chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 20,711
- 31,331
Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linaendelea na vikao vyake leo jumapili. Wabunge wanaendelea kujadili miswada mitatu ya mafuta na gesi asilia kwa pamoja.
Jana na juzi wabunge mbalimbali wa upinzani, wamefukuzwa na kufungiwa kuingia bungeni kwa siku tano. Huu mjadala kwa kiasi kikubwa unajadiliwa na Wabunge wa CCM tu kwani wale wa upinzani wote wanapinga miswada hii kwa kile wanachodai hawawezi kujadili miswada yenye manufaa makubwa kwa taifa kwa hati ya dharula. Wanataka wapate muda mrefu wa kuisoma hiyo mikataba na kuielewa kuliko hivi sasa ambapo wabunge wengi hawajaisoma na kuielewa.
Jana na juzi wabunge mbalimbali wa upinzani, wamefukuzwa na kufungiwa kuingia bungeni kwa siku tano. Huu mjadala kwa kiasi kikubwa unajadiliwa na Wabunge wa CCM tu kwani wale wa upinzani wote wanapinga miswada hii kwa kile wanachodai hawawezi kujadili miswada yenye manufaa makubwa kwa taifa kwa hati ya dharula. Wanataka wapate muda mrefu wa kuisoma hiyo mikataba na kuielewa kuliko hivi sasa ambapo wabunge wengi hawajaisoma na kuielewa.
Mama spika ameendelea kuwa ngangari hata leo baada ya kuukataa muongozo uliombwa na Selasini na Halifa ambao wamesema hawakujutia makosa kama ilivyotamkwa jana. Na kwamba wamezalilishwa kwa kauli hiyo ya kamati. Selasin ameamua kutoka. My take; Makinda kajiandaa kuwamaliza wote mle ndani anatumia rungu la spika na amekuwa mbogo. Hata wapinzani wasiosimamishwa kama wataingia bungeni labda wachangie kikawaida wakitumia miongozo atawatoa nje.
Dianna Chilolo: Hakuna hata mbunge mmoja wa UKAWA aliyewahi kukaa bugeni kama Anna Makinda
Wanawake wakatae UKAWA kwasababu Spika Makinda amedharalilishwa kama mwanamke kwa kumuona hafai. wanawake wawasome namba UKAWA wawakatae.
Misaada imeletwa kwa hati ya dhararu, haina maana imekuja kwa ajali. Hati ya dhararu maana yake imepewa kipaumbele.
Wanataka wawekee uataratibu wazawa na wageni katika kuwekeza katika mafuta na gesi asilia. Miswaada 3 ni mizuri, ni mizito na ina masilahi kwa watanzania. Ameunga mkono hoja.
Ismail Aden Rage: UKAWA ni watoto wadogo Spika awasamehe Mungu atawaadhibu.
Wabunge walipelekwa kujifunza utaratibu wa mabunge ya commonwealth. UKAWA ni wepesi kushiriki mafunzo ya nje.
Nimesoma taarifa ya Law Tanganyika society. Miswaada ni mizuri imekuja wakati muafaka ipitishwe ili kuongeza uwajibikaji.
Nilimuhoji CE wa TPDC kwanini hataki kutoa mikataba gesi na mafuta. Kwasababu TPDC wanalinda interest za wawekezaji. Miswaada hii inaleta huo uwazi.
Airtel tangu imeanzishwa serikali haijapata gawiwo hata kidogo. Makampuni yatakayokuja yajisajiri kwenye soka la hisa la DSE. Ameunga mkono miswaada yote mitatu.
Mtutula Abdallah Mtutula (Tunduru); Bei ya korosho imepungua
Mhimiri wa nne unapotosha watu. Hati ya dharura maana yake ni ofisi ya Spika kuipa miswaada kipaumbele.
Wabunge wa CCM kama wangekuwa na akili wangeacha kujadili miswaada hiyo. Hizo ni kauli za ajabu sana.
Unapokata jambo kata maudhui, maudhui ya miswaada ni kuhakikisha kwamba wananchi wananufaika na gesi.
Kambi ya upinzani walikuwa wanadai mafuta na gesi hayana sheria imara. Leo miswaada imeletwa wapinzani wanakimbia.
Miswaaada imeunda kamati mablimbali za usimamizi.
Sheria tume copy kutoka Uganda. Ukweli Uganda ndio wame copy kutoka kwetu. Mwisho ameunga hoja.