Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

YOU CANT APOLOGOZE FOR HAVING CAPITALIST MENTALITY...IN EVERY ONE HATE THERE ARE 100 MORE WHO ARE HAPPY WITH HIM...RIP RUGE
 
Hakuna anayesema wahusika wasingefaidika na jasho lao, hell no! Ninachosema ni wahusika kufaidika zaidi kuliko wasanii wenyewe! Nimetoa mfano wa show ambayo ilifanyika pale Billz... nikikutajia ambacho walilipwa majority ya wale washikaji unaweza kusema "am making it up!"

Na hoja hapa ni kwamba, hata kama na wenyewe wanatakiwa kula kutokana na jasho lao (coz' no free lunch as you said) lakini sio kula kwa staili ya simulizi ya ng'ombe wanaokamuliwa bila kupewa malisho!! Kabla TMK Wanaume haijakufa, nitajie msanii mmoja tu ambae alikuwa na cha kuonesha mbali na Nature aliyekuwa na Benz ya Mtumba na nyumba Mbagala!!

Kwamba, Fella kafanya kitu positively, sidhani kama kuna anayeweza kukataa hili! Kwanza, kuwaweka Masela pamoja sio jambo dogo!! Lakini ukweli mchungu mwingine ni kwamba, wengi waliokuwa top pale TMK tayari walishakuwa hivyo hata kabla ya Fella! GWM kwa mfano, tangia enzi hizo tuko pale NASACO, Kurasini tayari GWM walikuwa wanafahamika na shoo zao za kibabe, kipindi hata Saidi Fella hajaenda South na kurudi Fella mwingine!

Hata Nature tayari alishakuwa stori mjini kwa sababu, kama kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhani hata pini kama Kigheto gheto zilitoka wakati Fella ama kabla hajaenda SA au wakati yupo uko! Na kama sikosei, nadhani hata Chege alishakuwa ameshafahamika kupitia Manyema!!! Hata Mzimu ingawaje hakuwa TMK Cream na yeye tayari alishafahamika!

Wasanii ambao walianza kufahamika exclusively kupitia management ya Fella ni watu kama akina Y-Dash, YP, Kakaman, Mheshimiwa Temba, Doro, na wengine kadhaa! Ukitoa Mheshimiwa Temba, wote hawa walikuwa wanagongea hadi fegi!!!

Na kuhusu wengine could do even worse than Fella, sikatai na ndio maana hata hapa JF nimeshasema mara nyingi, Entertainment Industry (world wide) generally imejaa dhuluma lakini kuna dhuluma zingine zinakuwa too much!
Watakaokuelewa ni wachache...hasa ktk mapungufu ya watu tunaodhani hawastahili kulaumiwa kisa tu ni marehemu. Ukipata fursa ya kukaa na wasanii ndiyo utajua dhulma wanazofanyiwa na hawa mapromota.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Aisee heshima kubwa chige hawa jamaa unawafahamu ndani nje.... Y-dash ama P-dash kuna mmoja alifariki.... I thought Nature kujitenga na Fella angefanya kitu bora zaidi lakini naamini aliingizwa cha kike na kukosa miongozo bora la sivyo angelisimamisha kundi lililojitenga

Jr[emoji769]
Siyo kwamba media zilianza kumuacha?

Kuna kisa kimoja cha msanii. Alikosana na bosi wake ikawa kila akienda radio stations wanamnyima interview akipeleka CD hawachezi. Mwishowe akaibiwa siri kuwa akapatane na meneja wake wa zamani.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
My brother,

Ruge wasn't doing some charity work. He was not a Red Cross messiah or something. Alikuwa anatafuta kama wengine. Ndo kitu wengi tunaongelea humu. The story is the same kuanzia Makinikia ya Barrick mpaka machinga na kitambulisho cha JPM. Au house girl nyumbani kwako au kwangu anayelipwa 50k!!! Au mfanyakazi wa Bakhresa anayepewa laki mbili na nusu ingawa boss wake ndo richest man in the country!! Hakuna anayefanya kazi ya madhabahu. Kila mtu anataka kuchomoza. And in the process lazima wengine waumie. It is a cruel world. Kumlaumu Ruge au Masanja kwa hilo tunawakosea.

Are you aware kwamba nesi wa mshahara wa laki mbili au tatu analipa kodi.. Mbunge na mafao yake ya mamilioni au namba moja mwenyewe halipi kodi? Where's our rage? Au kwa sababu na sisi we are part of that crime pattern? Kwa sababu na sisi tukipata hizo nafasi we will do the same!

