Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

Sasa nashangaa waswahili wanamkomalia mswahili mwenzao anaedili na wasanii ambao hawazidi hata hamsini , wakati hawa mabilionea wanamiliki wafanyakazi hadi 20k, kwa bilionea mmoja. Na ukiugua haulupipwi[emoji41][emoji41] .

Sent using Jamii Forums mobile app
Sometimes ngozi yetu hii ya kibantu ni shida sana.... Tuko radhi kumsaidia ama kumsifia wakuja kuliko sisi wenyewe

Jr[emoji769]
 
Hukumu za wananchi wenye hasira zipo kikatiba? washindwa kina sugu, jide na ramadee? Anayetuhumiwa mbona hakuridhika ina maana nae alikuwa ngozi ya kende?
Ni zipi hizo hukumu za wananchi?

Jr[emoji769]
 
Hakuna anayesema wahusika wasingefaidika na jasho lao, hell no! Ninachosema ni wahusika kufaidika zaidi kuliko wasanii wenyewe! Nimetoa mfano wa show ambayo ilifanyika pale Billz... nikikutajia ambacho walilipwa majority ya wale washikaji unaweza kusema "am making it up!"

Na hoja hapa ni kwamba, hata kama na wenyewe wanatakiwa kula kutokana na jasho lao (coz' no free lunch as you said) lakini sio kula kwa staili ya simulizi ya ng'ombe wanaokamuliwa bila kupewa malisho!! Kabla TMK Wanaume haijakufa, nitajie msanii mmoja tu ambae alikuwa na cha kuonesha mbali na Nature aliyekuwa na Benz ya Mtumba na nyumba Mbagala!!

Kwamba, Fella kafanya kitu positively, sidhani kama kuna anayeweza kukataa hili! Kwanza, kuwaweka Masela pamoja sio jambo dogo!! Lakini ukweli mchungu mwingine ni kwamba, wengi waliokuwa top pale TMK tayari walishakuwa hivyo hata kabla ya Fella! GWM kwa mfano, tangia enzi hizo tuko pale NASACO, Kurasini tayari GWM walikuwa wanafahamika na shoo zao za kibabe, kipindi hata Saidi Fella hajaenda South na kurudi Fella mwingine!

Hata Nature tayari alishakuwa stori mjini kwa sababu, kama kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhani hata pini kama Kigheto gheto zilitoka wakati Fella ama kabla hajaenda SA au wakati yupo uko! Na kama sikosei, nadhani hata Chege alishakuwa ameshafahamika kupitia Manyema!!! Hata Mzimu ingawaje hakuwa TMK Cream na yeye tayari alishafahamika!

Wasanii ambao walianza kufahamika exclusively kupitia management ya Fella ni watu kama akina Y-Dash, YP, Kakaman, Mheshimiwa Temba, Doro, na wengine kadhaa! Ukitoa Mheshimiwa Temba, wote hawa walikuwa wanagongea hadi fegi!!!

Na kuhusu wengine could do even worse than Fella, sikatai na ndio maana hata hapa JF nimeshasema mara nyingi, Entertainment Industry (world wide) generally imejaa dhuluma lakini kuna dhuluma zingine zinakuwa too much!
Nilihiyqki kuwa mjamaa niwe na genge kama Nature?? Fid q kill it all hizo kitu mnazoongelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sometimes ngozi yetu hii ya kibantu ni shida sana.... Tuko radhi kumsaidia ama kumsifia wakuja kuliko sisi wenyewe

Jr[emoji769]
Ndipo shida ya ngozi nyeusi ilipo, na shida ya dudu baya ni ngeda kupita kiasi , na huku hapati diet nzuri. ngeda ikizidi mtu akategemea viazi vya kukaanga na kachumbari ya masalo, hawezi kuwa saw a upstair.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee heshima kubwa chige hawa jamaa unawafahamu ndani nje.... Y-dash ama P-dash kuna mmoja alifariki.... I thought Nature kujitenga na Fella angefanya kitu bora zaidi lakini naamini aliingizwa cha kike na kukosa miongozo bora la sivyo angelisimamisha kundi lililojitenga

Jr[emoji769]
YP ndo kadanja, na mwanangu mwingine Mark 2B aka Simba!! Ingawaje Simba hakuwa kiumeni lakini alikuwa haadimiki maskani manake kitambo alikuwa mtoto wa Kurasini kabla hawajahamia Yombo!

Suala la Nature kudhani angefanya kitu bora binafsi sikutarajia sana kwa sababu Bongo Flavor ilikuwa imejaa fitina za kimuziki! Amini usiamini, sijaona mtu anayezijua fitina za muziki kumlinganisha na Fella! Ilikuwa uki-mess na Fella, hesabu umepotea kiasi kwamba, hata washikaji maskani walikuwa wanaamini Fella ni mtu wa kupuliza; mwenye safari zisizoisha za kwa bibi!!

Kwa bahati mbaya sana, Nature mwenyewe hayupo organized kwahiyo kusonga baada ya kuachana na Fella kulihitaji apate mtu anayezijua fitina za kimuziki kumzidi Fella! Enzi zile waliokuwa wanazijua vizuri fitina za Bongo Flavor ni wawili tu, Said Fella na kwa mbali, Abdul Bonge (Kakake Babu Tale)! Ndo maana usishangae Babu Tale alipoona ukubwa wa Diamond Platnumz unaelekea kumuelemea, akaamua ku-partner na Fella kum-manage Chibu!
 
Nilimuangalia Dudubaya usoni anaonekana kabisa hayupo sawa
 
Watakaokuelewa ni wachache...hasa ktk mapungufu ya watu tunaodhani hawastahili kulaumiwa kisa tu ni marehemu. Ukipata fursa ya kukaa na wasanii ndiyo utajua dhulma wanazofanyiwa na hawa mapromota.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
Haya mambo, watu wafanye kuyasikia tu!
 
Quote ya akili sana hii mzee...[emoji106]
Hatimaye Ruge amelala kwa amani... Siku zake za mwisho hazikuwa rahisi... Amepambania uhai wake kwa nguvu zake zote... Yatasemwa mengi... Yataandikwa mengi... Lakini hatimaye yataisha na maisha kusonga mbele.... Ni wiki ya Ruge...

Kwenye haya maisha kuna makundi mawili.. Kundi la washindi na kundi la washindwa.... Huwa tunaaswa sana kujifunza toka kundi la washindi... Ogopa sana kundi la washindwa... Hili kundi la washindwa linaweza kukuzushia chochote.. Kisha wakakijengea uhalisia na kukitangaza hasa... Mara nyingi hawakuzushii mema bali mabaya.... Kundi hili lina fikra za ajabu kweli... Yani kushindwa kwao kwenye lolote wanakuhusisha na wewe
Mbali ya Ruge na wadau wengine waliofanya mengi kwenye mziki wetu wa kisasa na hata kuibua vipaji vingi ni Said Fella (mkubwa Fella) naye huyu ni mhanga kama Ruge [emoji1019] japo kwa asilimia tofauti
Miaka ya mwanzoni mwa 2000 alileta mapinduzi makubwa kwenye bongo fleva kwa kuwa na kundi la kwanza lililofanikiwa sana la TMK-WANAUME...
Kundi hili lilitikisa mno likiwakilisha Uswazi na ndio likawa chachu ya kuanzishwa kwa makundi mengine rasmi kama East coast nk... Vibao vya TMK vilikuwa moto wa kuotea mbali... Nani hakumbuki Dar mpaka Moro?
Vinara wa kundi kina Juma nature wakiwa ndio wanasikika sana, wakafitinishwa, wakajazwa maneno... Upeo wa kufikiri ukawa mdogo... Wakaambiwa Fella anawanyonya, anawatumikisha wakati yeye si msanii kwahiyo anakula jasho lao bure
Sumu hii ikawaingia baadhi na chini ya Juma nature kundi la TMK-WANAUME likagawika vipande viwili.... Wenye kuona mbali wakabaki na Fella... Wenye kuona karibu wakaondoka na kuunda kundi lingine kwa mbwembwe nyingi na kutoa kibao cha kwanza NDEGE TUNDUNI... wimbo huu ulikuwa masimango tupu kwa Fella...
Fella hakutaka majibizano... Alifahamu wakati ni hakimu mzuri..... Leo hii Fella ni nani na yuko wapi na Juma nature ni nani na yuko wapi! Washindi dhidi ya washindwa....!!!
Makubwa Ruge aliyoyafanya kwenye muziki wa bongo fleva hayaonekani kwa baadhi yetu... Anatuhumiwa, anabezwa, anatukanwa, anakejeliwa... Anaitwa mnyonyaji na kila aina ya jina baya... Lakini ukiangalia wanaofanya hivyo ni akina nani!? Ni kundi dogo la washindwa.

Ruge sio malaika, Ruge sio mkamilifu ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote yule ana changamoto zake ana kushinda na kushindwa kwake.. Ni mpambanaji anayehitaji naye kutoka kimaisha... Alifanikiwa kwa kiasi chake... Akapata alichopata.... Kuna wengine kati yetu tungepata nafasi yake pengine tungekuwa wabaya zaidi yake....
Washindwa wamepata pa kutolea nyongo zao.. Yani ugumu wao wa maisha na kushindwa kwingi lawama zote ni kwa Ruge... Ruge alikuwa mjasiriamali angefanyaje kulinda kazi yake? Rip brother!
Basi sasa kwa washindwa... Ruge kaondoka, yule mnyonyaji tapeli.. Aliyekuwa kashikilia funguo za maisha yenu.... Tunataka tuone tofauti sasa... Tunataka kuwaona mkitoka kimaisha sasa kwakuwa kikwazo kimeondoka!!!!

KATIKA MAISHA OGOPA SANA KUNDI LA WASHINDWA!!! ALWAYS LEARN FROM THE BEST....

Jr[emoji769]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa mtu mzima una mlalamikia marehemu ni ajabu kwa fikra fikilishi huyu nyuma yake ana watu ambao wanaona aibu kumzuhaki marehemu wanamtumia yeye kama chambo hakuna kitu kigumu kuishi na watu wanao lalamika
 
Ruge amefanya alichostahili kufanya.Ulimwengu unajua na Mwenyezi Mungu aliyemleta duniani na kumtwaa anajua.Wanaolalamika si tu wamekosa fadhila bali wamekosa utu na heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.Tuwahurumie adhabu yao itakuwa mbaya.RIP Ruge Mutahaba.Mbele yako nyuma yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani kwa kukutoa nje ya mada, lkn darasa si lazima madawati na ubao...naomba nijifunze ya ulimwengu kutoka walimwengu...HAPO KWENYE BOLD.

Mbele yetu nyuma yako ni maneno ninayoyasikia mara nyingi, lakini sielewi inakuwaje nyuma yetu hali ya kwamba yeye ndio ametutangulia?
 
Huyu sio yule aliyejitoa fiesta baada ya kusaini mkataba. Let's make this way... Unapewa mkataba unaosoma unaridhia pasi kulazimishwa na mtu unasaini. Unaenda Insta unapiga vigeregere yereeeeewi can't wait to be up on the stage. Halafu siku ya pili unaamka zako eti unajitoa na kuanza kelele eti mkataba wakinyonyaji. Tuiteje hii?!

Ni upumbafu
 
My brother,

Ruge wasn't doing some charity work. He was not a Red Cross messiah or something. Alikuwa anatafuta kama wengine. Ndo kitu wengi tunaongelea humu. The story is the same kuanzia Makinikia ya Barrick mpaka machinga na kitambulisho cha JPM. Au house girl nyumbani kwako au kwangu anayelipwa 50k!!! Au mfanyakazi wa Bakhresa anayepewa laki mbili na nusu ingawa boss wake ndo richest man in the country!! Hakuna anayefanya kazi ya madhabahu. Kila mtu anataka kuchomoza. And in the process lazima wengine waumie. It is a cruel world. Kumlaumu Ruge au Masanja kwa hilo tunawakosea.

Are you aware kwamba nesi wa mshahara wa laki mbili au tatu analipa kodi.. Mbunge na mafao yake ya mamilioni au namba moja mwenyewe halipi kodi? Where's our rage? Au kwa sababu na sisi we are part of that crime pattern? Kwa sababu na sisi tukipata hizo nafasi we will do the same!

My aunt served the country for 40 years kama nesi. Amestaafu, mafao hata 20M hayakufika! Where is our rage.

Hapa sijaribu kumtetea marehemu au wengineo. Point yangu tuangalie wider social and economic dynamics za mifumo yetu.

Mwisho wa siku kwenye hizi debates tunasahau ukweli kwamba ubepari ni unyama. Unfortunately we are all in the tent. Wakati tunawanyoshea vidole wengine.... Tusisahau na sisi tunategemea mifumo hiyo hiyo kuendesha maisha yetu.

Masanja
 
Hatimaye Ruge amelala kwa amani... Siku zake za mwisho hazikuwa rahisi... Amepambania uhai wake kwa nguvu zake zote... Yatasemwa mengi... Yataandikwa mengi... Lakini hatimaye yataisha na maisha kusonga mbele.... Ni wiki ya Ruge...

Kwenye haya maisha kuna makundi mawili.. Kundi la washindi na kundi la washindwa.... Huwa tunaaswa sana kujifunza toka kundi la washindi... Ogopa sana kundi la washindwa... Hili kundi la washindwa linaweza kukuzushia chochote.. Kisha wakakijengea uhalisia na kukitangaza hasa... Mara nyingi hawakuzushii mema bali mabaya.... Kundi hili lina fikra za ajabu kweli... Yani kushindwa kwao kwenye lolote wanakuhusisha na wewe
Mbali ya Ruge na wadau wengine waliofanya mengi kwenye mziki wetu wa kisasa na hata kuibua vipaji vingi ni Said Fella (mkubwa Fella) naye huyu ni mhanga kama Ruge [emoji1019] japo kwa asilimia tofauti
Miaka ya mwanzoni mwa 2000 alileta mapinduzi makubwa kwenye bongo fleva kwa kuwa na kundi la kwanza lililofanikiwa sana la TMK-WANAUME...
Kundi hili lilitikisa mno likiwakilisha Uswazi na ndio likawa chachu ya kuanzishwa kwa makundi mengine rasmi kama East coast nk... Vibao vya TMK vilikuwa moto wa kuotea mbali... Nani hakumbuki Dar mpaka Moro?
Vinara wa kundi kina Juma nature wakiwa ndio wanasikika sana, wakafitinishwa, wakajazwa maneno... Upeo wa kufikiri ukawa mdogo... Wakaambiwa Fella anawanyonya, anawatumikisha wakati yeye si msanii kwahiyo anakula jasho lao bure
Sumu hii ikawaingia baadhi na chini ya Juma nature kundi la TMK-WANAUME likagawika vipande viwili.... Wenye kuona mbali wakabaki na Fella... Wenye kuona karibu wakaondoka na kuunda kundi lingine kwa mbwembwe nyingi na kutoa kibao cha kwanza NDEGE TUNDUNI... wimbo huu ulikuwa masimango tupu kwa Fella...
Fella hakutaka majibizano... Alifahamu wakati ni hakimu mzuri..... Leo hii Fella ni nani na yuko wapi na Juma nature ni nani na yuko wapi! Washindi dhidi ya washindwa....!!!
Makubwa Ruge aliyoyafanya kwenye muziki wa bongo fleva hayaonekani kwa baadhi yetu... Anatuhumiwa, anabezwa, anatukanwa, anakejeliwa... Anaitwa mnyonyaji na kila aina ya jina baya... Lakini ukiangalia wanaofanya hivyo ni akina nani!? Ni kundi dogo la washindwa.

Ruge sio malaika, Ruge sio mkamilifu ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote yule ana changamoto zake ana kushinda na kushindwa kwake.. Ni mpambanaji anayehitaji naye kutoka kimaisha... Alifanikiwa kwa kiasi chake... Akapata alichopata.... Kuna wengine kati yetu tungepata nafasi yake pengine tungekuwa wabaya zaidi yake....
Washindwa wamepata pa kutolea nyongo zao.. Yani ugumu wao wa maisha na kushindwa kwingi lawama zote ni kwa Ruge... Ruge alikuwa mjasiriamali angefanyaje kulinda kazi yake? Rip brother!
Basi sasa kwa washindwa... Ruge kaondoka, yule mnyonyaji tapeli.. Aliyekuwa kashikilia funguo za maisha yenu.... Tunataka tuone tofauti sasa... Tunataka kuwaona mkitoka kimaisha sasa kwakuwa kikwazo kimeondoka!!!!

KATIKA MAISHA OGOPA SANA KUNDI LA WASHINDWA!!! ALWAYS LEARN FROM THE BEST....

Jr[emoji769]
Mkuu umenikumbusha kisa cha Nyani na binadamu. Nyani walikuwa wanakula mahindi ya binadamu. Binadamu akawa anawafukuza wasile mahindi yake. Nyani walikuwa wanamchukia sana binadamu kwa madai kwamba anawabania. Mwaka uliofuata binadamu akafa nyani wakafanya sherehe kwamba kizuizi kimeondoka. Guess what happened.. Msimu wa mahindi ulipo fika no mahindi ..mwisho wa siku nyani wote wale wakafa a natural death. This is what will.happen kwa wasanii wengi wa bongo. Watakao fanikiwa kusurvive watakuwa wachache sana. Kifo cha Ruge ni msiba kwa tasnia ya bongofleva. Halafu nashangaa mpaka sasa hivi Diamond hajapost chochote kuhusu Ruge
 
Back
Top Bottom