Mzee Mwanakijiji,
Sawa tumekusikia, na hakika najua upo hapo Marekani miaka mingi sana. Ebu tueleze wewe sera za Domokratic ktk Usalama wa Taifa tofauti na sera za Republican ambazo wananchi walizikubali.
Au tupe sera za vyama vya UK au nchi yeyote kwa tofauti ya vyama utanisaidia sana kuona vitu ambavyo sikuwahi kuvifikiria kwamba wananchi walitakiwa kuvifahamu kabla hawajaunga mkono utawla unaofuata..
Nijuavyo mimi Usalama wa Taifa ni dira ya kitaifa haihusiani kabisa na siasa za chama..
Watanzania wote na tofauti zetu za kiitikadi inapofikia swala la Usalama wa Taifa tunazitua tofauti zetu na kuchukua msimamo mmoja usiokuwa na itikadi.
Propaganda zingine hazina tija.
MKJJ hujatuambia wakati unadandia treni hewa ya CCJ ulikuwa unadandia ili ikufikishe wapi, ina maana wakati huo hukuwa na busara hata kidogo ya kujiuliza maswali unayotuuliza leo.
MKJJ sitaki kukulinganisha na Mrema kuanza kunadadisi manifesto za vyama vingine kama huna interest na vyama hivyo kwa namna moja ama nyingine.
Kwa nini leo uanze kuuliza Long-term plans za vyama vingine wakati chenu kilishindwa kuwa hata na Short-term plan ya mwezi mmoja kukiwezesha kisajiliwe, kwanini hukuwapa CCJ ushauri huu kama ni mzuri unakuja kumpa jirani yako, amaizing me.
Inawezekana kabisa kutosajiliwa kwa CCJ kulichangiwa na mawazo yako naweza kuyaita potofu ya kuanza kupanga mipango ya siku 100 za mwanzo madarakani kabla ya kupanga mtaingiaje madarakani.
Mzee Mwanakijiji,
Unajua inakuwa taabu sana kwangu kuweza kufikiria unachofikiria wewe au hata hilo swali lako linalenga kitu gani haswa ikiwa unajibu kihuni na mkato.. najaribu sana kukusoma lakini sikupati kabisa..
Mkuu Mwanakijiji,
Hivi tukiweka maslahi ya taifa mbele,cha muhimu ni sera zinazosema "tutafanya A,B,C...X,Y,Z" au commitments za dhati kuona matatizo ya nchi yetu yanapungua kama si kumalizika?
Kwa mana kama suala ni sera,mbona za CCM zimekuwa nzuri tangu tupate uhuru?Kwa mtizamo wangu wa mtaani,sera za chama ni kama mavazi na maandalizi mazuri ya harusi yanayosindikizwa na sherehe ya kufa mtu sambamba na hotuba za kutoa machozi kama si kuvunja mbavu.However,kinachodumisha ndoa si kimoja katika ya hivyo bali dhamira ya dhati ya wanandoa kuhakikisha wanafuata maadili,upendo na kujua thamani ya ndoa yao.
Kadhalika,sera "nzuri" hazina tofauti na hayo niliyoyataja kuhusu maandalizi hayo ya ndoa.Ila kuzitafsiri sera hizo katika vitendo ni sawa na namna wanandoa wanavyoweza kuifanya ndoa yao kuwa ya furaha na mafanikio.
Nalazimika kutumia mifano hii ya mitaani ili kuleta mantiki.
Hivi mkuu umeshaandika makala ngapi dhidi ya kila baya linaloendelea kufanywa na CCM.Je wakati unaandaa makala hizo,hujiulizi kuwa CCM wana sera,na kwamba,kwa upande mmoja,hawajali kutenda tofauti na sera hizo,na kwa upande mwingine,wanafahamu bayana kuwa katika mazingira tuliyonayo hata wakienda kinyume na sera walizoweka wenyewe hakuna madhara kwao na kwa maslahi yao.
Naomba kurejea kukumbusha tena.TATIZO LA MAENDELEO BARANI AFRIKA,NA PENGINE NCHI NYINGI ZA DUNIA YA TATU HALIJAWAHI KUWA KWENYE SERA MBOVU BALI UTEKELEZAJI.
Sasa kama tukikubaliana kuwa tatizo halijawa kwenye sera,then umuhimu wa sera hizo katika kufikia maendeleo/kuleta mabadiliko ya kweli unatoka wapi?
Hivi kwa mtizamo wako unadhani kwanini Ujamaa ulishindwa?
Chadema wanaweza kutueleza kuwa wakiingia madarakani wataifumua Idara ya Usalama wa Taifa,in and out.Until delivered,sera au ahadi hiyo itabaki kuwa ahadi kama hizo zinazoendelea kutolewa na JK.Cha muhimu ni utekelezaji.Kukurejesha tena mtaani,cha muhimu sio kutangaza dhamira ya kuoa bali cha muhimu ni kuoa...kwani kuna mafisadi kadhaa wa ngono wanaotangaza ndoa kwa mabinti kila mtaa lakini mabinti hao wanaishia kuachwa na mimba kama si kuambulia virusi vya ukimwi.Wanachofanya mafisadi hao wa ngono hakina tofauti na kinachofanywa na mafisadi wa CCM:kutoa sera na ahadi taaaamu lakini utekelezaji ni SIFURI,ZERO,ZILCH,NADA.
Tunaweza kusubiri CCJ ifanikiwe kuokoteza wanachama wake na kujipanga vizuri kisha wakatuletea kile ambacho hakuna chama kingine cha siasa kimeshawahi kufanya katika historia ya siasa za Tanzania.Tunaweza pia kusubiri hadi Chadema,CUF,na vyama vingine vya upinzani vitakapokuwa na sera za kuelweka ndipo tutoe wito wa CCM kung'olewa madarakani.Kadhalika,tunaweza kuiacha CCM madarakani kwa vile tu vyama vingine havina sera nzuri zinazotosheleza kuwa supported.However,wakati tunasubiri yote hayo,nchi yetu inazidi kuteketea.Kama "Dkt" Mzindakaya alivyotahadharisha,tunakoelekea si kuzuri.Tunaweza kusubiri sera njema na mbadala then wakati tukiwa tayari kuzi-apply tukajikuta tupo katika,God forbid,hali kama ya Somalia.And talking of Somalia,naamini Siad Barre nae alikuwa na sera nzuri pia lakini angalia leo Wasomali wako katika hali gani.
Mlalahoi,
Unajua ni vigumu sana kumwelewa huyu mkuu wetu Mwanakijiji hasa anapokuwa mpinzani wa mawazo yasiyokuwa sawa na yake. Nimeshindwa kumwelewa muda mrefu na nimejaribu kumwelewa lakini anapiga chenga kama za Messi za mguu mmoja wa shoto ambazo ukimjulia anakwenda wapi rahisi kumbana, tatizo ni hiyo mbio zake kuliko hata swala.
Alikuja na hilo la What Next - kwa sababu yeye anayaona matatizo yetu na anataka yakabiriwe na sera. lakini matatizo sio yanayotunga sera ila hutafutiwa ponya, ila Maendeleo ndio huwa zaidi ya ponya na ndio sera zinapotakiwa kufanya kazi.. Kama vile huko Marekani leo wanakabiriwa na kuvuja kwa mafuta ya BP, hili ni tatizo ambalo linataka ponya (suluhisho) na sio sera. Sasa itakuwa vigumu sana kumuuliza Obama atatumia sera gani kuhusiana na uvujaji au kumuuliza what next baada ya kudhibiti. Kwanza shughuli ni kuhakikisha mafuta hayavuji tena, kisha baada ya hapo umuhimu wa kuhakikisha vyanzo vya mafuta haviwezi kuvuja tena utatafutiwa ufumbuzi hatua kwa hatua.
Nadhani tatizo la mwanakijiji ni hawa Mafisadi ambao kama unakumbuka nilisema toka mwaka 2005 kwamba maendeleo ya Tanzania hayawezi kupatikana pasipo kudhibiti Ufisadi kwani uchumi wetu ulikuwa mzuri tu lakini ukikusanywa ktk pakacha lenye tobo na mirija ikinyonya kila ujazo..na kulingana na fikra zake kaona hakuna dawa isipokuiwa ku declare upya siasa ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA kama dira ya Taifa na kurudisha hadhi ile ya mwalimu.
Haya ni mawazo yake yeye na hao wana CCJ na tunayaheshimu, ila hata mimi mpenzi wa mwalimu sikubaliani na hizi hadithi za UJAMAA na KUJITEGEMEA, Sikubaliani na kurudisha AZIMIO LA ARUSHA isipokuwa kurekebisha makosa yatokanayo na hali tuliyopo. Kama vile tulivyokosea mwanzo kuingia Ubepari tulitakiwa kurekebisha Azimio la Arusha kulingana na wakati huo Kiuchumi na sio maamuzi ya Zanzibar kutoa RUKSA isiyohusiana na failure za Ujamaa.
RUKSA was a big mistake kwa sababu ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo leo..meaning matatizo ya Ujamaa kushindwa kutuletea maendeleo kulitafutiwa dawa hiyo ya RUKSA na imeshindwa kufanya kazi.. So What next? (maneno ya MMKJ) Huwezi kuivunja RUKSA kwa kurudia makosa ya mwanzo (Azimio la Arusha) ambalo pia kwa miaka 20 na upuuzi iliishindwa kufanya kazi.
Kama vile Malaria unapojaribu kuitibu unachukua dawa moja ikishindwa, inachukuliwa ya pili nayo ikishindikana unakwenda hatua ya tatu kutafuta dawa nyingine..Hivyo maadam mafisadi ni mavuno ya Ruksa kuna kila sababu ya 1. Kuwang'oa Mafisadi na mirija yao, 2. Kuziba tobo zote za mirija inayotunyonya, na mwisho kuondoa RUKSA ambayo ndio imezaa mafisadi. Hatua kwa hatua kama mwanzo..
Na hatuwezi kufikiria kuondoa ghafla RUKSA kwa sababu tu imeshindwa na imezaa mafisadi wengi zaidi, ila kinachotakiwa ni kutazama kwa nini Ruksa failed us kama tulivyotakiwa kuutazama Ujamaa na Kujitegemea, tutatazama loopholes zilizopo na kuzidhibiti na nina hakika kabisa miiko na maadili ya viongozi toka Azimio la Arusha ndio solution (mawazo yangu binafsi).
Wengi wanapinga sana kuwawekea vikwazo viongozi wa serikali kutotajirika lakini wanashindwa kuelewa kwamba hakuna sababu ya kuruhusu Utajiri wa viongozi au mtu yeyote yule kwa kupitia Ufisadi na kibaya zaidi viongozi wetu ndio wao majemedali wavita hii ya kuondoa Umaskini., uiweje wao wafikirie haki ya Utajiri hali taifa zima linapigana kuondokana na Umaskini?..Ni haki kwa nahodha kuwa wa kwanza kurukia ndani ya boti la kuokoameli inapozama?..sidhani na ndicho Mwinyi alichotupa. Meli yetu Tanzania ilikuwa ikizama, na RUKSA ikatoka kila mtu na msalaba wake..
For the last 20 years mingine sisi wote tumekuwa ktk hali ya kunyang'anyana maboya na kurukia ndani ya boti za kuokoa bila kujua kwamba boti hizo zina uwezo wa kuchukua abiria wachache tu. na kibaya zaidi viongozi wetu wakitumia wadhifa wao wamekuwa wa kwanza kuingia ktk boti hizo.. Yet, watanzania bado wanafikira au wana matumaini ya kuokolewa na manahodha ambao tayari wao wameisha okoa maisha yao...
Ni wakati wa viongozi kubeba uzito wa mzigo huu wa umaskini na njia pekee ni kuwavika magwanda na wao kuwa mstari wa mbele kupambana na maadui zetu..Utajiri haupatikani vitani isipokuwa kwa dhulma au wizi, na inapotosha malengo yaliyokusudiwa.
Nadhani hapa naiona wasiwasi ya Mwanakijiji kuhofia Chadema au viongozi wake kununuliwa au kutoweza kuwathibiti hawa Mafisadi. Na kama wataweza je Chadema wamejiandaa vipi kuhusu Usalama wa Taifa ambao CCM wamekuwa wakitishia kwamba bila wao hakuna usalama..
Asante sana Mkandara asante.Mzee Mwanakijiji,
Sawa tumekusikia, na hakika najua upo hapo Marekani miaka mingi sana. Ebu tueleze wewe sera za Domokratic ktk Usalama wa Taifa tofauti na sera za Republican ambazo wananchi walizikubali.
Au tupe sera za vyama vya UK au nchi yeyote kwa tofauti ya vyama utanisaidia sana kuona vitu ambavyo sikuwahi kuvifikiria kwamba wananchi walitakiwa kuvifahamu kabla hawajaunga mkono utawla unaofuata..
Nijuavyo mimi Usalama wa Taifa ni dira ya kitaifa haihusiani kabisa na siasa za chama.. Watanzania wote na tofauti zetu za kiitikadi inapofikia swala la Usalama wa Taifa tunazitua tofauti zetu na kuchukua msimamo mmoja usiokuwa na itikadi.
Jasusi labda niongeze kusema tukwamba hata zile vurugu za 2007 ni matunda yaliyovunwa kwenye shamba la KANUWildcard,
Kenya is better off today without KANU. Licha ya mauaji ya 2007 ambayo yalikuwa inevitable anyway, Kenya is better off, much better off without KANU. Wametunga katiba mpya na August 4 inapita kwa asilimia zaidi ya 60. Hujajiuliza kwa nini watu kama Moi wanakampeni kupinga katiba hiyo? Wataunda tume mpya ya uchaguzi. Hiyo ni step foward. Sisi Bongo hata kuzungumzia katiba tu imekuwa nongwa. Na kuhusu tume ya uchaguzi ndiyo sisemi kabisa.
Kuweka CCM kambi ya upinzani ni lazima liwe lengo mama la CHADEMA. Inawezekana sana, kama ilivyowezekana Kenya na Zambia.
CCM na mama yake TANU wametutawala kwa miaka 50 sasa, bila kuweza kuleta maendeleo. Miaka mitano mingine itasaidia nini? Hakuna mabadiliko ya msingi Tanzania bila kubadilisha kwanza chama tawala.
Itasikitisha sana kama sherehe zetu za mwakani za kuadhimisha miaka 50 tangu tujinyakulie UHURU zitasimamiwa na watu watu wale wale waliotufikisha kwenye lindi tulilomo.
CHADEMA is our hope. Iwapokee wote wale watakaonyimwa na CCM kugombea ubunge. Isiwaite makapi ya CCM.
ndiyo..