi wote nikama wanatafuta ubwabwa tu.

Hii kauli inamaanisha kuwa tukipata Rais kutoka upinzani tutakuwa tunapiga hatua 3 mbele alafu tunapiga hatua zingine 9 kurudi nyuma.
Kauli hii inaleta hari ya wasi wasi kwa kambi za ushindani kutoka upinzani kwani ni kama kombola lililoachiliwa kutoka angani na kupiga kambi ya adui, kwa sababu tuna fanya uchaguzi hili tupate kiongozi atakaye tuletea maendeleo sasa yeye anasema huko wote ni feki.

Kwa upande mwingine Magu anaweza kuwa na sababu za kusema hayo kwani upinzani hasa ukiongozwa na Chadema wamekuwa kinyume cha hayo maendeleo na kupinga kilakitu bila hata ya kuweka taadhali yoyote za kauli zao tata ambapo tafsiri yake ni kuwa kama wataingia wao madarakani maendeleo haya hawata fanya hila mambo mengine na hawajayataja ni yapi mbadala wa maendeleo watakaoufanya.

Kauli hii ya Magufuli imepokelewa kwa namna tofauti na makundi mbalimbali ya kijamii wakati wengine wakiishiwa punzi, wengine wanaona kama dongo la kisiasa wakati makundi mengine wanaona kama sehemu ya kujifunza hili kufanya maamuzi Octoba.
Hili pia linakuja baada ya siku kadhaa za uchaguzi tayari kuna picha inaonekana. Mfano:
Mgombea wa ACT yeye katorokea Uarabuni, hii ni mara ya kwanza duniani mgombea wa uraisi kutoka nje ya nchi wakati wa kinyang'anyilo ni kama bondia ameondoka ulingoni katikati ya pambano.

Mwingie ni Mzee Lungwe na sera yake ya ubwabwa huku kwetu Upogoloni ubwabwa ni kitu cha kawaida sana kwani kuanzia Januari hadi Desemba asubui mchana na jioni ni mpunga sasa hatuelewi kwani hari zetu ni duni sana na ubwabwa tunakula sana labda akija tutaweza kuuliza maswali hili tuelewe.

Mwingine ni Lisu yeye huko nyuma hakujulikana vizuri kuwa ni nani lakini sasa ameeleweka kuwa yeye ni mzungu hila baatimbaya alizaliwa Singida tu, tayari amekuja na sera yake kuwa watanzania hawajui kiingereza, kazi ipo. Huyu Lisu yeye ananadi risasi 16 na zingine anatembea nazo mwilini, hili la kupigwa risasi ni jambo baya lakini watanzania hawawezi kumpa nchi heti tu kwa sababu alipigwa lisasi hili ni ujinga ambao Chadema hawatakiwi kurudia tena, watengeneze sera.
 
Acha kuposha wewe,Mbali na kupokezana lazima wajiridhishe na utendaji kazi,Uwajibikaji na mahusiano na mataifa Mengine.
Sasa unachokisema sijui umekitolea wap ndugu yangu?

Wacha uongo wako,ile ni nafasi ya zamu zamu kila mwaka Rais wa nchi mojawapo anakua Chairman haina cha una mahusiano mazuri wala nini.

Tena achana hata na SADC ambayo ni regional block tu.Chukulia mfano huu:

OAU(hii ni ya Africa nzima,kwa sasa AU) Iddi Amini alishawahi kua Mwenyekiti wake mwaka 1975 je hapo Iddi Amin alikua ana mahusiano mazuri na nani,alikua na uwajibikaji gani?

Naandika hayo yote kukuonyesha hizo nafasi za wenyeviti kwny hizi jumuiya za Kanda SADC/EAC/COMESA etc ni za zamu zamu kwa nchi wanachama hazina mambo ya mpk uwe competent wala nini.
 
Tafuta Ratiba ya kampeni za wagombea Urais kwenye mtandao wa NEC. Usiwe mvivu na kuanza kulaumu. Mazoea mabaya
Ratiba imepitishwa na tume, leo tunaanza Kagera siku mbili, ccm ni ya watanzania lazima watanzania waongee na rais wao, mwendo ni mdundo.Lissu yeye kihoro cha kutaka aonekane kila mahali lakini output ni zero. Hana cha kupoteza, lakini Magu lazima apite kila wilaya kutoa shukrani na pia kusherekea mafanikio na wananchi.
 
Huyu bwana ata huko alikozaliwa hawamtaki, hawataki hata kumsikia, acheni propaganda uchwara.

Alo kudanganya nani wakati unaambiwa siku zote mcheza kwao hutunzwa, ukitaka kuamini kwamba wananchi wanaroho za wajumbe subiri 28 oct. Mitano tena lisu na chadema yake na kumchafua muheshimiwa kote kule, chalkkk
 
MKUTANO WA MGOMBEA URAIS JOHN POMBE MAGUFULI KUTOKEA CHATO, GEITA UKO LIVE

Tumia hizi Links Chini Kufuatilia Kila kitu kutokea Chato, Geita

===
MAGUFULI: MZEE MKAPA NDIYE ALIYENIOKOTA HUKO ‘JALALANI’

Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli amesema akimfikiria Hayati Rais Mkapa huwa anaumia kwenye nafsi yake

Amesema Rais Mkapa ndiye aliyemuokota ‘Jalalani’ amesema hayo kwa kuwa kuna watu wanadai siku hizi mtu akipata kazi anasemwa amokotwa jalalani na Magufuli

Dkt Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika Chato mkoani Geita. Aidha amewataka wananchi kuendelea kumuamini

Katika Kampeni hizo Magufuli amesema walisimama imara kukomesha uhalifu, kama maeneo ya Kibiti na Biharamulo. Amewapongeza sana vyombo vya ulinzi na usalama




 
Naiomba Serikali itolee ufafanuzi hii kauli, ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi,hususani wafanyakazi

Serikali imekopa mifuko ya hifadhi za jamii PSSSF na NSSF na haijaweza kurudisha. MBAYA zaidi, mwaka huu kuanzia April hivi, Mifuko imeshindwa kulipa mafao. Jana Mh. Lisu akasema kuwa CCM imechukua pesa Za KAMPENI huko kwenye mifuko ya PSSSF na NSSF. Je wafanyakazi mnalipwa mafao yenu ya uzee na fao la kukosa ajira kwa wakati?

Mimi sijui, kamuulizeni aliyesema ..ni Mh. Lisu. Sikilizeni clip za Mwananchi Youtube.

Na akiwa Morogoro, akasema Vigogo wa CCM wamepora mashamba makubwa mvomero, Morogoro. Mkapa elfu 60, Familia ya Mwinyi elfu 60, Sumaye 2000 etc. Sehemu mbali mbali za nchi na zile ranch. Wananchi wanakosa maeneo ya kulima na kulishia mifugo...

Ni Mh. Lisu alisema...Youtube.

Sasa hizi ndio hoja za kujibu kwa Serikali..na Sio kusema kuna mtu anatukanwa..
Hekta elfu 60 ni sawa na mikoa mitatu, inawezekana mtu mmoja akamiliki?
 
Bila wakulima wakubwa chakula kitatoka wapi? Wasipolima hawa wazee wenye pension kubwa Nani alime?
 
Back
Top Bottom