Binafsi sijabahatika kukisoma na kukimaliza kitabu kinachoelezea maisha yake kilichoandikwa na mzee huyu mwingi wa ucheshi, uungwana na mbobevu wa lugha tamu ya kiswahili.
Lkn kwa waliokisoma chote wanaeleza mengi sana yanayodhihirisha kuwa hakuwa mtu wa tamaa. Mojawapo ya maelezo hayo ni kwamba "mzee Mwinyi (rip) ktk maisha yake yote hajawahi KUKOPA wala KUKOPESHA.
Hii inaweza kuwa ndiyo siri ya mzee huyu kuishi maisha marefu? Hii inaweza kuwa ndiyo siri ya mzee huyu kuishi maisha yake yote pasipo kuugua (kama ilivuoelezwa na mwanaye Abdul)?
Umewahi kufikiri hali anayopitia mtu anapomkopesha pesa rafiki/ndugu/jamaa halafu akadhulumiwa? Au mtu amekopa fedha benki au kwa ndugu/jamaa halafu akashindwa kurejesha? Afya ya akili huyumba sana na kupelekea maradhi mengi mengine mwilini
Jambo jingine linaloonesha kuwa mzee huyu hakuwa na tamaa ni hili lifuatalo. Mzee Mwinyi amezaliwa 1925 lkn imeandikwa kwenye kitabu chake kwamba 1983 (akiwa na umri wa miaka 58) ndiyo alikuwa ananunua mifuko ya cement na mabati ili ajenge nyumba yake. Ndipo hapo inadaiwa alijiuzulu uwaziri wa mambo ndani na kukumbwa na mkasa wa kufukuzwa kwenye nyumba ya serikali na mrithi wa nafasi yake ya uwaziri wa mambo ya ndani na hakuweza kuondoka na vifaa hivyo.
My take:
Jamani tusiwe na tamaa kwenye maisha, tutakufa kwa stress. Tamaa ilimponza mzee fisi.