Shivji ataka Bunge libatilishe azimio la Mkataba wa Bandari na Serikali ya Dubai

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Mwanazuoni Profesa Issa Shivji amekosoa mkataba baina ya Tanzania na Dubai unaohusu uboreshaji na uendeshaji wa bandari, huku akishauri Bunge kubatilisha azimio la kuridhia mkataba huo wa awali.

Profesa huyo ambaye ni nguli wa sheria amependekeza njia hiyo leo Jumatano Juni 28, 2023 wakati akizungumza kwenye mjadala uliokuwa na mada isemayo: “Njia kuu za uchumi na tafakuri ya mkataba wa mahusiano ya kijamii na kiuchumi kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai.”

Mwanazuoni huyo amedai njia zilizochukuliwa na wadau wengine ikiwemo kwenda mahakamani, hazitasaidia kuondokana na sintofahamu iliyopo hivi sasa kuhusu mkataba huo ambao mjadala wake unazidi kupamba moto kila kukicha.

Katika mchango wake, Profesa Shivji amesema zipo njia nyingi zilizopendekezwa baadhi ya wadau wakiwemo viongozi wastaafu na watalaamu wa sheria, lakini kwa maoni yake hadhani kama zitasaidia Taifa kutoka katika sintofahamu hiyo, kwa madai kuwa Bunge limesharidhia mchakato huo.

“Haiwezekani hata kurekebisha vifungu kwa aina ya mkataba huo. Kuna wengine wanakwenda mahakamani, lakini kama mnavyojua mahakama zetu zinachukua muda mrefu kusikiliza kesi,” amesema Profesa Shivji.

Mjadala huo ambao uliandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), ndaki ya Sayansi ya Jamii, ulishirikisha wasomi na wadau mbalimbali ambapo walipa fursa ya kutoa maoni yao juu ya mada hiyo ambayo bado imeendelea kuwa gumzo.

Oktoba 25 mwaka 2022 Serikali ya Tanzania na Dubai ziliingia makubaliano katika ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari na uendeshaji wa miundombinu ya kimkakati ya bandari za bahari na maziwa makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maegesho ya utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.

Hatua hiyo imebua mjadala na kuwagawa baadhi ya wadau na vigogo wakiwemo viongozi wastaafu wa zamani. Wapo wanaounga mkono hatua ya Serikali huku wengine wakipinga mchakato huo wakidai hauna manufaa kwa Taifa, lakini kwa nyakati tofauti Serikali imekuwa ikisisitiza manufaa ya suala hilo.

Juni 25, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba alishauri kuangaliwa upya kwa vifungu vyenye mkanganyiko katika mkataba huo. Alisema ni kweli uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam haukuwa wa kuridhisha kwa muda mrefu, lakini makubaliano yaliyopo yana vipengele vinavyoleta wasiwasi.

Wakati Jaji Warioba akitoa ushauri huo jana Jumanne, kundi la mawakili wanne wa kujitegemea wakiongozwa na Alphonce Lusako walikwenda mahakamani kupinga mkataba huo.

Lakini leo Profesa Shivji amehoji,”hata ukiingia mahakamani utachallange nini? Utakuwa una challenge azimio la Bunge sio makubaliano yaliyoingiwa baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai,” amesema Profesa Shivji.

Mawazo ya Profesa Shivji hayana tofauti na mwanasheria mwingine Tundu Lissu ambaye hivi karibuni alisema haona haja kwenda mahakama kupinga mchakato huo, kulingana na mkataba wenyewe ulivyo.

Profesa Shivji amesema njia ya pekee ni Bunge kuketi upya na kusema kwamba baada ya maoni ya wananchi wameona na azimio walilolipitisha halikuwa sahihi, hivyo wanaazimia kulifuta, akisema jambo hilo linawezekana.

MWANANCHI
 
Tunahitaji sheria ya kunyonga na kusiwepo kinga dhidi ya mashtaka kwa viongozi ndiyo chanzo cha kiburi.

Tunawaacha tu wanakaza fuvu ila mambo yakienda sivyo ni vitanzi tu vinatembea.
 
Sijui hawa watu ni wagumu kiasi gani kuelewa, tulishawashauri watupilie mbali hicho wanachoita makubaliano.......TPA waje na utaratibu wa kutangaza tender kwa ajili ya kuendesha operation za mabehewa bandarini kama sheria ya manunuzi ya umma inavyotaka.​
 
Attachments

  • B8E4191F-3638-4F92-9288-E4851DACDAE6.jpeg
    B8E4191F-3638-4F92-9288-E4851DACDAE6.jpeg
    35.3 KB · Views: 5
Tunahitaji sheria ya kunyonga na kusiwepo kinga dhidi ya mashtaka kwa viongozi ndiyo chanzo cha kiburi.
Sheria ya kunyongwa na mali zao kufilisiwa ndio itakua dawa yao hawa ccm. Sasa hivi kila kitu ruksa kwa kuwa hakuna la kuwafanya.
 
