Yaliyojiri bungeni Dodoma: Jumapili, 5 Julai 2015

Yaliyojiri bungeni Dodoma: Jumapili, 5 Julai 2015

Alipokuwa akielezea jinsi kifungu na 21 kilivyoweka adhabu ya kifungo cha miaka 30, Kulipa na kufilisiwa mwizi wa mfuko wa mapato ya gesi, hukumusikia.

Alipokuwa akielezea jinsi sheria ilivyoweka utaratibu wa uwazi katika mapato hukumsikia?

Alipokuwa akielezea furaha yake jinsi mswaada ulivyoweka utaratibu wa mgawanyo wa mapato katika maeneo raslimali hiyo inapopatikana Hukumusikia?

Hukumusikia alipokuwa...... ( aaaah hamna faidi ya kuendelea sababu hukuyasikia yale unayotaka wewe kuyasikia)

inaonekana wewe ni mgeni tanzania. maccm yanasema kingine na yanatekeleza kingine. miswada hii kwa nje ni mizuri lakini kwa ndani kuna matatizo mazito...
 
Huyo mwenyekiti wa kamati ya maadili na madaraka ya bunge anapaswa kuchukuliwa hatua kwa kulidanganya na kulipotosha bunge
 
hukumu itawajia mapema tu hao maccm kwa kuwadhulumu watz maliasili yao.
 
Dr. Asha Rose Migiro. Kosa kubwa analolifanya Spika Makinda ni kuwavumilia wapinzani.

Mchakato wa kutunga sheria hizi ulianza mwaka 2011. Maandalizi ya sera hizi yalianza 2005. Mchakato ulishika kasi 2011 kwasababu ndipo gesi ilipogunduliwa.

Serikali iliwashirikisha wadau mbalimbali, kama Norway, ESRF, TLS etc.

Marejeo ya sheria kutoka nchi mbalimbali yalipitiwa Togo, Uganda, Norway, etc Serikali hajakurupuka.

Makundi 8 ya wabunge yalitembelea nchi mbalimbali Thailand, China, Uganda, Qatar, Trinidad and Tobago.

Ziara za mafunzo kama Kunduchi, bungeni ukumbi wa Msekwa, public hearing ya wataalamu.

Miswaada ulichapishwa kwenye gazeti la serikali, wadau waliitwa kwenye kamati wakatoa maoni.

Neno dharura ni kipindi sio kuruka taratibu, ni neno la kiufundi.

Maudhui ya miswaada ni kudhibiti uendeshaji. Ugunduzi na matayarisho yatumike kuendeleza wananchi wetu.

Uwazi, sasa miswaada hii inajibu kilio cha uwazi. Inatoa maelekezo ya jinsi mapato yakavyotumika.

Mfumo wa kisheria ndio unasubiriwa, hakuna kusubiri serikali ijayo, kwani hakuna serikali itakayokuja itabadilisha mfumo huu.

Ameunga mkono hoja.
 
Niko kwenye luninga na mm naangalia bunge leo. Ukiachia vijembe vya hapa na pale naona walio wengi wanajaribu kuongelea mazuri ya hii miswaada. Ambacho sijakiona wala kusikia ni wote kuzungumzia mgawo wetu kutokana na mapato ya gas. Nadhani kilio chetu ni gawio letu hasa kwenye madini kwani ndio sehemu wengi wetu tumeitumia kama sehemu ya angalizo letu. Kila mtu anajua tutapata hela hilo hakuna asiyejua ila tutapata kiasi gani na kwanini hapo ndio ngoma.

Tunaomba wabunge wa ccm waliseme hili kwani kuna mmoja kasema kwa jazba hapa kwamba kaangalia kwenye mtandao muda huu na kuona wabunge wa ccm na spika wanakashifiwa.

NB: inaonekana kuna upotoshaji wa makusudi ama kukosa umakini kwa wabunge wa ccm, wapinzani hawajasusia bali wametolewa wengi baada ya kutoridhishwa na muda wa muswaada ulioletwa kwa hati ya dharura.
 
ndani ya ccm hata ukawa na madigirii mangapi utakuwa sawa tu na wenzako. namuona dr. asha rozi anatetea muswada huu haramu ili tu kuhakikisha anapata kula yake. eti huyo ndo mgombea urais wa ccm. watanzania mwezi oktoba tusiangalie mtu usoni.
 
siasa za nchi hii ni za hovyo tu,wote wanatafuta umaarufu tu,
 
Kwa hasira wananchi wameacha kutizama bunge na kuelekea kupanga foleni kwenye BVR.
 
Chombo; Miswaada hii ina manufaa sana kwa Wazanzibari. Anamshukuru Mungu kuuleta miswaada hii kwenye mwezi wa Ramadhani.

Sheria ya mwaka 80 ya mafuta na gesi ni suala muungano. Sheria hii inatoa zuio kwa Zanzibar kuchimba mafuta.

UKAWA ni ndugu zetu lakini si wenzetu. hata kwenye BLW walitoka nje.

ZNZ inatafuta kupata mamlaka kamili, lakini ndugu zetu wanakimbia kwani miswaada hii inaipatia ZNZ mamlaka kamili.

Wale wanaojidai wana masilahi na ZNZ hawana masilahi na ZNZ wana masilahi na MABWANA zao. Hao ni wanafiq, siku zimekaribia za kuwaondoa mbali, hao sio wazanzibari.

Kuna makampuni yako tayari yanasubiri miswaada hii ipite yaanze kuchimba mafuta ZNZ. Ameunga hoja kwa 100%

Mafuta ya zanzibar yatachimbwa na wazanzibar wenyewe na sio kwa miswada toka dodoma.
 
NDIPO Wtz mtakapo jua CCM ndiyo chanzo cha umasikini wetu.TANGU AFE NYERERE ALIYE KUWA UPANDE WAWA WATZ HIKI CHAMA KIMEWATUPA WANANCHI

Ukawa watuambie kasoro za miswada hii mitatu ili tuwarudishe bungeni.
 
wachngiaji wamekwisha/hawapo,kaamua kuwaleta mawaziri kumalizia kabla hawajaenda kwenye kamati ya bunge zima
 
inaonekana wewe ni mgeni tanzania. maccm yanasema kingine na yanatekeleza kingine. miswada hii kwa nje ni mizuri lakini kwa ndani kuna matatizo mazito...

Inayojadiliwa hapa ni sheria sio ahadi za wana CCM. Sheria ni kitu ambacho kinalazimisha utekelezaji utake usitake utake usitake.
 
Dr. Asha Rose Migiro. Kosa kubwa analolifanya Spika Makinda ni kuwavumilia wapinzani.

Mchakato wa kutunga sheria hizi ulianza mwaka 2011. Maandalizi ya sera hizi yalianza 2005. Mchakato ulishika kasi 2011 kwasababu ndipo gesi ilipogunduliwa.

Serikali iliwashirikisha wadau mbalimbali, kama Norway, ESRF, TLS etc.

Marejeo ya sheria kutoka nchi mbalimbali yalipitiwa Togo, Uganda, Norway, etc Serikali hajakurupuka.

Makundi 8 ya wabunge yalitembelea nchi mbalimbali Thailand, China, Uganda, Qatar, Trinidad and Tobago.

Ziara za mafunzo kama Kunduchi, bungeni ukumbi wa Msekwa, public hearing ya wataalamu.

Miswaada ulichapishwa kwenye gazeti la serikali, wadau waliitwa kwenye kamati wakatoa maoni.

Neno dharura ni kipindi sio kuruka taratibu, ni neno la kiufundi.

Maudhui ya miswaada ni kudhibiti uendeshaji. Ugunduzi na matayarisho yatumike kuendeleza wananchi wetu.

Uwazi, sasa miswaada hii inajibu kilio cha uwazi. Inatoa maelekezo ya jinsi mapato yakavyotumika.

Mfumo wa kisheria ndio unasubiriwa, hakuna kusubiri serikali ijayo, kwani hakuna serikali itakayokuja itabadilisha mfumo huu.

Ameunga mkono hoja.

ndani ya ccm hata ukawa msomi mzuri namna gani lazima uungane na wenzako. mfumo wao wote ni wa kulindana tu. dr. asha rozi hajalisaidia taifa letu kulingana na utaalamu wake.
 
Naibu waziri Charles Mwijage ndio anahutubia sasa! Lakini bahati mbaya huku TANESCO wamechukua kilicho chao!
 
Ukawa watuambie kasoro za miswada hii mitatu ili tuwarudishe bungeni.

nadhani hayo lazima wayaseme. maana miswada hii ipo. wataalamu wa sheria kina lissu watafafanua kwa wananchi kila kipengele madhaifu yake kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom