Yah: Kuunga mkono CHADEMA kwa sasa

Mzee Mwanakijiji,
Sawa tumekusikia, na hakika najua upo hapo Marekani miaka mingi sana. Ebu tueleze wewe sera za Domokratic ktk Usalama wa Taifa tofauti na sera za Republican ambazo wananchi walizikubali.

Au tupe sera za vyama vya UK au nchi yeyote kwa tofauti ya vyama utanisaidia sana kuona vitu ambavyo sikuwahi kuvifikiria kwamba wananchi walitakiwa kuvifahamu kabla hawajaunga mkono utawla unaofuata..

Nijuavyo mimi Usalama wa Taifa ni dira ya kitaifa haihusiani kabisa na siasa za chama.. Watanzania wote na tofauti zetu za kiitikadi inapofikia swala la Usalama wa Taifa tunazitua tofauti zetu na kuchukua msimamo mmoja usiokuwa na itikadi.
 
swali hilo ningeweza kuuliza wewe vile vile kwani uko Canada kwa muda mrefu na unaijua Marekani vizuri zaidi labda kushinda mimi.
Au tupe sera za vyama vya UK au nchi yeyote kwa tofauti ya vyama utanisaidia sana kuona vitu ambavyo sikuwahi kuvifikiria kwamba wananchi walitakiwa kuvifahamu kabla hawajaunga mkono utawla unaofuata..

Hili halijibu sera za Chadema kwa Tanzania kama ni tofauti na za CCM au tunahitaji tu kuwachagua watu tofauti hata kama sera zinafanana.

Nijuavyo mimi Usalama wa Taifa ni dira ya kitaifa haihusiani kabisa na siasa za chama..

Hii dira haitengenezwi na wanasiasa na wala haijadiliwi katika mabunge, huundwa na wanajeshi na watu wa vyombo vya usalama bila kuhusisha au kupata uongozi wa kisiasa. Nimekupata.

Watanzania wote na tofauti zetu za kiitikadi inapofikia swala la Usalama wa Taifa tunazitua tofauti zetu na kuchukua msimamo mmoja usiokuwa na itikadi.

hata kama utekelezaji wa usalama wa taifa ni mbovu kiasi gani tunatakiwa kuzitua "tofauti zetu na kuchukua msimamo mmoja usiokuwa na itikadi" hata kama msimamo huo ndio ule ule uliotuingiza kwenye matatizo in the first place. Hatuhitaji kufanya mabadiliko katika sera na mwelekeo wa idara hizo kwa sababu kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaonesha kutokuwa na umoja. Nimekupata.
 
Ninawasiwasi na mpendazote asijekuwa anatumikana CCM kuua upinzani kwani style yake aliyoingilia upinzani ni kama ya mrema. Sidhani kuwa katika mazingira ya kawaida anaweza mtz kuacha zaidi ya 40m kama kiinua mgongo CCM wana mbinu hivyo CHADEMA inabidi wawe makini kwa hili
 
MKJJ hujatuambia wakati unadandia treni hewa ya CCJ ulikuwa unadandia ili ikufikishe wapi, ina maana wakati huo hukuwa na busara hata kidogo ya kujiuliza maswali unayotuuliza leo.

MKJJ sitaki kukulinganisha na Mrema kuanza kunadadisi manifesto za vyama vingine kama huna interest na vyama hivyo kwa namna moja ama nyingine.

Kwa nini leo uanze kuuliza Long-term plans za vyama vingine wakati chenu kilishindwa kuwa hata na Short-term plan ya mwezi mmoja kukiwezesha kisajiliwe, kwanini hukuwapa CCJ ushauri huu kama ni mzuri unakuja kumpa jirani yako, amaizing me.

Inawezekana kabisa kutosajiliwa kwa CCJ kulichangiwa na mawazo yako naweza kuyaita potofu ya kuanza kupanga mipango ya siku 100 za mwanzo madarakani kabla ya kupanga mtaingiaje madarakani.
 
Wildcard,
Kenya is better off today without KANU. Licha ya mauaji ya 2007 ambayo yalikuwa inevitable anyway, Kenya is better off, much better off without KANU. Wametunga katiba mpya na August 4 inapita kwa asilimia zaidi ya 60. Hujajiuliza kwa nini watu kama Moi wanakampeni kupinga katiba hiyo? Wataunda tume mpya ya uchaguzi. Hiyo ni step foward. Sisi Bongo hata kuzungumzia katiba tu imekuwa nongwa. Na kuhusu tume ya uchaguzi ndiyo sisemi kabisa.
 
Mzee Mwanakijiji,
Unajua inakuwa taabu sana kwangu kuweza kufikiria unachofikiria wewe au hata hilo swali lako linalenga kitu gani haswa ikiwa unajibu kihuni na mkato.. najaribu sana kukusoma lakini sikupati kabisa..

Unapozungumzia Usalama wa Taifa (be specific) hili ni swala kubwa sana ambalo linaingia hadi kulinda Uhuru tulioupata, kwa maana hiyo inazungumzia toka Uhuru wa wananchi, ardhi, mahusiano ya kimataifa, Ulinzi wa ndani na nje na mengine mengi ambayo Katiba yetu ndio kioo. Kuna swala ktk katiba hukubaliani nao liweke wazi laa sivyo Chadema hawana sababu ya kuzungumzia usalama kinyume cha katiba..

Sasa basi unapozungumzia sera za Chadema kuhusiana na Usalama wa taifa inanipa shida kama unalenga kusema katiba ibadilishwe au unataka kuzijua ahadi za uongozi wa Chadema kuhusiana na Usalama wa taifa ktk kuuboresha au kuendeleza secta zilizokuwepo au ni sehemu zipi za katiba zinazokukwaza. kwa mfano unaweza kuwa una maanisha kuimarisha Jeshi letu la Taifa (JWTZ) na Polisi kwa kuwapa vifaa vya kisasa. hata hivyo nasikia JWTZ linavunjwa na kuwa Jeshi la Umoja wa nchi za Afrika ya Mashariki..

Hizi ni ahadi na wakati mwingine huziita ilani za mgombea na sidhani kama Chadema wapo katika position ya kuzungumzia zaidi watafanya nini ikiwa bado hawajapewa tuksa ya kujitangaza. Na hakika ikifika waklati huo wakisema watanunua ndege za kijeshi za kisasa Mig 29 arobaini tutawauliza watazinunua kwa fedha gani, ni sehemu gani ya matumizi ya serikali watayakata ili kutuwezesha kupata vifaa hivyo..

Laa sivyo tutakuwa tunazungumzia lkugha kama ya JK ambaye alituahidi vitu 10 kama alivyoorodhesha yeye ktk hotuba yake lakini maadam hatuna kipimo cha malengo imekuwa kila hatua moja ya makuzi imehesabika kama mafanikio. Kwa mfano JK kazungumzia jitihada za serikali kuanzisha TAKUKURU na kujisifia kwamba wameweza kuwafikisha mahakamani mahalifu mia saba na upuuzi na kati yao sijui 163 serikali imeshinda kesi tofauti na mwaka 2005 walipokuwa nakesi chache zaidi na walishinda sijui 50 tu..

Haya unaweza kuyaita mafanikio kwa mtazamo wa JK lakini kama nchi ina malengo, Kwa kila pungufu la waharifu na kesi mahakamani ndio huitwa mafanikio. Meaning ikiwa Ulinzi unafanya kazi yake vizuri, hizo kesi za uhalifu zinatakiwa kupungua..less crimes ndio mafanikio sio wingi wa waliokamatwa na kuhukumiwa ndio kunahesabiwa kuwa mafanikio.

Kwa hiyo kama unataka kujua Chadema watafanya nini tofauti na CCM ili kuhakikisha Ufisadi na Ujambazi unapungua nchini, wahalifu wote wanafikishwa mahakamani ili nao wajisifu kwa idadi ya kesi ambazo serikali imeshinda. Sidhani kama kwa mazingira yetu sera za chama zinaweza kukuhakikishia chochote isipokuwa mgombea wa kiti cha Urais ndiye atakuja na ahadi, kisha atapanga yeye jinsi ya kulishughulikia swala zima aiha kubadilisha mkuu wa Usalama na kumweka Mwanakijiji na kadhalika.

Nadhani kwa ufasaha wake, hili ni swala litakuja baadaye kwani hata huku sera za chama huzungumzia zaidi UCHUMI kwa kiwango kikubwa sana na ULINZI au Usalama wa Taifa ni swala nyeti sana ambalo hakuna hata mbunge mmoja anataka kuligusa bila sera hizo kuwa specific kw ADUI fulani.. laukama unalenga kusema Mafisadi ni adui zetu, nadhani Chadema wameisha sema wazi wala sii mara moja tena kwa majina yao watu hao wanatakiwa kufikishwa mahakamani.

Kama unakumbuka Dr.Slaa alisema wazi kwamba kumfikisha Mkapa mahakamani haiwezekani chini ya uongozi wa JK..Kina Lowassa, Karamagi na wengine woote imeshindikana kutokana na wabunge wachache wa upinzani bungeni..Lakini kikubwa zaidi mshika mpini JK anaweza kabisa kutoa amri na wakafikishwa mahakamani pasipo kamati ya bunge ya enquiry..

Na mwisho, kama kweli unalo la ziada kwanini usiwakilishe mawazo yakokama walivyofanya kina Mpendazoe ili nawe ushiriki ktk uchaguzi huu..kwani ni unafiki mkubwa kwa wale woote wanaomtukana Mpendazoe kujiunga na Chadema hali watu hawa hawa wanataka upinzani washike viti vingi bungeni kuleta mabadiliko. Haya tuseme Mpendazoe na wengine waliojiunga na Chadema wasijiunge na CCMichukue majimbo ambayo hawa watu wangeweza kabisa kushinda tutamlalamikia nani?

Kama ni ukubwa Mpendazoe alikuwa mkubwa CCM, hakuwa na sababu ya kuondoka CCM alipokuwa akila meza moja na JK, leo kajiunga na Chadema ili kuongeza nguvu Upinzani tayari kisha kuwa mwenye tamaa hali Mpendazoe hakujiunga CCJ kwa sababu CCJ ilikuwa na mwelekeo bora.. CCJ haikuwepo ila kivuli chao wenyewe, hivyo iliposhindikana kuweka upinzani na CCM kajiunga na team inayoweza kuweka Upinzani kwa vitendo na sio kuandika vitabu vya falsafa na itikadi kama kila Karl Max.

Mkuu kuna tofauti kubwa sana kati ya watu kama Mpendazoe na nyie waandishi, hivyo kama huwezi kujiunga isipokuwa kukaa pembeni na kukosoa hilo tunakupa pongezi na endelea kuandika tutakusoma na kujifunza..
 
