Yah: Kuunga mkono CHADEMA kwa sasa

Tunakuuliza wewe utajibu vipi?.. au wataka hao Chadema wakujibu vipi.. frankly kama mimi ni kiongozi wa Chadema sintakuwa na jibu, ikiwa wewe hukupata jibu toka ktk katiba,sera, na ilani za chama - sijui unategemea jibu litoke wapi kujibu swali lisilojulikana..

Hapo mkandara i agree with you, huwezi kutekeleza mambo ya kwako binafsi kwa niaba ya taifa lazima yawe documented ili yeyote atakaepewa madaraka aweze kutekeleza na wananchi wampime ya aliyoyaeleza. CHADEMA wameeleza kila kitu kwenye Katiba, ilani ya uchaguzi na sera zao pia. kama kama hukubaliani nadhani unatakiwa kukosoa kwenye hizo documents zao. Then what??? zipelekwe kwenye hizo sera na zionyeshwe mapungufu yake ili Then what??? ipate majibu kwa kukosoa na kutoa ALTERNATIVES.
 
Chadema ni tumaini kubwa sana kwa wengi wetu na kwa muda mrefu limekuwa kwangu ni tumaini vile vile. Lakini bado haijataka kuvuta mstari ule wa kiungozi kwa miaka kadhaa sasa. Siamini kama ndani ya siku chache zilizobakia wataweza kuvuka mstari huo. Na watakapogundua kuwa walipaswa kuuvuka watajikuta wanagalagazwa kwenye uchaguzi mkuu huku wakilalamika "CCM", "Tume ya uchaguzi", "Wizi wa kura", "Vyombo vya dola".
MM

Mkuu MMKJ,

Nashukuru hatimaye umejitokeza na kuweka msimamo wako! Lakini kutokana na quote hapo juu nini ilikuwa lengo la CCJ? Unataka kutueleza mlitaka kueneza itikadi tuuuuuuu, halafu basi?!! Kama sikosei mliwahi kusema CCJ itafanya nini ndani ya siku 100 ikipata kuingia magogoni!!! Kama nakumbuka sawa, moja ya mkakati ilikuwa kuwafikisha mahakamani wote waliohujumu nchi hii katika ufisadi tunaoendelea kuuona!!

Hebu tueleze kama CCJ ingepata usajili wa kudumu ndani ya muda huu ingefanya nini pia? Maana kuna post moja uliwahi sema mabadiliko nchi hii yatatokea Oct 2010, what did you really mean? Maana muda si mrefu tukaona CCJ, mara tukajua wewe ni kati ya wanachama waanzilishi!!!

Je unataka kutueleza CCJ ingepata usajili isingekuta na vikwazo unavyotueleza hapa!!! TUME YA UCHAGUZI, DOLA, WIZI WA KURA...et cetera!!!

Mkuu mimi nadhani kuna haja na kusubiri uthubutu wa CHADEMA tuone!!! Niliwahi kusema hapa, kwamba sikibezi kamwe CCJ, ila disappointments ndizo zinazoumiza, specifically nilizitaja zile za 1995!!! Sasa mnatuelezaje CCJ?

Kwanini msiingie/msitoe ushauri kwa CHADEMA wa kuvuka mstari unaouongelea!!! Namna hii CCM imeshansinda mkuu. Maana inaanzia kushinda kwenye fikra zetu!!!
 
Ukweli utabaki palepale, watanzania wanahitaji kiongozi anayeweza kubadilisha hali zao kuwa bora zaidi. Na huyu lazima aweze kuwaambia atafanyaje hili. Na aweze kuwaambia kwa lugha rahisi sana na si huendelea kuorodhesha matatizo wanayoletwa na uongozi uliopo. Hili wanalijua vyema pengine kuliko hao wanasiasa. Hili la vipi watafanya hilo vizuri kuliko CCM na kipi so far wamefanya kuelekea huko ni muhimu kwa wapiga kura wasikie.

Ukilalamika kwa mwenye njaa kuwa chakula kipo humu ndani ila tu nimenyimwa ufunguo wa chumba ningekupatia haimsaidii chochote mwenye njaa. Anakuona nguvu yako na yake ni sawa. Ukiweza kuvunja huo mlango au ukamweleza mbinu atakazoziamini utakazotumia kumpatia hicho chakula anaweza kukulinda utumie hizo mbinu. Mwamuzi mpiga kura
 
Chadema ni tumaini kubwa sana kwa wengi wetu na kwa muda mrefu limekuwa kwangu ni tumaini vile vile. Lakini bado haijataka kuvuta mstari ule wa kiungozi kwa miaka kadhaa sasa. Siamini kama ndani ya siku chache zilizobakia wataweza kuvuka mstari huo. Na watakapogundua kuwa walipaswa kuuvuka watajikuta wanagalagazwa kwenye uchaguzi mkuu huku wakilalamika "CCM", "Tume ya uchaguzi", "Wizi wa kura", "Vyombo vya dola".

MM

Mkuu MMKJ,

Nashukuru hatimaye umejitokeza na kuweka msimamo wako! Lakini kutokana na quote hapo juu nini ilikuwa lengo la CCJ? Unataka kutueleza mlitaka kueneza itikadi tuuuuuuu, halafu basi?!! Kama sikosei mliwahi kusema CCJ itafanya nini ndani ya siku 100 ikipata kuingia magogoni!!! Kama nakumbuka sawa, moja ya mkakati ilikuwa kuwafikisha mahakamani wote waliohujumu nchi hii katika ufisadi tunaoendelea kuuona!!

Hebu tueleze kama CCJ ingepata usajili wa kudumu ndani ya muda huu ingefanya nini pia? Maana kuna post moja uliwahi sema mabadiliko nchi hii yatatokea Oct 2010, what did you really mean? Maana muda si mrefu tukaona CCJ, mara tukajua wewe ni kati ya wanachama waanzilishi, tukaunganisha dots tukaelewa maneno yako!!! Sasa mara hii yamebadilika...!!!

Je unataka kutueleza CCJ ingepata usajili isingekuta na vikwazo unavyotueleza hapa!!! TUME YA UCHAGUZI, DOLA, WIZI WA KURA...et cetera!!!

Mkuu mimi nadhani kuna haja na kusubiri uthubutu wa CHADEMA tuone!!! Niliwahi kusema hapa, kwamba sikibezi kamwe CCJ, ila disappointments ndizo zinazoumiza, specifically nilizitaja zile za 1995!!! Sasa mnatuelezaje CCJ?

Kwanini msiingie/msitoe ushauri kwa CHADEMA wa kuvuka mstari unaouongelea!!! Namna hii CCM imeshansinda mkuu. Maana inaanzia kushinda kwenye fikra zetu!!!
 
Kwa kadiri ya kwamba lengo ni kutaka tu kuwang'oa CCM madarakani halafu ndiyo mfikirie mtafanya nini kwa taifa na kutuambia basi mtaendelea kuwa wasindikizaji kama ilivyokuwa kuanzia 1995 hadi sasa na itakavyokuwa milele na milele.


Bila ya shaka, lakini tushikamane kwenye kitu gani? bado naambiwa "kuing'oa CCM madarakani"; nauliza ili kiwe nini? jibu "ili itoke madarakani", nauliza halafu kifuate nini? naambiwa "hilo si la msingi kwa sasa kujua, tukishawatoa madarakani ndiyo tutawaambia"! Well.. mshikamano wa namna ndugu zangu nyie shikamaneni na ng'anganianeni kabisa na mgandane kama yule sungura alivyojagandishwa kwenye sanamu akidhania anaikomoa kule shambani.

Mzee mimi sijaelewa unaposema wanataka kuiondoa CCM halafu basi, ni nani atakayewapa kura? je hii CHADEMA haina manifesto, watakayotumia kusema watawafanyia nini watanzania? ni kweli hawana wanachokipanga? mimi siamini hilo. Labda mzee tusubiri mkutano mkuu wa CHADEMA ni lazima watatuambia watatufanyia nini. Hakuna shaka kwamba CHADEMA ndio wamekuwa mstari wa mbele kupinga ufisadi wa Meremeta, Tanggold, Kagoda, Mwananchi Gold, EPA etc,na wamekuwa wakiishinikiza serikali mpaka dakika ya mwisho ichukue hatua, halafu wasituambie kuwa wakiingia madarakani watawafanya nini hawa watu? Hapana mzee tuvute subira, kama kwenye ilani yao hawataweka hilo, mimi nitakuwa wa kwanza kuwakataa.
 
Nadhani labda unafikiria namaanisha CCM ising'olewe madarakani. Mbali kutoka hilo. Ninachomaanisha ni kuwa CCM kuondolewa madarakani haliwezi kuwa lengo na ajenda ya uchaguzi kwa sababu kuondolewa kwa CCM kunakuwa ni matokeo ya kukubalika kwa sera, mipango, na ahadi za CHADEMA. Sera, mipango na ahadi hizo ni lazima ziweze kuwashawishi wananchi kuwa CCM ni mbaya na hafai; ni lazima ziwe bora na zinazowezekana kuliko zile za CCM. Nje ya hapo CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa kuunganisha chuki dhidi yake. Kwa sababu kama mnavyoona kuna watu wanaoipenda CCM kwa kiasi cha ajabu zaidi na wengine licha ya kujua ubovu wa CCM bado wanajipanga mstari na kuishangilia.

Hivyo, ni mambo gani Chadema inaahidi kuyafanya na kwa muda gani ambayo ni bora kuliko ya CCM ambayo yatafanya wananchi waikatae CCM na hivyo kuing'oa madarakani? Maana kama leo JK anasema atajenga Chuo Kikuu kingine, Hospitali, barabara na akaonesha "mafanikio" ya CCM Chadema wataonesha nini au kuahidi nini zaidi ya kile cha CCM?

Kwa mfano, mkisema ufisadi JK atasema wamepeleka watu kadhaa mahakamani, fedha za EPA zimerudishwa, watu wamefukuzwa kazi n.k Chadema itasema nini juu ya hilo ambalo ni bora kuliko hilo? Si tumeona wapinzani kama kina Mrema wakisifia juhudi hizo na hata baadhi ya wana Chadema wenyewe?

Mkuu,
Asante, mchango wako umeonekana. May i say, hii ndo rai ya wengi kwako. Yawezekana CHADEMA wamekosa techinical team kwenye hili. Ndo maana tunataka kuunganisha nguvu. Umetueleza ulikuwa unafahamu uwepo wa mazungumzo kati yenu (CCJ na Chadema). Kwani hamku-identify mapungufu yao, ushauri wenu kabla ya kuwaruhusu to layer waende?

Issue mkuu wangu, why not joining forces against the common enemy?
 
pole pole karibu unanipata...

mwenzenu Obama alisema mapema kabisa kuwa akiingia madarakani atafanya nini... watu hawakuwa na kukisia kuwa sera yake ilikuwa ni kuwaondoa tu republican madarakani halafu mengine yangekuja mbele ya safari. Wapiga kura waliambiwa sera za Obama kuhusu Guantanamo, vita, uchumi n.k

Inamaana chadema hawana sera? Kama ni vyama vyote nafikiri vinazo.
 
Msiulize ulize maswali mengi kwenye kazi za watu!. Wata wanauliza tuu, wanauliza tuu, wanauliza tuu na hawajibiwi, hivi hamuelewi tuu!.
Na wewe endelea kuuliza.

Pasco nimekusoma mkuu, mimi nahisi Mkuu MKJJ ni aidha yuko kazini au ni selfish! Mimi sioni tofauti ya kuwashauri wale walio kwenye nafasi ya kupambana na adui na kung'ang'ania lazima uwe wewe. Hivi kuna nini kwenye hili swali la MKJJ? CCJ imeshindwa kuchomoza, si ungetumia nafasi ya amzungumzo kuwapa CHADEMA terms za CCJ kuungana nao; mkaelezea benefit watakazopata mkijoin forces, maana CCJ mlikuwa na mikakati mizuri!!! Nini tatizo?

Wewe si ndiyo ulitueleza mabadiliko ni 2010 na siyo 2015!!! What happenend mkuu? This hurts mkuu!! So baada ya kushindwa mmeshindwa hata kutoa press conference kuelezea way forward?
 
Mkuu wangu wewe ndio hujui dhamira ya Marekani kwenda Iraq lakini sisi tunajua na haina kificho isipokuwa wamekutana na vichaa wenye historia ya kutotawaliwa. Hawapewi pumzi ya kuyafanya waliyokusudia kuyafanya..

Hata siku moja Marekani haendi mahala pasipo malengo na wanaweza hata kutunga itikadi ili mradi malengo yao yakubalike kwa wajinga kina sisi tusioona nje ya CNN. Kumbuka mwisho wa yoote haya siku zote - TRUTH wil prevail!

Salaam,

You are right kuwa America as a nation doesn't go anywhere without knowing watapata nini BUT what MM is trying to say kwa uelewa wangu ni kuwa waliwa-underestimate Iraqis and now angalia death toll and the whole region is not stable.
 
we MM, please usiwachanganye wana JF... kubali ulichemsha kuunga mkono mawazo yaliyodhoofu kiasi cha kufa yakiwa na umri wa miezi mitano tu.....

najua mbegu ikianguka ardhini, lazima ife na ioze kiasi ili iweze kuota na kumea... lakini inachekesha kuwa ccj imeoza kiasi cha kutoweza kumea tena..... hahaha... MM tafakari upya kuhusu siasa za TZ...
 
Pengine Mwanakijiji unatumia lugha ngumu kueleweka.Pengine tatizo liko kwangu kwamba ni mgumu kuelewa.Lakini hadi sasa nashindwa kabisa kukuelewa unapojaribu kuonyesha kuwa ufumbuzi wa matatizo yaliyopo nchini mwetu hautopatikana kwa kuing'oa CCM madarakani.

Inawezekana pia japo nilifaulu PS 101 pale Mlimani katika mwaka wangu wa kwanza,sikumwelewa Mhadhiri aliyekuwa akifundisha somo hilo (wakati huo) Dkt Max Mmuya ambaye katika mihadhara yake alikuwa akitueleza kuwa mmoja ya maelngo makuu ya kuanzisha chama cha siasa ni kukamata dola.Na hiyo,kwa namna flani,ndio inatofautisha political parties from interest and pressure groups.

Lakini hata kama wakati huo akili yangu ilikuwa changa kukamata mafundisho hao muhimu kuhusu siasa,nimetumia muda mwingine wa kutosha kusoma na kutafiti siasa kama stadi (hasa katika namna theory zinavyoendana au kukinzana na uhalisia uliopo).Na katika muda wote huo sijakutana na maandiko au njozi kwamba moja ya malengo ya msingi ya kuanzisha chama cha siasa sio kukamata dola.Umuhimu wa chama cha siasa kukamata dola unatokana na ukweli kwamba ili sera zake ziweze kufanya na/au kufanyiwa kazi ni lazima kiwe na mamlaka ya kiutawala na dola kwa umma.Na mfano mwepesi ni namna "sera za kipekee za CCJ" zitakavyoendelea kubaki "sera nzuri tu" pasipo namna ya "kulazimisha utekelezaji wake" kwa vile chama hicho hakijakamata dola.Na ni katika namna hiyohiyo,tunalazimika kukubali mabaya mengi tusiyotaka kuhusu CCM kwa vile tu chama hicho kina mamlaka ya kutekeleza matakwa yake-tupende tusipende.

Kwa vile wewe ni mchambuzi mzuri wa siasa zetu,naamini unafahamu fika kwamba kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu ni CCM.Sasa pasipo kuondoa kikwazo hicho tutawezaje kufikia mema tunayotaka kuyafikia?Au mwenzetu utuelezeje njia mbadala ya kufikia malengo yetu wakati CCM imekumbatia dola,na kutumia vyombo vya dola kukandamiza vyama vingine vya siasa na walalahoi kwa ujumla.

Siasa na utabibu ni fani mbili tofauti lakini zinaweza kuafikiana katika namna hii:kama una matatizo ya kiafya yanayosababishwa na uvimbe unaokwaza damu kufika mahala fulani,ufumbuzi pekee ni kuundoa uvimbe huo unless kwa kuuondoa mgonjwa atakufa.Ni katika namna hiyhiyo ndio maana baadhi ya majeruhi wa ajali au vita hushauriwa kukatwa viungo vyao ili waendelee kuishi hususan kama sehemu zilizoathiiriwa zinaweza kupelekea usaha au kuoza na kuusababishia mwili madhara makubwa zaidi.Na katika siasa,ufumbuzi ni kuondoa kikwazo kinachokwaza nchi kupiga maendeleo.Na ndio maana ufumbuzi wa kadhi na uonevu wa mkoloni dhidi ya wenye nchi ulikuwa kumg'oa mkoloni.Na pia Nduli Idi Amini alipovamia Tanzania,ufumbuzi pekee tuliobakiwa nao ni kumtimua,na pel tulipoweza tukamng'ao kabisa katika utawala.

Sasa iweje kuindoa CCM madarakani kusilete ufumbuzi?Unauliza tukishaing'oa CCM itafuata nini?Kwani mwanamke anayeishi kwenye manyanyaso katika ndoa akishamtaliki mumewe mnyanyasaji kinafuata nini?Au kama gogo limeziba barabara na hivyo kukwaza magari kupita,likishaondolewa kinafuata nini?

Kuna wakati tunaoaswa kuangalia uhalisia na kukepuka matamanio ya kutaka njozi zigeuke kuwa uhalisia.Kuna wanaotaka Watanzania "waende darasani kwanza" kabla ya kuanzisha jitihada za kujikomboa.Wanachosahau ni kwamba kuna uwezekano mkubwa "tutakapohitimu somo la mbinu za kujikomboa na kujitawala" tunaweza kukuta hakuna mahala pa kufanyia kazi "kanuni tulizofundishwa darasani" kwani nchi itakuwa imeshauzwa.


Na jibu jepesi kwa swali "je CCM ikishatoka madarakani kinafuata nini" linaweza kupatikana kwenye mfano halisi wa je baada ya kumuondoa mkoloni au kumtimua nduli Idi Amin kilifuata nini.

Well said!!
 
katibu wa muda wa CCJ Renatus Muabhi amesema haya:
1. kuhama akina mpendazoe, ngihili na kiyabo si kuhama kwa chama kizima
2. si lazima kila mwanasiasa agomee ubunge
3. waliojiunga CCJ kwa ajili ya kugombea ubunge ama urais bila malengo ya muda mrefu na chama waanze sasa kuonda kuwafuata hao akina mpendazoe wanaotangatanga kutafuta ubunge na maarufu wa kujidanganya
4. CCJ bado ipo na bado ina wanachama
5. CCJ itaendelea kushrikiana na msajili wa vyama vya siasa ili kuhakikisha kinapata usajili wa kudumu
6. kana lengo la mpendazoe lilikuwa kugombea ubunge, ni heri angebaki CCM
7. kwa umaarufu mpendazoe alioingia nao CCJ, kuondoka kwake kumekipa CCJ ahueni kubwa

my take:
mpendazoe (aka mpendazote) ni mrema mwingine hatari zaidi kutoka kishapu. ni mrema wa awamu ya nne. kama mrema alivyojiunga NCCR mageuzi akaksambaaratisha na kuhamia TLP na kukia umaarufu wa muda kabla ya kukisambaratisha pia na kurudi nyumbani (CCM) ndivyo alivyofanya mpendazote. karukia chama-mimba (CCJ) kakisambaratisha na sasa kaparamia chadeA. NAWATAHADHARISHA CHADEMA WASIJE WAKAJIDANGANYA KUMPA CHEO CHOCOTE. ABAKI KAMA MWANACHAMA WA KAWAIDA TU A KAMWE WASIMKABIDHI MIKE KUKISEMEA CHAMA,. wasithubutu hata kumpa u-MC katika sherehe za chama, histoia itakulakwao.

hongera muabhi kwani angalau umedhihirisha kuwa wewe na wenzio wachache ndio mlijua nini mnakifanya na harakati za kisiasa kupitia CCJ

ole wenu chadema. hukumu ya NCCR mageuzi inawanyemelea, huyo mliyempokea jana ni "mrema mpya"....

ni mtazamo tu..
 
Wale wote wakina mpendazote ni najaa nakikundi chake kwani hapa tanzania tunahitaji upinzani waweli sio upinzani njaa!!
 
inanikumbusha kisa cha jamaa walioenda kuwaokoa watu waliokuwa katika shida; watu wale kwa vile walikuwa katika shida walikumbatia kwa haraka "waokoaji" wao hao ambao walisema wamekuja kuwatoa katika shida zao. Baada ya kutoka kwenye shida wakawauliza waokoaji wao "sasa mnatupeleka wapi"? waokoaji wakasema "msiwe na wasiwasi tutajua baada ya muda si mrefu, nyie tufuateni tu".. guess what happened?

this makes sense. Lakini nadhani sera za Chadema zipo wazi! Labda kwa sasa hawajazipa kipaumbele...lakini mimi najua 100% kuwa wao wana mipango gani baada ya kumuondoa CCM. Kwa hiyo sidhani kama ni Chama kisicho na mbele wala nyuma...chenye dhumuni la kuiondoa CCM tu...au kwa kutumia mfano wako...kuokoa watu tu! nadhani kwa sasa wewe umeumia sana kutokana na tarumbeta nyingi ulizopuliza juu ya CCJ. Kwa hiyo unajaribu kwa hali na mali kuwapa wenzako jeraha. Ivi CCJ ilikuwa na sera gani tofauti? Kushtaki mafisadi?

Tuaangalia mfano wa moja ya sera za Chadema:
Sera ya Utawala

Utawala wa Ukiritimba na Urasimu, ukoje?​
  1. Serikali kuu inaingilia mamlaka ya Serikali za mitaa. Katiba haipo wazi juu ya mamlaka ya serikali za mitaa.
  2. Serikali ni kubwa mno na haina ufanisi.
  3. Halmashauri za Wilaya zimebanwa, hazina uhuru wa kutosha na zinaingiliwa na watawala kutoka Serikali kuu.
  4. Wakuu wa wilaya wanaingilia utendaji wa halmashauri za wilaya na kudhoofisha demokrasia.
  5. Mikoa ni mingi sana na haina ufanisi kiutawala na kiuchumi.
  6. Mfumo wa Muungano ni tata na hautoi nafasi kwa Muungano mkubwa zaidi wa shirikisho la Afrika Mashariki.


Serikali ya CHADEMA itaondoa ukiritimba na urasimu kwa kufanya yafuatayo.

