Yaliyojiri bungeni Dodoma: Jumapili, 5 Julai 2015

Yaliyojiri bungeni Dodoma: Jumapili, 5 Julai 2015

Huo ni uongo haiwezekani kuzuia mafao yao, hata wakizuia haina maana watawazuia kuingia bungeni teni
 
Naomba wanasheria mnisaidie; Hivi mtu akiiba na ikathibitishwa alafu akaambiwa arudishe alicho iba ni adhabu kweli?
 
mbwiga mmoja kaomba mabomba ya gesi yaanze kusambazwa vijiji at the same time anataja vijiji vya jimboni mwake visivyo na umeme tangu uhuru miaka hamsini iliyopita,kama umeme ni ishu kwenye vijiji, mabomba ya gesi je??!!
 
Kuna mbunge kawashukuru wanawake zake wa pwani.
 
Mkuu habari ndio hiyo, eti miswaada ya Muhimu kama hiyo yenye vifungu zaidi ya 200 ijadiliwe kwa hati ya dharura. Utashangaa wakati wote walikuwa wapi kama sio zima moto hii. Ndio maana UKAWA walikataa
Labda wakongwe na wenye umr mkubwa watujuze kama iliwah tokea pia inamana hawa wabunge wa chama changu wamesoma vizur line aftet line
 
Hivi kumbe kanuni zinatenguliwa,,,,,,,napita tu
 
Kinachoshangaza wabunge wote wa ccm wanaonga mkono hoja ya serikali na kila anaeunga mkuno Spika anampongeza. naomba wanchi wasikubali kumchagua mbunge yeyote wa ccm kuwarudisha bungeni hawatutendei haki sisi wenye wasiwasi na suala hilo. wabunge wote wa ccm wamekuwa kama wao ndio walioupeleka huu mswada bungeni
 
Kuna mama moja mbunge wa huko pwani, anaongea kama mtu anayetafuta huruma ya Watanzania, amekuwa excited kweli na amekuwa hasemi kivipi sheria hiyo itakavosaidia watanzania bali kulazimisha tu tuamini kuwa itasaidia, jaman tusirudie kufanya makosa ya kuwapeleka bungeni watu kama hawa ifikapo October 25!
 
yaani kila sheria inayopitishwa na ccm, wanaipamba utadhani ni njema halafu baada ya mwaka mmoja wanataka kurekebisha
 
Mtutula Abdallah Mtutula (Tunduru); Bei ya korosho imepungua

Mhimiri wa nne unapotosha watu. Hati ya dharura maana yake ni ofisi ya Spika kuipa miswaada kipaumbele.

Wabunge wa CCM kama wangekuwa na akili wangeacha kujadili miswaada hiyo. Hizo ni kauli za ajabu sana.

Unapokata jambo kata maudhui, maudhui ya miswaada ni kuhakikisha kwamba wananchi wananufaika na gesi.

Kambi ya upinzani walikuwa wanadai mafuta na gesi hayana sheria imara. Leo miswaada imeletwa wapinzani wanakimbia.

Miswaaada imeunda kamati mablimbali za usimamizi.

Sheria tume copy kutoka Uganda. Ukweli Uganda ndio wame copy kutoka kwetu. Mwisho ameunga hoja.
 
kati ya watangaza wa ccm kuna aliepinga mswaada kama hakuna.. ni disqualification mojawapo.
 
hahaaha,wamekunja ndita as if wako siriaz
 
Kuna mama moja mbunge wa huko pwani, anaongea kama mtu anayetafuta huruma ya Watanzania, amekuwa excited kweli na amekuwa hasemi kivipi sheria hiyo itakavosaidia watanzania bali kulazimisha tu tuamini kuwa itasaidia, jaman tusirudie kufanya makosa ya kuwapeleka bungeni watu kama hawa ifikapo October 25!

Alipokuwa akielezea jinsi kifungu na 21 kilivyoweka adhabu ya kifungo cha miaka 30, Kulipa na kufilisiwa mwizi wa mfuko wa mapato ya gesi, hukumusikia.

Alipokuwa akielezea jinsi sheria ilivyoweka utaratibu wa uwazi katika mapato hukumsikia?

Alipokuwa akielezea furaha yake jinsi mswaada ulivyoweka utaratibu wa mgawanyo wa mapato katika maeneo raslimali hiyo inapopatikana Hukumusikia?

Hukumusikia alipokuwa...... ( aaaah hamna faidi ya kuendelea sababu hukuyasikia yale unayotaka wewe kuyasikia)
 
kuna mmoja kaomba mabomba ya gesi yasambazwe vijijini,haladfu baadae anataja vijiji ambavyo havina umeme kwa miaka hamsini ya uhuru,mtu kama huyu hata maji ya bomba jimboni kwake ni ishu,sembuse mabomba ya gesi
 
haa haa hili bunge limebaki kama komedi tu. yaani wabunge wa ccm wote wamejigeuza mawaziri.masikini watanzania hawa watu hawatakiwi kurudi bunge lijalo.
 
Chombo; Miswaada hii ina manufaa sana kwa Wazanzibari. Anamshukuru Mungu kuuleta miswaada hii kwenye mwezi wa Ramadhani.

Sheria ya mwaka 80 ya mafuta na gesi ni suala muungano. Sheria hii inatoa zuio kwa Zanzibar kuchimba mafuta.

UKAWA ni ndugu zetu lakini si wenzetu. hata kwenye BLW walitoka nje.

ZNZ inatafuta kupata mamlaka kamili, lakini ndugu zetu wanakimbia kwani miswaada hii inaipatia ZNZ mamlaka kamili.

Wale wanaojidai wana masilahi na ZNZ hawana masilahi na ZNZ wana masilahi na MABWANA zao. Hao ni wanafiq, siku zimekaribia za kuwaondoa mbali, hao sio wazanzibari.

Kuna makampuni yako tayari yanasubiri miswaada hii ipite yaanze kuchimba mafuta ZNZ. Ameunga hoja kwa 100%
 
Tumempa Simba ufalme wa pori na tukampamba kwa,manyoya shingon leo hii ametugeuka anatutafuna atakavyo ndio Ccm hiyo ila kila kilicho na mwanzo hakikosi mwisho na pia historia inaonyesha kua chama kinachoelekea kufa kilianza mambo ya hovyo kama Ccm. Mungu ibarik Tanzania
 
Back
Top Bottom