Yalipaswa kuwa makubaliano kati ya Dubai na Ilala, tena yapitishwe na baraza la madiwani na sio bunge.

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,131
35,168
Kwenye sakata la Bandari tumegundua kumbe Dubai sio nchi na haina hadhi ya kuridhia mikataba ya kinchi, hivyo kilikuwa ni kimbelembele cha kijinga cha bunge la Tanzania kuingia kichwa kichwa na kuridhia ule mkataba wa kifedhuli.

Sasa wataalamu wetu wanasema lile deal la makubaliano ya ushirikiano lilipaswa kutengenezwa na kuwa kati ya jiji la Ilala (Dar?) na kuja kupitishwa na baraza la madiwani wa Ilala ili kutengeneza mazingira ya kibiashara kwa kampuni ya Dp world ya kule Dubai kuja kutafuta fursa ya kuwekeza kwenye wilaya ya Ilala mahali ambapo bandari ya Dar ipo.

Ule uwendawazi wa kumpatia muarabu wa Dubai bandari zote za Tanzania tena umiliki wa milele uliofanywa na bunge lolote hauna tofauti na mwanaume mmoja tajiri sana mwenye wake wanne wazuri na mabinti zake warembo zaidi ya kumi aliyeamua kumpatia wake zake wote, mabinti zake wote na mali zake zote kijana mmoja asiyefahamika vyema kutoka mbali alionyesha nia ya kutaka kuchumbia binti yake mmoja.
 
Walete walete... Akina Lord denning Faizafoxy aka bi kidu na mfia CCM flan hivi!!
 
Back
Top Bottom