Yah: Kuunga mkono CHADEMA kwa sasa

Yah: Kuunga mkono CHADEMA kwa sasa

mzee hayo ndiyo majibu yako wewe; na hayafurahishi hata kidogo. Majibu yako aidha yako kwenye dini, mambo ya mke na mume au mashambulizi mepesi tu ya mtu. Labda uchukue muda kusoma unavyonijibu na uone kama majibu yako siyo ya kihuni na ya mkato.
Duh! yamekuwa hayo tena... napotumia dini au mme/mke ni kutoa mifano ambayo ipo karibu na maisha ya wasomaji wengi..Haihusu kabisa.
Situmii uhuni hata chembe pengine mwenzangu hata hili neno la kihuni unalichukulia tofauti. Majibu ya mkato, swali linalojibiwa na swali, ndio uhuni wa lugha mengineyo mkuu hatutaelewana..
Pengine itakuwa vizuri sana nikiachia hapa maanake naona mkuu wangu una lako jambo!
 
aah hapana bwana.. tuendelee nilikuwa natoa mawazo yangu tu maana na miye nilifikiria una lako jambo. Kumbe ni tafsiri mbaya tu.. na uzee wenyewe huu.
 
aah hapana bwana.. tuendelee nilikuwa natoa mawazo yangu tu maana na miye nilifikiria una lako jambo. Kumbe ni tafsiri mbaya tu.. na uzee wenyewe huu.
Laa mwenzangu hutumia mifano ya Ka inzi, sungura, tetere na tunakuelewa ingekuwa tunachukulia mambo hiyvo basi kazi mpya!
 
WanaJF,

Kwa muda nimekosa kuchangia ndani ya jukwaa hili, hata hivyo nimevutwa na mjadala huu unaondelea kuandika machache. Yapo makundi makubwa mawili ya mawazo katika michango mbalimbali inayotolewa; upande mmoja ni wale wanaojenga hoja kwamba jambo la msingi la kwanza kabisa ni KUINDOA CCM MADARAKANI na mengine yatafuata; kundi la pili ni lile linalotaka kwanza MBADALA WA CCM UONEKANE BAYANA KWANZA na ndio iwe sababu na msingi wa kuiondoa CCM madarakani. Kundi hili linataka swali la nini kinafuata baada ya kuiondoa CCM madarakani litangulie kabla ya uamuzi wa kuindoa CCM madarakani. Kwa maoni yangu, nakubaliana na wenye mtizamo kwamba mambo yote haya mawili yanapaswa kwenda sambamba ama kwa pamoja; yote ni muhimu na yote yanahitajiana.

Kwa hatua ambayo nchi yetu imekifikia hivi sasa ya dola kutekwa (state capture) na chama kinachotawala kufunga fungate na ufisadi/mafisadi ni dhamira yoyote ya kuleta sera na uongozi mbadala haiwezi kutimia bila kubadili mfumo wa utawala. Utatu uliopo baina ya watendaji wa serikali kwa upande mmoja, wanasiasa viongozi wa kuchaguliwa na wananchi na viongozi wa chama kwa upande mwingine na maslahi ya kibiashara ya ndani na nje ya nchi kwa upande wa tatu; mkazo wowote wa kufikiria sera unakuwa ni mchezo wa kinadharia kama hautaenda sambamba na kubadili mfumo wa utawala labda kama kubadili huko mfumo wa utawala kuwe ndio sera yenyewe.

Katika hali iliyofikia sasa kuiondoa CCM madarakani ambayo ni sawa na kuikomboa dola iliyotekwa kunaonekana kuwa ni suala la lazima na la dharura kwa ajili ya demokrasia, maendeleo na hata kudumisha usalama na amani ya nchi ambayo inaelekea kuwa mashakani siku za usoni kama hali itaendelea kama ilivyo sasa.

Lakini katika kutekeleza azma hii, vipo vyama vimeonyesha uthabiti na uthubutu wa kuwa mbadala, CHADEMA ikiwa moja ya tumaini jipya la watanzania ndio maana naamini mjadala huu umejikita katika chama tajwa. Unaweza kujiuliza kwanini katika msururu wa vyama kumi na nane (18) vya Tanzania, mabadiliko ya kweli yaonekane yanaweza kupatikana kupitia CHADEMA?

Harakakati za kisiasa zilizofanywa na CHADEMA ndani na nje ya Bunge kwa kushirikiana na vyombo vya habari na wadau wengine waliokubali kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa zimesalisha AJENDA ya kisiasa-ambayo imepewa jina la ‘mapambano dhidi ya ufisadi na kutetea rasilimali za taifa’ ambayo yamefanya uwajibikaji katika utawala kutazamwa kama moja ya sera za muhimu sana za taifa letu.

Naamini jambo hili lisingepata mafanikio ya kutosha kama CHADEMA kwa upande wake isingekuwa na misingi mizuri ya uongozi na ya kisera tangu kuasisiwa kwake. Kama falsafa, itikadi na sera za CHADEMA zingekuwa kinyume sana na matarajio tunayoyatazamia harakati hizi za miaka ya karibuni zingeonekana kama kiini macho ama upepo wa wakati.

(Falsafa, itikadi na malengo ya chama yanaweza kutazamwa kupitia katiba ya chama ambayo inapatikana pia katika mtandao www.chadema.or.tz, pia katika mtandao huo inapatikana ilani fupi(popular version) ya CHADEMA ya mwaka 2005)

Hata hivyo katika nchi yenye uoza katika utawala kwa kiwango cha Tanzania taasisi zake nyingi huru- si CHADEMA tu, hujikuta katika hali ya kupinga uozo iliopo na kukosoa badala ya kutumia muda mwingi zaidi katika kueleza mbadala na kutoa matumaini. Huu ni mtego wa kawaida kwa silika ya binadamu na ubinadamu na taasisi zake; huwezi kwenda eneo lenye rundo la takataka kubwa kuliko usafi uliopo ukazungumza usafi kabla ya kuzungumzia kuondoa uchafu. Katika mazingira hayo unaweza kujikuta unazungumzia kuliondoa rundo la taka kabla hata ya kufikiria utafanya nini mbadala baada ya kuliondoa.

Lakini maelezo haya hayaondoi wala kupinga umuhimu wa swali la msingi lililoulizwa; kwamba CHADEMA ITAFANYA NINI IKIINGIA MADARAKANI ama NINI TAIFA LITARAJIE KUTOKANA NA MABADILIKO YA MFUMO WA UTAWALA?

Jibu la muda mrefu la swali hili linapatikana katika misingi ya muda mrefu ya kifalsafa, kiitikadi, kisera, kimalengo na kitaasisi ya CHADEMA. Je, misingi hii haitoi tumaini kwa watanzania na dira ya mabadiliko ya kweli? Ni maeneo gani yanayohitaji kuboreshwa zaidi? Hapa ni muhimu badala ya viongozi wa CHADEMA kujibu, mawazo yangetoka kwanza kwa wanachama na wananchi kwa ujumla. Naamini viongozi wa CHADEMA wapo tayari kusikiliza.

Jibu la muda mfupi linapatikana katika ilani ya uchaguzi (2010-2015) ambayo kutokana na misingi ya muda mrefu na hali ya taifa ya sasa inapaswa kutolewa; jibu ya swali hili kwa maoni yangu hawawezi kulitoa kwa ukamilifu wake leo kwa kuwa chama bado hakijazindua ilani yake ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Chama kiko kwenye mchakato wa majadiliano na mashauriano ya ndani (consultations), kabla ya kupata maoni ya nje na kabla ya kupitisha ilani katika vikao vya kikatiba vya chama ambavyo ni kamati kuu, baraza kuu na mkutano mkuu.

Hivyo, chama kiko wazi kupokea maoni kuhusu nini ambacho wanachama na wananchi kwa ujumla wangependa kitiliwe mkazo katika ilani ya CHADEMA. Hivyo, nawaomba wote ambao mngependa kushiriki katika kupanga CHADEMA IFANYE NINI IKIINGIA KWENYE UONGOZI au TAIFA LITARAJIE NINI KUTOKANA NA MABADILIKO YA MFUMO WA UTAWALA mtuandikie; unaweza kuandika kupitia info@chadema.or.tz, nakala kwa slaa@chadema.or.tz na mnyika@chadema.or.tz ama unaweza kumtumia kiongozi mwingine wa CHADEMA.

Kwa tafsiri rahisi, chama cha siasa ni jumuia ya watu wenye dhamira inayoendana wenye kulenga kuchukua mamlaka ya dola kupitia uchaguzi ama njia nyingine za kidemokrasia kwa lengo la kuitekeleza azma hiyo. Kwa hiyo badala ya kuhoji tu, CHADEMA itafanyaje ama taifa litarajie nini ni muhimu kushiriki katika kuamua hatma yako na ya taifa kwa ujumla. Badala ya kusubiri chama kutoa ilani na baadaye kuikosoa ama kuikana ni muhimu kushiriki katika kuiandika.

Nitaomba kwa kadiri inavyowezekana mawazo ya awali ya ujumla yafike kabla ya tarehe 20 Julai 2010. Mawazo mahususi yanaweza kutolewa katika hatua za baadaye kwenye rasimu kabla ya mkutano mkuu wa chama ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti. Hata hivyo, kuna mtanziko(dilemma) katika mchakato wa utengenezaji wa ilani kwa kuwa kwa upande mmoja unaweza kuwa na shauku ya kumhusisha kila mtu/mwanachama katika hatua zote lakini kwa upande mwingine unataka baadhi ya mambo katika ilani yawe siri hususani yale yenye ubunifu wa pekee ili yazinduliwe wakati wa kampeni au wakati wa karibu na uchaguzi kuweza kumsha hamasa ya kuungwa mkono; changamoto ipo katika kuwianisha(balancing) matakwa hayo mawili. Najua vipo vyama ambavyo vimeshazindua ilani zao, CHADEMA itafanya hivyo kwa kadiri ya ratiba yake ambayo ilishaitangaza toka Aprili 27 mwaka huu. Nawatakia mjadala mwema

JJ
 
Mzee Mwanakijiji;991260]Hii commitment ya dhati wewe unaijuaje?

Mkuu,list of shame,kufukua EPA na skandali nyingine bado haitoshi kuonyesha angalau Chadema wamekwenda mbali zaidi ya kutoa maneno pasipo vitendo?Na pengine,kama wasemavyo Waingereza,the answer is in the question.Kwani wewe commitment ya dhati ya CCJ wewe uliionaje?

Hiyo "dhamira ya dhati" kwa wanandoa unaiona vipi? Si inaanzia na kwenye "Ndiyo nataka".. baada ya kuulizwa "Je wewe x,y unakubali kumchukua".. au ndiyo mnasema tu tutajua mbele ya safari hiyo commitment?

Ofkoz,Chadema wameshatuonyesha wanataka kukomesha ufisadi kwa kuwatangaza mafisadi hadharani,kisha mafisadi wakatusaidia kuthibithisha tuhuma hizo kwa kutishia kwenda mahakamani lakini hakuna mmoja wao aliyefanya hivyo.Kwahiyo,kama ni "ndiyo nataka..." mifano ni lukuki katika namna chama hicho kilivyoweza kusimama kidete kwenye mapambano dhidi ya ufisadi na japo hawajaweza kumaliza kabisa tatizo hilo (kwa vile dola bado iko mikononi mwa CCM),yayumkinika kabisa kuamini kuwa hata swali "nakubali kumchukua" linajijibu hapohapo.

Hebu nipe msingi wa kuamini kuwa Chadema ilivyo sasa itatafsiri hizo ahadi kwa vitendo. Ni kitu gani kinakufanya uamini hivi? Usinielewe vibaya, sisemi kwamba hawawezi au hawatofanya, ninachosema msingi wa imani hiyo ni nini?

Nimeshakupa mifano ya namna walivyojitoa mhanga kuhamasisha mapambano dhidi ya ufisadi.Lakini hata tukiweka kando mifano hiyo HAI,naomba nikuulize nawe "HEBU TUPE MSINGI WA KUAMINI KUWA CCJ KAMA ILIVYO SASA ITATAFSIRI HIZO POROJO ZAKE KWA VITENDO".Na "KIPI KINAKUAMINISHA KUWA WATAFANYA WANACHOAHIDI KUFANYA?".Kadhalika,nami sisemi kuwa CCJ hawawezi au hawatofanya (kama watafanikiwa kujisajili na kuwa chama cha siasa badala ya "chama cha press conferences"),bali nami nahoji imani yako kubwa inatokana na nini maana angalau mie ninayeiamini Chadema nimeshawishiwa na harakati zao katika miaka mitano hii

Mifano yako ni mibaya kwa kweli japo inaweza kuvutia fikra nyepesi nyepesi.
Katika hilo sina la kusema kwa vile unachokiona wewe kuwa kibaya kinaweza kuwa kizuri kwangu na kwa wengine.Mara nyingi wanasosholojia wanaepepuka sana "kujipa madaraka ya kuhukumu" kwa vile kauli au matendo ya mwanajamii yanaweza kuwa na tafsiri au/na dhamira zaidi ya anayoiona mtoa hukumu.Japo unaona mifano yangu ni mibaya na inayoweza kuvutia hisia nyepesi,naomba kukupa mfano mwingine MREEEEFU kuhusu point of view

The optimist says the glass is half full.
The pessimist says the glass is half empty.
And the cynic... wonders who drank the other half.
The school teacher says it's not about whether the glass is half empty or half full, it's whether there is something in the glass at all.
Anyway... Attitude is not about whether the glass is half full or half empty, it's about who is paying for the next round.
The inquisitive troublemaker wants to know what's in the glass anyhow... and wants the rest of it.
The homebuilder sees the dirty glass, washes and dries it, then puts it away in a custom oak and etched glass cabinet that he built himself using only hand tools.
The worrier frets that the remaining half will evaporate by next morning.
The fanatic thinks the glass is completely full, even though it isn't.
The entrepreneur sees the glass as undervalued by half its potential
The logician says that where the glass is in process of being filled then it is half full; where it is in the process of being emptied then it is half empty; and where its status in terms of being filled or emptied is unknown then the glass is one in which a boundary between liquid and gas lies exactly midway between the inside bottom and the upper rim, assuming that the glass has parallel sides and rests on a level surface, and where it does not then the liquid/gas boundary lies exactly midway between the upper and lower equal halves of the available total volume of said glass.
The scientist says a guess based on a visual cue is inaccurate, so mark the glass at the bottom of the meniscus of the content, pour the content into a bigger glass; fill the empty glass with fresh content up to the mark; add the original content back in; if the combined content overflows the lip, the glass was more than half full; if it doesn't reach the top, the glass was more than half empty; if it neither overflows nor fails to reach the top then it was either half-full or half-empty. Now what was the question again?
The grammarian says that while the terms half-full and half-empty are colloquially acceptable the glass can technically be neither since both full and empty are absolute states and therefore are incapable of being halved or modified in any way.
The waiter will hurry to replace the glass with a full one. For him there are no doubts: the glass was empty when he took it away; it is full in the bill that he brings you.
The magician will show you the glass with the full half at the top.
The physician says that the glass is not empty at all - it is half-filled with water and half-filled with air - hence, fully filled on the whole!
The musician says he/she is unimpressed with the promoter of the concert for not providing more alcohol.
The ineffective organization would discuss the question during the board of directors meeting, convene a committee to research the problem, and assign tasks for a root cause analysis, usually without a complete explanation of the problem to those assigned the tasks. The directors would consider the problem to be above the pay grade of those assigned root cause analysis tasks.

And more strangely:

The dog just wonders: can he eat the glass or will you throw it so he can bring it back... The cat wonders why the glass is only half full (or empty)... is it a trick... poison perhaps...
The eternally optimistic eccentric would say, the glass is consistently overflowing (or is that the neurotic?...)
The person who is no longer trapped in The Matrix (whatever one might call him/her) says: "There is no glass..."

More generationally:

The adolescent student says the glass is just another dirty trick played by the teacher to prove that students are dumb.

More scientifically:

The research scientist says that following initial observation and testing a working hypothesis for further research is: "The glass is both half full and half empty," and that these findings warrant further investigation with a more representative sample of glasses and contents, which may or may not be liquid.
The algebraic simultaneous equation theorist says that if the glass is equally half full and half empty, then half full = half empty; therefore ½ x F = ½ x E; therefore (by multiplying both sides of the equation by 2) we show that F = E; i.e. Full equals Empty!

The efficiency analyst says the glass is operating substantially below optimization level, being consistently exactly 50% under-utilized during the period of assessment, corresponding to an over-resourcing in meeting demand equating to precisely 200% of requisite capacity in volume terms, not accounting for seasonal trends and shrinkage, and that if the situation continues there is in theory opportunity for savings or expansion.

Lengo la mfano huo mreeefu ni kujaribu kujibu mtizamo wako kuhusu mifano ninayotumia

Nimeandika nyingi sana na ninaamini CCM watafanyia kazi mapema zaidi kuliko ndugu zetu wa upinzani.

At least hapa unatusaidia kutuonyesha your true colours.Sasa kama unaamini kuwa CCM watafanyia kazi mapema zaidi kuliko ndugu zetu wapinzani,sasa CCJ ni tawi la CCM au?Maana kama CCJ unayoipigia debe ni sehemu ya upinzani,na unaamini CCM watafanyia kazi matatizo yetu mapema kuliko wapinzani (including CCJ),umuhimu wa wapinzani (including CCJ) unatoka wapi tena?

Unaweza ukafikiria tatizo ni utekelezaji, lakini kuna tatizo kubwa zaidi linalofanya utekelezaji uwe mgumu. Fikiria kwa sekunde chache tu unaweza kufahamu.
Well,kwa mujibu wa uelewa wangu MDOGO,utekelezaji ni tatizo la msingi.Na napenda kukuthibitishia kuwa huwa nafikiria kabla ya kuandika japo hiyo haimaanishi kuwa kila nachofikiria na kuandika kitakuwa sahihi.Lakini kwa vile naamini wote tuna lengo moja,yaani kuona Tanzania ikiwa kwenye mwelekeo stahili,hudhani ingekuwa vema zaidi kama ungebainisha bayana kuwa tatizo kubwa zaidi ya utekelezaji ni lipi badala ya kunitaka nifikiri zaidi (which implies kuwa sikufikiri vya kutosha)?Wenzetu wenye ufahamu mkubwa mnaweza kuwa raslima muhimu kwa maendeleo ya taifa letu kama mtachangia mitizamo yenu katika namna ya majadiliano na kuelimishana badala ya kutuonyooshea vidole sie "tusiofikiri vya kutosha".
Well, tatizo liko kwenye sera vile vile. CCM haina nzuri kama wengi wanavyoamini. Ni mojawapo ya sera mbaya kabisa hasa katika miaka hii 20 iliyopita. Wakati wengine wanaamini kuwa CCM ina sera nzuri "vitabuni" mimi siamini hivyo kwani nimezisoma na kwa kweli hazitofautini kabisa na za Chadema. Sijui kama umepata nafasi ya kumsikiliza Kikwete leo.
Again,hapa ni suala la mtizamo tu.Last time I read nini CCJ wanataka kufanya sikuona tofauti kati yao na kinachohubiriwa na CCM.Sijui,labda baada ya kupata usajili wa kudumu CCJ watakuja na sera nzuri na zinazoambatana na guarantee ya kudumu ya utekelezaji wa sera hizo.

Ujamaa haukushindwa, haukujaribiwa ipasavyo. Ndiyo maana leo nchi zenye kufuata ujamaa (hata kwa jina jingine) zinazidi kuongezeka!
Mkuu,hata Uholanzi wanaweza kutoa maelezo kama hayo kuhusu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Spain kwamba hawakushindwa bali "hawakujiandaa vya kutosha,hawakufanya mazoezi ipasavyo,nk".Lakini suala ni matokeo,mwisho wa pambano score board ilisomeka Spain 1 Holland 0.Na katika mantiki hiyohiyo,kama tunauzungumzia Ujamaa katika misingi ya KUFANIKIWA na KUSHINDWA,suala la whether ulijaribiwa vizuri au vibaya linapoteza umuhimu wake.Tangu lini kujaribu kitu vibaya kukawa na maana ileile ya kufanikiwa?Hoja ya kujaribiwa vibaya ingekuwa na uzito kama swali lingekuwa "kwanini ujamaa ulishindwa",ambalo kwa mtizamo wangu jibu jepesi linarejea kwenye hoja ya sera nzuri,utekelezaji mbovu.

Je haikuwa itikadi nzuri?Je sera mbalimbali zilizoambatana na itikadi hiyo hazikuwa na malengo mazuri kwa Watanzania?
Kwa mtizamo wangu,ambao ni ruksa kutoafikiana nao,baadhi ya mahubiri kuhusu ujamaa yaliwalenga walalahoi pasipo kuangalia kundi la watu kama akina Kingunge na vigogo wengine waliotuaminisha kuwa "binadamu wote ni sawa ilhali wao wanawekeza fedha za kigeni kwenye akaunti zao nje ya nchi".Kulikuwa pia na mapungufu ya kuwa putting too much ambition infront of common sense.Unapomhamisha mtu kwenye eneo productive na ambalo ana local connection na kumpeleka sehemu inayopata mvua kwa kudra za Mwenyezi Mungu untarajia nini?Na kwa vile tangu tupate uhuru,uchumi wetu ulielemea kwenye utegemezi wa misaada,hatukuwa tumejenga msingi wa kukwamisha "kujitegemea" kwetu?Je si kweli kwamba miongoni mwa sababu zilizopelekea "kifo cha ujamaa" ni uchumi tegemezi ambapo "wafadhili" walishinikiza matakwa yao,nasi kulazimika kuyafuata kwa vile hatukuwa na alternative nyingine?
Ninachosikia ni kuwa "twende tu" hata kama hakuna sera, hakuna ahadi, hakuna kipiimo twende tu tufuate jina!.. really? I'm still sane, at least the last time I checked.
Na sie tunaoamini kuwa ni muhimu kuiondoa CCM sasa tunasukumwa na ukweli kwamba tumeshasikia sera lukuki,ahadi kibwena,na vipimo vilivyozidi hata uwezo wetu lakini bado tuna mark-time...actually,tunarudi nyuma zaidi ya alipotuacha mkoloni.Kuhusu hiyo sanity,I believe hata sie tunaotaka CCM iondoke SASA ni sane pia (aidha vipimo vya wataalamu au uwezo wetu binafsi).Kudai CCM iondoke sasa hakumfanyi mtu kuwa insane.Na ni katika namna hiyohiyo si haki wala sahihi kuhitimisha kuwa mtu anayamini chama cha kizushi kama CCJ is not sane.

well, hakuna sababu ya kusubiri kwa kweli, nimeandika toka mwanzo, mwaka huu huu Chadema ikitaka kushika madaraka ya nchi 'INAWEZA'. Lakini hadi hivi sasa imethibitisha kuwa haitaki. Inaombea.
Labda uko sahihi maana inaelekea tatizo la KUTOTAKA linazidi kusambaa kwa vyama vya siasa kwani hata CCJ wangetaka kupata usajili wa kudumu wangeweza kupata lakini wametuthibitishia kuwa sio tu kuwa hawakutaka bali pia walikuwa na ajenda ya kuwazuga watu.Na angalau Chadema inaombea kwa vitendo kuliko CCJ inayoombea kwa press conferences na huruma ya mabalozi wa kigeni.
 
Mlalahoi, tatizo lako unaangalia kwa macho ya "mwanakijiji aliunga mkono CCJ kwa hiyo basi anahoji mambo ya Chadema kwa sababu ya CCJ". Hapa ndipo unapomiss time. Sasa hivi CCJ siyo ishue tena. Chadema ndicho ni issue. NI issue kwa sababu tunatakiwa tuamini na kukubali. CCJ ni chama ambacho kingeweza kuwa kwani kilikuwa tayari kukubali na kujifunza kufanya upya na bado kina uwezo mkubwa tu huko mbeleni kama katika jina lake la sasa au jingine. Lakini kwa wakati huu tunazungumzia chadema tu.
 
Ha ha haa! I can see (using squint eyes) Mwanakijiji on a mission; but also a depressed Mwanakijiji (from your writings of course!).
 
Mlalahoi, tatizo lako unaangalia kwa macho ya "mwanakijiji aliunga mkono CCJ kwa hiyo basi anahoji mambo ya Chadema kwa sababu ya CCJ". Hapa ndipo unapomiss time. Sasa hivi CCJ siyo ishue tena. Chadema ndicho ni issue. NI issue kwa sababu tunatakiwa tuamini na kukubali. CCJ ni chama ambacho kingeweza kuwa kwani kilikuwa tayari kukubali na kujifunza kufanya upya na bado kina uwezo mkubwa tu huko mbeleni kama katika jina lake la sasa au jingine. Lakini kwa wakati huu tunazungumzia chadema tu.

Mkuu,mie naomba nimalizie mchango wangu katika hoja hii kwa kutoa wito huu wenye lengo jema.Kwa vile CCJ sio issue kwa sasa,basi unaonaje tukiunganisha nguvu zetu (kama Watanzania wenye nia ya dhati kuona nchi yetu ikipiga hatua) na kuipatia sapoti inayostahili?Sapoti hiyo inajumuisha pia kuwakosoa pale walipo/wanapokosea.Na obmi hili linaendana na alichoandika Bwana Mnyika hapo awali.Ni kwa maslahi ya taifa letu sote.

Natoa wito huu nikizingatia ukweli kwamba angalau Dkt Slaa na Mnyika ni wenzetu hapa,na mara kadhaa wameonyesha nia ya kusikia upande wa pili wa hoja au mitizamo tofauti na yao/chama chao.

Ni wazo tu,mkuu.
 
Wote mmekutana shambani na mnawaalika wengine waje kuwasaidia kulima na kusema kuwa tutapanda mazao; na tunauliza tunataka tupande nini na tutatunza vipi mnasema hapana, tufyeke kwanza, tulime halafu ndiyo tutajua tunachotaka kupanda. Wanaouliza mpango wa shamba wanaambiwa maswali hayo siyo muhimu waje tu "kuunganisha nguvu" ili kulima. "Tulime nini"? jibu ni "hakuna sababu ya kujua kwani tukishalima ndiyo tutajua cha kupanda!

