Mzee Mwanakijiji,
Mkuu nimekusoma sana kule kwenye - Chadema 2010: Kutoka HAPA kwenda KULE
Na sikupenda kwenda kule kuharibu Uhondo wa mada ile kwa kuanzisha hoja pinzani ndani ya elimu kubwa uloitoa. Nimeona bora kuleta hapa hoja zangu tuzijadili kwa mapana.
Sehemu kubwa ya mchakatuo wako nimeukubali isipokuwa sehemu moja tu ulipogusia Mahusiano ya Itikadi, sera na Ilani kwa kuitazama Chadema. Na nitakueleza kwa kirefu baadaye isipokuwa sasa hivi nitasema kwamba yale makosa unayoyaona kwa sera za Chadema ndizo zinazokufanya wewe usiwe muumini wa mrengo wa kati - (Reform Party). Sidhani kama sera zao hazikulingana na mrengo wa kati
Pili, mimi naamini kabisa kwamba Itikadi au elimu yoyote ya kiitikadi hutokana na mazingira yaliyopo. Vyama vyote vya Conservative, Progressive na hata Liberal, itikadi zao zimeibuka baada ya fikra chachu ku challenge malengo ya itikadi iliyotangulia hivyo kuweka ushindani wa kifikra mbele ya wananchi ambao ndio wenye kuguswa na uhuru nahaki ya sheria zitokanazo na mfumo huo. Kwa hiyo Hawa jamaa zetu wanapotaka ku challenge CCM ni lazima itokane na mazingira yaliyopo kutofungamana na itikadi iliyotawala pamoja na ile pinzani ktk kutekeleza ibada zake.
Na hakika Conservative wa Marekani hawako sawa kwa kila kitu na wale wa UK, Japan, Ufaransa au China wala hao Democratic wote hawafanani kwa kila kitu.
Mara zote fikra chachu za kuzaa hizi itikadi kiutawala zimetokana na KUPINGA sheria tangulizi iliyokataza au inayoruhusu wajibu fulani kutoka kwa wananchi. Na huwezi kupinga tu ili mradi unapinga pasipo reasoning, na ndipo unakuta wazo moja huzaa fikra ikaleta Falsafa ambayo kwa kukubalika ikawa Itikadi (imani) inayofuatwa na wafuasi wake kupinga sheria iliyotokana na sera au itikadi inayowaongoza watu hao.
Trust me mkuu wangu ktk hili hakuna mawazo mbadala wala itikadi inayoweza tungwa na kuwa UNIVERSAL isipokuwa wazo,fikra,falsafa na Itikadi zote zimetokana na WATU katika MAZINGIRA waliyokuwepo wao. Hata Mapinduzi ya China yamefanyika na Wajamaa kupinga Wajamaa wenzao ktk hatua za kiutawala ambazo hazikufungamana na itikadi yenyewe.
Kwa hiyo ndio maana unanikuta mimi Mkandara nasimama mrengo wa KULIA nikiwa Tanzania, lakini huku majuu nimekaa KUSHOTO na siasa za nyumbani kwangu zipo kati kushoto - LIBERAL kwa sababu ni mazingira uliyopo ndiyo hutengeneza maamuzi mengi ya kisheria. Kama vile leo siwezi kukubaliana na baadhi ya sheria za kiislaam kutumika ktk mazingira ya Tanzania. Na ndio maana ukifuata falsafa ya mrengo wa kulia (conservatism) ktk nchi zetu maskini, hakika mambo mengi yatapingana na itikadi hiyo ya nchi za magharibi (tajiri) pamoja na kwamba wao wanaona wanayo kila haki ya ku conserve asili na tamaduni zao lakini sio sisi.
Nitaendelea zaidi baadaye kuhusiana na Chadema. kama kuna hoja au swali tuanzie hapa.