Yahusu kuchanjiwa muku

Yahusu kuchanjiwa muku

9363e1edc473b7a33c68947b49b28467.jpg
Hili neno laweza kuwa na tafsiri nyingine kwa wengine lakini kwa watu wa Tanga lina maana yake muhimu ya ugumu ujasiri na roho ngumu
Hili nililishuhudia huko Lushoto kwa watu kadhaa waliochanjiwa muku ni wagumu kuugua kuumia na kiboko ya yote kufa aliyechanjiwa muku ni mtu mwenye roho ngumu hasa akikamatwa kwa mfano kwenye tukio la ujambazi au wizi na wananchi wenye hasira kali wanaweza kumpiga mpaka wakadhani wameua lakini siku inayofuta akakutwa bado anapumua.

Muku ni mzuri Unapokuwa hai lakini ni kitu kibaya kabisa unapokaribia kuachana na dunia hii kwa maana ya kifo...watu waliochanjiwa muku hufa kwa mateso makubwa sana kutokana na madawa aliyokunywa na kufanyiwa...akifanikiwa kufa mapema basi si chini ya siku tatu na hata akipata ajali mbaya kabisa au hata kuchomwa moto au kukatwa shingo mwili wake huchukua muda mrefu mno kupo.

Ninafahamu wengi wanapenda ujasiri na kuwa na kinga ya muku lakini kumbuka mateso siku roho yako ikitaka kuachana na mwili wako
Ukiweza kafanye lakini madhara yake ndio hayo
Kuna wengine hadi aage dunia wanaweza enda hata wiki 2 wanakoromaga tu na nishashuhudia mmoja hata madawa hakua anayajua ila ilimchukua wiki 1 kuaga dunia ilhali dalili zote anazo.
tujitahidi saana matendo yetu maana yataendana nasi hadi mwisho ili tuwe na mwisho mzuri.
 
Lakini pia hii ya kuugua mpaka kuoza lakini mtu hafi inatokana na maagano nadhiri na viapo hasa na nguvu za giza...huyo mtu hafi mpaka atengue hayo mambo
Wazee wetu wa zamani waliyapenda saana maagano, kuna bibi mmoja alinisimulia yy alimeza hirizi ya mandondo, anakwambia jinsi ya kuimeza hadi kwenye jeneza unawekwa...nilikuaga namsikiliza namuona anatunga tu huyu hizi hadithi za afu lela ulela! Alas, kumbe haya mambo yapo. Aliteseeeka saanaa zamu yake ilipofika.
I wish hii Muku ingekua haufi milele
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom