Ya Magufuli na Dr. Tulia ni mpango wa CCM dhidi ya Lowassa

Ya Magufuli na Dr. Tulia ni mpango wa CCM dhidi ya Lowassa

Tatizo lilikuwa ni kufa kwa Chadema. Baada ya Chadema kununuliwa na fisadi mkuu kilichobaki hakikuwa Chadema tena. Agenda zote na falsafa ya Chadema iliyowafanya Watanzania waamini kuwa ndicho chama kitakacholeta mageuzi na mabadiliko Tanzania yalifutika. Iliingia Team Lowasa, ile ile iliyokuwa CCM na kuja kuvaa joho la Chadema ndio wakaingia kwenye uchaguzi. Je, kwa akili za haraka haraka, ulitegemea Team Lowasa iweke ufisadi kwenye agenda? Si wangechekwa??? Kwanza wangekuwa wanamsema nani kama sio kujisema wenyewe?

Subiri bunge lianze ndipo utajuwa Ukawa ni kitu gani. "Unauliza nyeti za kuku wakati upepo unavuma"
 
Hivi nani asiyeijua CCM? Kura zitapigwa jioni/usiku halafu itaonekana muda umeisha, kura zitalala mpaka kesho yake ndipo zihesabiwe na matokeo yatoke na Tulia Kutangazwa. Kwani hukuona kwa magufuli kwenye kinyanganyiro cha akina Asha rose na Balozi Fatuma, Kwani walishindwa kuzihesabu siku hiyohiyo? Yaani demikrasia ya CCM ni kiini macho.
Afadhali ccm,chadema wamempa kadi lowassa siku hiyo hiyo kapewa ugombea urais
 
hivi nani asiyeijua ccm? Kura zitapigwa jioni/usiku halafu itaonekana muda umeisha, kura zitalala mpaka kesho yake ndipo zihesabiwe na matokeo yatoke na tulia kutangazwa. Kwani hukuona kwa magufuli kwenye kinyanganyiro cha akina asha rose na balozi fatuma, kwani walishindwa kuzihesabu siku hiyohiyo? Yaani demikrasia ya ccm ni kiini macho.

mbona unachuki na ccm. We vipi. Uliwahi kusoma kitabu "i love idi amin". Au anae muoa mama ndiye baba, lazima umpende hakuna namna. Ushauri wa bure uzingatie au ujinyonge tu. Maana ccm hii itaendelea hadi 2050. Ndipo wapinzani nao watapewa kwa majaribio. Hata mzee ruksa analijua hili. Si ajabu kwa umri wako hautakuepo dunia hi tena. Uwahusie wapinzani waanze kumpika mtu wao mapema ili kuepuka kashfa za kuazima wagombea urais kama hi ya 2015. Cdm iliazima ktka ccm na cuf. Aibu kwa chama makini. Ukweli unauma lakini utabaki mkavu
 
Ha ha ha ha haaa ngoja nidandie na mimi maana mtoa mada si ndiyo kashamtangaza sasa tufanyeje? Teh teh teh
zidumu fikra za mtoa mada :bump2:

Aupate uspika kwa CCM ipi? Mmesahau kuwa ni ileile. Hapo kaandaliwa Ndugai
hili ni swala la experience beats exposure anyday of the week.

Starajii spika awe mtu ambaye hajawahi kuongoza kikao cha bunge japo kwa kukaimu tu
there is a first time for everything. naona kama Kamati Kuu wanajaribu kum-contain Magufuli.. time will tell.
 
Kinachonishangaza kidogo ni kuona TimuLowassa wengi wanampigia kampeni Ndugai ili awe Spika!

Hoja ya msingi kwa sasa, kwa nini wanampigia kampeni mwanaCCM?

Ndugai ana mahusiano gani ya karibu na Lowassa/TimuLowassa?

Tayari ameshapita maana wenzake wamejitoa, doc. Ackson amechukuwa form ya kugombea unaibu speaker baada ya kuteuliwa kuwa mbunge.ULIPO TUPO
 
Jikumbushe na huyu.


Nalikumbuka hilo tukio lililotokea kwenye kanda ya Ziwa.
Kibaya zaidi aliyefanya tendo hilo alikuwa Waziri kamili wa Mifugo katika serikali ya awamu ya nne ya Kikwete.
Inapaswa kirefu cha chama hiko kibadilishwe na kuwa Chama Cha Mabondia!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom