Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,865
- 730,439
Hili nililishuhudia huko Lushoto kwa watu kadhaa waliochanjiwa muku ni wagumu kuugua kuumia na kiboko ya yote kufa aliyechanjiwa muku ni mtu mwenye roho ngumu hasa akikamatwa kwa mfano kwenye tukio la ujambazi au wizi na wananchi wenye hasira kali wanaweza kumpiga mpaka wakadhani wameua lakini siku inayofuta akakutwa bado anapumua.
Muku ni mzuri Unapokuwa hai lakini ni kitu kibaya kabisa unapokaribia kuachana na dunia hii kwa maana ya kifo...watu waliochanjiwa muku hufa kwa mateso makubwa sana kutokana na madawa aliyokunywa na kufanyiwa...akifanikiwa kufa mapema basi si chini ya siku tatu na hata akipata ajali mbaya kabisa au hata kuchomwa moto au kukatwa shingo mwili wake huchukua muda mrefu mno kupo.
Ninafahamu wengi wanapenda ujasiri na kuwa na kinga ya muku lakini kumbuka mateso siku roho yako ikitaka kuachana na mwili wako
Ukiweza kafanye lakini madhara yake ndio hayo