  1. Cheo cha Mkuu wa Wilaya kitafutwa na kazi zote za Ofisi ya Mkuu wa Wilaya zitajuimshwa na Kazi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji pamoja na Meya.
  2. Halmashauri za Wilaya zitapewa mamlaka na uhuru zaidi kwa mujibu wa Katiba Mpya itakayotungwa kwa ushiriki wa wananchi.
  3. Mfumo wa serikali za mitaa utaimarishwa kwa kuimarisha serikali ya Kijiji kama chombo cha msingi cha uongozi (governance).
  4. Mameya watachaguliwa na wananchi moja kwa moja na watakuwa na majukumu ya utendaji pia.
  5. Mikoa ya sasa itaunganishwa na kuwa na mikoa kumi tu ili kuwezesha ufanisi wa kazi na pia kuleta ushindani wa kiuchumi miongoni mwa mikoa ndani ya nchi.
  6. Mikoa itakayoundwa itakuwa na mabunge yao na kuchagua viongozi wao kidemokrasia.
  7. Tutarekebisha mfumo wa Muungano ili kuiweka nchi tayari kwa shirikisho la Afrika Mashariki bila kuathiri uhuru na dola ya Zanzibar na Tanganyika.
  8. Mabadiliko yote ya mfumo wa Utawala wa nchi yatafanywa kufuatia zoezi la kutunga katiba mpya nchi kufuatia
  9. Mkutano Mkubwa wa Katiba utakaoshirikisha wananchi wote.
  10. Nafasi za uongozi wa serikali zitakuwa na mtazamo mkubwa wa kijinsia.
  11. Serikali itakayoongozwa na CHADEMA itahakikisha nafasi za Mawaziri, Manaibu Mawaziri na Makatibu Wakuu zinashikiliwa na idadi ya kutosha ya Wanawake ili kuweka uwiano wa kijinsia katika utawala wa nchi.
  12. Serikali ya CHADEMA itahakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi katika Mahakama na
  13. Bunge kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake wengi zaidi kusomea sheria na kuajiriwa kuwa mahakimu wa mwanzo, wa wilaya na mahakimu wakazi na baadae kuwa Majaji.
Ii this not good enough as an answer to your 'what then' question? Labda tatizo ni wewe kudhani kuwa unajua zaidi ya wengine!
 
Mzee Mwanakijiji,

Binafsi nakupata kwa nguvu ya mia! Tangu nilipoona kwenye TV kwamba hawa ndugu zetu wameamua kutoka CCJ na kujiunga na CHADEMA nilipatwa na mshangao mkubwa. Kumbe wenzetu hao wao walikuwa wakiwaza namna ya kupata ubunge tu zaidi ya kitu kingine chochote?

Mabandiko mengi yanayong'ang'ania ulazima na umuhimu wa kuungana na CHADEMA ili kuing'oa CCM yanadhihirisha jinsi ambavyo bado mawazo yetu yamejikita kwenye madaraka na kutaka kutawala zaidi ya ni kwa mbinu gani na namna gani tunapanga kuuendesha utawala huo ili uweze kukidhi haja iliyopo ya utawala uliotukuka utakaonufaisha wananchi wetu na kulitoa Taifa letu katika lindi la tope.

Tunao mfano hai wa namna ambavyo Watanzania wengi kwa miaka mingi sana tulikuwa hatuelewi ama hatutaki kukubali ukweli wa yale tuliyokuwa tukiyasikia na kuyasoma kwenye hotuba za Mwalimu Nyerere juu ya mambo mengi yanayohusu mustakabali wa nchi yetu. Wapo wengi ambao walifika mbali na kudiriki hata kumkejeli Mwalimu kwamba Mzee huyu 'mchonga' naye tumechoka anaongea sana n.k. Wale wale waliokuwa wakimbeza Mwalimu, baada ya Mwalimu kuondoka kwenye ulingo wa siasa na kutoweka duniani, wamerudi na kuanza kushangaa kuona kwamba mengi aliyokuwa akiyasema Mwalimu yalikuwa ni sahihi na yenye manufaa makubwa kwa mustakabali wa nchi yetu, Afrika na hata dunia kwa ujumla.

Swali ni lilelile, watu wenye imani na mitazamo tofauti ya kisiasa tukishaungana na CHADEMA na kuiondoa CCM nchi tunaiendesha kwa mfumo upi? Au ndio ili mradi tumepata huo ubunge na urais basi itakuwa 'bora liende'. Tutakuwa hatujajitendea haki wala kutendea haki wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mie kwa 'ujinga' wangu nilidhani kwamba hata kama CCJ kimenyimwa usajili wa kudumu, kazi iliyopo ni kujipanga upya na si kukimbilia kujiunga na vyama vingine kwa ajili ya kuwania ubunge ambao unaweza usipatikane!
 
Boramaisha,
Mkuu maelezo yako yanaweza kuonekana yana mantiki sana kifikra lakini mkuu wangu haya ndio mawazo ya Wadanganyika..Mawazo ya Kisoshalist ambayo yametufunga Tanzania kwa miaka 50 chini ya utawala wa chama kimoja pasipo maendeleo na kila siku tukifikiria labda kesho au mimi ndiye mwenye suluhisho..

Wala sioni ajabu kwa Wadanganyika kwani ubishi ni utamaduni wetu. Fikra za kupaka rangi juu ya rangi ya zamani tukifikiria ndio ukarabati, kushindwa kuziba ufa kwa kuhofia gharama zake..lakini hata siku moja hatuwezi kukubali moja kwa moja hofu yetu isipokuwa kutunga sababu za kutaja wachawi.

Ni kwa mtaji kamahuu tumeshindwa kuunda jumuiya imara za Kitanzania nchi zote za nje isipokuwa kwa makundi makundi..kila kundi likilaumu kundi jingine kwa kutokuwa na sera zinazokubalika. Kila mmoja wetu ana mawazo yake, nia yake na mengine mengi ya kibinafsi hadi siku wanaposhikwa na shida ndipo hutafuta umoja wa watanzania ambao haupo isipokuwa kwa kualikana ktk Facebook na Michuzi.

Hapa nilipo tumeshindwa kuunda Jumuiya ya Watanzania kwa UMOJA isipokuwa tumegawanyika kwa makundi wengine wakifikiria wao ni wasomi na wenye nguvu ya kuunda jumuiya kuliko wengine. Matokeo yake tuna Jumuiya tatu za Kitanzania mji mmoja na hakuna hata mojawapo iliyojijenga kukabiliana na maswala yoyote ya kimaendeleo isipokuwa majungu na kurushiana maneno baada ya..It's sad!

Wadanganyika kwa umaskini wetu tuna wivu, inda na hasira za kwa nini hasa kutokana na Ujinga, umaskini na maradhi ambayuo kama huna wewe basi ndugu zako wapo ktk hali hiyo. Na kila mmoja wetu anajitahidi yeye mwenyewe atoke kama samaki kaa waliokusanywa ndani ya tenga. Mwisho wa yoote haya kaa wote watachomwa na mafuta ya moto na kuishia mezani.

Mkuu wangu haya maswala hayakuanza jana, nakumbuka uchaguzi wa mwaka 2005, hibvi hivi tulianza karibia na uchaguzi tukiipinga Chadema kwa kuanzisha mijadala inayowadhalilisha Chadema ili mradi kuwapa nguvu CCM. Na hakika naweza sema Mzee Mwanakijiji anatumia nafasi hii kwa fikra zile zile za Kidanganyika..ili mradi Chadema kionekane ni chama dhaifu badala ya yeye mwenyewe kujiunga nao na kukiimarisha chama hiki. Nakumbuka vizuri Mbowe akizungumzia fikra za mwalimu ktk uchaguzi uliopita akabezwa na matusi kibao sikuwaona mkijitokeza kumpa support kama kweli nyie mlikuwa wafuasi wa mwalimu.

Mimi sii mvivu wa kufikiri wala mchovu wa kumbukumbu..kwani nakumbuka hata kijiwe hiki cha JF kilipoanza kilipigwa vita sana tena vibaya sana tukabakia watu wachache sana tukiendelea kuchangia mawazo yetu na kushirikiana na wahusika pamoja na vishindo vyuoote vilivyokuwepo. Tulibezwa kwa maneno ya kila aina lakini JF survived na leo hao hao Wadanganyika wamerudi na wengine ndio wasemaji wakubwa na hakika wamesahahu kwamba walisema hiki ni kijiwe cha watu 1,000 tu, has no impact to the nation.

Kwa hiyo mkuu wangu nakuelewa sana unapozungumza hoja yako. Na hakika hakuna mtu hapa JF ambaye alikuwa mshabiki wa fikra za mwalimu kama mimi toka tumeanza nimekuwa nikizitetea hata kabla ya kuona mapungufu ya Utawala uliopo. Toka nimejiunga JF na kabla hya hapa nimetetea fikra za mwalimu pamoja na kushindwa kwake Kiuchumi, leo hii nawaona mkirudi na kukubali matokeo baada ya miaka 20 kupita. Sikujiweka pembeni na Watanzania wenzangu kwa sababu nyote mlimkubali Mwinyi, Mkapa na hata JK na falsafa zao zinazotupeleka ktk utandawazi na soko huria mikono mitupu kama vile tupo ktk maonyesho ya sabasaba.

Wakuu zangu najua wapo watu wangu wa karibu sana kina Rev.Kishoka, Brutus, Kichuguu, Nyani Ngabu na wengine wengi ambao wana mashaka na utaratibu wa uongozi wa Chadema. Na mimi wala siko mbali nanyi, ila kinachoniunganisha nao sio kujua nani ni nani ktk utawala isipokuwa swala zima tunalokabiliana nalo sasa hivi. Trust me, I would rather deal with Chademna tomorrow kuliko kuona CCM wakichukua madaraka tena mwaka 2010. Na hakika nitajikata kabisa na maswala haya kama nilivyokata tamaa ktk kuunda jumuiya za Kitanzania.