Mkuu Mwanakijiji,

Hivi tukiweka maslahi ya taifa mbele,cha muhimu ni sera zinazosema "tutafanya A,B,C...X,Y,Z" au commitments za dhati kuona matatizo ya nchi yetu yanapungua kama si kumalizika?Kwa mana kama suala ni sera,mbona za CCM zimekuwa nzuri tangu tupate uhuru?Kwa mtizamo wangu wa mtaani,sera za chama ni kama mavazi na maandalizi mazuri ya harusi yanayosindikizwa na sherehe ya kufa mtu sambamba na hotuba za kutoa machozi kama si kuvunja mbavu.However,kinachodumisha ndoa si kimoja katika ya hivyo bali dhamira ya dhati ya wanandoa kuhakikisha wanafuata maadili,upendo na kujua thamani ya ndoa yao.Kadhalika,sera "nzuri" hazina tofauti na hayo niliyoyataja kuhusu maandalizi hayo ya ndoa.Ila kuzitafsiri sera hizo katika vitendo ni sawa na namna wanandoa wanavyoweza kuifanya ndoa yao kuwa ya furaha na mafanikio.

Nalazimika kutumia mifano hii ya mitaani ili kuleta mantiki.Hivi mkuu umeshaandika makala ngapi dhidi ya kila baya linaloendelea kufanywa na CCM.Je wakati unaandaa makala hizo,hujiulizi kuwa CCM wana sera,na kwamba,kwa upande mmoja,hawajali kutenda tofauti na sera hizo,na kwa upande mwingine,wanafahamu bayana kuwa katika mazingira tuliyonayo hata wakienda kinyume na sera walizoweka wenyewe hakuna madhara kwao na kwa maslahi yao.

Naomba kurejea kukumbusha tena.TATIZO LA MAENDELEO BARANI AFRIKA,NA PENGINE NCHI NYINGI ZA DUNIA YA TATU HALIJAWAHI KUWA KWENYE SERA MBOVU BALI UTEKELEZAJI.Sasa kama tukikubaliana kuwa tatizo halijawa kwenye sera,then umuhimu wa sera hizo katika kufikia maendeleo/kuleta mabadiliko ya kweli unatoka wapi?

Hebu rejea kwenye sera mbalimbali zilizoambatana na itikadi ya Ujamaa.Hivi si kweli kwamba nyingi,kama si zote,zililenga kundi kubwa la walalahoi lakini zikaacha mwanya kwa wajanja (isomeke mafisadi) kujitengenezea mazingira ya kusubiri Nyerere aondoke kisha waanze kutumia utajiri waliokuwa wakikusanya ktk kipindi tulichoaminishwa kuwa binadamu wote ni sawa?

Hivi kwa mtizamo wako unadhani kwanini Ujamaa ulishindwa?Je haikuwa itikadi nzuri?Je sera mbalimbali zilizoambatana na itikadi hiyo hazikuwa na malengo mazuri kwa Watanzania?

Chadema wanaweza kutueleza kuwa wakiingia madarakani wataifumua Idara ya Usalama wa Taifa,in and out.Until delivered,sera au ahadi hiyo itabaki kuwa ahadi kama hizo zinazoendelea kutolewa na JK.Cha muhimu ni utekelezaji.Kukurejesha tena mtaani,cha muhimu sio kutangaza dhamira ya kuoa bali cha muhimu ni kuoa...kwani kuna mafisadi kadhaa wa ngono wanaotangaza ndoa kwa mabinti kila mtaa lakini mabinti hao wanaishia kuachwa na mimba kama si kuambulia virusi vya ukimwi.Wanachofanya mafisadi hao wa ngono hakina tofauti na kinachofanywa na mafisadi wa CCM:kutoa sera na ahadi taaaamu lakini utekelezaji ni SIFURI,ZERO,ZILCH,NADA.

Tunaweza kusubiri CCJ ifanikiwe kuokoteza wanachama wake na kujipanga vizuri kisha wakatuletea kile ambacho hakuna chama kingine cha siasa kimeshawahi kufanya katika historia ya siasa za Tanzania.Tunaweza pia kusubiri hadi Chadema,CUF,na vyama vingine vya upinzani vitakapokuwa na sera za kuelweka ndipo tutoe wito wa CCM kung'olewa madarakani.Kadhalika,tunaweza kuiacha CCM madarakani kwa vile tu vyama vingine havina sera nzuri zinazotosheleza kuwa supported.However,wakati tunasubiri yote hayo,nchi yetu inazidi kuteketea.Kama "Dkt" Mzindakaya alivyotahadharisha,tunakoelekea si kuzuri.Tunaweza kusubiri sera njema na mbadala then wakati tukiwa tayari kuzi-apply tukajikuta tupo katika,God forbid,hali kama ya Somalia.And talking of Somalia,naamini Siad Barre nae alikuwa na sera nzuri pia lakini angalia leo Wasomali wako katika hali gani.
 
Kuweka CCM kambi ya upinzani ni lazima liwe lengo mama la CHADEMA. Inawezekana sana, kama ilivyowezekana Kenya na Zambia.

CCM na mama yake TANU wametutawala kwa miaka 50 sasa, bila kuweza kuleta maendeleo. Miaka mitano mingine itasaidia nini? Hakuna mabadiliko ya msingi Tanzania bila kubadilisha kwanza chama tawala.

Itasikitisha sana kama sherehe zetu za mwakani za kuadhimisha miaka 50 tangu tujinyakulie UHURU zitasimamiwa na watu watu wale wale waliotufikisha kwenye lindi tulilomo.

CHADEMA is our hope. Iwapokee wote wale watakaonyimwa na CCM kugombea ubunge. Isiwaite makapi ya CCM.
 
Mlalahoi,
Unajua ni vigumu sana kumwelewa huyu mkuu wetu Mwanakijiji hasa anapokuwa mpinzani wa mawazo yasiyokuwa sawa na yake. Nimeshindwa kumwelewa muda mrefu na nimejaribu kumwelewa lakini anapiga chenga kama za Messi za mguu mmoja wa shoto ambazo ukimjulia anakwenda wapi rahisi kumbana, tatizo ni hiyo mbio zake kuliko hata swala.

Alikuja na hilo la What Next - kwa sababu yeye anayaona matatizo yetu na anataka yakabiriwe na sera. lakini matatizo sio yanayotunga sera ila hutafutiwa ponya, ila Maendeleo ndio huwa zaidi ya ponya na ndio sera zinapotakiwa kufanya kazi.. Kama vile huko Marekani leo wanakabiriwa na kuvuja kwa mafuta ya BP, hili ni tatizo ambalo linataka ponya (suluhisho) na sio sera. Sasa itakuwa vigumu sana kumuuliza Obama atatumia sera gani kuhusiana na uvujaji au kumuuliza what next baada ya kudhibiti. Kwanza shughuli ni kuhakikisha mafuta hayavuji tena, kisha baada ya hapo umuhimu wa kuhakikisha vyanzo vya mafuta haviwezi kuvuja tena utatafutiwa ufumbuzi hatua kwa hatua.

Nadhani tatizo la mwanakijiji ni hawa Mafisadi ambao kama unakumbuka nilisema toka mwaka 2005 kwamba maendeleo ya Tanzania hayawezi kupatikana pasipo kudhibiti Ufisadi kwani uchumi wetu ulikuwa mzuri tu lakini ukikusanywa ktk pakacha lenye tobo na mirija ikinyonya kila ujazo..na kulingana na fikra zake kaona hakuna dawa isipokuiwa ku declare upya siasa ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA kama dira ya Taifa na kurudisha hadhi ile ya mwalimu.

Haya ni mawazo yake yeye na hao wana CCJ na tunayaheshimu, ila hata mimi mpenzi wa mwalimu sikubaliani na hizi hadithi za UJAMAA na KUJITEGEMEA, Sikubaliani na kurudisha AZIMIO LA ARUSHA isipokuwa kurekebisha makosa yatokanayo na hali tuliyopo. Kama vile tulivyokosea mwanzo kuingia Ubepari tulitakiwa kurekebisha Azimio la Arusha kulingana na wakati huo Kiuchumi na sio maamuzi ya Zanzibar kutoa RUKSA isiyohusiana na failure za Ujamaa.

RUKSA was a big mistake kwa sababu ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo leo..meaning matatizo ya Ujamaa kushindwa kutuletea maendeleo kulitafutiwa dawa hiyo ya RUKSA na imeshindwa kufanya kazi.. So What next? (maneno ya MMKJ) Huwezi kuivunja RUKSA kwa kurudia makosa ya mwanzo (Azimio la Arusha) ambalo pia kwa miaka 20 na upuuzi iliishindwa kufanya kazi.

Kama vile Malaria unapojaribu kuitibu unachukua dawa moja ikishindwa, inachukuliwa ya pili nayo ikishindikana unakwenda hatua ya tatu kutafuta dawa nyingine..Hivyo maadam mafisadi ni mavuno ya Ruksa kuna kila sababu ya 1. Kuwang'oa Mafisadi na mirija yao, 2. Kuziba tobo zote za mirija inayotunyonya, na mwisho kuondoa RUKSA ambayo ndio imezaa mafisadi. Hatua kwa hatua kama mwanzo..

Na hatuwezi kufikiria kuondoa ghafla RUKSA kwa sababu tu imeshindwa na imezaa mafisadi wengi zaidi, ila kinachotakiwa ni kutazama kwa nini Ruksa failed us kama tulivyotakiwa kuutazama Ujamaa na Kujitegemea, tutatazama loopholes zilizopo na kuzidhibiti na nina hakika kabisa miiko na maadili ya viongozi toka Azimio la Arusha ndio solution (mawazo yangu binafsi).

Wengi wanapinga sana kuwawekea vikwazo viongozi wa serikali kutotajirika lakini wanashindwa kuelewa kwamba hakuna sababu ya kuruhusu Utajiri wa viongozi au mtu yeyote yule kwa kupitia Ufisadi na kibaya zaidi viongozi wetu ndio wao majemedali wavita hii ya kuondoa Umaskini., uiweje wao wafikirie haki ya Utajiri hali taifa zima linapigana kuondokana na Umaskini?..Ni haki kwa nahodha kuwa wa kwanza kurukia ndani ya boti la kuokoameli inapozama?..sidhani na ndicho Mwinyi alichotupa. Meli yetu Tanzania ilikuwa ikizama, na RUKSA ikatoka kila mtu na msalaba wake..

For the last 20 years mingine sisi wote tumekuwa ktk hali ya kunyang'anyana maboya na kurukia ndani ya boti za kuokoa bila kujua kwamba boti hizo zina uwezo wa kuchukua abiria wachache tu. na kibaya zaidi viongozi wetu wakitumia wadhifa wao wamekuwa wa kwanza kuingia ktk boti hizo.. Yet, watanzania bado wanafikira au wana matumaini ya kuokolewa na manahodha ambao tayari wao wameisha okoa maisha yao...