My aunt served the country for 40 years kama nesi. Amestaafu, mafao hata 20M hayakufika! Where is our rage.

Hapa sijaribu kumtetea marehemu au wengineo. Point yangu tuangalie wider social and economic dynamics za mifumo yetu.

Mwisho wa siku kwenye hizi debates tunasahau ukweli kwamba ubepari ni unyama. Unfortunately we are all in the tent. Wakati tunawanyoshea vidole wengine.... Tusisahau na sisi tunategemea mifumo hiyo hiyo kuendesha maisha yetu.

Masanja
umemaliza 👏👏👏👏👏👏👏
 
Sio walioshindwa, malalamiko na rawama dhidi ya RUGE hayakuanza leo, wapo kina sugu, kina jide, ramadee hao nao wote wameshindwa. Dudu baya hajaanza kuongea leo dhidi ya Ruge na Clouds maana hadi alishatoa mixtape ya Manguruwe, msimpangie Dudu baya muda wa kushambulia adui yake.
 
Aisee ok sawa ni kweli kabisa RAWAMA hazikuanza leo wala tuhuma lakini kulaumiwa ama kutuhumiwa ni jambo la kwanza na kuthibitisha lawama ama tuhuma ni jambo lingine.... Kwanini wahanga waliishia tu kulalama bila kuchukua hatua zozote...!!!! Bila lawama utaishia kuota mafanikio

Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kumshitaki katika mahakama ya umma kupitia mixtape za manguruwe na antivirus vol 1 na 2, na hiki ambacho anakiendeleza dudubaya kupitia mitandao ya kijamii.
 
Najiuliza hii imetokea kwa Ruge tu, mbona kuna wanyonyaji wa kutupwa wa miaka mingi. Tena ni matajiri wa kutupa ambao wanaajiri watu kwa mikataba ya kitapeli inayohudhunisha . Na watu wanawashabikia na kubishana tajiri yupi anawazidi wenzake, ina maana Ruge alimiliki idadi gani ya wasanii kulinganisha na hawa ma bilionea wanaovuna mabilioni ya fedha kwa kutumia jasho la hao waliowaajiri ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kumshitaki katika mahakama ya umma kupitia mixtape za manguruwe na antivirus vol 1 na 2, na hiki ambacho anakiendeleza dudubaya kupitia mitandao ya kijamii.
Hii ndio naisikia leo ipo kikatiba kweli hii mahakama? Sio ya washindwa kweli hii..!? Hivi unafahamu kuwa baadhi ya watu ni kama ngozi ya kende? Kamwe hawaridhiki

Jr[emoji769]
 
Najiuliza hii imetokea kwa Ruge tu, mbona kuna wanyonyaji wa kutupwa wa miaka mingi. Tena ni matajiri wa kutupa ambao wanaajiri watu kwa mikataba ya kitapeli inayohudhunisha . Na watu wanawashabikia na kubishana tajiri yupi anawazidi wenzake, ina maana Ruge alimiliki idadi gani ya wasanii kulinganisha na hawa ma bilionea wanaovuna mabilioni ya fedha kwa kutumia jasho la hao waliowaajiri ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapo kibao hapo kariakoo wanajiita wahindi wenye asili ya wapi huko sijui

Jr[emoji769]
 
Ruge amefanya alichostahili kufanya.Ulimwengu unajua na Mwenyezi Mungu aliyemleta duniani na kumtwaa anajua.Wanaolalamika si tu wamekosa fadhila bali wamekosa utu na heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.Tuwahurumie adhabu yao itakuwa mbaya.RIP Ruge Mutahaba.Mbele yako nyuma yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Umejuaje adhabu yao itakua mbaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapo kibao hapo kariakoo wanajiita wahindi wenye asili ya wapi huko sijui

Jr[emoji769]
Sasa nashangaa waswahili wanamkomalia mswahili mwenzao anaedili na wasanii ambao hawazidi hata hamsini , wakati hawa mabilionea wanamiliki wafanyakazi hadi 20k, kwa bilionea mmoja. Na ukiugua haulupipwi[emoji41][emoji41] .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio naisikia leo ipo kikatiba kweli hii mahakama? Sio ya washindwa kweli hii..!? Hivi unafahamu kuwa baadhi ya watu ni kama ngozi ya kende? Kamwe hawaridhiki

Jr[emoji769]
Hukumu za wananchi wenye hasira zipo kikatiba? washindwa kina sugu, jide na ramadee? Anayetuhumiwa mbona hakuridhika ina maana nae alikuwa ngozi ya kende?
 
Back
Top Bottom