Yaani Rais anafitinishwa hivi hivi - Usajili wa laini simu usilete chuki

Sio kila anayemiliki simu amenunua yeye. Mwenyewe mama yangu,na ndugu wengine kadhaa nimewanunulia mimi zile simu za tochi! Mama anaweka credit ya shilingi elfu 2 kwa mwezi. Leo unataka atoke Idukilo kwenda Shinyanga mjini au Kishapu kwa ajili ya kuwatafuta NIDA!? Na anaweza akaenda siku ya kwanza asifanikiwe. Kuwa na uhakika kukamilisha zoezi lote hilo ni lazima aende mjini mara mbili hadi tatu hivi. Kumbuka hilo hakuwa kalipanga pia halina bajeti. Kinachobaki ni Rais kufitinishwa tu kwa watu hawa! Anyway labda atabadili tena statement yake kwa kurudia ile ya kwanza.

Zikizimwa watu mtashughulika, hadi ifanywe kweli mtaendelea na vijisababu mara hiki mara kile, kitambulisho ni haki ya kila mmoja, na kitamsaidia mama yako kwa mambo mengine mengi, hivyo msaidie hivyo hivyo ulivyomsaidia akapata simu.
 
Zikizimwa watu mtashughulika, hadi ifanywe kweli mtaendelea na vijisababu mara hiki mara kile, kitambulisho ni haki ya kila mmoja, na kitamsaidia mama yako kwa mambo mengine mengi, hivyo msaidie hivyo hivyo ulivyomsaidia akapata simu.
Majibu ya kibabe babe tu - umeshiba ndugu yetu. Wanavyosaidiwa huko kwenu Chato sio kama wanvyosaidiwa huku kwetu Shinyanga.
 
Majibu ya kibabe babe tu - umeshiba ndugu yetu. Wanavyosaidiwa huko kwenu Chato sio kama wanvyosaidiwa huku kwetu Shinyanga.

So kila mtu anayekubali jitihada nzuri za rais, atakua ametokea Chato, usajiri wa simu ni muhimu sana kwa usalama wa taifa, kitambulisho pia kina umuhimu mkubwa, kawasaidie bibi,babu na wazazi kijijini wacha vijisababu, siku ukijua umuhimu wake utakesha ukipambana kuwasaidia.
 
Mtu unayemiliki simu hauwezi kushindwa kufuata kitamulisho, acheni uzushi rais anafanya jitihada za kulinda watu wake dhidi ya matapeli.
Hata muda ukiongezwa miaka kumi bila kuwa mkali bado mtaendelea kusuasua.
Tayari zoezi lishaingia dosari ujayasikia ya shortuct kukwepa foleni,imekuwa biashara za watu watz ni watu wa fursa wanauza line zilizosajiliwa tayari.
 
Naweza kukuamini. Kwa idadi ya watu waliobaki kusajiliwa kwa mujibu wa TCRA hawatamalizika ndani ya siku hizi 23 zilizobaki. Na hata watakaojisajili kipindi hiki hawapati namba papo hapo. Haileti mantiki kumfungia mtu laini wakati hajapata namba hiyo japo alishajiandikisha tayari!

Sent using Jamii Forums mobile app
Rais angekuwa serious kama.badala ya kuwaagiza TCRA wafunge line ifikapo 21/01/2020, angeanza kuwaagiza Nida wahakikishe ama wametoa vitambulisho vyote ama namba kabla ya tarehe hiyo. Nimetoka Nida wilaya yangu, nikaambiwa kwamba niwe tu mpole kwa sababu ndio kwanza wanamalizia kupiga picha na kwamba hata kuzituma nida makao makuu bado. Mimi nimeandikishwa mwaka mmoja uliopita, vyote viwili nanba au kitambulisho sijapata.
 
Tayari zoezi lishaingia dosari ujayasikia ya shortuct kukwepa foleni,imekuwa biashara za watu watz ni watu wa fursa wanauza line zilizosajiliwa tayari.

Ukiuza laini yako halafu itumike kwa uhalifu, itakula kwako, akikamatwa mmoja na itangazwe nchi yote kwamba aliuza laini na ikatumika vibaya, watu watatia akili.
 
Mimi naona huo muda ni mkubwa sana,nimeshachoshwa na zile SMS za ile pesa itume kwa hii namba xxxxxxxxx jina litakuja mwanaidi mwakatope

Sent using Jamii Forums mobile app
Alitakiwa kuwahimiza NIDA wamalize kszi yao sio kuweka meisho au kama ni mwisho awape NIDA sio wananchi, ni mwaka wa 3 sasa sijawahipata hicho kitambulisho nakila mara najiandikisha
 
Ukiuza laini yako halafu itumike kwa uhalifu, itakula kwako, akikamatwa mmoja na itangazwe nchi yote kwamba aliuza laini na ikatumika vibaya, watu watatia akili.
Ujaelewa sio muhusika anauza line yake bali taarifa zake zawezatumika kuwasajilia watu wengine kuna usalama gani tunapoacha taarifa zetu kwenye database za makampuni binafsi?
 
Wakiongeza nguvu kazi NIDA na masaa ya kufanya kazi wana uwezo wa kuwamaliza watu wote hata kabla ya hizi siku 20 kwisha
 
Leo ndo mwisho trh 31 kwa mujibu wa ujumbe za Simu.Mtakaofungiwa mjiandae kuwasiliana,kwa barua
 
Moja ya taarifa muhimu unapojaza fomu ya NIDA ni namba ya simu ya mkononi na email. Sasa kwanini NIDA wanapokamilisha usajili wanashindwa kuwatumia wahusika namba zao za utambulisho kwenye email zao au namba zao za simu mpaka waende wakapange foleni kuchukua namba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehem pekee Magu atakapowanyanyua tena ni hapa hapa,itaitwa fungua mwaka atakapositisha zoez zima mpk watu wapate namba za nida... Halaf tutashangilia hureeeeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshangaa sana baada ya Rais kubadili Maelekezo yake. Mwanzoni alikiri kuwa ni vigumu usajili kukamilika kwa kutumia Vitambulisho vya Taifa lkn jana ameelekeza kuwa kufikia Tarehe 20 Januari 2020 usajili huo uwe tayari. Nikaangalia nilipo mimi huku Idukilo - ukitaka kukutana na NIDA mpaka uende Kishapu, nafuu mie nina kabaiskeli. Nikiangalia kaya kama 792 huku Idukilo wenye vitambulisho vya NIDA au namba za NIDA hawazidi 200 (hizi ni kaya zenye uelewa kidogo). Kati ya kaya hizo 792 kaya kama 500 hivi wanamiliki simu - ingawa nyingi zao ni za tochi. Sasa hawa 500 ambao pengine wanaweza kusajili laini zao kwa Vitambulisho vya NIDA ni kama hao 200 niliosema. Kwa maana hiyo kufikia Tarehe 21 Januari 2020 kijijini kwetu laini za simu zisizopungua 300 zitakuwa disabled kupata mawasiliano. Hebu chukua kijiji kingine na kingine. Yawezekana Chato, Darisalama na Dodoma hali hii isiwepo lkn kwa Tanzania nzima vitambulisho au namba za NIDA hazijawafikia wengi sana.

Maelekezo aliyoyatoa Rais kama yametoka kwa kupitia kwa washauri wake basi siamini km hawakujua ni ushauri unaoelekea kumjengea chuki Rais na wanachi wa hali ya chini ambao siku zote amesimama kidete kuwatetea. Angeweza kueleweka vizuri Rais pengine angeeleza pia ni kwa nini kabadili kauli yake ya mwanzo au angeelekeza basi usajili utumie hata utambulisho mwingine kama vile barua za watendaji, vitambulisho vya kupigia kura au namna yeyote ile wakati wananchi husika wakifuatilia vitambulisho vya NIDA. Zaidi ya yote Rais angeweza kuongeza muda usiopungua miezi minne na kuwaelekeza NIDA wafike hadi vijijini. Kwa kweli maelekezo yenye dalili za ubabe kutoka kwa Rais yanazidi kujenga chuki na yanaweza kufanya Uchaguzi ujao watu wakawa wameshazoea ubabe na wakakubaliana nao na kura wakambania kabisa.
Wakifunga line tarehe 20 January wataziletea hasara kubwa kampuni za simu ni mara mia wangezishauri kampuni za simu zipungue zisalie 3 mfano sasa Tigo kawanunua Zantel na TTCL wawanunue Airtel, voda wawanunue Halotel kuwepo na kampuni 3 kubwa itakuwa kuwa rahisi kwao, hakuna Nchi Duniani yenye kampuni. Nyingi za simu kama Tanzania.
 
Sera zinazoenda na wakati ziko Chadema usitegemee CCM kuja na jipya la kumuonea huruma Mwananchi

Ndugu zangu Watanzania uchaguzi 2020 ndio wakati wa kuiadhibu CCM
Lakini wako wachache wana mawazo haya hapa.
Sijui tuwafanyeje?
IMG_20191230_125043.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni sheria fata sheria mkuu.
Mbona walitoa mda wa kutosha kwanini ujajisajili mda wote huo???

Sent using Jamii Forums mobile app
Nchi zilizoendelea kama China South Africa na sehemu nyingi Duniani hawana Sheria za hivyo kule unanunua line kwa kitambulisho cha aina yeyote na ukitumia unatupa ukitaka ingine unanunua tena, Sheria zingine ni ni Sheria zisizo na Tija kwa Taifa mda wa kutosha ndiyo nini?
 
Back
Top Bottom