Yahusu: Majini mahaba...

Yahusu: Majini mahaba...

excel

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
22,434
Reaction score
17,862
Husika na kichwa cha habari hapo juu...

Habari za jioni mabibi na mabwana, natumai kuwa mu wazima wa afya kabisa!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naombeni kupewa knowledge hasa juu ya huyu kiumbe (sijui ni kiumbe ama ni roho? kiukweli sijui).

The so called jini mahaba, ni kiumbe wa aina gani? inakuwaje mpaka anamuingia binadamu na kuwa na mahusiano nae mpaka kuzaa nae na kujenga maisha?

kwanini jini mahaba akishamuingia mwanaume, basi mwanaume inakuwa ni vigumu sana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke yeyote yule ama kutelekeza familia kabisa?

Hawa viumbe wanapendelea kuishi mazingira ya aina gani? wanapenda nini kiujumla na hawapendi nini katika maisha yao?

wakuu, naombeni tuelezane kila kitu kuhusiana na majini mahaba, kiukweli kuna kitu cha msingi sana nataka kufahamu kutoka kwenu, nimepitia maandiko mengi mtandaoni, lakini nimeona si mbaya kama tukijadili na hapa!

562406_391824147537162_261686161_n.jpg



Huyu ni JINI MAHABA wa Kike anaitwa SUCCUBI huwajia wanaume na kufanya nao Mapenzi wakati usiku umelala.


578827_428643790521864_1903783179_n.jpg


Huyu ni JINI Subiani Jıni Dume huyo anaye wapenda wanawake,akikupenda huwa anakuja usingizini kwa sura kama hiyo hapo juu ndio amejitahidi hapo kujiweka Bonge la Handsome kwa ajili ya kuwafuata wanawake usiku usingizini.


Ukikubwa na Jini Mahaba ikiwa wewe ni Mwanamke basi utakumbwa na Jini Mahaba wa kiume la kam wewe ni Mwanamme utakumbwa na Jini Mahaba Mwanamke na akisha kukingia kutoka kwake ni kwa kazi ngumu sana mpak umpate mtu anayeweza

kumuondowa tena kwa gharama kubwa sana. Na ukiwa na Jini Mahaba anakutia mikosi ikiwa wewe ni Mwanamke basi hutoolewa au ukiwa ndani ya ndoa hutoweza kupata mtoto au kam unapata watoto watakuwa watoto wengine wanakufa bila ya

sababu muhimu, na ukiwa kwenye siku zako unatowa damu nyingi au siku zako zinakuwa zinabadilika bila ya mpango maalumu.au ukiwa kwenye tendo la ndoa unakuwa hujisikii raha kimapenzi basi ukiwa na hizo dalili ujijuwe kuwa wewe uan Jini Mahaba na

ukiwa nalo hilo Jini Mahaba hata kam ukienda Hospitali hawawezi kumuona kwenye vipimo vya Ma-Hospitali utakuwa unaumwa kila wakati maradhi ya kichwa au homa zisizo kwisha kila wakati utakuwa unaumwa asubuhi jioni uu mzima.au unaumwa kila jioni

asubuhi wewe ni mzima. Kwa Mwanamme akikubwa na Jini Mahaba atakuwa ni mtu asiyependa wanawake kila anapo lal usiku huyo Jini Mahaba humjia huyo Mwanamme atakuwa wakati wmwengine aana upungufu wa nguvu za kiume hasira zisizo kwisha

kila wakati anapo amkaanakuwa yupo mchovu bila ya sababu atakuwa mtu mwenye mikosi anafukuzwa kazi bila ya sababu atakuwa huyo mwanamme anapotezakila wakati pesa na kuchukiwa na marafiki zake hapendi kuw ana watu kwa pamoja hizo ni baadhi ya dalili ya mtu mwenye Jini wa mahaba kwa mwanamme. Kwa ufupi Sio kitu kizuri kuwa na Jini Mahaba kwa sababu anakutia wewe mikosi unakuwa huna pesa wala masiha yako yanaharibika.


Majini ni nini?

Majini ni viumbe ambao wameumbwa kwa Moto na walikuwa wakiishi duniani kabla ya binadamu miaka Milioni nyingi iliyopita.
Viumbe hawa wana tabia kubwa mbili;
Yaani ya kibinadamu kwa maana wanakuwa wanafanya mapenzi, wanazaa na wanakufa.
Tabia nyingine ni ya Kimalaika ambayo ni kwamba wana uwezo wa kujigeuza katika umbo lolote wanalotaka na vile vile wanaruka na kwenda wanakotaka au kupita wanakotaka bila kutumia chombo chochote.
Taifa la Majini limegawanyika katika makabila Milioni Sabini na mbili (72,000,000) na wana uwezo wa kujifunza lugha yeyote wanaoitaka.

Idadi ya Majini ni kila Binadamu mmoja kuna Majini 300 na wanaishi katika Majumba yetu, kwenye Miti, Majangwani, Kwenye Mapango na Sehemu zenye Misitu Mikubwa.


Majini wako katika aina Mbili (2); Maruhani na Mashetani.
Maruhani ni Majini wema ambao wanamtii Mwenyezi Mungu na wanawasaidia Binadamu katika mambo mengi.
Mashetani ni Majini Waovu ambao ni wakorofi na wanawaletea Watu madhara na Matatizo mara kwa mara.
Baba wa Majini anaitwa JANN ambaye kimaumbile yeye ana tofauti ndogo na wenzie kwamba yeye ameumbwa kwa ulimi wa Moto.
Pamoja na mambo mengi wanayoyafanya Majini na kujihusisha na binadamu, Majini vilevile wanafanya kazi za Malaika hasa zile za mambo ya kupeleka Habari na kuwalinda Binadamu, mambo ya doria za Angani. Kazi hizi siyo zao lakini kwa vile wanapenda kuiga mambo basi huiga hata kazi ambazo siyo zao.

Majini na Binadamu wana sifa zinazofanana kwani wote wana akili na wote watahesabiwa siku ya Kiama na watazawadiwa kwa mema yao na maovu yao, wote wanakula na kuzaa.

Kama ilivyo, kuna wataalamu wa Kijini wenye fani sawa na Wataalamu wa Kibinadamu wenye kufanya kazi zinazofanana.
Tofauti kubwa iliyopo kati ya Majini na Binadamu ni kwamba; Majini hawana maumbile maalum na wana uwezo wa kujibadilisha katika maumbile mbalimbali ingawa wengi wa Majini wapo katika maumbile ya paka, nyoka na ndege.
Binadamu wao wana umbile maalum ambalo halibadiliki.
Majini wana uwezo wa kuwaingia Binadamu wakati Binadamu hawana uwezo wa kuwaona Majini isipokuwa kwa ufundi maalum.

Namna Majini wanavyowaingia Binadamu iko katika njia tatu:-


  1. Njia ya kwanza (1): ni kama Remote Control; Hii inamfanya yule aliyedhibitiwa kuweza kuelewa au kuwa na fahamu zake lakini anakuwa hawezi yeye mwenyewe kuudhibiti mwili wake na anasema yale anayotaka yule Jini.
  2. Njia ya Pili (2); Jini humwingia Binadamu ndani ya utosi na kuingia katika Mfumo wa Damu. Hii inamfanya yule Binadamu kupoteza fahamu na anakuwa haelewi kabisa kinachoendlea na anafanya yote anayotaka yule Jini.
  3. Njia ya Tatu (3) ni ile ya Jini kukaa nyuma ya Binadamu. Njia hii humfanya yule Binadamu anakuwa hapotezi fahamu ila anakuwa hawezi kufanya lolote na mwili wake.
{mospagebreak}

Majini vilevile wana uwezo wa Kusafiri kwa kasi ya upepo bila kutumia chombo chochote; Binadamu hana uwezo huo isipokuwa kwa msaada wa Majini.

Hiyo ni kusema kwamba mambo yote yanayofanywa na Wachawi na Wanga hayawezekani isipokuwa kwa msaada wa Kijini.
Jambo la muhimu ni kwamba pamoja na uwezo mkubwa walionao Majini, Wanadamu wana uwezo wa Kumtawala na Kumdhibiti Jini na vivyo hivyo Majini nao wanaweza kumtawala na kumdhibiti Binadamu wote kwa kutumia utaalamu maalum.
Wako Majini wa kila Dini na kila Kabila, na kuna watu wanaofuga Majini kwa kujikinga, na kwa kuboresha kazi zao au kujipatia utajiri. Pia kuna watu wanaofunga ndoa na Majini kwa kutumia utaalamu au kwa hiari za Majini hao.
Wabaya wa Majini ni Mashetani ambao wengi hawana Dini na ndio wanaoharibu mimba za Wazazi na kufanya mapenzi na watu usingizini bila hiari zao.
Kuepuka usichafuliwe kimapenzi, kabla ya kulala piga Bismillahi kwa Muislamu au taja jina la Yesu mara tatu kwa Mkristo.

MAUMBILE YAO YAKOJE?


  • Majini wana maumbile makuu manne (4);
  • Wanakuwa katika maumbile ya Nyoka.
  • Wanakuwa katika maumbile ya Nge.
  • Wanakuwa katika maumbile ya Mbwa.
  • Wanakuwa katika maumbile ya Paka (Mweusi).
  • Kuna Majini wengine hawana maumbile yeyote na hawa shughuli yao ni kuruka hewani kuzunguka huku na kule na husafiri mbali kwa mara moja yaani kufumba na kufumbua.

SURA ZA MAJINI NA MASHETANI:

Majini sura zao ni za kutisha na mfano wake ni kama Matunda ya Mti wa Zaqum ambao unatoa matunda yenye sura mbaya na yanayofanana na mawe.
Majini wanakuwa na mkutano kila siku nyakati za kuchomoza na kuzama Jua na nyakati hizo ndizo ambazo wanafanya maasi yao.
Fitna na Maasi yao mengi wanafanyia upande wa Mashariki.
Majini vilevile wanaweza kujigeuza kama mbwa mweusi au paka mweusi kwa sababu Majini wanapenda Rangi Nyeusi kwa sababu ya kiza.

WANAKULA NINI?

Majini wao wanakula mifupa na mavi ya farasi. Hivyo ni vyaluka vyao vikuu pamoja na kwamba wengine wanakula Moshi (Ubani) na wengine wanapenda kunywa damu.
Wanapokula au kunywa, wao hutumia mkono wa kushoto na Majini wazuri ndio ambao wanakula mifupa mizuri na kuwaachia mifupa mibaya na uchafu Majini wabaya au Mashetani.

JE MAJINI WANAZAA?

Majini wanaoa na kuongezeka kama tulivyo Binadamu na huzaana kwa wingi sana.
Katika wao kuna wale wanaokula na kuoana na kuna wale ambao hawafanyi hayo.
Binadamu Mwanamume ana uwezo wa kumuoa Jini Mwanamke na Jini wa Kiume ana uwezo wa kumuoa Binadamu Mwanamke pamoja na kwamba ndoa inayotambulika na Mwenyezi Mungu ni ya kiumbe kwa kiumbe yaani Binadamu kwa Binadamu na Jini kwa Jini.
Haya ni baadhi ya maelezo kuhusu Majini, zidi kutembelea tovuti hii mara kwa mara kwani hii ni mwanzo tu na tutazidi kuwaletea habari za ndani kuhusu majini na tabia zao, jinsi ya kujikinga nao au kushirikiana nao.

Uktaka Tiba ya kuyaondowa Majini Mwilini Mwako unaweza kuniandikia Baruwa ya Pepep Email yangu hii fewgoodman@hotmail.com au pia waweza kunitembelea blog yangu bonyeza hapa.
JITIBU MAGONJWA MBALIMBALI KWA KUNYWA MAJI YA UVUGUVUGU

UKIWA NA DALILI ZIFUATAZO BASI WEWE UNA MASHEYTWANI WA KIJINI.



Leon sijaulizwa swali ila naomba nitoe faida kwa wanaofatilia mada zangu hata kila mtu ajielewe.
Watu wengi sana wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo ambayo wao wanashindwa kujua ufumbuzi wake, leo mimi nitataja dalili hapa ili mwenye dalili hizo ajijue kuwa anasumbuliwa na Masheytwani ya kijini.

HATUA YA KWANZA KABLA YA KUHISI UNA MAJINI HAKIKISHA UMEENDA HOSPITAL NA UMEFANYA TAKRIBAN VIPIMO VYOTE ALIVYOSEMA DAKTARI LAKINI BADO HUJAPATA UFUMBUZI WA TATIZO LAKO BASI UJUE HUENDA UNASUMBULIWA NA MAJINI

DALILI YA (1) Kuumwa kichwa upande mmoja, masikio, meno, mgongo,kiuno na kifua kubana.....

2) Kuumwa tumbo chini ya kitovu kwa akina mama, na kwa kina baba( JAMAA KUKOSA NGUVU) wakati unamuhitaji mkeo..........Nikisema Jamaa nafikiri nimeelewekwa kwa watu wazima sio vizuri kutaja kuna watoto huku.

3)Moyo kwenda mbio na kushtuka bila sababu kisha mwili husisimka.

4)Kupatwa na kizunguzungu pamoja na wenge( wenge yani unakuwa wakati fulani hujielewi elewi ama vituko fulani kuna saa unaweza kutafuta kitu sana ukawa hukioni lakini gafla wakiona mezani na wakati ulishatafuta)

5)Kuumwa na tumbo sana kwa kina mama wakati wa hedhi na kutoa damu nyingi sana ama damu chache
, na wakati mwingine hedhi huja mfululizo hata mwezi mzima...........hii pia huenda ikawa ni ISTIHADHA.......na pia huenda ikawa ni dalili za masheytwnai wa kjini............hakikisha unachunguza vizuri.

6)Wakina mama kupata maumivu saa ya (tendo la ndoa)
na pia hukosa hata hamu ya tendo hilo la ndoa Sex......na kwa upande wa wanaume.....unaweza kutaka kufanya tendo la ndoa Sex mkeo ukatafuta njia hadi ukachoka

7)Kutembea tembea vitu mwilini kama vichomi fulani.

8)Kutingishika bila sababu na kutetemeka bila sababu na wakati mwingine kulia bila sababu.

9) Hasira za gafla na mara kwa mara hasa kwa wanawake............Usipoangalia vizuri unaweza kumpa talaka mwenzio kwani huwa wanakuwa wakali sana na macho yao ukiwaangalia huonyesha msimamo wa hali ya juu.

10)Kuhisi uzito wa mwili umeongezeka....kuna wakati ukikaa pia unajihisi hauko peke yako.unahisi kama kuna mtu lakini humuoni na wakati fulani unaweza kuona kama kitu fulani kimepita gafla

11) Chuki ndani ya ndoa na kutamani kuachwa ama kumuacha.

12) Kufunga hedhi bila ujauzito, kuota unazaa, au kunyonyesha au kubeba mtoto, na wakati mwingine ukiwa mja mzito kisha ukaota tu umekabidhiwa mtoto basi mimba huanza kuvuja na kuharibika.......Pia kuharibika kwa mimba baada ya kuota unananihii na mtu anaetisha ama kijana mzuri sana wa sura..pia kuharibka mimba bila sababu ya msingi

13.) Kuvurugikiwa na mipango ya kuoa, na kwa wanawake kila anaekuposa basi mambo huenda vizuri kisha yanaishia hewani.......PIA kujihisi unaingiliwa siyo ndotoni

14)Kuhisi unasimamiwa na mtu mbele yako, nyuma yako, pembeni na hata ulalapo na kua na hofu kubwa sana juu ya hilo.wakati mwingine ukaogopa hata kukaa peke yako

15) Kupatwa na usingizi wakati unasoma Qur an au unasoma Biblia, ama kuisikiliza, lakini ukisikilza music usingizi hauji au ukisoma story za shigonga husikii usingizi lakini ukishika tu quran au biblia basi unapata usingizi hadi unakoroma.

16) Mwanamke kupenda kujipamba sana awape nje ya nyumba yake na hajipambi mbele ya mume wake, pia kupenda sana starehe kujiona mzuri na wathamani sana.

17) Kuota unafanya ibada zisizo mwelekeo, kuota uko mbinguni ama mwezi unakusujudia, kuota umezingirwa na maadui, mijuzi, nyoka,kifo,jeneza,kuota unakimbizwa na panya au mtu alieficha sura yake.

18) Kugombana na kuwachukia watu wa dini nk Wachungaji, Masheik ama wakina mama walioshika dini sana, kukimbia kusomewa Qur ani au Biblia ama kusikia adhana unakuwa mkali sana.

19.Kulia, kucheka sana na kupiga kelele usingizini

20.Kuota kufanya ama kufanywa tendo la ndoa kawaida ama kinyume na maumbile kwa mwanamke ama mwanaume, kisha ukiamka unajihisi kweli umefanyiwa au usijihi, pia huenda ukamuota anaekufanyia ni mtu unaemjua, aidha kazini, shuleni, jirani au rafiki, wakati mwingine hata mzazi wako au mtu aliekufa.

Ukiota sana ama kuwa na dilili hizi tafadhali wahi haraka kwa Sheikh au Mchungaji akuombee ukiwa na shida mbali mbali au maswali yanayokukiza wasiliana na mimi kwa njia ya Email nitumie baruwa ya pepe Email Address yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com au waweza pia kunitembelea Blog yangu bonyez hapa.
VYAKULA BORA NAFAIDA ZAKE MWILINI

ENDELEA HAPA KUONA MAJINA YA MAJINI NA KAZI ZAKE
 
Na mimi nipate darasa hapa waje wataalamu watiririke
 
Haya mambo yanahitaji mtaalam wa mambo ya jadi mkuu...subiri waje.

mkuu nawangoja aisee..

kuna hili suala la kuingiliwa usiku na hawa viumbe, hapo ndipo naachwa hoi kabisa!

sielewi...
 
Ngoja waje!
Tatizo wapo wanaojua ila hawako wazi,
R. I. P Sheikh Yahya!!!!
 
mkuu nawangoja aisee..

kuna hili suala la kuingiliwa usiku na hawa viumbe, hapo ndipo naachwa hoi kabisa!

sielewi...

Mm hayo mambo huwa naogopa sana...yani mm npigwe miti?!...mungu aepushie mbali.
 
hupenda kuuliza maswali kama haya uliyouliza...kwi kwi kwi!

Nachungulia majiubu kwa kona mkuu.

Are u ok?
 
Mkuu Excel hili swala umelileta muda muafaka kabisa.

Haya mambo yapo kabisa sio stori za kusimuliawa, ilisha mtokea mtu wangu wa karibu.

Mwanzoni nilikuwa najua ni hadithi tu lakini nilkuja kubadili mtazamo wangu baada ya kumtokea mtu ambae tunajuana vizuri sana!

Kuna siri kubwa sana nyuma ya haya mambo umenipa hamasa ya kutaka kujua zaidi kuhusu hili swala

Naanza utafiti rasmi kuanzia leo, tena naanzia hapa hapa baada ya hapo namalizia huku mtaani kwangu.

Nina imani nitapata majibu ya uhakika juu ya majini mahaba!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Excel hili swala umelileta muda muafaka kabisa.

Haya mambo yapo kabisa sio stori za kusimuliawa, ilisha mtokea mtu wangu wa karibu.

Mwanzoni nilikuwa najua ni hadithi tu lakini nilkuja kubadili mtazamo wangu baada ya kumtokea mtu ambae tunajuana vizuri sana!

Kuna siri kubwa sana nyuma ya haya mambo umenipa hamasa ya kutaka kujua zaidi kuhusu hili swala

Naanza utafiti rasmi kuanzia leo, tena naanzia hapa hapa baada ya hapo namalizia huku mtaani kwangu.

Nina imani nitapata majibu ya uhakika juu ya majini mahaba!
mkuu nimehamasika sana kufahamu kuhusiana na hawa viumbe,

si unajua tena tumeingia maeneo ya PWANI huku ambako ndiko karibu makao ya hawa wadudu?

nina kesi nzito sana na roho yangu, nina imani itajibiwa na wana JF, nimejikuta nakiogopa kitanda...
 
hupenda kuuliza maswali kama haya uliyouliza...kwi kwi kwi!

Nachungulia majiubu kwa kona mkuu.

Are u ok?

nani huyo mkuu hupenda kuuliza?

niko ok ndugu, siku nyingi sana hatujaonana hewani.

nangoja wajuzi wanidadavulie kuhusu hawa viumbe.
 
ukweli nami nasikia sana haya naamini hapa tutaelimika....
 
Mm hayo mambo huwa naogopa sana...yani mm npigwe miti?!...mungu aepushie mbali.

Hahahaaa!! kwani we ndio unaamua mkuu? si kiumbe chenyewe kinakuja na kufungua zipu halafu kinaingiza na kutoa as many times as it wants? we kuja kustuka tu unakuta ushalowa vibaya sana!
 
Inawezekana hata humu MMU wapo

majini mahaba ama?

ile kesi ya kasnde aliisolv vipi? unajua wengi walichukulia kiutani, ila kwel haya mambo yapo kabisa!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom