Nadhani itabidi niende ndani zaidi kuelezea kile ninachokiita "Tatizo la Chadema". Natumaini nitaeleweka, na siyotkuwa nimechelewa. Niwatoe hofu kabisa kwangu mimi hata CCM ikiondolewa kesho madarakani sitolia!! Lakini sitorukaruka kwa furaha! Nitauliza swali hili hili ninaloliuliza sasa.. "then what"? Nakataa kabisa kuwa hatuwezi kuwa na ajenda ya uchaguzi inayosema "tuiondoe CCM kwanza"! Hii ni ajenda ya kuondoa chama kimoja na kukiweka kingine. Yatakuwa yale yale ya KANU na RAINBOW coalition! Well RAINBOW walifanikiwa kabisa kuiondoa KANU, lakini is Kenya better today than during KANU's rule? Tutapata majibu tofauti sana kwenye hilo. Je Zambia chini ya Chiluba baada ya kuiangusha ZANU je walikuwa bora zaidi kwa sababu kina Chiluba walitimiza ndoto yao ya kumuangusha Kaunda?
Hili swali hata kama mtalikwepa, mtalibeza au mtajaribu kuonesha kuwa hamlielewi mtalazimika kulijibu tu one of these days. I know you will.
Kwa vile linaonekana ni gumu mno/halielewi au halijaulizwa sawasawa itabidi nilivunje vunje katika vipande vyake vidogovidogo. CHADEMA WAKILIELEWA NA KULIJIBU KABLA YA UCHAGUZI WATASHINDA KWA KISHINDO!
Mkuu,pamoja na heshima kubwa niliyonayoa kwako lakini naomba kutamka kuwa mawazo yako katika suala hili yanafaa zaidi katika nchi ya KUFIKIRIKA.Hivi kwa busara zako unadhani hata tukikubali kwamba solution kwa sasa sio kuiondoa CCM,then tufanye hicho usichotaka kutuambia bayana,CCM itakuwa imelala tu pasipo kuhujumu huo mkakati unaopendekeza pasipo kuubainisha?Kwanini hujiuliza BAWATA ilihujumiwa,kwanini hujiulizi kwanini mashushushu wanapenyezwa kwenye NGOs na civil society kwa ujumla?
Inanilazimu ku-guess kuwa mkakati unaodhani utakuwa mafanikio as opposed to ajenda ya kuiondoa CCM ni kutengeneza mazingira yatakayowezesha kuwapo serikali ya watu kwa ajili ya watu.Wazo zuri lakini kufanikiwa kwake ni sawa na jithada ya kutengenisha chumvi ndani ya bahari wakati ukiwa baharini tena kwa kutumia chandarua.It simply wont work.Nilipata F ya fizikia ndio maana nikaamua kuwa "ngwini" lakini nakumbuka kwenye masuala ya velocity kuna ishu ya kuneglect pressure (kama nimepatia,remember I got an F).Lakini kwenye siasa ya uhalisia huwezi ku-neglect pressure kutoka kwa ruling party kuhakikisha inaendelea kuwa madarakani,huku ikitumia vyombo vya dola kuhujumu kila jitihada za kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii.
Hivi unafahamu kuwa miongoni mwa sababu zinazopelekea waheshimiwa kutojihangaisha sana na kuondoa umasikini ni kwa vile umasikini huo unawasaidia wao kuendelea kuwapo madarakani?Unadhani Watanzania watapopiga hatua na kumudu maisha yao pasipo kusubiri pishi za mchele (in form of takrima) watakubali kuuza uhuru na kura zao kwa doti za kanga,kilo za sukari au hizo pishi za mchele?Katika mantiki hiyohiyo ya namna umasiki wa Watanzania wengi unavyotumika kama mtaji wa CCM,jithada zozote za kumkwamua Mtanzania asitegemee ridhaa ya CCM zitakumbana na nguvu kubwa za vyombo vya dola ambavyo kwa kiasi kikubwa zina symbiotic relationship na CCM.JK anapoteau washkaji zake kuongoza vyombo vya dola anafahamu vema kuwa atawalinda nao watamlinda.
Unaweza kutushwishi hapa kuwa kuiondoa CCM sio ufumbuzi wa matatizo ya Tanzania lakini unachoshindwa kusema hadharani ni ukweli kwamba CCM kwa sasa ni zaidi ya chama cha siasa.Ni mfumo onevu wa kifisadi unao-survive kwa kulinda hata majambazi as long as wanausaidia mfumo huo kudumu.Utamwambia nini afisa usalama anayeamini kuwa laiti Chadema au CUF ikiingia madarakani atakosa ajira kwa vile aliingizwa kwenye taasisi hiyo kutokana na ushkaji wa mzazi au nduguye na kigogo flani?
Tumeshuhudia Obama na Democrats walivyofanya kila liwezekanalo kuwaondoa Republicans.Hizo changes alizoahidi Obama (hata kama hazijaonekana) zitawezekana tu kwa vile Democrats wako madarakani.Wamarekani walikuwa wamechoshwa na Bush na neo-cons wenzie na njia pekee ilikuwa kuwaondoa madarakani japo kwa muda.Licha ya ukweli kwamba sera za Democrats zilichangia kuwaondoa wapinzani wao (kwa maana ya kuwavutia wapiga kura),ukweli unabaki kuwa dhamira ya kuwaondoa Republicans (iliyokuwa shared na Democrats na Wamarekani wengi) ndiyo hatimaye ilisababisha Obama kuingia Ikulu.
Hizi habari za sera,mikakati na alinacha kama hizo tumekuwa tukizisikia tangu tunapata uhuru.Kwani kuna chama chenye sera za kupendeza na kutoa matumaini kama CCM.Hebu rejea manifesto ya Kikwete 2005.Laiti angeweza kutimiza japo 10% tu ya mazuri aliyoahidi basi sasa hivi tungekuwa sio tu tuko mbali kiimaendeleo bali pengine tungetamani urais wake usiwe na kikomo.Kwa vile wewe ni Mwafrika mwenzangu,naamini unafahamu fika kuwa kikwazo cha maendeleo ya bara letu hakijawahi kuwa kokusekana sera tamu zenye kuleta matumaini.Tatizo ni utekelezaji wa sera hizo.Sasa unapoletea habari za sera,itikadi na ngonjera kama hizo nashindwa kanisa kukuelewa.Kinachotufanya baadhi yetu tuiamini Chadema ni kwamba angalau wamesimamia yale yanayotarajiwa na Watanzania walalahoi.Yani pamoja na hekima zako zote huamini kuwa Chadema imechangia kwa kiasi kikubwa kufunua ishu kama za ufisadi kama wa EPA ,Meremeta,Tangold,List of Shame,nk?Hivi hudhani kuwa mtu kama Dkt Slaa amekuwa na manufaa sana kwa Watanzania zaidi ya Kamati Kuu nzima ya CCM au hata kabineti nzima kuuuubwa ya JK?Wafanye kipi kukuridhisha kuwa angalau wao wameonyesha njia kwa namna flani licha ya vitisho na manyanyaso ya kusimamishwa ubunge (refer ishu ya Zitto)?
Kwa kumalizia,tafsiri ya haraka ya mkakati wako ni doing nothing is better than doing something.Nasema hivyo kwa vile umeshabainisha kuwa ni bora kubaki na CCM kuliko kuwa na chama mbadala unachodhani kitarudia madudu yaleyale ya CCM.Kwahiyo mwenzetu ukipatwa na malaria kisha ukatumia dawa lakini baada ya muda malaria ikarejea tena basi unaamua kuacha kuitibu kwa vile unahofia kuwa itarejea tena?Unahofia kuwa kuiondoa CCM madarakani kunaweza kusiwe ufumbuzi wa matatizo yetu hivyo ni bora kubaki na CCM?
Binafsi naamini kabisa kuwa unatuelewa sana tuotaka kuiona CCM iking'oka madarakani ila kwa vile ulishaamua tangu awali kusimama upande wa pili unaona kujumuika nasi ni kama kubadili dini.Ni vizuri kuwa na msimamo na pia ni sehemu ya matumizi mema ya jhaki yako ya kikatiba kuamini kile unachodhani ni sahihi hata kama wengi hawakiamini.However,japo imani ni imani,kuna tofauti kati ya kumwamini Mungu na kumwamini shetani.Na hapa sizungumzii idadi ya wanaomwamini Mungu dhidi ya wanaomwamini shetani bali naangalia itikadi za Mungu dhidi ya za shetani.Katika namna hiyo hiyo,kuamini kuwa ufumbuzi sio kuing'oa CCM madarakani sio kosa la jinai au dhambi,lakini katika uhalisia,hiyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.