Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

Ajabu ya watanzania.... ktk wanaomlaumu RUGE... wapo wezi wa mali za umma! wapo wawindaji haramu! wapo wauza "sembe", wapo wasaii wezi wa nyimbo za wenzao.. wapo matapeli wa pesa, mapenzi... wapo waliokataa watoto... wapo.... wanatuaminisha wao ni watakatifu......kwa kifupi ni hadithi za Boriti na Kibanzi!
 
Wakati fulani nikiwa nasoma darasani ulitolewa mfano ambao ulizungumzia haki ni nini?

Jaji aliyeulizwa swali hilo akajibu kuwa mfano wa haki ni kama ambapo kesi ingekuwepo mahakamani, na jaji ni yeye, halafu wanaoshitakiana mbele zake ni shetani na baba yake na jaji.

Akasema tena kuwa ikiwa katika kesi ile shetani atatoa utetezi wa kweli basi atampa ushindi dhidi ya baba yake mzazi hata kama yeye ni shetani. Hiyo ndiyo haki.

Bandiko hili la ndugu Mshana tayari limeshawachora watu wanaomlalamikia marehemu kama WASHINDWA. Na marehemu amechorwa kama MSHINDI.

Kabla ya kuhitimisha hivyo mapema, ni vyema kama tungejiridhisha kuwa hayo madai ya miaka mingi ya baadhi ya wasanii yana ukweli wowote?

Je ni kweli marehemu alikuwa anatenda hayo mabaya yaliyolalamikiwa sana? Hao walioitwa kuwa ni washindwa huenda wana hoja za msingi zinazohitaji kutupiwa jicho bila kuathiriwa na emotions/sympathy za msiba. Maana it is understandable kuwa panapokuwa na msiba emotions side ya ubinadamu inaweza kuathiri mjadala dhidi ya marehemu kwani sisi wanadamu tunayo hali ya kumuhurumia marehemu na kuyasahau mabaya yake.

Iwe iwavyo, mfumo wa kibiashara tulionao ni wa kibepari, na hata ktk mziki wetu pia. Ni wanamuziki wachache sana hapa bongo waliweza kufaidishwa na mziki kwa kiwango cha kuridhisha...labda kidogo kwa sasa unaweza kuona namna mziki unavyowalipa wasanii...sijui ni industry imechange? Msanii unakuta ana jina kubwa lakini haliendani na assets zake. Where has the money gone? Hapo katikati kuna system inayokula kabla msanii hajala. Na hii ndiyo imekuwa lalamiko la wasanii for years....so hao wanaoitwa washindwa wasibezwe sana.

Upo mfumo ambao wao wasanii wengi hawawezi kuushinda kwa kuwa mmoja ana capita mwingine hana, and that is capitalism. Mfumo huu pia umeenea duaniani kote, hata huko holywood ma don ni recording companies, wasanii hulipwa a decent sum tu.
 
Sasa yule wa jumba jeupe anakosa nn kwa mfano? Mutu una kila kitu majeshi yako pesa zako aridhi yako ila bado unakomoa kila mutu. Yani sijui icho cheo ningepewa mm basi tu.
Wewe wasema mkuu
 
Hatimaye Ruge amelala kwa amani... Siku zake za mwisho hazikuwa rahisi... Amepambania uhai wake kwa nguvu zake zote... Yatasemwa mengi... Yataandikwa mengi... Lakini hatimaye yataisha na maisha kusonga mbele.... Ni wiki ya Ruge...

Kwenye haya maisha kuna makundi mawili.. Kundi la washindi na kundi la washindwa.... Huwa tunaaswa sana kujifunza toka kundi la washindi... Ogopa sana kundi la washindwa... Hili kundi la washindwa linaweza kukuzushia chochote.. Kisha wakakijengea uhalisia na kukitangaza hasa... Mara nyingi hawakuzushii mema bali mabaya.... Kundi hili lina fikra za ajabu kweli... Yani kushindwa kwao kwenye lolote wanakuhusisha na wewe
Mbali ya Ruge na wadau wengine waliofanya mengi kwenye mziki wetu wa kisasa na hata kuibua vipaji vingi ni Said Fella (mkubwa Fella) naye huyu ni mhanga kama Ruge [emoji1019] japo kwa asilimia tofauti
Miaka ya mwanzoni mwa 2000 alileta mapinduzi makubwa kwenye bongo fleva kwa kuwa na kundi la kwanza lililofanikiwa sana la TMK-WANAUME...
Kundi hili lilitikisa mno likiwakilisha Uswazi na ndio likawa chachu ya kuanzishwa kwa makundi mengine rasmi kama East coast nk... Vibao vya TMK vilikuwa moto wa kuotea mbali... Nani hakumbuki Dar mpaka Moro?
Vinara wa kundi kina Juma nature wakiwa ndio wanasikika sana, wakafitinishwa, wakajazwa maneno... Upeo wa kufikiri ukawa mdogo... Wakaambiwa Fella anawanyonya, anawatumikisha wakati yeye si msanii kwahiyo anakula jasho lao bure
Sumu hii ikawaingia baadhi na chini ya Juma nature kundi la TMK-WANAUME likagawika vipande viwili.... Wenye kuona mbali wakabaki na Fella... Wenye kuona karibu wakaondoka na kuunda kundi lingine kwa mbwembwe nyingi na kutoa kibao cha kwanza NDEGE TUNDUNI... wimbo huu ulikuwa masimango tupu kwa Fella...
Fella hakutaka majibizano... Alifahamu wakati ni hakimu mzuri..... Leo hii Fella ni nani na yuko wapi na Juma nature ni nani na yuko wapi! Washindi dhidi ya washindwa....!!!
Makubwa Ruge aliyoyafanya kwenye muziki wa bongo fleva hayaonekani kwa baadhi yetu... Anatuhumiwa, anabezwa, anatukanwa, anakejeliwa... Anaitwa mnyonyaji na kila aina ya jina baya... Lakini ukiangalia wanaofanya hivyo ni akina nani!? Ni kundi dogo la washindwa.

Ruge sio malaika, Ruge sio mkamilifu ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote yule ana changamoto zake ana kushinda na kushindwa kwake.. Ni mpambanaji anayehitaji naye kutoka kimaisha... Alifanikiwa kwa kiasi chake... Akapata alichopata.... Kuna wengine kati yetu tungepata nafasi yake pengine tungekuwa wabaya zaidi yake....
Washindwa wamepata pa kutolea nyongo zao.. Yani ugumu wao wa maisha na kushindwa kwingi lawama zote ni kwa Ruge... Ruge alikuwa mjasiriamali angefanyaje kulinda kazi yake? Rip brother!
Basi sasa kwa washindwa... Ruge kaondoka, yule mnyonyaji tapeli.. Aliyekuwa kashikilia funguo za maisha yenu.... Tunataka tuone tofauti sasa... Tunataka kuwaona mkitoka kimaisha sasa kwakuwa kikwazo kimeondoka!!!!

KATIKA MAISHA OGOPA SANA KUNDI LA WASHINDWA!!! ALWAYS LEARN FROM THE BEST....

Jr[emoji769]
good post
 
Wakati fulani nikiwa nasoma darasani ulitolewa mfano ambao ulizungumzia haki ni nini?

Jaji aliyeulizwa swali hilo akajibu kuwa mfano wa haki ni kama ambapo kesi ingekuwepo mahakamani, na jaji ni yeye, halafu wanaoshitakiana mbele zake ni shetani na baba yake na jaji.

Akasema tena kuwa ikiwa katika kesi ile shetani atatoa utetezi wa kweli basi atampa ushindi dhidi ya baba yake mzazi hata kama yeye ni shetani. Hiyo ndiyo haki.

Bandiko hili la ndugu Mshana tayari limeshawachora watu wanaomlalamikia marehemu kama WASHINDWA. Na marehemu amechorwa kama MSHINDI.

Kabla ya kuhitimisha hivyo mapema, ni vyema kama tungejiridhisha kuwa hayo madai ya miaka mingi ya baadhi ya wasanii yana ukweli wowote?

Je ni kweli marehemu alikuwa anatenda hayo mabaya yaliyolalamikiwa sana? Hao walioitwa kuwa ni washindwa huenda wana hoja za msingi zinazohitaji kutupiwa jicho bila kuathiriwa na emotions/sympathy za msiba. Maana it is understandable kuwa panapokuwa na msiba emotions side ya ubinadamu inaweza kuathiri mjadala dhidi ya marehemu kwani sisi wanadamu tunayo hali ya kumuhurumia marehemu na kuyasahau mabaya yake.

Iwe iwavyo, mfumo wa kibiashara tulionao ni wa kibepari, na hata ktk mziki wetu pia. Ni wanamuziki wachache sana hapa bongo waliweza kufaidishwa na mziki kwa kiwango cha kuridhisha...labda kidogo kwa sasa unaweza kuona namna mziki unavyowalipa wasanii...sijui ni industry imechange? Msanii unakuta ana jina kubwa lakini haliendani na assets zake. Where has the money gone? Hapo katikati kuna system inayokula kabla msanii hajala. Na hii ndiyo imekuwa lalamiko la wasanii for years....so hao wanaoitwa washindwa wasibezwe sana.

Upo mfumo ambao wao wasanii wengi hawawezi kuushinda kwa kuwa mmoja ana capita mwingine hana, and that is capitalism. Mfumo huu pia umeenea duaniani kote, hata huko holywood ma don ni recording companies, wasanii hulipwa a decent sum tu.
Hoja zako zimenikumbusha jinsi nchi za ulaya zinavyofaidika na rasilimali za africa huku africa ikiendelea kuwa maskini.....The system is the same km aliyokuwa anaitumia ruge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ALWAYS LEARN FROM THE BEST

Jr[emoji769]

I like your idea that "ALWAYS LEARN FROM THE BEST". Unfortunately, majority of us aren't even able to identify who are the best!!. Ndiyo tatizo kubwa linaloendelea kututafuna wa-Tanzania mpaka leo, tangu enzi za Mwalimu!
 
Hatimaye Ruge amelala kwa amani... Siku zake za mwisho hazikuwa rahisi... Amepambania uhai wake kwa nguvu zake zote... Yatasemwa mengi... Yataandikwa mengi... Lakini hatimaye yataisha na maisha kusonga mbele.... Ni wiki ya Ruge...

Kwenye haya maisha kuna makundi mawili.. Kundi la washindi na kundi la washindwa.... Huwa tunaaswa sana kujifunza toka kundi la washindi... Ogopa sana kundi la washindwa... Hili kundi la washindwa linaweza kukuzushia chochote.. Kisha wakakijengea uhalisia na kukitangaza hasa... Mara nyingi hawakuzushii mema bali mabaya.... Kundi hili lina fikra za ajabu kweli... Yani kushindwa kwao kwenye lolote wanakuhusisha na wewe
Mbali ya Ruge na wadau wengine waliofanya mengi kwenye mziki wetu wa kisasa na hata kuibua vipaji vingi ni Said Fella (mkubwa Fella) naye huyu ni mhanga kama Ruge [emoji1019] japo kwa asilimia tofauti
Miaka ya mwanzoni mwa 2000 alileta mapinduzi makubwa kwenye bongo fleva kwa kuwa na kundi la kwanza lililofanikiwa sana la TMK-WANAUME...
Kundi hili lilitikisa mno likiwakilisha Uswazi na ndio likawa chachu ya kuanzishwa kwa makundi mengine rasmi kama East coast nk... Vibao vya TMK vilikuwa moto wa kuotea mbali... Nani hakumbuki Dar mpaka Moro?
Vinara wa kundi kina Juma nature wakiwa ndio wanasikika sana, wakafitinishwa, wakajazwa maneno... Upeo wa kufikiri ukawa mdogo... Wakaambiwa Fella anawanyonya, anawatumikisha wakati yeye si msanii kwahiyo anakula jasho lao bure
Sumu hii ikawaingia baadhi na chini ya Juma nature kundi la TMK-WANAUME likagawika vipande viwili.... Wenye kuona mbali wakabaki na Fella... Wenye kuona karibu wakaondoka na kuunda kundi lingine kwa mbwembwe nyingi na kutoa kibao cha kwanza NDEGE TUNDUNI... wimbo huu ulikuwa masimango tupu kwa Fella...
Fella hakutaka majibizano... Alifahamu wakati ni hakimu mzuri..... Leo hii Fella ni nani na yuko wapi na Juma nature ni nani na yuko wapi! Washindi dhidi ya washindwa....!!!
Makubwa Ruge aliyoyafanya kwenye muziki wa bongo fleva hayaonekani kwa baadhi yetu... Anatuhumiwa, anabezwa, anatukanwa, anakejeliwa... Anaitwa mnyonyaji na kila aina ya jina baya... Lakini ukiangalia wanaofanya hivyo ni akina nani!? Ni kundi dogo la washindwa.

Ruge sio malaika, Ruge sio mkamilifu ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote yule ana changamoto zake ana kushinda na kushindwa kwake.. Ni mpambanaji anayehitaji naye kutoka kimaisha... Alifanikiwa kwa kiasi chake... Akapata alichopata.... Kuna wengine kati yetu tungepata nafasi yake pengine tungekuwa wabaya zaidi yake....
Washindwa wamepata pa kutolea nyongo zao.. Yani ugumu wao wa maisha na kushindwa kwingi lawama zote ni kwa Ruge... Ruge alikuwa mjasiriamali angefanyaje kulinda kazi yake? Rip brother!
Basi sasa kwa washindwa... Ruge kaondoka, yule mnyonyaji tapeli.. Aliyekuwa kashikilia funguo za maisha yenu.... Tunataka tuone tofauti sasa... Tunataka kuwaona mkitoka kimaisha sasa kwakuwa kikwazo kimeondoka!!!!

KATIKA MAISHA OGOPA SANA KUNDI LA WASHINDWA!!! ALWAYS LEARN FROM THE BEST....

Jr[emoji769]
Kwa mtazamo wangu, Ruge alishindwa kutofautisha mahusiano na kazi, kwamba tunaweza kutofautiana kwenye mtazamo na still tukaendelea kufanya kazi pamoja......wengi aliopishana nao kwa mawazo aliwaona maadui zake
 
Hivi P Funky anasemaje? Hajasema chochote kuhusu Ruge kweli?

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Ni hulka ya binadamu kulaumu wengine kwa kushindwa kwake. Mwisho wa siku ndo maana yakaitwa maisha. Kikubwa kama kwenye nafasi yako unaweza kutenda haki au kuwapa tabasamu walio chini yako basi fanya hivyo. Haijalishi wewe ni nani.. Hata kama ni mfagizi au mtunza bustani ya Mshana. Dunia hii tunateswa na uchoyo na tamaa za kumiliki kila kitu.

Tunapambana mwisho wa siku ni ubatili mtupu. Nadhani håtma ya binadamu hapa duniani.. Ndo kitu pekee kinachoiunganisha dini na sayansi. Bila kujali kama kuna maisha baada ya haya tuliyonayo. Ukikaa ukajiuliza binadamu anahangaikia nini.... Hutakaa upate jibu... What a cruel world!

Pumzika kwa amani brother!
Masanja umeongea vema. Anayelea wanao na kuangalia nyumba yako unamlipa Sh.50K halafu unamlaumu Ruge ni mnyonyaji na matusi tele. Pamoja na mifano kadha wa kadha uliyotoa unastahili zawadi ya insha bora. RIP Ruge .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dudu baya kajipambanua kwa kuwa muwazi ila kuna wengi wanalia kama samaki machozi yanaenda na maji. Rubi na wengine wengi kutoka THT walishalalamika sana juu ya mawingu media. Unaweza ukaona bifu kati ya WCB. Jide wengine walioachwa kwenye fiesta kisa waligomea ujira mdogo. Yanayofanywa na clouds media wanayajua wasanii. Sie wasikilizaji tutege masikio na macho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesema kuna watu waliachwa kwenye fiesta kisa waligomea ujira kidogo.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waliodhulumiwa ndio wanaolalamika, kwanini halalamikiwi mzee Mengi?
 
Sioni tatizo sana kwa watu kusema mabaya ya Ruge au awaye yoyote yule. Maana kwa kujua mabaya ya mtu, tunapata nafasi nzuri zaidi ya kupima mazuri yake.

Binafsi huwa sipendi a "single story"! I like "SWOT analysis" ya mtu au kitu. Jambo linalofanana na hili linafanywa pia na Kanisa kabla ya kumtangaza mtu "Mwenyeheri" au "Mtakatifu".

Si sawa kuwaita wanaosema mabaya ya Ruge kuwa ni washindwa. Ruge alikuwa binadamu tu na bila ya shaka alikuwa na mapungufu mengi tu kama tulivyo wengine. Waacheni waseme, ili tunaobakia tujifunze na pengine kuepuka kufanya mambo ambayo tinasikia Marehemu Ruge akituhumiwa kufanya ambayo hayakupendeza baadhi ya watu.

RIP Ruge. Bila ya shaka Tanzania imekupoteza mtu muhimu sana. Tutakukumbuka na kuishi mazuri yako.
 
Back
Top Bottom