Ya Magufuli na Dr. Tulia ni mpango wa CCM dhidi ya Lowassa

Ya Magufuli na Dr. Tulia ni mpango wa CCM dhidi ya Lowassa

Kama.watapigiwa.kura na.jamaa.zetu baai tutarajie.kilio.kwa.dada
.....
Umesema kama watapigiwa kura?? Hehehee... Mwendo wa style ya Lubuva tu, inategemea wanataka nani ashinde sio suala la kura wala ushindani. Labda kama kura zitapigwa kwa kunyoosha vidole kama primary school
 
MAGUFULI ANAMTAKA NANI?
Katika mchakato wa kumpata Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, agenda kubwa imekua mawazo ya Rais Magufuli ni yapi?
1. Je Magufuli anamtaka kijana Abdulla Mwinyi mbunge wa Afrika Mashariki?

2. Je, Rais Magufuli anamtaka Job Ndugai?

3. Je, Rais anamtaka Dkt. Tulia Ackson, aliyekua naibu mwanasheria mkuu wa serikali?
Nafasi ya Spika ni nafasi nyeti sana katika utendaji wa serikali na Bunge. Inahitaji mtu ambaye ni mtulivu, mwenye hekima na busara katika kuendesha mambo.
Rais Magufuli anahitaji Spika ambaye hatakua mkorofi wala mpenda sifa kupitiliza. Bali Spika mwenye kufuata weledi na kanuni katika kuongoza bunge.
Rais Magufuli hahitaji mamluki wala kibaraka wa waliokua wasaka Urais. Anahitaji mtu msafi asiye na madoa wala kashfa.
Rais Magufuli hahitaji watu walewale katika serikali na safu ya mihimili ya serikali. Hawa watamsumbua na kuleta ujuaji mwingi.

Rais Magufuli ni mtu wa kazi tu. Anahitaji weledi na sio ubabaishaji.
Spika atatoka upande wa Tanzania bara, kwakua Zanzibar tayari wanalo baraza la wawakilishi. Hivyo ukimtoa Abdulla Mwinyi, wanabaki Job Ndugai mtaalamu wa wanyamapori na Dkt Tulia Ackson mwanasheria msomi wa chuo kikuu cha Dar es salaam.
Ukiniuliza Magufuli anamtaka nani? Nitakuuliza unadhani mtu anaweza kuacha nafasi yake ya mwanasheria mkuu wa serikali ili abahatishe uspika? Unadhani kafanya kwa bahati mbaya?
Nani alitarajia kuwa Magufuli angekua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kama jibu ni hakuna, basi tumtazame vizuri Dr. Tulia Ackson. Hapo ndipo jicho la wenye kuona mbali lilipo.
Twende na Dr. Tulia.
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kaka labda nikwambie huu ndo mfumo wa ccm, dr. Tulia keshapangwa, ndio speaker wetu, na huu mfumo hauwezi kufa,
 
ushahidi nyumba alompa hawara pale ubungo kwani uongo?nyumba zaidi ya 20 alizojenga chato je?kebbys hotel je!!! yote tisa kivuko kipya_kibovu cha bgm posta tena kwa bei ya mara mbili ya kivuko kipya,acha ujinga huyu hafai tu ila akili za watanzania zilimpa urais kijingajinga

watanzania hatukumpa urais huyu, naomba utuombe radhi
 
Kama kawa kura zitapigwa na hazitahesabiwa mshindi tayari wanayee
 
Hivi huyo jamaa Ndugai si ndiye alimchapa fimbo kichwani mgombea mwenziwe wa ubunge wa CCM kule Kongwa hadi akazirai na kulazwa hospitali wakati wa uchaguzi uliopita?
Kwa tukio hilo peke yake, kama CCM ingekuwa chama makini kinachojali maadili hata huo ubunge angekuwa disqualified na asingeupata, lakini kwa kuwa CCM ni chama kinachoendekeza mambo ya 'ovyo' usishangae Job Ndugai akaukwaa Uspika licha ya kuwa sasa angestahili kuwa jela badala ya kuitwa Mheshimiwa Mbunge, kama serikali ya CCM ingekuwa inazingatia utawala wa sheria badala ya mtindo inaotumia wa kuwafanya wateule wachache ndani ya nchi kuwa UNTOUCHABLES na kuwa above the law.
Jikumbushe na huyu.

 
Last edited by a moderator:
Kama.watapigiwa.kura na.jamaa.zetu baai tutarajie.kilio.kwa.dada
.....
Hivi nani asiyeijua CCM? Kura zitapigwa jioni/usiku halafu itaonekana muda umeisha, kura zitalala mpaka kesho yake ndipo zihesabiwe na matokeo yatoke na Tulia Kutangazwa. Kwani hukuona kwa magufuli kwenye kinyanganyiro cha akina Asha rose na Balozi Fatuma, Kwani walishindwa kuzihesabu siku hiyohiyo? Yaani demikrasia ya CCM ni kiini macho.
 
Na hii ndio inaonyesha ccm hakunaga demokrasia bali wanakuwa na mtu wao wa kitengo tayari. Wana tabia ya kudhalilisha wagombea

Kuliko walivyomdhalilisha Dr slaa chadema kwa kumpeleka hadi mafunzoni ili aje kua rais ila gia ikabadilishwa na mbowe ghafla.
 
Hivi nani asiyeijua CCM? Kura zitapigwa jioni/usiku halafu itaonekana muda umeisha, kura zitalala mpaka kesho yake ndipo zihesabiwe na matokeo yatoke na Tulia Kutangazwa. Kwani hukuona kwa magufuli kwenye kinyanganyiro cha akina Asha rose na Balozi Fatuma, Kwani walishindwa kuzihesabu siku hiyohiyo? Yaani demikrasia ya CCM ni kiini macho.

Bora demokrasia ya chadema inafaa maana tumeishuhudia kipindi chakumchagua mgombea urais kupitia chama hicho Tena imekomaa haswa inatakikana na vyama vingine kuiga mfano huu si ndio.
 
Back
Top Bottom