Pengine hii ndio aliyokuwa akizungumzia mwana JF mmoja kwamba UJAMAA na KUJITEGEMEA haviwezi kuwa pamoja kwani nachokiona ni kizazi cha (mwalimu) Watanzania WABINAFSI wanaotaka kuunda UMOJA - Haiwezekani....
 
Nilifahamu juu ya mazungumzo ya baadhi ya uongozi wa juu wa CCJ na Chadema kwa muda kidogo; Yalitokana vile vile na ushauri wa watu mbalimbali kuwa CCJ iunganishe nguvu na Chadema. Hata hivyo hadi hivi sasa kilichofanyika ni baadhi tu yaviongozi wake kujiunga na Chadema na siyo CCJ nzima. Kuna sababu.

Wapo wanaosema kwa vile hawa ndugu zetu wameingia Chadema basi CCJ na wazo la CCJ nalo limekufa kwa hiyo sote tuliounga mkono CCJ tuinamishe vichwa vyetu kwa kushindwa na kujiunga na Chadema. Hizi ni fikra potofu. Ni potofu kwa sababu zinafikiria Chama kikifa au kikishindwa ina maana mawazo yake nayo yameshindwa. Yanafikiria kuwa kama watu wakitoka kujiunga na chama kingine au kutoka katika siasa maana yake siasa za chama hicho nazo zimeshindwa.

Ukweli unabakia kuwa ukweli kwamba siasa za kutaka ushirikiano wenye lengo la kuitoa tu CCM madarakani halafu ndiyo tujue tunataka kufanya nini ni siasa ambazo katika dhamira yangu siwezi kuziunga mkono. Siasa za kutosema nini unataka kufanya, kwa vipi na kwa muda gani ukionesha ukali kuhusu ufisadi miye siziwezi kwa sababu niaamini tatizo la Tanzania ni ufisadi kuliko kitu kingine chochote kile.

Kutuambia kuwa "panya hawakamatani" lakini hutuambii wewe utawakamata vipi na kwa namna gani, haitoshi vile vile.

Chadema ni tumaini kubwa sana kwa wengi wetu na kwa muda mrefu limekuwa kwangu ni tumaini vile vile. Lakini bado haijataka kuvuta mstari ule wa kiungozi kwa miaka kadhaa sasa. Siamini kama ndani ya siku chache zilizobakia wataweza kuvuka mstari huo. Na watakapogundua kuwa walipaswa kuuvuka watajikuta wanagalagazwa kwenye uchaguzi mkuu huku wakilalamika "CCM", "Tume ya uchaguzi", "Wizi wa kura", "Vyombo vya dola".

Ninawatakia kila la kheri wale wanaojiunga na Chadema wakiamini kitabeba matarajio yao. Hiyo ni demokrasia na kwa hakika kabisa nawatakia mafanikio.

Kwangu mimini bora nirudi na kutokuwa na chama nikiendelea kusimamia fikra na itikadi na mambo ninayoyaamini kuliko kupanda treni ambalo siju linakwenda wapi na kwa nini ati kwa sababu wengine wamepanda na wanashangilia!

Kundi zima la wabunge wa CCM wanaweza kutoka baada ya bunge kuvunjwa na kujiunga na Chadema na kutoka hao akapatikana mgombea wa Urais wa Chadema kama inavyotarajiwa. Hii inaweza kuwa habari kubwa sana na mtikisiko kwa jukwaa la siasa. Kwa wengine hilo laweza kutosha kabisa kufanya waamini kuwa saa ya mabadiliko imefika. Kwangu mimi bado nitaangalia kwa macho ya shuku hadi nijue wanataka kufanya nini. Wakisema wanataka tu KUINDOA CCM MADARAKANI au KUONGEZA IDADI WA WABUNGE, nitawaangalia halafu nitacheeeeeeeka!

Chadema kinaweza kabisa kuwa chama ambacho kitachukua uongozi wa nchi mwaka huu, endapo tu KITATAKA.

MM

Mkuu sometimes huwa unaniacha hoi sana,huwa nashindwa kukupata unachokisimamia hasa..Unaenda mbele halafu unarudi nyuma..
 
Here is the problem that I see with Mwanakijiji. First, I've got to give it up to him...the phrase 'giving up' does not exist in his book. Secondly, and this is what I see is his main problem (not necessarily a bad problem). He has a propensity for ballyhooing things. I often say it to myself that this guy would've made a good salesman (if he's not one already). He has a way with words that he can persuade just about anyone into believing in something he believes in. I remember when he launched his KLHNews...man...you should've heard how he was hyping it up...but where is it now? It's defunct. And the same thing goes for this CCJ thing. He almost got me sold into believing they were for real.
 
Back
Top Bottom