Mwanazuoni Profesa Issa Shivji amekosoa mkataba baina ya Tanzania na Dubai unaohusu uboreshaji na uendeshaji wa bandari, huku akishauri Bunge kubatilisha azimio la kuridhia mkataba huo wa awali.

Profesa huyo ambaye ni nguli wa sheria amependekeza njia hiyo leo Jumatano Juni 28, 2023 wakati akizungumza kwenye mjadala uliokuwa na mada isemayo: “Njia kuu za uchumi na tafakuri ya mkataba wa mahusiano ya kijamii na kiuchumi kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai.”

Mwanazuoni huyo amedai njia zilizochukuliwa na wadau wengine ikiwemo kwenda mahakamani, hazitasaidia kuondokana na sintofahamu iliyopo hivi sasa kuhusu mkataba huo ambao mjadala wake unazidi kupamba moto kila kukicha.

Katika mchango wake, Profesa Shivji amesema zipo njia nyingi zilizopendekezwa baadhi ya wadau wakiwemo viongozi wastaafu na watalaamu wa sheria, lakini kwa maoni yake hadhani kama zitasaidia Taifa kutoka katika sintofahamu hiyo, kwa madai kuwa Bunge limesharidhia mchakato huo.

“Haiwezekani hata kurekebisha vifungu kwa aina ya mkataba huo. Kuna wengine wanakwenda mahakamani, lakini kama mnavyojua mahakama zetu zinachukua muda mrefu kusikiliza kesi,” amesema Profesa Shivji.

Mjadala huo ambao uliandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), ndaki ya Sayansi ya Jamii, ulishirikisha wasomi na wadau mbalimbali ambapo walipa fursa ya kutoa maoni yao juu ya mada hiyo ambayo bado imeendelea kuwa gumzo.

Oktoba 25 mwaka 2022 Serikali ya Tanzania na Dubai ziliingia makubaliano katika ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari na uendeshaji wa miundombinu ya kimkakati ya bandari za bahari na maziwa makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maegesho ya utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.

Hatua hiyo imebua mjadala na kuwagawa baadhi ya wadau na vigogo wakiwemo viongozi wastaafu wa zamani. Wapo wanaounga mkono hatua ya Serikali huku wengine wakipinga mchakato huo wakidai hauna manufaa kwa Taifa, lakini kwa nyakati tofauti Serikali imekuwa ikisisitiza manufaa ya suala hilo.

Juni 25, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba alishauri kuangaliwa upya kwa vifungu vyenye mkanganyiko katika mkataba huo. Alisema ni kweli uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam haukuwa wa kuridhisha kwa muda mrefu, lakini makubaliano yaliyopo yana vipengele vinavyoleta wasiwasi.

Wakati Jaji Warioba akitoa ushauri huo jana Jumanne, kundi la mawakili wanne wa kujitegemea wakiongozwa na Alphonce Lusako walikwenda mahakamani kupinga mkataba huo.

Lakini leo Profesa Shivji amehoji,”hata ukiingia mahakamani utachallange nini? Utakuwa una challenge azimio la Bunge sio makubaliano yaliyoingiwa baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai,” amesema Profesa Shivji.

Mawazo ya Profesa Shivji hayana tofauti na mwanasheria mwingine Tundu Lissu ambaye hivi karibuni alisema haona haja kwenda mahakama kupinga mchakato huo, kulingana na mkataba wenyewe ulivyo.

Profesa Shivji amesema njia ya pekee ni Bunge kuketi upya na kusema kwamba baada ya maoni ya wananchi wameona na azimio walilolipitisha halikuwa sahihi, hivyo wanaazimia kulifuta, akisema jambo hilo linawezekana.

MWANANCHI
😭😭😭Yaani tangu Prof alipo ongea Jana, Moyo unalia Sana na kulaani I maamuzi hayo. Hapa unajiuliza, hivi kumbe ni kweli mwanamke hapaswi kuongoza ehh... Mama Mia ndio hivi, mama Bunge la haula... Tulikosa wapi sisi... Mbona wamama wa nakuwa na huruma na watoto wao... Hawa Wa nawaza nini juu ya watoto wa kitanzania... Hivi mtu anaweza abadili kabisa utu anapokua madarakani... Au Hawa watu wamekuwa-cloned? Naamini sio Muda watalipa machozi ya watanzania... Vizazi vyao vitalaumu kuzaliwa na wao... Muda utaongea😭😭😭
 
Relax mkuu. Nadhani wahusika watarekebisha the atmosphere and things gonna be alright.

-Kaveli-
 
Sijui hawa watu ni wagumu kiasi gani kuelewa, tulishawashauri watupilie mbali hicho wanachoita makubaliano.......TPA waje na utaratibu wa kutangaza tender kwa ajili ya kuendesha operation za mabehewa bandarini kama sheria ya manunuzi ya umma inavyotaka.​

Kwani DP WORLD walipatikanaje mkuu, single sourced? ama kiaje?

-Kaveli-
 
Long live Prof Shivji.

You are among the best icons katika Taifa la Tanzania.

-Kaveli-
 
Mwanazuoni Profesa Issa Shivji amekosoa mkataba baina ya Tanzania na Dubai unaohusu uboreshaji na uendeshaji wa bandari, huku akishauri Bunge kubatilisha azimio la kuridhia mkataba huo wa awali.

Profesa huyo ambaye ni nguli wa sheria amependekeza njia hiyo leo Jumatano Juni 28, 2023 wakati akizungumza kwenye mjadala uliokuwa na mada isemayo: “Njia kuu za uchumi na tafakuri ya mkataba wa mahusiano ya kijamii na kiuchumi kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai.”

Mwanazuoni huyo amedai njia zilizochukuliwa na wadau wengine ikiwemo kwenda mahakamani, hazitasaidia kuondokana na sintofahamu iliyopo hivi sasa kuhusu mkataba huo ambao mjadala wake unazidi kupamba moto kila kukicha.

Katika mchango wake, Profesa Shivji amesema zipo njia nyingi zilizopendekezwa baadhi ya wadau wakiwemo viongozi wastaafu na watalaamu wa sheria, lakini kwa maoni yake hadhani kama zitasaidia Taifa kutoka katika sintofahamu hiyo, kwa madai kuwa Bunge limesharidhia mchakato huo.

“Haiwezekani hata kurekebisha vifungu kwa aina ya mkataba huo. Kuna wengine wanakwenda mahakamani, lakini kama mnavyojua mahakama zetu zinachukua muda mrefu kusikiliza kesi,” amesema Profesa Shivji.

Mjadala huo ambao uliandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), ndaki ya Sayansi ya Jamii, ulishirikisha wasomi na wadau mbalimbali ambapo walipa fursa ya kutoa maoni yao juu ya mada hiyo ambayo bado imeendelea kuwa gumzo.

Oktoba 25 mwaka 2022 Serikali ya Tanzania na Dubai ziliingia makubaliano katika ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari na uendeshaji wa miundombinu ya kimkakati ya bandari za bahari na maziwa makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maegesho ya utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.

Hatua hiyo imebua mjadala na kuwagawa baadhi ya wadau na vigogo wakiwemo viongozi wastaafu wa zamani. Wapo wanaounga mkono hatua ya Serikali huku wengine wakipinga mchakato huo wakidai hauna manufaa kwa Taifa, lakini kwa nyakati tofauti Serikali imekuwa ikisisitiza manufaa ya suala hilo.

Juni 25, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba alishauri kuangaliwa upya kwa vifungu vyenye mkanganyiko katika mkataba huo. Alisema ni kweli uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam haukuwa wa kuridhisha kwa muda mrefu, lakini makubaliano yaliyopo yana vipengele vinavyoleta wasiwasi.

Wakati Jaji Warioba akitoa ushauri huo jana Jumanne, kundi la mawakili wanne wa kujitegemea wakiongozwa na Alphonce Lusako walikwenda mahakamani kupinga mkataba huo.

Lakini leo Profesa Shivji amehoji,”hata ukiingia mahakamani utachallange nini? Utakuwa una challenge azimio la Bunge sio makubaliano yaliyoingiwa baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai,” amesema Profesa Shivji.

Mawazo ya Profesa Shivji hayana tofauti na mwanasheria mwingine Tundu Lissu ambaye hivi karibuni alisema haona haja kwenda mahakama kupinga mchakato huo, kulingana na mkataba wenyewe ulivyo.

Profesa Shivji amesema njia ya pekee ni Bunge kuketi upya na kusema kwamba baada ya maoni ya wananchi wameona na azimio walilolipitisha halikuwa sahihi, hivyo wanaazimia kulifuta, akisema jambo hilo linawezekana.

MWANANCHI
Mzee ashajichokea . He is irrelevant.
 
Back
Top Bottom