Historia ya Ali Hassan Mwinyi kama Rais haiko wazi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,261
HISTORIA YA UONGOZI YA ALI HASSAN MWINYI KAMA RAIS HAIKO WAZI

UTANGULIZI

Makala hii nimeiandika baada ya kuulizwa maswali baada ya kufanya kipindi cha Maisha ya Rais Ali Hassan Mwinyi na Afrika TV2.

Najaribu hapo chini kujieleza.

Katika kipindi hiki cha televisheni yapo mengi katika maisha ya Rais Ali Hassan Mwinyi ambayo hayakuzungumzwa.

Pengine hayakuzungumzwa kwa kuwa mtayarishaji wa kipindi alipenda kumjua Sheikh Ali Hassan Mwinyi kwa upande wake mmoja tu kama Rais Muislam.

Hakutaka kuniingiza katika siasa.

Kwa uhakika hapa ndipo alipokazia katika maswali yake.

Huu ni upande mmoja wa historia ya Rais Mwinyi.

Upo upande mwengine wa Rais Mwinyi katika utawala wake.

Upande huu wa utawala wake unazunguka ndani ya serikali, unazunguka ndani ya CCM na mwisho unazunguka ndani ya taasisi zote nchini zenye uhusiano wa kuendesha nchi ukianzia vyama vya siasa hadi "argencies."
Hizi ni "ecological factors," mfano wa viumbe wanavyo uhusiana mazingira wanayoishi.

Mathalan ndani ya mbuga kuna majani ambacho ni chakula cha swala na kuna simba ambae chakula chake ni swala.

Simba kama hakula swala na swala wakawa wengi zaidi na majani ni yale yale mbuga si muda mrefu itakuwa jangwa.

Mbuga ikiwa jangwa simba na swala wote wataathirika.

Humu ndimo ilipo historia nyingine ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

Historia hii inasisimua.
Historia hii Rais Mwinyi hakuieleza katika kitabu chake, "Mzee Rukhsa Safari ya Maisha Yangu."

Historia si kama haipo kabisa lakini alipoigusia alipita pembeni kama vile hataki kukanyaga ukoka wake alioupanda na kuutunza vizuri.

Kwani ikiwa atapita katikati ya ukoka wake kuna hatari ya kutengeneza njia na wengine watapita.

Hawa wengine wakipita patakuwa njia na uzuri wa ukoka utapotea, utanywea na kuwa mfano wa majani ya kawaida yaliyokauka.

Bustani itapoteza haiba yake yaani itapoteza uzuri wake.

Mengi Rais Mwinyi kayanyamazia ndani ya kitabu chake.

Haya hayakuwa mambo ya kawaida.

Naamini waliokuwa karibu na yeye katika serikali na CCM walishangaa kuona yale mazito na muhimu kwake karashiarashia na mengine hakuyasema kamwe.

Mlango bado uko wazi kwa watafiti na wanafunzi wa historia kulijaza ombwe hili.
 
Hakika.
 
Mkubwa,

Autobiographies huwa zina tatizo la kuandika historia inayorashia rashia mambo fulani, ndiyo maana wenzetu kama Wamarekani mpaka leo wanaandika vitabu vipya kuhusu maisha ya Abraham Lincoln aliyeishi miaka zaidi ya mia mbili iliyopita.

Kitambo kidogo, zaidi ya miaka 14 iliyopita, alinitembelea rafiki yangu mmoja hapa kwangu, akaangalia maktaba yangu. Aliifurahia sana. Akakuta upande mmoja una vitabu mamia kwa mamia, angalau vitabu 500 hivi kwa hesabu za haraka. Akaniambia una vitabu vingi sana, nikamwambia hivi hapa vyote ni sehemu maalum ya biographies za marais wa Marekani tu. Akasema wewe kiboko, sasa hawa wote marais wa Marekani tu, marais wa Tanzania vipi?

Nikaona aibu sana, nikamwambia mimi nina makosa kwa sababu sijatafuta sana historia hizo za maisha ya marais wa Tanzania, lakini kuna tatizo kubwa zaidi, historia hizo hazijaandikwa sana. Nimeweza kununua vitabu zaidi ya 500 vya historia za marais wa Marekani kwa sababu vitabu hivyo vipo, sasa hivi, hata nikitaka kutafuta vitabu 500 vingine vya historia za maisha ya marais wa Tanzania siwezi kuvipata, hata nikisema tuondoe 400 kwa sababu hatuna marais wengi, nitafute vitabu 100 tu vya historia za maisha ya marais wa Tanzania, hatuna vitabu hivyo.

Kwa hivyo, nasema haya kukuunga mkono kwamba tunahitaji kuandika zaidi historia zetu. Wewe umeongelea kitabu cha Mwinyi.Nimesoma kitabu cha Mkapa nikaona hayo hayo uliyoyasema, mengi ya muhimu hayajaandikwa.

Ukisoma kitabu cha muandishi kama David McCullough "Truman" akimuelezea rais Harry S. Truman wa Marekani, alivyomchambua mwanzo mwisho, halafu ukasoma kitabu kama cha Mkapa au cha Mwinyi, utagundua kuwa vile si vitabu vya kuelezea maisha yao, zile ni documents tu za kutumika na wachambuzi kuhakiki mambo fulani katika kuandika vitabu comprehensive kuhusu maisha yao, na tunahitaji vitabu vingi kupata picha halisi. Siku hizi kuna biographies mpaka za kisaikolojia. Inawezekana kukahitajika uchunguzi wa changamoto za mtu aliyezaliwa bara, kukulia Zanzibar na kuwa rais wa Zanzibar na Tanzania, katika kuongoza Tanzania. Au kitabu cha kuelezea humility ya Mwinyi faida zake zilikuwa ni zipi, alivyowathamini watendaji wake na kuwaamini, na jinsi gani humility hiyo ilikuwa udhaifu kwa sababu aliwaachia sana wafanye watakavyo. Haya mengi mwenyewe hakuweza kuyaandika au kama aliyaandika aliyaandika kwa juu juu tu.

Unaposema wataalamu watafiti wandike, mmoja wa hao wataalam watafiti ni wewe. Hivyo tukurudishie changamoto. Si lazima iwe kitabu, hata makala ndefu tu inaweza kuwa chanzo kizuri kwa watakaokuja.

Nilikuwa naangalia mtandao wa Twitter (X), kuangalia maneno ya watu kuhusu msiba wa rais Mwinyi. Nikakutana na tweet ya dada mmoja Mtanzania anaitwa Carol Ndosi, anasema anasikitika sana alikuwa anatafuta hotuba za rais Mwinyi mtandaoni, lakini anazoziona ni chache sana.

Inaonekama kunatakiwa juhudi za kuanzisha Ali Hassan Mwinyi digital archive kama alivyoanzishiwa Salim Ahmed Salim ili wachunguzi wapate vyanzo muhimu katika kazi zao.
 
FB_IMG_1709567421385.jpg
 
Huwa nikionaga vijana wa hovyo wakikuletea mizaa Huwa nawashangaa maana kichwani mwako umewekeza maarifa mengi sanaaa..
 
Mkuu,

Shukurani sana. Wazee wenyewe wa hekima ndio hao wanaondoka, mwisho sisi ndio tunajikuta ndio hao wazee. Na ukianza kuchukua majukumu ya wazee, mara nyingine unatakiwa kukubali tu kuwa kuna vijana wa ovyo watasema yao tu. Ni sehemu ya demokrasia.

Nimeshangaa sana kutoa historia ya siku za Mwinyi alivyoondoa dhiki ya kununua bidhaa maduka ya kaya kwa vidaftari, kula ugali wa Yanga, kukimbizana na magari ya ugawaji, kuvaa nguo za midabwada, vijana wengi wanasikia historia hii na kuona vitu vilivyotokea zamani sana. Kuna mtu aliniuliza historia hii imeandikwa wapi?

Nikakosa hata kitabu cha kumtajia kilichoandika dhiki ya kiuchumi ya 1980-1985 kwa ukamilifu.
 
Umenena vyemaa
Pia Kwa kuongezea Kuna jamaa anaitwa ANNANIAS EDGER Huwa anasimulia simulizi za sauti zilizo andikwa na DENIS MPAGAZE...

Huwa wanatoa simulizi za viongozi mbali mbali wa afrika na Dunia Kwa ustad mkubwa...

Rai yangu watu wanaweza kuingia you tube na ku search raisi mwinyi by denis mpagaze ukapata material ya maana (adding body of knowledge)
 
Swali langu ni kweli Sheikh Thabit Kombo alikuwa akiaminiwa sana na Nyerere, je ni kwa sababu ya urafiki wao? Au kuaminiwa huko kulitokana na nini?

Ni kweli Thabit Kombo ndiye aliyependekeza Mwinyi awe mgombea Urais kutokea Zanzibar?
 
HISTORIA YA UONGOZI YA ALI HASSAN MWINYI KAMA RAIS HAIKO WAZI

UTANGULIZI

Makala hii nimeiandika baada ya kuulizwa maswali baada ya kufanya kipindi cha Maisha ya Rais Ali Hassan Mwinyi na Afrika TV2.

Najaribu hapo chini kujieleza.

Katika kipindi hiki cha televisheni yapo mengi katika maisha ya Rais Ali Hassan Mwinyi ambayo hayakuzungumzwa.

Pengine hayakuzungumzwa kwa kuwa mtayarishaji wa kipindi alipenda kumjua Sheikh Ali Hassan Mwinyi kwa upande wake mmoja tu kama Rais Muislam.

Hakutaka kuniingiza katika siasa.

Kwa uhakika hapa ndipo alipokazia katika maswali yake.

Huu ni upande mmoja wa historia ya Rais Mwinyi.

Upo upande mwengine wa Rais Mwinyi katika utawala wake.

Upande huu wa utawala wake unazunguka ndani ya serikali, unazunguka ndani ya CCM na mwisho unazunguka ndani ya taasisi zote nchini zenye uhusiano wa kuendesha nchi ukianzia vyama vya siasa hadi "argencies."
Hizi ni "ecological factors," mfano wa viumbe wanavyo uhusiana mazingira wanayoishi.

Mathalan ndani ya mbuga kuna majani ambacho ni chakula cha swala na kuna simba ambae chakula chake ni swala.

Simba kama hakula swala na swala wakawa wengi zaidi na majani ni yale yale mbuga si muda mrefu itakuwa jangwa.

Mbuga ikiwa jangwa simba na swala wote wataathirika.

Humu ndimo ilipo historia nyingine ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

Historia hii inasisimua.
Historia hii Rais Mwinyi hakuieleza katika kitabu chake, "Mzee Rukhsa Safari ya Maisha Yangu."

Historia si kama haipo kabisa lakini alipoigusia alipita pembeni kama vile hataki kukanyaga ukoka wake alioupanda na kuutunza vizuri.

Kwani ikiwa atapita katikati ya ukoka wake kuna hatari ya kutengeneza njia na wengine watapita.

Hawa wengine wakipita patakuwa njia na uzuri wa ukoka utapotea, utanywea na kuwa mfano wa majani ya kawaida yaliyokauka.

Bustani itapoteza haiba yake yaani itapoteza uzuri wake.

Mengi Rais Mwinyi kayanyamazia ndani ya kitabu chake.

Haya hayakuwa mambo ya kawaida.

Naamini waliokuwa karibu na yeye katika serikali na CCM walishangaa kuona yale mazito na muhimu kwake karashiarashia na mengine hakuyasema kamwe.

Mlango bado uko wazi kwa watafiti na wanafunzi wa historia kulijaza ombwe hili.
samahani mzee wangu niko nje ya maada yako, hivi unaweza tujuza japo kwa uchache tukio la kifo cha mwandishi wa habari ndg Stan Katabaro enzi za utawala wa Mwinyi?.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom