Mkuu
Mshana Jr!!
Baada ya kutoka nje ya Daslam, hatimae nikarejea! Kama kawaida yangu, siku ya pili tu nikatimba Kiumeni kuonana na wana!! Mkubwa Fella hakuwepo na kwahiyo Washikaji walikuwa huru sana kuongea chochote!! Kuna baadhi walidhani ningeweza kuwa mkombozi wao huku wakishindwa kufahamu nilianza kufahamiana na Fella kabla ya wote hao collectively, au hata kabla ya wenyewe kwa wenyewe hawajafahamiana!!
In short, nisingeweza kufanya jambo la kumkwaza mshikaji wa siku nyingi haidhuru hata kama kuna wakati aliwahi kuninunia kwa kudhani nawashika masikio mabwana mdogo, kwa sababu miongoni mwao kuna wengine walikuwa jeuri kwa Mkuu wao; na Mkuu wao akaamini hakuna mwingine zaidi ya huyu jamaa!!!
Wiki chache baadae ukafanyika uzinduzi wa albamu ambayo nimeisahau jina lake lakini kulikuwa na ngoma kama Twende Zetu, Chai, n.k! Sijui ilikuwaje show kubwa kama ile ifanyike Billz!
Yaliyotokea kwenye ile show, ndugu yangu ningekuomba usijimalize sana kuhusu Fella!! Ni kweli Fella aliwafanya wengi sana wafahamike but trust me, majority hakuna walichokuwa wanapata... I repeat, ukitoa wachache kama akina Nature, Temba na Chege, majority hakuna walichokuwa wanapata! Majority ya hawa kama sio wote nilikuwa nawafahamu vema (except Chege ambae hakuwa mtoto wa Temeke) na sio kuwafahamu kupitia tv!
Hata huyo Nature mwenyewe alichokuwa anakipata huwezi kulinganisha na jina lake wakati ule!!
Baada ya siku zangu za kuwa Daslam kukamilika, nikasepa zangu lakini nikawaambia washikaji kwamba TMK iki-survive kwa mwaka mmoja zaidi, basi sio mimi!! And of course, ilichukua less than 4 months kabla TMK haijasambaratika!
Hata hivyo, nadhani pale Kiumeni wapo waliokuwa wananufaika zaidi kuliko hata huyo Fella mwenyewe!!! Ujue Fella ni mjanja mjanja tu wa mjini sasa juu yake kukawa na wajanja wajanja wengine lakini wenye elimu!! Ninachotaka kusema ni kwamba, ukisikia mtu anamlalamikia Fella wala usimbishie!!!
Mimi mwenyewe nilishawahi kuzunguka kwenye radio stations zote kusambaza kazi za mmoja wa wana-TMK! Hii ilikuwa ni awamu nyingine ya kuwapo Daslam! Jambo ambalo nakumbuka hadi leo, tumefika pale Magic, jamaa wakaonekana hawana furaha kabisa na ujio wetu! Yaani wakati wanachukua CD walionekana wazi waliichukua kutoa lawama!!
Hadi siku zangu za kuwapo Daslam zinaisha, sikuwahi kusikia ngoma yoyote ikipigwa, ingawaje tulishapata taarifa kabla kwamba Mkubwa Fella alishapita kabla yetu kufanya fitina!!!! And trust me, narudia, trust me, linapokuja suala la fitina kwenye Bongo Flavor, ile namba kaa nayo mbali!!!! Huyo Ruge inawezekana alikuwa juu ya Fella kwa sababu yeye alikuwa na nyenzo!!!
Tukija kwa upande wa marehemu, lazima niseme wazi mimi nimekuwa mtetezi mkubwa wa Ruge hapa jamvini kwa sababu nafahamu mchango wake! Lakini kingine, wengi waliokuwa wanamlalamikia Ruge ni wale ambao walikuwa wanalalamika baada ya kuwa wamesha-drop!! Na wengine ulalamishi wao ulikuwa wa kijinga; unaoonesha walikuwa hawafahamu vizuri biashara kati yao na Clouds!
Lakini habari za Ruge hata Juma Nature mwenyewe anazifahamu! Mchizi akalazimika kuweka usela na ustaa pembeni na kwenda kupiga goti kwa Ruge! Hapa nazungumzia enzi hata akina Diamond hawafahamiki!!!