Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

Ni hulka ya binadamu kulaumu wengine kwa kushindwa kwake. Mwisho wa siku ndo maana yakaitwa maisha. Kikubwa kama kwenye nafasi yako unaweza kutenda haki au kuwapa tabasamu walio chini yako basi fanya hivyo. Haijalishi wewe ni nani.. Hata kama ni mfagizi au mtunza bustani ya Mshana. Dunia hii tunateswa na uchoyo na tamaa za kumiliki kila kitu.

Tunapambana mwisho wa siku ni ubatili mtupu. Nadhani håtma ya binadamu hapa duniani.. Ndo kitu pekee kinachoiunganisha dini na sayansi. Bila kujali kama kuna maisha baada ya haya tuliyonayo. Ukikaa ukajiuliza binadamu anahangaikia nini.... Hutakaa upate jibu... What a cruel world!

Pumzika kwa amani brother!
Sasa yule wa jumba jeupe anakosa nn kwa mfano? Mutu una kila kitu majeshi yako pesa zako aridhi yako ila bado unakomoa kila mutu. Yani sijui icho cheo ningepewa mm basi tu.
 
Amesema ameitwa na polisi tena kwa kupigiwa cm! Na hpo ndipo nilipoona dalili za kuhojiwa na kuachiwa, wanazidi kumpa ujiko uchwara wangemshikilia hta miezi 7 lupango ili usela mavi umtoke,

Sent using Jamii Forums mobile app
Anataka publicity... Na waandishi wetu hawa wa bongo watamsubiri na vikamera vyao uchwara watamsubiri... Huyu anyakuliwe kimyakimya nite kali

Jr[emoji769]
 
Mkuu Mshana Jr!!

Baada ya kutoka nje ya Daslam, hatimae nikarejea! Kama kawaida yangu, siku ya pili tu nikatimba Kiumeni kuonana na wana!! Mkubwa Fella hakuwepo na kwahiyo Washikaji walikuwa huru sana kuongea chochote!! Kuna baadhi walidhani ningeweza kuwa mkombozi wao huku wakishindwa kufahamu nilianza kufahamiana na Fella kabla ya wote hao collectively, au hata kabla ya wenyewe kwa wenyewe hawajafahamiana!!

In short, nisingeweza kufanya jambo la kumkwaza mshikaji wa siku nyingi haidhuru hata kama kuna wakati aliwahi kuninunia kwa kudhani nawashika masikio mabwana mdogo, kwa sababu miongoni mwao kuna wengine walikuwa jeuri kwa Mkuu wao; na Mkuu wao akaamini hakuna mwingine zaidi ya huyu jamaa!!!

Wiki chache baadae ukafanyika uzinduzi wa albamu ambayo nimeisahau jina lake lakini kulikuwa na ngoma kama Twende Zetu, Chai, n.k! Sijui ilikuwaje show kubwa kama ile ifanyike Billz!

Yaliyotokea kwenye ile show, ndugu yangu ningekuomba usijimalize sana kuhusu Fella!! Ni kweli Fella aliwafanya wengi sana wafahamike but trust me, majority hakuna walichokuwa wanapata... I repeat, ukitoa wachache kama akina Nature, Temba na Chege, majority hakuna walichokuwa wanapata! Majority ya hawa kama sio wote nilikuwa nawafahamu vema (except Chege ambae hakuwa mtoto wa Temeke) na sio kuwafahamu kupitia tv!

Hata huyo Nature mwenyewe alichokuwa anakipata huwezi kulinganisha na jina lake wakati ule!!

Baada ya siku zangu za kuwa Daslam kukamilika, nikasepa zangu lakini nikawaambia washikaji kwamba TMK iki-survive kwa mwaka mmoja zaidi, basi sio mimi!! And of course, ilichukua less than 4 months kabla TMK haijasambaratika!

Hata hivyo, nadhani pale Kiumeni wapo waliokuwa wananufaika zaidi kuliko hata huyo Fella mwenyewe!!! Ujue Fella ni mjanja mjanja tu wa mjini sasa juu yake kukawa na wajanja wajanja wengine lakini wenye elimu!! Ninachotaka kusema ni kwamba, ukisikia mtu anamlalamikia Fella wala usimbishie!!!

Mimi mwenyewe nilishawahi kuzunguka kwenye radio stations zote kusambaza kazi za mmoja wa wana-TMK! Hii ilikuwa ni awamu nyingine ya kuwapo Daslam! Jambo ambalo nakumbuka hadi leo, tumefika pale Magic, jamaa wakaonekana hawana furaha kabisa na ujio wetu! Yaani wakati wanachukua CD walionekana wazi waliichukua kutoa lawama!!

Hadi siku zangu za kuwapo Daslam zinaisha, sikuwahi kusikia ngoma yoyote ikipigwa, ingawaje tulishapata taarifa kabla kwamba Mkubwa Fella alishapita kabla yetu kufanya fitina!!!! And trust me, narudia, trust me, linapokuja suala la fitina kwenye Bongo Flavor, ile namba kaa nayo mbali!!!! Huyo Ruge inawezekana alikuwa juu ya Fella kwa sababu yeye alikuwa na nyenzo!!!

Tukija kwa upande wa marehemu, lazima niseme wazi mimi nimekuwa mtetezi mkubwa wa Ruge hapa jamvini kwa sababu nafahamu mchango wake! Lakini kingine, wengi waliokuwa wanamlalamikia Ruge ni wale ambao walikuwa wanalalamika baada ya kuwa wamesha-drop!! Na wengine ulalamishi wao ulikuwa wa kijinga; unaoonesha walikuwa hawafahamu vizuri biashara kati yao na Clouds!

Lakini habari za Ruge hata Juma Nature mwenyewe anazifahamu! Mchizi akalazimika kuweka usela na ustaa pembeni na kwenda kupiga goti kwa Ruge! Hapa nazungumzia enzi hata akina Diamond hawafahamiki!!!
chige the end justifies the means.... No free lunch popote... Fella ni mpambanaji akipata nafasi anaitumia vema.. Anybody can do this... Even worse than Fella.... Lakini in general sense kuna kitu Fella kafanya positively n remarkable kwenye bongo fleva

Jr[emoji769]
 
Pitieni Pitieni na uzi aloandika lady Jay dee pia maana watu wanataka kuaminisha wengne kuamarehemu hakua na mapungufu pia. Kiukweli wanaolalamika ukichunguza kinawaumiza ni kwamba Mr ruge licha ya kuofautiana na mtu bado alikua anapambana kw njia nyingne kukata mrija wa ridhki ya wengne kwa vikwazo kupitia wadau wengine
Vinaitwa vikwazo nj lazima uta-surrender tu si unamuona N .Korea yaan msanii yeyote atakayeshilikiana na wewe naye anakuwa adui.Hiyo ndo the art of war ila ngoja tuone bas akina Dudubaya kama watafanya la maana kipindi hiki Ruge hayupo
 
chige the end justifies the means.... No free lunch popote... Fella ni mpambanaji akipata nafasi anaitumia vema.. Anybody can do this... Even worse than Fella.... Lakini in general sense kuna kitu Fella kafanya positively n remarkable kwenye bongo fleva

Jr[emoji769]
Reserve your comment it may be needed for future use.
 
Hatimaye Ruge amelala kwa amani... Siku zake za mwisho hazikuwa rahisi... Amepambania uhai wake kwa nguvu zake zote... Yatasemwa mengi... Yataandikwa mengi... Lakini hatimaye yataisha na maisha kusonga mbele.... Ni wiki ya Ruge...

Kwenye haya maisha kuna makundi mawili.. Kundi la washindi na kundi la washindwa.... Huwa tunaaswa sana kujifunza toka kundi la washindi... Ogopa sana kundi la washindwa... Hili kundi la washindwa linaweza kukuzushia chochote.. Kisha wakakijengea uhalisia na kukitangaza hasa... Mara nyingi hawakuzushii mema bali mabaya.... Kundi hili lina fikra za ajabu kweli... Yani kushindwa kwao kwenye lolote wanakuhusisha na wewe
Mbali ya Ruge na wadau wengine waliofanya mengi kwenye mziki wetu wa kisasa na hata kuibua vipaji vingi ni Said Fella (mkubwa Fella) naye huyu ni mhanga kama Ruge [emoji1019] japo kwa asilimia tofauti
Miaka ya mwanzoni mwa 2000 alileta mapinduzi makubwa kwenye bongo fleva kwa kuwa na kundi la kwanza lililofanikiwa sana la TMK-WANAUME...
Kundi hili lilitikisa mno likiwakilisha Uswazi na ndio likawa chachu ya kuanzishwa kwa makundi mengine rasmi kama East coast nk... Vibao vya TMK vilikuwa moto wa kuotea mbali... Nani hakumbuki Dar mpaka Moro?
Vinara wa kundi kina Juma nature wakiwa ndio wanasikika sana, wakafitinishwa, wakajazwa maneno... Upeo wa kufikiri ukawa mdogo... Wakaambiwa Fella anawanyonya, anawatumikisha wakati yeye si msanii kwahiyo anakula jasho lao bure
Sumu hii ikawaingia baadhi na chini ya Juma nature kundi la TMK-WANAUME likagawika vipande viwili.... Wenye kuona mbali wakabaki na Fella... Wenye kuona karibu wakaondoka na kuunda kundi lingine kwa mbwembwe nyingi na kutoa kibao cha kwanza NDEGE TUNDUNI... wimbo huu ulikuwa masimango tupu kwa Fella...
Fella hakutaka majibizano... Alifahamu wakati ni hakimu mzuri..... Leo hii Fella ni nani na yuko wapi na Juma nature ni nani na yuko wapi! Washindi dhidi ya washindwa....!!!
Makubwa Ruge aliyoyafanya kwenye muziki wa bongo fleva hayaonekani kwa baadhi yetu... Anatuhumiwa, anabezwa, anatukanwa, anakejeliwa... Anaitwa mnyonyaji na kila aina ya jina baya... Lakini ukiangalia wanaofanya hivyo ni akina nani!? Ni kundi dogo la washindwa.

Ruge sio malaika, Ruge sio mkamilifu ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote yule ana changamoto zake ana kushinda na kushindwa kwake.. Ni mpambanaji anayehitaji naye kutoka kimaisha... Alifanikiwa kwa kiasi chake... Akapata alichopata.... Kuna wengine kati yetu tungepata nafasi yake pengine tungekuwa wabaya zaidi yake....
Washindwa wamepata pa kutolea nyongo zao.. Yani ugumu wao wa maisha na kushindwa kwingi lawama zote ni kwa Ruge... Ruge alikuwa mjasiriamali angefanyaje kulinda kazi yake? Rip brother!
Basi sasa kwa washindwa... Ruge kaondoka, yule mnyonyaji tapeli.. Aliyekuwa kashikilia funguo za maisha yenu.... Tunataka tuone tofauti sasa... Tunataka kuwaona mkitoka kimaisha sasa kwakuwa kikwazo kimeondoka!!!!

KATIKA MAISHA OGOPA SANA KUNDI LA WASHINDWA!!! ALWAYS LEARN FROM THE BEST....

Jr[emoji769]

splendid
 
Asante mkuu katika makundi hayo mawili mimi nimechagua katika uhai wangu wote kuwa upande wa kundi la washindi.
 
Huyu sio yule aliyejitoa fiesta baada ya kusaini mkataba. Let's make this way... Unapewa mkataba unaosoma unaridhia pasi kulazimishwa na mtu unasaini. Unaenda Insta unapiga vigeregere yereeeeewi can't wait to be up on the stage. Halafu siku ya pili unaamka zako eti unajitoa na kuanza kelele eti mkataba wakinyonyaji. Tuiteje hii?!

Mkuu tatizo ni elimu na unafiki.
 
Let's wait and how they gonna thrive now, waliyetuaminisha kuwa ni ukuta between them and success ameshatutoka so no more excuses.
 
chige the end justifies the means.... No free lunch popote... Fella ni mpambanaji akipata nafasi anaitumia vema.. Anybody can do this... Even worse than Fella.... Lakini in general sense kuna kitu Fella kafanya positively n remarkable kwenye bongo fleva

Jr[emoji769]
Hakuna anayesema wahusika wasingefaidika na jasho lao, hell no! Ninachosema ni wahusika kufaidika zaidi kuliko wasanii wenyewe! Nimetoa mfano wa show ambayo ilifanyika pale Billz... nikikutajia ambacho walilipwa majority ya wale washikaji unaweza kusema "am making it up!"

Na hoja hapa ni kwamba, hata kama na wenyewe wanatakiwa kula kutokana na jasho lao (coz' no free lunch as you said) lakini sio kula kwa staili ya simulizi ya ng'ombe wanaokamuliwa bila kupewa malisho!! Kabla TMK Wanaume haijakufa, nitajie msanii mmoja tu ambae alikuwa na cha kuonesha mbali na Nature aliyekuwa na Benz ya Mtumba na nyumba Mbagala!!

Kwamba, Fella kafanya kitu positively, sidhani kama kuna anayeweza kukataa hili! Kwanza, kuwaweka Masela pamoja sio jambo dogo!! Lakini ukweli mchungu mwingine ni kwamba, wengi waliokuwa top pale TMK tayari walishakuwa hivyo hata kabla ya Fella! GWM kwa mfano, tangia enzi hizo tuko pale NASACO, Kurasini tayari GWM walikuwa wanafahamika na shoo zao za kibabe, kipindi hata Saidi Fella hajaenda South na kurudi Fella mwingine!

Hata Nature tayari alishakuwa stori mjini kwa sababu, kama kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhani hata pini kama Kigheto gheto zilitoka wakati Fella ama kabla hajaenda SA au wakati yupo uko! Na kama sikosei, nadhani hata Chege alishakuwa ameshafahamika kupitia Manyema!!! Hata Mzimu ingawaje hakuwa TMK Cream na yeye tayari alishafahamika!

Wasanii ambao walianza kufahamika exclusively kupitia management ya Fella ni watu kama akina Y-Dash, YP, Kakaman, Mheshimiwa Temba, Doro, na wengine kadhaa! Ukitoa Mheshimiwa Temba, wote hawa walikuwa wanagongea hadi fegi!!!

Na kuhusu wengine could do even worse than Fella, sikatai na ndio maana hata hapa JF nimeshasema mara nyingi, Entertainment Industry (world wide) generally imejaa dhuluma lakini kuna dhuluma zingine zinakuwa too much!
 
Ruge amefanya alichostahili kufanya.Ulimwengu unajua na Mwenyezi Mungu aliyemleta duniani na kumtwaa anajua.Wanaolalamika si tu wamekosa fadhila bali wamekosa utu na heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.Tuwahurumie adhabu yao itakuwa mbaya.RIP Ruge Mutahaba.Mbele yako nyuma yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwenyezi Mungu na Sanaa, na nyimbo za kidunua, na madisko na mambo yasiyomtukuza yeye wapi na wapi?

Binadam tuache kumdhihaki Mungu, aisee.

Hivi unaweza kutenganisha mmomonyoko wa maadili na muziki!!!???

Na hivyo vitu vina uhusiano gani na Mungu?
 
Kazi yangu ikiisha nami nikiondoka...nitakapovaa kutokuharibika... nitamjua Mwokozi nifikapo ng'amboni, nitakuwa wa kwanza kumlaki.
 
Back
Top Bottom