Yahusu: Majini mahaba...

Yahusu: Majini mahaba...

Ignorance at its best

Kwa mwendo huu watz hatutoendelea
 
Ignorance at its best

Kwa mwendo huu watz hatutoendelea

Kama huna experience na kitu unapiga kimya.Sio lazima uponde kila kitu.Haya mambo yapo.Kwa wale yanayowasumbua elimu inawasaidia kutoka matatizoni
 
Mkuu Mzizi Mkavu, umesema Majini yalikuwepi miaka miaka mingi kabla ya binadamu kuumbwa, sasa nafahamu kuna Majini mpaka ya Kimaasai (sio mizimu ) je? walianza kuzaliwa Majini ya Kimaasai kabla ya binadamu?
Inaonyesha wewe hujasoma jinsi nilivyo andika hapo juu? ninakujibu Tena Taifa la Majini limegawanyika katika makabila Milioni Sabini na mbili (72,000,000) na wana uwezo wa kujifunza lugha yeyote wanaoitaka kidonto
 
Mkuu Excel,
Sisi binadamu tuna sehemu kuu mbili, mwili na roho!. (physical body na spiritual body). Mwili ni hili umbo lililojengwa kwa udongo, na roho ni nafsi, uhai, iliyopuliziwa na Mungu. Mwili ulioumbwa kwa udongo, umetiwa uhai na nafsi, roho hivyo kuwa viumbe hai. Siku roho ikitoka (kufa) nafsi inaacha mwili na kuondoka zake, mwili ambao ni udongo, ni mavumbi, unazikwa unarudi mavumbini, na roho, inakwenda kwenye ulimwengu wa roho.

Dunia au ulimwengu nao unazo sehemu kuu mbili, ulimwengu wa miili, physical world na ulimwengu wa roho, the spiritual world. Ulimwengu wa milli ndio hii dunia tunayoishi yenye vitu viavyoonekana, na ulimwengu wa roho ni vile visivyo onekana, roho, malaika, liroho, shetani, majini, mizimu, wanga, wachawi, majini, mapepo, mbinguni, peponi, motoni, jehanum, toharani, kwenye nguvu na mwanga na nguvu za giza etc!.

Wanaoishi kwenye ulimwengu wa mwili ndio sisi binadamu, wanaoishi kwenye ulimwengu wa roho ndio viumbe hao wengine niliowataja wakiwemo majini!.

Hao majini wako wa aina nyingi, wako majini ya bahati, wanaokuletea bahati, wako majini wa majanga wanaokuletea majanga, na wako majini mahaba wao shida yao ni mapenzi tuu, uwapende, wakupende!. Mambo yoyote yanayohusiana na majini, ni mambo ya "liroho", shetani, ni mambo ya kishetani!.

Jini mahaba ni shetani la mapenzi, likikupenda, litakupa kila kitu isipokuwa mwenza!, litakuwa linafanya mapenzi na wewe ya kijini jini, au ukiwa usingizini kama ndoto. Tatizo la jini mahaba, huwezi kuwa na mahusiano na mpenzi wa kawaida wa kibinaadamu na akitokea mtu akakupenda, yatamkuta ya kumkuta!.

Majini yananunuliwa hadi e-bay.

Kitu kimoja amacho siku zote akisemwi kwenye mahusiano kati ya binadamu na majini, ni kitu kinachoitwa "bondage!", unakuwa ni mtumwa wa hilo jini na chochote litakachohitaji kutoka kwako lazima lipate!, litaanza na kuzitaka roho za wapendwa wako, wazazi, mke, watoto na mwisho wa siku ni roho yako mwenyewe!.

Haya ni mambo ya kishetani na mwisho wake siku zote ni kule kwenye jehenum ya moto wa milele.

Mambo yoyote ya ulimwengu wa giza, ni mambo ya kujiepusha nayo.

Pasco

Nashukuru sana Mkuu kwani hata mimi nimejifunza vitu vingi kwa post hii.
 
Tatizo imani yangu ngumu sana.

Huwezi amini siamini katika hii kitu
 
Naomba sana wataalamu waje jamani mtaalam sogea huku kuna kaz
 
Ulikutana naye ana kwa ana na nani? jini mahaba? Akiwa katika umbile gani? la paka au?

Nilikua na rafiki yangu, tunatembea then rafiki yangu akaniambia tumepishana na mwanamke ananiangalia kama ananijua but mimi sikumwona then ikabidi nigeuke ndipo nikakuta kasimama muda, tukawa tunaangaliana bila mtu kuongea kwa muda.
 
Ukweli ni kwamba watu wengi wana matatizo haya na mpaka mtu kuamini anakua keshavurugwa kila kitu.
 
Majini au jini, ndiye huyo pepo au malaika waliofukuzwa mbinguni na kungoja kutupwa motoni pamoja na Ibilisi
[MT 25:41].
 
nijibu swali langu la msingi, ulijuaje yeye ni jini?

Story ni ndefu kifupi kaniachanisha na mke wangu wa kwanza, then majuzi akapanda kwa mke wangu wa sasa wakati mke wangu hana hizo mambo, then akaanza kuongea vile alivyosababisha kuniachabisha na mke wangu wa kwanza na kwamba hata mke wangu wa sasa kamwingilia kwenye mahusiano yake hivyo lazima tuachane na kwamba hakuna ntachofanya kikafanikiwa, baada ya miaka 6 nikaamini kuwa ni kweli jini ananisumbua. Achilia mbali matukio mengi ambayo nlikua baptizing.
 
ina maana wote wanaoachana na wake zao wana majini?

na una hakika gani kilichompanda mkeo ni jini?

Story ni ndefu kifupi kaniachanisha na mke wangu wa kwanza, then majuzi akapanda kwa mke wangu wa sasa wakati mke wangu hana hizo mambo, then akaanza kuongea vile alivyosababisha kuniachabisha na mke wangu wa kwanza na kwamba hata mke wangu wa sasa kamwingilia kwenye mahusiano yake hivyo lazima tuachane na kwamba hakuna ntachofanya kikafanikiwa, baada ya miaka 6 nikaamini kuwa ni kweli jini ananisumbua. Achilia mbali matukio mengi ambayo nlikua baptizing.
 
alikuwaje? Naulijuaje umekutana na jini?

Baada ya kama week kupita toka nlipokutana naye nikajikuta kila ikifika Ijumaa naenda msikitini nasubiri Waislam watoke msikitini then naanza kuwauliza kuhusu Majini, mwanzoni nlikua sijui kwa nini, na sikujua msukumo huo naupata wapi wakati mimi ni Mkristu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom