Ya Magufuli na Dr. Tulia ni mpango wa CCM dhidi ya Lowassa

Ya Magufuli na Dr. Tulia ni mpango wa CCM dhidi ya Lowassa

Nachukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa spika wa bunge la 11 Dkt. Tulia. Ongera sana!!!
 
Ndugai ndio spika wa bunge la 11..... Mimi ni mbunge na nakwambia huyo dada wako akishinda walahi naacha ubunge....

Ndugai alimsifu sana LOWASSA kuhusu kuunda tume ya kutatua migogoro kama mungu angemsaidia kufika ikulu kama raisi
Lakini ile ikaleta Vijimaneno hamuoni kama inaweza kutumika kama silaha ya kumpigia??

NA TULIA ASIPOPITA ATARUDI TENA KUWA AAG??
 
Tulia ndiye aliyetoa tafsiri ya shauri la kibatala kuhusu utata wa mita mia mbili baada ya kupiga kura. Kama kweli anagombea kupitia ccm inamaana alitoa hukumu kwa kutotaka kumuuzi mwenyekiti wa chama chake.
 
Ha ha ha ha ha.
Unaleta mikwara kama ya Sitta.
Angalia usijelikimbia jukwaa bure
Mzee Sitta asingepitishwa na Kamati Kuu kwa sababu mchakato wa Katiba Mpya bado haujahitimishwa.

Kuna uwezekano mkubwa wa bunge maalum la Katiba kuitishwa tena ili kuboresha Katiba Inayopendekezwa.
 
Kazikwelikweli yoyoteatakaeshinda. Hatokuwanatofautina. Maspikawaliopita.hamnajipya
 
Mzee Sitta asingepitishwa na Kamati Kuu kwa sababu mchakato wa Katiba Mpya bado haujahitimishwa.

Kuna uwezekano mkubwa wa bunge maalum la Katiba kuitishwa tena ili kuboresha Katiba Inayopendekezwa.

Mbona Samia kapitishwa?
 
MsemajiUkweli

Katiba mpya iliotukuka, basi kama katiba mpya ndiyo mafanikio ya huyu binti basi apewe kura za ndiyo awe spika
 
Last edited by a moderator:
Ndugai ndio spika wa bunge la 11..... Mimi ni mbunge na nakwambia huyo dada wako akishinda walahi naacha ubunge....

Ndugai huyo aliyetaka kumwua mgombea mwenzake? Hastahili hata kuwa Mbunge. ! Pia awamu hii hatutaki vijembe bungeni. Tunataka KAZI TU.
 
Tulia ndiye aliyetoa tafsiri ya shauri la kibatala kuhusu utata wa mita mia mbili baada ya kupiga kura. Kama kweli anagombea kupitia ccm inamaana alitoa hukumu kwa kutotaka kumuuzi mwenyekiti wa chama chake.
Siyo suala la kumuuzi Mwenyekiti wa CCM-Taifa, hufahamu kama serikali niya CCM?

Unadhani Mwenyekiti wa CCM-Taifa, Rais Kikwete angeweka Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye siyo CCM?

Huu ni ukweli pamoja na kwamba ni ukweli mchungu!
 
Mzee Sitta asingepitishwa na Kamati Kuu kwa sababu mchakato wa Katiba Mpya bado haujahitimishwa.

Kuna uwezekano mkubwa wa bunge maalum la Katiba kuitishwa tena ili kuboresha Katiba Inayopendekezwa.

Afu mzee sitta hakua na weledi wa kuliona hata hili.
Endapo bunge lile litaitishwa tena inakuwa imempunguzia point kadhaa
 
Dkt Magufuli uwa hana timu. Yeye ufanya kazi na yoyote yule ambae ni msafi kwa maana hana ufisadi na wizi.Hivyo katika hao watatu atafanya kazi na yeyote yule. Makundi na timu sio hulka ya Dkt Magufuli.

Lakini tufanye stori iwe fupi, spika ni Job Ndungai. Wabunge wengi wa CCM wanamkubali Job Ndungai.

Kisa cha kumkubali hiki hapa:

Pamoja na kwamba kwa sasa hakuna spika, ila aliyekuwa naibu wa spika (ambae ni Job Ndungai) ushirikiana na katibu wa Bunge kufanya maandalizi ya wabunge wapya mjengoni. Ndungai kaifanya hii kazi usiku na mchana tangu Novemba 6 huko. Kwa ufupi, tayari ana kura nyingi za wabunge wa CCM.

Hivyo basi, msipoteze muda kufanya mjadala kuhusu hili la uspika. Ni Ndungai tu. Labda mjadala uhamie kwa nani atakuwa waziri mkuu wa JMT.

#NdungaiForSpeaker

Ndugai ni teamLowasa ,,anafaa sana huyu anajielewa
 
Mmmh....not again, please.After what we had gone through with highly sensitive Makinda now you want to shovel another woman down our throats? Like seriously?
 
Watanzania wrote wezi kwa taarifa yako watanzania wanapenda ufisadi kuliko hats dini zao
 
Ndugai alimsifu sana LOWASSA kuhusu kuunda tume ya kutatua migogoro kama mungu angemsaidia kufika ikulu kama raisi
Lakini ile ikaleta Vijimaneno hamuoni kama inaweza kutumika kama silaha ya kumpigia??

NA TULIA ASIPOPITA ATARUDI TENA KUWA AAG??
Kinachonishangaza kidogo ni kuona TimuLowassa wengi wanampigia kampeni Ndugai ili awe Spika!

Hoja ya msingi kwa sasa, kwa nini wanampigia kampeni mwanaCCM?

Ndugai ana mahusiano gani ya karibu na Lowassa/TimuLowassa?
 
Back
Top Bottom