Well.. mkija kutuambia tupande mihogo kwenye hali ya hewa isiyo stahili mihogo au miwa mpunga mahali ambapo hakuna mvua wala vyanzo vya uhakika vya maji si ndo mtakuwa mmetununua jumla jumla maana tayari tumeshaweka nguvukazi yetu, na tumewekeza matumaini yetu vile vile.

Sasa wanasema

Tuunganishe nguvu => ili kiwe nini?
Tuing'oe CCM madarakani => ili kiwe nini?
Ili isiwe madarakani tena => ili kiwe nini?
Ili sisi tuwe madarakani => ili mfanye nini?
Ili tufikirie tukishakuwa madarakani => ili mfikirie nini?
Ili tufikirie kwanini tuliitoa CCM madarakani => mkishajua mfanye nini?
Ili tuhakikishe hairudi tena madarakani =>
 
Mheshimiwa,wazo langu la kukuomba ujumuike na harakati za Chadema zilipewa changamoto na hoja zako zinazoashiria mwenzetu una ufumbuzi.Sasa labda utusaidie kuhitimisha hoja hii inayoelekea kutokuwa na mwisho kwa kutupa mawazo yako juu ya NINI KIFANYIKE.Maana laiti wenzetu huko Afrika Kusini wangekuwa wanajiuliza maswali hayo unayouliza basi hadi leo makaburu wangeendelea kuwanyanyasa.Na laiti Wahutu na Watustsi huko Rwanda wangepoteza muda wao kujiuliza "tumalize mauaji ya kimbari then waht" basi wangekuwa wanachinjana hadi leo.Kadhalika,laiti waliopigani uhuru wangeendelea kuwaskiza sceptics waliotaka uhuru ucheleweshwe basi mkoloni angeendelea kuwa madarakani hadi dakika hii.Pia,tungetumia muda mwingi kujiuliza maswali kama hayo tulipovamiwa na Amini basi leo hii sijui ingekuwaje!

Katika matukio hayo yote,doing nothing was not an option.

Tunaweza kukesha tukibishana as to whether kuiondoa CCM ni ufumbuzi au la,na tusifikie mwafaka kwa vile japo siasa si soka lakini lililo bayana ni kuwa vyovyote itakavyokuwa hakuna linaloweza kumfanya shabiki wa Yanga aishangilie Simba or vice versa,na once mpinzani wako akitokea kukushabikia au kuombea ufanikiwe basi ujue kuna namna.Pamoja na mapungufu waliyonayo,Chadema wanajua wanachofanya,sceptics wataendelea kuwepo kwani hata zama za kupigania uhuru walikuwepo.Whether CCJ ni issue au sio issue lakini linalojidhihirisha ni kuwa Chadema haiwezi kupata ushauri wa maana kutoka CCJ au/na wafuasi wake.By the way,wataishauri vipi ilhali wao pekee ndio wenye sera na itikadi za kihistoria?

No matter how long the night the day is sure to come!Mnaoamini kuwa kuing'oa CCM sio ufumbuzi muendelee tu na mtizamo wenu,na sie tunaoamini kuwa CCM ni sawa na bakteria ambaye ili mgonjwa apone ni lazima andolewe mwilini tutaendelea kuwa na imani hiyo.

Let's agree to disagree.
 
sijui kama kuna mahali popote nimesema CCM isiondolewe madarakani au ising'olewe. Wakati wenzetu mtasherehekea CCM kung'olewa madarakani mimi nataka nijue tunawaingiza nani na kwa nini madarakani. Haitoshi kuindoa CCM madarakani halafu tuwape CCM wengine madaraka. Sasa nyinyi ambao hamtaki kufikiria zaidi ya siku ya uchaguzi endelee ni kufikiri hivyo hivyo kwani a rude awakening awaits you. Kuingoa CCM madarakani ni rahisi zaidi, kuweka nini mbadala wake ni gumu zaidi. Na ni gumu zaidi kujua tunataka kuweka nini. Nimeuliza hapo nyuma ni lipi rahisi, kujenga au kubomoa? Nina uhakika kabisa kuwa tunaweza kuiondoa CCM madarkani wakati wowote hata kesho tukitaka - ukasome tena ujumbe wangu wa "Kuanguka kwa CCM" ndiyo utaelewa kuwa naisubiri siku hiyo kwa hamu kubwa, lakini siisubiri kama mwisho wa harakati hizi.
 
Well,pengine hata bila kusoma huo ujumbe wa "kuanguka kwa CCM" kuna haya maandiko yako (yafuatayo) katika moja ya posts zako huko nyuma yanaweza kutusaidia

Lakini vyovyote vile ilivyo, kama kweli Tanzania inataka kupati nafasi ya kufanikiwa na kuanza kuelekea nchi ile tuitamaniyo, CCM kama ilivyo sasa haistahili kuendelea kuliongoza Taifa letu baada ya 2010. Aidha wanyang'anywe Urais (kama ilivyotokea Afrika Kusini, au wanyang'anywe Bunge (kama ilivyotokea Kenya), au wanyang'anywe vyote viwili (kama ilivyotokea Marekani). Kuwaachia waendelee walivyo sasa, ni kuwapa baraka ya kutudumaza.

Jibu la swali lako kuwa tukiing'oa CCM tunamwingiza nani madarakani ni matokeo ya kura yako.The more votes a party of your choice gets the more the chances kuwa wataunda serikali.Si ndio mfumo wetu wa uchaguzi ulivyo?Jibu la swali kuwa kwanini tunawaingiza madarakani linapatikana kwenye hiyo quote niliyonukuu maandiko yako mwenyewe ie kama kweli Tanzania inataka kupati nafasi ya kufanikiwa na kuanza kuelekea nchi ile tuitamaniyo, CCM kama ilivyo sasa haistahili kuendelea kuliongoza Taifa letu
 
Well,pengine hata bila kusoma huo ujumbe wa "kuanguka kwa CCM" kuna haya maandiko yako (yafuatayo) katika moja ya posts zako huko nyuma yanaweza kutusaidia

Jibu la swali lako kuwa tukiing'oa CCM tunamwingiza nani madarakani ni matokeo ya kura yako.The more votes a party of your choice gets the more the chances kuwa wataunda serikali.Si ndio mfumo wetu wa uchaguzi ulivyo?Jibu la swali kuwa kwanini tunawaingiza madarakani linapatikana kwenye hiyo quote niliyonukuu maandiko yako mwenyewe ie kama kweli Tanzania inataka kupati nafasi ya kufanikiwa na kuanza kuelekea nchi ile tuitamaniyo, CCM kama ilivyo sasa haistahili kuendelea kuliongoza Taifa letu

Angalau umeninukuu kwa usahihi kwa sababu watu wengine wameanza kudai kuwa mimi nataka CCM waendelee kukaa madarakani. Kwa vile hoja hii imekuwa ngumu kwa wengi kunielewa nimeamua kujipa jukumu la kuivunja vunja katika vipengele vyake ili hatimaye ujumbe ambao nataka niutume kwa Chadema na mashabiki wake uweze kuelewa. Yaani, KUTOKA HAPA MPAKA KULE.
 
sijui kama kuna mahali popote nimesema CCM isiondolewe madarakani au ising'olewe. Wakati wenzetu mtasherehekea CCM kung'olewa madarakani mimi nataka nijue tunawaingiza nani na kwa nini madarakani. Haitoshi kuindoa CCM madarakani halafu tuwape CCM wengine madaraka. Sasa nyinyi ambao hamtaki kufikiria zaidi ya siku ya uchaguzi endelee ni kufikiri hivyo hivyo kwani a rude awakening awaits you. Kuingoa CCM madarakani ni rahisi zaidi, kuweka nini mbadala wake ni gumu zaidi. Na ni gumu zaidi kujua tunataka kuweka nini. Nimeuliza hapo nyuma ni lipi rahisi, kujenga au kubomoa? Nina uhakika kabisa kuwa tunaweza kuiondoa CCM madarkani wakati wowote hata kesho tukitaka - ukasome tena ujumbe wangu wa "Kuanguka kwa CCM" ndiyo utaelewa kuwa naisubiri siku hiyo kwa hamu kubwa, lakini siisubiri kama mwisho wa harakati hizi.
MKJJ for how long will you keep on thinking WHAT IS NEXT, two years...five years.....or 20 years?, and while doing that will you be sitting on a sofa enjoying your thoughts without any other alternatives?

If the answer is NO then what is your alternative or what are your suggestions, and if the answer is YES what is the Time Frame of your project. My worry is, it might take you ages and ages to get on the conclusion you wanted.

The time you think you have gotten the real answer you needed is the time you come to realize that you have'nt, and I think you will never get a right answer of your hypothesis.

As Mr. Mnyika suggested let us do both simultaneously THINK and REMOVE the obstacle from our way. Otherwise i wish you all the best with your wishful thinking and let the others do the necessary for you.
 
Wote mmekutana shambani na mnawaalika wengine waje kuwasaidia kulima na kusema kuwa tutapanda mazao; na tunauliza tunataka tupande nini na tutatunza vipi mnasema hapana, tufyeke kwanza, tulime halafu ndiyo tutajua tunachotaka kupanda. Wanaouliza mpango wa shamba wanaambiwa maswali hayo siyo muhimu waje tu "kuunganisha nguvu" ili kulima. "Tulime nini"? jibu ni "hakuna sababu ya kujua kwani tukishalima ndiyo tutajua cha kupanda!

Well.. mkija kutuambia tupande mihogo kwenye hali ya hewa isiyo stahili mihogo au miwa mpunga mahali ambapo hakuna mvua wala vyanzo vya uhakika vya maji si ndo mtakuwa mmetununua jumla jumla maana tayari tumeshaweka nguvukazi yetu, na tumewekeza matumaini yetu vile vile.

Sasa wanasema

Tuunganishe nguvu => ili kiwe nini?
Tuing'oe CCM madarakani => ili kiwe nini?
Ili isiwe madarakani tena => ili kiwe nini?
Ili sisi tuwe madarakani => ili mfanye nini?
Ili tufikirie tukishakuwa madarakani => ili mfikirie nini?
Ili tufikirie kwanini tuliitoa CCM madarakani => mkishajua mfanye nini?
Ili tuhakikishe hairudi tena madarakani =>

mwanakijiji ni pasua kichwa.naomba atuambie kama alishajuwa kama ccm imekaa madarakani miaka yote ili kiwe nini.kwa sababu naona anang'ang'ani a maswali yake ambayo sitakosea nikiita ya kitoto.ameshaambiwa asubiri ilani hataki.asome katiba sijui kama ameshafikiria kwenda kuisoma kwanza ndipo aone kama maswali yake hayana majibu huko.ccj ilimharibu kichwa kiasi kwamba naona kama amechanganyikiwa anatafuta wakufa na ccj,nampa pole kama ninavyowapa wote waopatwa na msiba.nimefikiria kwa miaka mingi sana kuhusu mbadala wa ccm mwisho nimeona tumaini la kweli lipo chadema na nawakaribisha wote wenye mapenzi mema na taifa hili wajiunge chadema.pamoja tutashinda.
 
Kusema za ukweli, arguments za huyu "Mzee wa CCJ" juu ya topic hii kwangu mimi hazipandi kabisa .......... it's like am watching a circus show!
Mawili.... (1)mimi ni kilaza kupindukia (du!!?); au (2)the arguments are all over the pitch
I think I need some counciling kabla sijachangia nilichonacho.....
 
Mwanakijiji,
Hayo unayoyasema yanatoka kweli moyoni? mimi nadhani kuing'oa CCM ni jambo la kwanza kabisa, hata akisha mtu leo akisema anataka kuingo'a CCM sitamuuliza atafanya nini baada ya hapo- issue CCM iondoke . Machungu tunayoyapata kwa CCM ni makubwa sana, labda wewe kwa vile huyapati moja kwa moja ndo maana huoni kama ni jambo la muhimu.

BTW kwa mara ya mwisho ulirudi nchini hapa lini (swali hili ni muhimu sana) maana lina connection na huo msimamo wako
 
mwanakijiji ni pasua kichwa.naomba atuambie kama alishajuwa kama ccm imekaa madarakani miaka yote ili kiwe nini.kwa sababu naona anang'ang'ani a maswali yake ambayo sitakosea nikiita ya kitoto.ameshaambiwa asubiri ilani hataki.asome katiba sijui kama ameshafikiria kwenda kuisoma kwanza ndipo aone kama maswali yake hayana majibu huko.ccj ilimharibu kichwa kiasi kwamba naona kama amechanganyikiwa anatafuta wakufa na ccj,nampa pole kama ninavyowapa wote waopatwa na msiba.nimefikiria kwa miaka mingi sana kuhusu mbadala wa ccm mwisho nimeona tumaini la kweli lipo chadema na nawakaribisha wote wenye mapenzi mema na taifa hili wajiunge chadema.pamoja tutashinda.

classical ad hominem..
 
Wote mmekutana shambani na mnawaalika wengine waje kuwasaidia kulima na kusema kuwa tutapanda mazao; na tunauliza tunataka tupande nini na tutatunza vipi mnasema hapana, tufyeke kwanza, tulime halafu ndiyo tutajua tunachotaka kupanda. Wanaouliza mpango wa shamba wanaambiwa maswali hayo siyo muhimu waje tu "kuunganisha nguvu" ili kulima. "Tulime nini"? jibu ni "hakuna sababu ya kujua kwani tukishalima ndiyo tutajua cha kupanda!

Well.. mkija kutuambia tupande mihogo kwenye hali ya hewa isiyo stahili mihogo au miwa mpunga mahali ambapo hakuna mvua wala vyanzo vya uhakika vya maji si ndo mtakuwa mmetununua jumla jumla maana tayari tumeshaweka nguvukazi yetu, na tumewekeza matumaini yetu vile vile.

Sasa wanasema

Tuunganishe nguvu => ili kiwe nini?
Tuing'oe CCM madarakani => ili kiwe nini?
Ili isiwe madarakani tena => ili kiwe nini?
Ili sisi tuwe madarakani => ili mfanye nini?
Ili tufikirie tukishakuwa madarakani => ili mfikirie nini?
Ili tufikirie kwanini tuliitoa CCM madarakani => mkishajua mfanye nini?
Ili tuhakikishe hairudi tena madarakani =>
Mkuu wangu hapo ndipo tunaposhindwa kuelewana.. Hivi kweli wewe utaalika watu kulima shamba vipi ikiwa shamba hilo sii lako? sii watakuoa kichaa kimekupanda kichwani..
Tunacho suggest sisi ni kwanza - Kukusanya nguvu zetu tupate mtaji wa kulinunua shamba hilo toka kwa mtu anayemiliki shamba hilo. Tunajua Chadema hana nguvu hiyo hivyo wewe na mimi tukiungana nao tunaweza kulinunua shamba hilo. Thaminisho ni ARDHI kwa wakati huu lakini kama leo Chadema wakianza maneno ya tuchukue shamba tulime mahindi au mpunga watu watawaona vichaa wao kwa sababu hawana ardhi hayo mahindi au mpunga utaulima wapi?.

Kinachofanyika sasa hivi ni kuwaonyesha wananchi ardhi na kuwadadisi thamani ya ardhi hiyo ikiwa tunataka kulima mpunga, mahindi, kujenga nyumba na kadhalika yote haya yanawezekana chini ya utawala bora wenye mipango safi (sera za chama). Hukubaliani na sera basi zungumza maoni yako kama unataka mchango wako lijengengwe ngome ya kuzia wezi wasivamie tena shamba - kwa swali kama hilo utajibiwa..
Kwa hiyo mkuu wangu WAPI inatangulia what next!
 
Back
Top Bottom