Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

Hakuna anayesema wahusika wasingefaidika na jasho lao, hell no! Ninachosema ni wahusika kufaidika zaidi kuliko wasanii wenyewe! Nimetoa mfano wa show ambayo ilifanyika pale Billz... nikikutajia ambacho walilipwa majority ya wale washikaji unaweza kusema "am making it up!"

Na hoja hapa ni kwamba, hata kama na wenyewe wanatakiwa kula kutokana na jasho lao (coz' no free lunch as you said) lakini sio kula kwa staili ya simulizi ya ng'ombe wanaokamuliwa bila kupewa malisho!! Kabla TMK Wanaume haijakufa, nitajie msanii mmoja tu ambae alikuwa na cha kuonesha mbali na Nature aliyekuwa na Benz ya Mtumba na nyumba Mbagala!!

Kwamba, Fella kafanya kitu positively, sidhani kama kuna anayeweza kukataa hili! Kwanza, kuwaweka Masela pamoja sio jambo dogo!! Lakini ukweli mchungu mwingine ni kwamba, wengi waliokuwa top pale TMK tayari walishakuwa hivyo hata kabla ya Fella! GWM kwa mfano, tangia enzi hizo tuko pale NASACO, Kurasini tayari GWM walikuwa wanafahamika na shoo zao za kibabe, kipindi hata Saidi Fella hajaenda South na kurudi Fella mwingine!

Hata Nature tayari alishakuwa stori mjini kwa sababu, kama kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhani hata pini kama Kigheto gheto zilitoka wakati Fella ama kabla hajaenda SA au wakati yupo uko! Na kama sikosei, nadhani hata Chege alishakuwa ameshafahamika kupitia Manyema!!! Hata Mzimu ingawaje hakuwa TMK Cream na yeye tayari alishafahamika!

Wasanii ambao walianza kufahamika exclusively kupitia management ya Fella ni watu kama akina Y-Dash, YP, Kakaman, Mheshimiwa Temba, Doro, na wengine kadhaa! Ukitoa Mheshimiwa Temba, wote hawa walikuwa wanagongea hadi fegi!!!

Na kuhusu wengine could do even worse than Fella, sikatai na ndio maana hata hapa JF nimeshasema mara nyingi, Entertainment Industry (world wide) generally imejaa dhuluma lakini kuna dhuluma zingine zinakuwa too much!
Aisee heshima kubwa chige hawa jamaa unawafahamu ndani nje.... Y-dash ama P-dash kuna mmoja alifariki.... I thought Nature kujitenga na Fella angefanya kitu bora zaidi lakini naamini aliingizwa cha kike na kukosa miongozo bora la sivyo angelisimamisha kundi lililojitenga

Jr[emoji769]
 
Kama tunakubaliana kuwa Ruge alikuwa binadamu kama wengine na alikuwa akikosea na mwingine awaye yote tuache kila mtu amdiscribe kwa upande anaoona ni sawa. Kulazimisha kila mtu kuongea mazuri tu ni udikteta kama udikteta mwingine. Turuhusu uhuru wa maoni unaolindwa na katiba yetu. Kama wapo wanaoona Ruge alikuwa mpiganaji na mkombozi wa vijana kwa kuibua fursa waachwe waseme. Wale wanaaona jamaa alikuwa mnyonyaji nao waachwe waseme.
 
Ndio msemo mpya umeingia baada ya kifo cha kaka mkubwa nini, "watanzania wanafki, Sipendi unafki, muache unafki, huo ni unafki..."

Sasa hao ambao sio wanafki waliokua wananyonywa na marehemu walishawahi kwenda kushtaki kwenye vyombo husika??
 
Basi sasa kwa washindwa... Ruge kaondoka, yule mnyonyaji tapeli.. Aliyekuwa kashikilia funguo za maisha yenu.... Tunataka tuone tofauti sasa... Tunataka kuwaona mkitoka kimaisha sasa kwakuwa kikwazo kimeondoka!!!!
Kazi kwao, tuwaone sasa!!😡😡😡
 
Tatizo kubwa hatujui wamenyonywa nini, ndio maana mi naona ni haki yao kulalamika kama tungejua vyote walivyonyonywa tungewalaumu ila kwa kuwa hatuji na inawezaekana tungevijua na sisi tungewaunga mkono na kuwalaumu hata marehemu
 
We are living in a very cruel world ndugu yangu.... Its a battle of win or lose.. Survival of the fittest.... Kuna vita ya kibiashara haikwepeki popote.... Na Ili ushinde unahitaji hata mbinu chafu... Sometimes kuwakanyaga wengine migongoni mwao kama kipandio chako.. No free lunch....

Jr[emoji769]
Mkuu hawa ndo kila siku wanataka biashara za soko huria lakini undani wa baishara hizo hawaujui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingekua ni jambo la busara sana kama ungetuambia walipo hao unaosema waliona mbali walikua na fella sasa hivi wapo wapi
 
Ruge invested in Creativity Platform and Network then wewe unakuja na kisaut chako unataka upate kila kitu,Pumbavu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji123][emoji123][emoji123]

Jr[emoji769]
 
Ingekua ni jambo la busara sana kama ungetuambia walipo hao unaosema waliona mbali walikua na fella sasa hivi wapo wapi
Ni mada huru... Yeyote anaweza kuongeza atakacho

Jr[emoji769]
 
Haya malalamiko vs utetezi vinanifanya nipate mwangaza wa kitu gani hasa kilichokuwa kinajiri huko kwenye indastri
 
Mkuu tuachane kuzungumzia habari za Marahemu tuzungumzie walio hai na mfano mzuri umemzungumzia mkubwa Fela huyu ndugu anasifika kwa unyonyaji na ni ukweli uliowazi kuwa ni muibua vipaji mzuri lakini kuibua kwake vipaji hakumuondolei sifa yake ya unyonyaji

Mfano mzuri hata wale watoto kina Aslay aliilaghai mpaka jamii kuwa amewajengea nyumba kumbe hakuna lolote na ukumbuke kitu kimoja Mnyonyaji ndio anaetajirika kwa kasi na mvuja jasho huwa aambulii chochote cha mana
Hatimaye Ruge amelala kwa amani... Siku zake za mwisho hazikuwa rahisi... Amepambania uhai wake kwa nguvu zake zote... Yatasemwa mengi... Yataandikwa mengi... Lakini hatimaye yataisha na maisha kusonga mbele.... Ni wiki ya Ruge...

Kwenye haya maisha kuna makundi mawili.. Kundi la washindi na kundi la washindwa.... Huwa tunaaswa sana kujifunza toka kundi la washindi... Ogopa sana kundi la washindwa... Hili kundi la washindwa linaweza kukuzushia chochote.. Kisha wakakijengea uhalisia na kukitangaza hasa... Mara nyingi hawakuzushii mema bali mabaya.... Kundi hili lina fikra za ajabu kweli... Yani kushindwa kwao kwenye lolote wanakuhusisha na wewe
Mbali ya Ruge na wadau wengine waliofanya mengi kwenye mziki wetu wa kisasa na hata kuibua vipaji vingi ni Said Fella (mkubwa Fella) naye huyu ni mhanga kama Ruge [emoji1019] japo kwa asilimia tofauti
Miaka ya mwanzoni mwa 2000 alileta mapinduzi makubwa kwenye bongo fleva kwa kuwa na kundi la kwanza lililofanikiwa sana la TMK-WANAUME...
Kundi hili lilitikisa mno likiwakilisha Uswazi na ndio likawa chachu ya kuanzishwa kwa makundi mengine rasmi kama East coast nk... Vibao vya TMK vilikuwa moto wa kuotea mbali... Nani hakumbuki Dar mpaka Moro?
Vinara wa kundi kina Juma nature wakiwa ndio wanasikika sana, wakafitinishwa, wakajazwa maneno... Upeo wa kufikiri ukawa mdogo... Wakaambiwa Fella anawanyonya, anawatumikisha wakati yeye si msanii kwahiyo anakula jasho lao bure
Sumu hii ikawaingia baadhi na chini ya Juma nature kundi la TMK-WANAUME likagawika vipande viwili.... Wenye kuona mbali wakabaki na Fella... Wenye kuona karibu wakaondoka na kuunda kundi lingine kwa mbwembwe nyingi na kutoa kibao cha kwanza NDEGE TUNDUNI... wimbo huu ulikuwa masimango tupu kwa Fella...
Fella hakutaka majibizano... Alifahamu wakati ni hakimu mzuri..... Leo hii Fella ni nani na yuko wapi na Juma nature ni nani na yuko wapi! Washindi dhidi ya washindwa....!!!
Makubwa Ruge aliyoyafanya kwenye muziki wa bongo fleva hayaonekani kwa baadhi yetu... Anatuhumiwa, anabezwa, anatukanwa, anakejeliwa... Anaitwa mnyonyaji na kila aina ya jina baya... Lakini ukiangalia wanaofanya hivyo ni akina nani!? Ni kundi dogo la washindwa.

Ruge sio malaika, Ruge sio mkamilifu ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote yule ana changamoto zake ana kushinda na kushindwa kwake.. Ni mpambanaji anayehitaji naye kutoka kimaisha... Alifanikiwa kwa kiasi chake... Akapata alichopata.... Kuna wengine kati yetu tungepata nafasi yake pengine tungekuwa wabaya zaidi yake....
Washindwa wamepata pa kutolea nyongo zao.. Yani ugumu wao wa maisha na kushindwa kwingi lawama zote ni kwa Ruge... Ruge alikuwa mjasiriamali angefanyaje kulinda kazi yake? Rip brother!
Basi sasa kwa washindwa... Ruge kaondoka, yule mnyonyaji tapeli.. Aliyekuwa kashikilia funguo za maisha yenu.... Tunataka tuone tofauti sasa... Tunataka kuwaona mkitoka kimaisha sasa kwakuwa kikwazo kimeondoka!!!!

KATIKA MAISHA OGOPA SANA KUNDI LA WASHINDWA!!! ALWAYS LEARN FROM THE BEST....

Ila kwa Fella na kisa cha Nature umetulisha matango pori
 
Back
Top Bottom