Ni wakati wa viongozi kubeba uzito wa mzigo huu wa umaskini na njia pekee ni kuwavika magwanda na wao kuwa mstari wa mbele kupambana na maadui zetu..Utajiri haupatikani vitani isipokuwa kwa dhulma au wizi, na inapotosha malengo yaliyokusudiwa.

Nadhani hapa naiona wasiwasi ya Mwanakijiji kuhofia Chadema au viongozi wake kununuliwa au kutoweza kuwathibiti hawa Mafisadi. Na kama wataweza je Chadema wamejiandaa vipi kuhusu Usalama wa Taifa ambao CCM wamekuwa wakitishia kwamba bila wao hakuna usalama..
 
MKJJ hujatuambia wakati unadandia treni hewa ya CCJ ulikuwa unadandia ili ikufikishe wapi, ina maana wakati huo hukuwa na busara hata kidogo ya kujiuliza maswali unayotuuliza leo.

MKJJ sitaki kukulinganisha na Mrema kuanza kunadadisi manifesto za vyama vingine kama huna interest na vyama hivyo kwa namna moja ama nyingine.

Kwa nini leo uanze kuuliza Long-term plans za vyama vingine wakati chenu kilishindwa kuwa hata na Short-term plan ya mwezi mmoja kukiwezesha kisajiliwe, kwanini hukuwapa CCJ ushauri huu kama ni mzuri unakuja kumpa jirani yako, amaizing me.

Inawezekana kabisa kutosajiliwa kwa CCJ kulichangiwa na mawazo yako naweza kuyaita potofu ya kuanza kupanga mipango ya siku 100 za mwanzo madarakani kabla ya kupanga mtaingiaje madarakani.

Hivi kweli unaamini moyoni mwako nimeanza kuuliza ya Chadema "leo"? kwamba ni baada ya kushindwa kwa CCJ kupata usajili ndiyo mara moja nimeanza kufikiria kuuliza kuhusu ya Chadema? really..? labda uwe umeanza kunisoma hivi karibuni.
 
Mzee Mwanakijiji,
Unajua inakuwa taabu sana kwangu kuweza kufikiria unachofikiria wewe au hata hilo swali lako linalenga kitu gani haswa ikiwa unajibu kihuni na mkato.. najaribu sana kukusoma lakini sikupati kabisa..

mzee hayo ndiyo majibu yako wewe; na hayafurahishi hata kidogo. Majibu yako aidha yako kwenye dini, mambo ya mke na mume au mashambulizi mepesi tu ya mtu. Labda uchukue muda kusoma unavyonijibu na uone kama majibu yako siyo ya kihuni na ya mkato.
 
Mkuu Mwanakijiji,

Hivi tukiweka maslahi ya taifa mbele,cha muhimu ni sera zinazosema "tutafanya A,B,C...X,Y,Z" au commitments za dhati kuona matatizo ya nchi yetu yanapungua kama si kumalizika?

Hii commitment ya dhati wewe unaijuaje?

Kwa mana kama suala ni sera,mbona za CCM zimekuwa nzuri tangu tupate uhuru?Kwa mtizamo wangu wa mtaani,sera za chama ni kama mavazi na maandalizi mazuri ya harusi yanayosindikizwa na sherehe ya kufa mtu sambamba na hotuba za kutoa machozi kama si kuvunja mbavu.However,kinachodumisha ndoa si kimoja katika ya hivyo bali dhamira ya dhati ya wanandoa kuhakikisha wanafuata maadili,upendo na kujua thamani ya ndoa yao.

Hiyo "dhamira ya dhati" kwa wanandoa unaiona vipi? Si inaanzia na kwenye "Ndiyo nataka".. baada ya kuulizwa "Je wewe x,y unakubali kumchukua".. au ndiyo mnasema tu tutajua mbele ya safari hiyo commitment?
Kadhalika,sera "nzuri" hazina tofauti na hayo niliyoyataja kuhusu maandalizi hayo ya ndoa.Ila kuzitafsiri sera hizo katika vitendo ni sawa na namna wanandoa wanavyoweza kuifanya ndoa yao kuwa ya furaha na mafanikio.

Hebu nipe msingi wa kuamini kuwa Chadema ilivyo sasa itatafsiri hizo ahadi kwa vitendo. Ni kitu gani kinakufanya uamini hivi? Usinielewe vibaya, sisemi kwamba hawawezi au hawatofanya, ninachosema msingi wa imani hiyo ni nini?

Nalazimika kutumia mifano hii ya mitaani ili kuleta mantiki.

Mifano yako ni mibaya kwa kweli japo inaweza kuvutia fikra nyepesi nyepesi.

Hivi mkuu umeshaandika makala ngapi dhidi ya kila baya linaloendelea kufanywa na CCM.Je wakati unaandaa makala hizo,hujiulizi kuwa CCM wana sera,na kwamba,kwa upande mmoja,hawajali kutenda tofauti na sera hizo,na kwa upande mwingine,wanafahamu bayana kuwa katika mazingira tuliyonayo hata wakienda kinyume na sera walizoweka wenyewe hakuna madhara kwao na kwa maslahi yao.

Nimeandika nyingi sana na ninaamini CCM watafanyia kazi mapema zaidi kuliko ndugu zetu wa upinzani.

Naomba kurejea kukumbusha tena.TATIZO LA MAENDELEO BARANI AFRIKA,NA PENGINE NCHI NYINGI ZA DUNIA YA TATU HALIJAWAHI KUWA KWENYE SERA MBOVU BALI UTEKELEZAJI.

Unaweza ukafikiria tatizo ni utekelezaji, lakini kuna tatizo kubwa zaidi linalofanya utekelezaji uwe mgumu. Fikiria kwa sekunde chache tu unaweza kufahamu.

Sasa kama tukikubaliana kuwa tatizo halijawa kwenye sera,then umuhimu wa sera hizo katika kufikia maendeleo/kuleta mabadiliko ya kweli unatoka wapi?

Well, tatizo liko kwenye sera vile vile. CCM haina nzuri kama wengi wanavyoamini. Ni mojawapo ya sera mbaya kabisa hasa katika miaka hii 20 iliyopita. Wakati wengine wanaamini kuwa CCM ina sera nzuri "vitabuni" mimi siamini hivyo kwani nimezisoma na kwa kweli hazitofautini kabisa na za Chadema. Sijui kama umepata nafasi ya kumsikiliza Kikwete leo.

Hivi kwa mtizamo wako unadhani kwanini Ujamaa ulishindwa?

Ujamaa haukushindwa, haukujaribiwa ipasavyo. Ndiyo maana leo nchi zenye kufuata ujamaa (hata kwa jina jingine) zinazidi kuongezeka!

Je haikuwa itikadi nzuri?Je sera mbalimbali zilizoambatana na itikadi hiyo hazikuwa na malengo mazuri kwa Watanzania?

Chadema wanaweza kutueleza kuwa wakiingia madarakani wataifumua Idara ya Usalama wa Taifa,in and out.Until delivered,sera au ahadi hiyo itabaki kuwa ahadi kama hizo zinazoendelea kutolewa na JK.Cha muhimu ni utekelezaji.Kukurejesha tena mtaani,cha muhimu sio kutangaza dhamira ya kuoa bali cha muhimu ni kuoa...kwani kuna mafisadi kadhaa wa ngono wanaotangaza ndoa kwa mabinti kila mtaa lakini mabinti hao wanaishia kuachwa na mimba kama si kuambulia virusi vya ukimwi.Wanachofanya mafisadi hao wa ngono hakina tofauti na kinachofanywa na mafisadi wa CCM:kutoa sera na ahadi taaaamu lakini utekelezaji ni SIFURI,ZERO,ZILCH,NADA.

Ninachosikia ni kuwa "twende tu" hata kama hakuna sera, hakuna ahadi, hakuna kipiimo twende tu tufuate jina!.. really? I'm still sane, at least the last time I checked.

Tunaweza kusubiri CCJ ifanikiwe kuokoteza wanachama wake na kujipanga vizuri kisha wakatuletea kile ambacho hakuna chama kingine cha siasa kimeshawahi kufanya katika historia ya siasa za Tanzania.Tunaweza pia kusubiri hadi Chadema,CUF,na vyama vingine vya upinzani vitakapokuwa na sera za kuelweka ndipo tutoe wito wa CCM kung'olewa madarakani.Kadhalika,tunaweza kuiacha CCM madarakani kwa vile tu vyama vingine havina sera nzuri zinazotosheleza kuwa supported.However,wakati tunasubiri yote hayo,nchi yetu inazidi kuteketea.Kama "Dkt" Mzindakaya alivyotahadharisha,tunakoelekea si kuzuri.Tunaweza kusubiri sera njema na mbadala then wakati tukiwa tayari kuzi-apply tukajikuta tupo katika,God forbid,hali kama ya Somalia.And talking of Somalia,naamini Siad Barre nae alikuwa na sera nzuri pia lakini angalia leo Wasomali wako katika hali gani.

well, hakuna sababu ya kusubiri kwa kweli, nimeandika toka mwanzo, mwaka huu huu Chadema ikitaka kushika madaraka ya nchi 'INAWEZA'. Lakini hadi hivi sasa imethibitisha kuwa haitaki. Inaombea.
 
Mlalahoi,
Unajua ni vigumu sana kumwelewa huyu mkuu wetu Mwanakijiji hasa anapokuwa mpinzani wa mawazo yasiyokuwa sawa na yake. Nimeshindwa kumwelewa muda mrefu na nimejaribu kumwelewa lakini anapiga chenga kama za Messi za mguu mmoja wa shoto ambazo ukimjulia anakwenda wapi rahisi kumbana, tatizo ni hiyo mbio zake kuliko hata swala.

Alikuja na hilo la What Next - kwa sababu yeye anayaona matatizo yetu na anataka yakabiriwe na sera. lakini matatizo sio yanayotunga sera ila hutafutiwa ponya, ila Maendeleo ndio huwa zaidi ya ponya na ndio sera zinapotakiwa kufanya kazi.. Kama vile huko Marekani leo wanakabiriwa na kuvuja kwa mafuta ya BP, hili ni tatizo ambalo linataka ponya (suluhisho) na sio sera. Sasa itakuwa vigumu sana kumuuliza Obama atatumia sera gani kuhusiana na uvujaji au kumuuliza what next baada ya kudhibiti. Kwanza shughuli ni kuhakikisha mafuta hayavuji tena, kisha baada ya hapo umuhimu wa kuhakikisha vyanzo vya mafuta haviwezi kuvuja tena utatafutiwa ufumbuzi hatua kwa hatua.

Nadhani tatizo la mwanakijiji ni hawa Mafisadi ambao kama unakumbuka nilisema toka mwaka 2005 kwamba maendeleo ya Tanzania hayawezi kupatikana pasipo kudhibiti Ufisadi kwani uchumi wetu ulikuwa mzuri tu lakini ukikusanywa ktk pakacha lenye tobo na mirija ikinyonya kila ujazo..na kulingana na fikra zake kaona hakuna dawa isipokuiwa ku declare upya siasa ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA kama dira ya Taifa na kurudisha hadhi ile ya mwalimu.

Haya ni mawazo yake yeye na hao wana CCJ na tunayaheshimu, ila hata mimi mpenzi wa mwalimu sikubaliani na hizi hadithi za UJAMAA na KUJITEGEMEA, Sikubaliani na kurudisha AZIMIO LA ARUSHA isipokuwa kurekebisha makosa yatokanayo na hali tuliyopo. Kama vile tulivyokosea mwanzo kuingia Ubepari tulitakiwa kurekebisha Azimio la Arusha kulingana na wakati huo Kiuchumi na sio maamuzi ya Zanzibar kutoa RUKSA isiyohusiana na failure za Ujamaa.

RUKSA was a big mistake kwa sababu ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo leo..meaning matatizo ya Ujamaa kushindwa kutuletea maendeleo kulitafutiwa dawa hiyo ya RUKSA na imeshindwa kufanya kazi.. So What next? (maneno ya MMKJ) Huwezi kuivunja RUKSA kwa kurudia makosa ya mwanzo (Azimio la Arusha) ambalo pia kwa miaka 20 na upuuzi iliishindwa kufanya kazi.

Kama vile Malaria unapojaribu kuitibu unachukua dawa moja ikishindwa, inachukuliwa ya pili nayo ikishindikana unakwenda hatua ya tatu kutafuta dawa nyingine..Hivyo maadam mafisadi ni mavuno ya Ruksa kuna kila sababu ya 1. Kuwang'oa Mafisadi na mirija yao, 2. Kuziba tobo zote za mirija inayotunyonya, na mwisho kuondoa RUKSA ambayo ndio imezaa mafisadi. Hatua kwa hatua kama mwanzo..

Na hatuwezi kufikiria kuondoa ghafla RUKSA kwa sababu tu imeshindwa na imezaa mafisadi wengi zaidi, ila kinachotakiwa ni kutazama kwa nini Ruksa failed us kama tulivyotakiwa kuutazama Ujamaa na Kujitegemea, tutatazama loopholes zilizopo na kuzidhibiti na nina hakika kabisa miiko na maadili ya viongozi toka Azimio la Arusha ndio solution (mawazo yangu binafsi).

Wengi wanapinga sana kuwawekea vikwazo viongozi wa serikali kutotajirika lakini wanashindwa kuelewa kwamba hakuna sababu ya kuruhusu Utajiri wa viongozi au mtu yeyote yule kwa kupitia Ufisadi na kibaya zaidi viongozi wetu ndio wao majemedali wavita hii ya kuondoa Umaskini., uiweje wao wafikirie haki ya Utajiri hali taifa zima linapigana kuondokana na Umaskini?..Ni haki kwa nahodha kuwa wa kwanza kurukia ndani ya boti la kuokoameli inapozama?..sidhani na ndicho Mwinyi alichotupa. Meli yetu Tanzania ilikuwa ikizama, na RUKSA ikatoka kila mtu na msalaba wake..

For the last 20 years mingine sisi wote tumekuwa ktk hali ya kunyang'anyana maboya na kurukia ndani ya boti za kuokoa bila kujua kwamba boti hizo zina uwezo wa kuchukua abiria wachache tu. na kibaya zaidi viongozi wetu wakitumia wadhifa wao wamekuwa wa kwanza kuingia ktk boti hizo.. Yet, watanzania bado wanafikira au wana matumaini ya kuokolewa na manahodha ambao tayari wao wameisha okoa maisha yao...

Ni wakati wa viongozi kubeba uzito wa mzigo huu wa umaskini na njia pekee ni kuwavika magwanda na wao kuwa mstari wa mbele kupambana na maadui zetu..Utajiri haupatikani vitani isipokuwa kwa dhulma au wizi, na inapotosha malengo yaliyokusudiwa.

Nadhani hapa naiona wasiwasi ya Mwanakijiji kuhofia Chadema au viongozi wake kununuliwa au kutoweza kuwathibiti hawa Mafisadi. Na kama wataweza je Chadema wamejiandaa vipi kuhusu Usalama wa Taifa ambao CCM wamekuwa wakitishia kwamba bila wao hakuna usalama..

there you are!!! umeanza kunigusa.. taratibu unaanza kuja ninakoamini unaweza kuja. I'm waiting.
 
Mzee Mwanakijiji,
Sawa tumekusikia, na hakika najua upo hapo Marekani miaka mingi sana. Ebu tueleze wewe sera za Domokratic ktk Usalama wa Taifa tofauti na sera za Republican ambazo wananchi walizikubali.

Au tupe sera za vyama vya UK au nchi yeyote kwa tofauti ya vyama utanisaidia sana kuona vitu ambavyo sikuwahi kuvifikiria kwamba wananchi walitakiwa kuvifahamu kabla hawajaunga mkono utawla unaofuata..

Nijuavyo mimi Usalama wa Taifa ni dira ya kitaifa haihusiani kabisa na siasa za chama.. Watanzania wote na tofauti zetu za kiitikadi inapofikia swala la Usalama wa Taifa tunazitua tofauti zetu na kuchukua msimamo mmoja usiokuwa na itikadi.
Asante sana Mkandara asante.
 
Wildcard,
Kenya is better off today without KANU. Licha ya mauaji ya 2007 ambayo yalikuwa inevitable anyway, Kenya is better off, much better off without KANU. Wametunga katiba mpya na August 4 inapita kwa asilimia zaidi ya 60. Hujajiuliza kwa nini watu kama Moi wanakampeni kupinga katiba hiyo? Wataunda tume mpya ya uchaguzi. Hiyo ni step foward. Sisi Bongo hata kuzungumzia katiba tu imekuwa nongwa. Na kuhusu tume ya uchaguzi ndiyo sisemi kabisa.
Jasusi labda niongeze kusema tukwamba hata zile vurugu za 2007 ni matunda yaliyovunwa kwenye shamba la KANU
 
Kuweka CCM kambi ya upinzani ni lazima liwe lengo mama la CHADEMA. Inawezekana sana, kama ilivyowezekana Kenya na Zambia.

CCM na mama yake TANU wametutawala kwa miaka 50 sasa, bila kuweza kuleta maendeleo. Miaka mitano mingine itasaidia nini? Hakuna mabadiliko ya msingi Tanzania bila kubadilisha kwanza chama tawala.

Itasikitisha sana kama sherehe zetu za mwakani za kuadhimisha miaka 50 tangu tujinyakulie UHURU zitasimamiwa na watu watu wale wale waliotufikisha kwenye lindi tulilomo.

CHADEMA is our hope. Iwapokee wote wale watakaonyimwa na CCM kugombea ubunge. Isiwaite makapi ya CCM.

Teh teh teh
Mtaalam PWEZA PAULO ameshaitabilia CCM ushindi wa kishindo.
 
Mjadala ni kuunga mkono chadema kwa sasa. Tumekwamia kwenye MMJ vs Others katika hilo. Tukubali kutofautiana. Ila for sure Tanzania inahitaji kuwa na upinzani ulio imarika na ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa hilo linatokea. CCM haiwezi kubadirika yenyewe, imeshafika a point of no return. Kwa hali waliomo sasa ile kanuni ya kwanza ya mwendo ya newton inatumika. Kwa kujua au bila kujua treni ya CCM imesha-derail na hakuna utaalm wa dreva aliyemo mle ndani atakeyekuwa na uwezo wa kuigeuza, ni watu walioko nje tu, wewe na mimi tunaoweza kuibadirisha kwa kuiwekea kigingi au kitu chochote kitafachofanya ipunguze kasi ya kurudi nyuma na hatimaye isimame. Itengenezwe ili hatimaye ianze kuelekea mbele.

CCM haiwezi kujirekebisha kwa hali yao ya sasa. Lazima nguvu ya kuwarekebisha itoke nje yao. Bila hivyo, hatimaye wataanguka na kuiangusha nchi pamoja nao. Tutakuwa tumefanya makosa makubwa sana tukiwaachia waanguke wenyewe. Hawataanguka vizuri. Wataiangusha na nchi yote pamoja nao kama vile kuanguka kwa Siad Bare kulivyoiangusha Somalia.

Kusimamisha upinzani wenye nguvu na uwezo wa kuchukua Dola ndo njia pekee ya kuisaidia CCM na kuisaidia nchi. CCM itapoona upinzani wenye nguvu unaipumulia mabegani kwa karibu sana ndo ama wataweza kujirekebisha. Vinginevyo upinzani uingie madarakani kabisa wajifanyie marekebisho wakiwa nje ya madaraka kwa matumaini ya kurudi tena. Ikiwa suala la kuwa na upinzani wenye nguvu si la mjadala tena kuna uwezekano tukashindana sana ni nani ni upinzani sahihi.

Mimi napendekeza wapenda mabadiriko wote angalau waangalie ishara na mwelekeo halafu waunganishe nguvu zao kule. Chadema si bora sana. Ila ukiangalia kule kwenye upinzani angalau wanaonesha uhai. Je si wakati muafaka wa nguvu zetu wote kuzielekeza kule? Hata kama hatuna uhakika kule wanakokwenda, lakini kwa pale walipo, Chadema ndo chama ambacho kuna uwezekano bado wa kukiongezea fikra na nguvu. Ingawa hata Chadema inaanza kujenga inertia, lakini bado kina uwezekano mkubwa zaidi wa kupokea mawazo mapya. Si lazima tujiunge nacho, ila tunaweza kipa material na moral support kama alivyofanya mzee Sabodo. Kuna uwezekano bado wa kukibadili kwa sababu kwanza kiko nje ya madaraka na mawazo mapya yana nafasi pale.

CCM haiwezi kamwe kujirekebisha yenyewe bila kuwepo na upinzani imara wenye nguvu. Hii inertia ya CCM haitwaweza kuondolewa na CCM yenyewe.
 
Sasa mkuu, kama ulikuwa unapata updates, I assume you (CCJ) laid down your terms... kama hivi ndivyo didn't you gave them what you believe to be fundamental to be done before joining forces? Haya masuala ya sera si ndo ingekuwa wakati muafaka wa kuwaonyesha wapi wanakosea au wanpatia, ili kutengeneza CHADEMA strong with CCJ? Mkuu kama kweli mko na startegy ambazo unasema wao (CHADEMA) wakitumia wanaweza kushinda kwa kishindo, kwa nini msikubaliane ali mradi kufanya strong side to challenge green & yellow!!!

Ndo maana mkuu tunaona uko hapa kuvunja moyo/kuwauwa wanaojitahidi ku-challenge CCM!!!

Tutafika kweli!!! Au mlitaka lazima muwe CCJ....!!! Huu si ubinfsi mkuu?
 
Back
Top Bottom