mchawi wa kusini
JF-Expert Member
- Apr 18, 2018
- 830
- 897
HABARI YA PASAKA JF,Je Ulishawahi Kujiuliza Unaenda Wapi Ukisha kufa? Fuatana na Mimi Asubuhi Upate Elimu.
MTU AKIFA ANAENDA WAPI?
Mwili hushushwa ardhini baada ya pumzi kurudi kwa muumba,yaani baada ya nafsi kufa!
Kifo kinauma sana,na ukizingatia wengi hatujui nini kinafuatia baada ya kifo.Hatujui kama wapendwa wetu wanaunguzwa kwenye moto,wamepumzika paradisoni au wanahangaika peponi.Haya maswali yanasumbua watu wengi,mtu akifa nini kinafanyika?Lakini kwa bahati nzuri majibu tunayo....ebu tujifunze.
Tunakwenda wapi tukifa? Mbinguni? Jehanum? Toharani? (Toharani ni mahali ambapo baadhi ya watu hudai marehemu hupitia kupata mateso ili aruhusiwe kuingia ahera) au Ahera? Ndugu zetu waliokufa wako wapi? Je, tunaweza kuwaona?Hata Biblia linauliza hili swali, “Mtu akifa, je! atakuwa hai tena?” (Ayubu 14:14).
Lakini pia Biblia linatupa jibu thabiti ambalo halina utata. Majibu yake yanaeleweka, yanaridhisha, na zaidi ya yote, yanafariji.
MTU ANAPOKUFA, HUWA KUNATOKEA NINI?
“Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.” Mhubiri 12:7.Tukumbuke kitu kimoja hapa, neno "roho" iliyotumika hapa haina tofauti na "pumzi".Mara nyingi sana imetumika neno hilo roho kwenye Biblia kama tafasiri ya neno "spirit" pamoja na neno "breath".Yaani neno breath limetumika mara chache....
Mwili huyarudia mavumbi na pumzi/roho humrudia Mungu aliyeitoa. Pumzi ya mtu aliyekufa, awe mwenye haki au mwovu – humrudia Mungu wakati wa kufa,kwakuwa ni yeye aliitoa na sasa anakuwa ameitwaa.
ROHO AU PUMZI INAYOMRUDIA MUNGU NI KITU GANI?
Biblia inasema “Mwili pasipo roho(pumzi) umekufa.” Yakobo 2:26. “Roho(pumzi) ya Mungu i katika pua yangu.” Ayubu 27:3.
Roho inayomrudia Mungu wakati wa kufa ni ile pumzi ya uhai. Hakuna mahali katika Biblia ambapo tunaambiwa kuwa roho(pumzi) inakuwa na uhai, hekima au hisia baada ya mtu kufa. Ni “pumzi ya uhai”, na si ya kifo.Yaani kukosa pumzi matokeo yake ni KIFO!
NAFSI NI NINI?
“BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” Mwanzo 2:7. Nafsi ni muunganiko wa vitu viwili: Mwili(nyama, mifupa, damu, mishipa n.k) na pumzi(roho). Nafsi haiwezi kuwepo bila mwili na pumzi kuunganishwa. Neno la Mungu linafundisha kuwa sisi ni nafsi.
NAFSI HUFA?
Ndiyo,nafsi hufa.
Biblia inathibitisha hili kwenye Warumi 7:24," Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?" na kwenye Waebrania 9:16, "Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya."Pia Ezekiel 18:20,"Roho(spirit) itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa.”
Kulingana na Neno la Mungu, nafsi inaweza kufa! Sisi ni nafsi na nafsi zinaweza kufa. Mwanadamu hufa. Mungu pekee hapatikani na mauti (1 Tim. 6:15,16). Dhana ya nafsi isiyokufa inapingana na Biblia inayofundisha kuwa nafsi hazina budi kufa.
MTU ALIYEKUFA ANAWEZA KUJUA AU KUELEWA KITU?
Hapana! “Walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote linalofanyika chini ya jua.” “Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu (kaburini) uendako wewe.” Mhubiri 9:5,6,10. “Sio wafu wamsifuo Bwana.” Zab. 115:17.
Mungu anasema wafu hawajui kitu chochote.
WAFU WANAWEZA KUWASILIANA NA WALIO HAI?
Hapana! "Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, wala kuamshwa usingizini.” “Wanawe hufikiria heshima, wala yeye hajui; kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao.” Ayubu 14:12,21. “Wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua.” Mhubiri 9:6.
Wafu hawawezi kuwasiliana na walio hai. Wamekufa. Mawazo yao yamepotea (Zab. 146:4).
SASA KWANINI SISI TUNAPATA NDOTO KUTOKA KWA WAFU KAMA HAWAELEWI KITU CHOCHOTE?
Natoa mfano hai kwenye Biblia,kwa sababu Biblia haifichi mambo. Mfalme Sauli na majeshi yake walikuwa vitani kaskazini mwa Israeli. Walikabili jeshi lenye kuogopesha la Wafilisti. Sauli alipoona majeshi ya Wafilisti, “akaogopa, na moyo wake ukaanza kutetemeka sana.” Wakati huo, Sauli alikuwa tyari ameacha ibada ya kweli. Kwa sababu hiyo, Yehova hakumjibu sala zake. Sauli angefanya nini ili apate msaada? Samweli, nabii wa Mungu naye alikuwa ameshafariki(1 Samweli 28:3, 5, 6).
Sauli aliamua kumtafuta mwongozo kutoka kwa mwanamke mmoja aliyekuwa na uwezo wa kuwasiliana na pepo huko En-dori. Alimsihi mwanamke huyo “nipandishie Samweli” kutoka kwa wafu. Mwanamke huyo alipandisha mzuka(mapepo) na kuweza kumuona “Samweli”. Na huyo Samweli aliyetokea aliongea na Sauli na kumwambia kuwa Wafilisti wangeshinda vita na kwamba Sauli na wanawe wangekufa vitani. (1 Samweli 28:7-19) Je, huyo alikuwa Samweli aliyeonekana alikuwa wa kweli aliyerudi kutoka wafu?Jibu ni hapana,lakini majibu ya huyo mama yalikuwa ya ukweli mtupu! Hii inawezekanaje?
Fikiria jambo hili kwa makini zaidi. Biblia inasema kwamba mtu anapokufa ‘anarudi kwenye udongo wake’ na kwamba “mawazo yake hupotea.” (Zaburi 146:4).Biblia haijichanganyi hata siku moja. Sauli na Samweli wote walijua kwamba Mungu anachukizwa sana na mawasiliana kati ya binadamu na mapepo(Mambo ya Walawi 19:31).
Kilichotokea,na kinachotokea mara kwa mara hata mpaka leo hio ni mawasiliano kupitia kwa malaika waasi,ambao ni viumbe vya kiroho(spirits),na ambao waliasi mamlaka ya Mungu mapema katika historia ya wanadamu(Mwanzo 6:1-4; Yuda 6). Mashetani hawa wanaweza kututazama na kuona binadamu hai.Wanajua mawazo yetu,uwezo wetu na madhaifu yetu.Pia wanajua ndugu zetu walikwisha kufa tangia walipokuwa hai,wanajua mahusiano kati ya hao marehemu na watu waliopo duniani. Kwa hiyo wanajua jinsi mtu alivyokuwa anazungumza, alivyotenda, na sura yake alipokuwa hai. Wanataka kuendeleza dhana kwamba Biblia na Mungu ni uwongo(dhana ambalo shetani alilianzisha tangia shamba la Edeni). Biblia inatuonya tusiwe na mawasiliano yoyote na roho kama hao! (Kumbukumbu la Torati 18:10-12) Mashetani hao bado wanatenda kazi leo na wataendelea mpaka muda wao utakapoisha.
Sasa tunaweza kuelewa ni kwa nini wengi wanasema kwamba “wamewaona” wapendwa wao waliokufa au “kusikia” sauti yao. Ingawa wafu hao wanapotokea kama mizuka wanaweza kuonekana kuwa na nia nzuri, kumbuka kwamba roho waovu wameazimia kuwadanganya watu (Waefeso 6:12),hata kwa habari njema.
Kila binadamu anapokuwa hai hapa duniani,ni kiumbe cha kiroho ndani ya mwili wa nyama.Ni pumzi ndani ya mwili.Ndiyo maana anaweza kuwasiliana aidha na Mungu au shetani kiroho na siyo kimwili.Binadamu yuko huru kufanya mawasiliano kupitia roho mtakatifu wa Mungu au roho mtakavitu na chafu wa shetani.Mungu ni roho,na anataka tumuabudu kwa ROHO na KWELI (Yohana 4:24)"Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."
Hii inamaanisha kuna kuabudu kwa ROHO na WONGO pia,right?Ni wewe uchague uko pande ipi....Mungu halazimishi ila matokeo ya chaguo lako hayaepukiki.
Kumbuka kwamba siyo ndoto zote ni mbaya au dhambi,kuna ndoto zinazotoka kwa Mungu kwajili ya watu wa Mungu.Alafu kuna ndoto zingine zinazotokea kwa ibilisi kwajili ya watu wake.Kuna mifano mingi mno ndani ya Biblia.
Ukisoma Matendo ya Mitume 2:17 inathibitisha kwamba hata siku za mwisho watu wataota ndoto kutoka kwa Mungu,inasema hivi,"Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto."
#MunguNiRoho