Husika na kichwa cha habari hapo juu...
habari za jioni mabibi na mabwana, natumai kuwa mu wazima wa afya kabisa!
kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naombeni kupewa knowledge hasa juu ya huyu kiumbe (sijui ni kiumbe ama ni roho? kiukweli sijui).
The so called jini mahaba, ni kiumbe wa aina gani? inakuwaje mpaka anamuingia binadamu na kuwa na mahusiano nae mpaka kuzaa nae na kujenga maisha?
kwanini jini mahaba akishamuingia mwanaume, basi mwanaume inakuwa ni vigumu sana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke yeyote yule ama kutelekeza familia kabisa?
Hawa viumbe wanapendelea kuishi mazingira ya aina gani? wanapenda nini kiujumla na hawapendi nini katika maisha yao?
wakuu, naombeni tuelezane kila kitu kuhusiana na majini mahaba, kiukweli kuna kitu cha msingi sana nataka kufahamu kutoka kwenu, nimepitia maandiko mengi mtandaoni, lakini nimeona si mbaya kama tukijadili na hapa!

Kwa mafundisho nlioyaskia mimi ni kua majini mahaba wana njia kadhaa za kumuingia binadam mojawapo ni ile kama watu tunaokutana nao njiani kwenye maisha ya kilasiku.wengine sio watu.wanakua wamevaa sura tuu za kibinadam atakuomba urafiki ukadhani unajipatia mchumba unagawa no zako kitendo cha wewe kukutana nae kimwili maramoja tuu haumwoni tenaa.anakua kama amefanya maagano na wewe/mmefunga ndoa.wewe ndo unakua mume wake/mke wake.na ndio maana kupata wako kihalali inakua vigumu kwasababu hataki kukushare.ukijitahdi sana kikawaida kua na mpenzi mpaka mnataka kuoana anaweza kukufanya umuone huyo mpenzi wako hafai ana kasoro kibao yani unajishangaa imekuaje nilimkubali mwanzo,unaamua kumuacha mwenyewee.ndo maana wengi wanaliaga wanaachwa for no reason kumbe wamevamia ndoa za kijini.au inaweza kua vise versa,kama ni mdada na uzuri wako woteee hauonekani kwa wakaka,like umepakwa mavi.hukubaliki.hata ufanyaje hauattract right suitors..kama hujui utakua unajililia mwenyewe unasononeka ila cha kufanya ni kupiga goti tuu na kuomba kibali kwa baba.(Mungu)tena kiuhakika sio kilelemama.lasivo utaiziskilizia ndoa bombani,utabaki kucheza kwaito na skeleuu wedding za wenzako,mafanikio hayatakuja maana spiritual husbands hawapendi ufanikiwe,natumai nimeeleweka.
"wakristo hatukupewa huduma ya kupunga majini(pepo) bali kuyatoa kila aina ya majini ! [luka 10:17-20; marko 16:17-20 ].
memgine ni mauza uza ya hofu tu.
Utaingiliwaje na kitu hakina mwili?
Mkuu Excel,
Sisi binadamu tuna sehemu kuu mbili, mwili na roho!. (physical body na spiritual body). Mwili ni hili umbo lililojengwa kwa udongo, na roho ni nafsi, uhai, iliyopuliziwa na Mungu. Mwili ulioumbwa kwa udongo, umetiwa uhai na nafsi, roho hivyo kuwa viumbe hai. Siku roho ikitoka (kufa) nafsi inaacha mwili na kuondoka zake, mwili ambao ni udongo, ni mavumbi, unazikwa unarudi mavumbini, na roho, inakwenda kwenye ulimwengu wa roho.
Dunia au ulimwengu nao unazo sehemu kuu mbili, ulimwengu wa miili, physical world na ulimwengu wa roho, the spiritual world. Ulimwengu wa milli ndio hii dunia tunayoishi yenye vitu viavyoonekana, na ulimwengu wa roho ni vile visivyo onekana, roho, malaika, liroho, shetani, majini, mizimu, wanga, wachawi, majini, mapepo, mbinguni, peponi, motoni, jehanum, toharani, kwenye nguvu na mwanga na nguvu za giza etc!.
Wanaoishi kwenye ulimwengu wa mwili ndio sisi binadamu, wanaoishi kwenye ulimwengu wa roho ndio viumbe hao wengine niliowataja wakiwemo majini!.
Hao majini wako wa aina nyingi, wako majini ya bahati, wanaokuletea bahati, wako majini wa majanga wanaokuletea majanga, na wako majini mahaba wao shida yao ni mapenzi tuu, uwapende, wakupende!. Mambo yoyote yanayohusiana na majini, ni mambo ya "liroho", shetani, ni mambo ya kishetani!.
Jini mahaba ni shetani la mapenzi, likikupenda, litakupa kila kitu isipokuwa mwenza!, litakuwa linafanya mapenzi na wewe ya kijini jini, au ukiwa usingizini kama ndoto. Tatizo la jini mahaba, huwezi kuwa na mahusiano na mpenzi wa kawaida wa kibinaadamu na akitokea mtu akakupenda, yatamkuta ya kumkuta!.
Majini yananunuliwa hadi e-bay.
Kitu kimoja amacho siku zote akisemwi kwenye mahusiano kati ya binadamu na majini, ni kitu kinachoitwa "bondage!", unakuwa ni mtumwa wa hilo jini na chochote litakachohitaji kutoka kwako lazima lipate!, litaanza na kuzitaka roho za wapendwa wako, wazazi, mke, watoto na mwisho wa siku ni roho yako mwenyewe!.
Haya ni mambo ya kishetani na mwisho wake siku zote ni kule kwenye jehenum ya moto wa milele.
Mambo yoyote ya ulimwengu wa giza, ni mambo ya kujiepusha nayo.
Pasco