Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
MAGUFULI ANAMTAKA NANI?
Katika mchakato wa kumpata Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, agenda kubwa imekua mawazo ya Rais Magufuli ni yapi?
1. Je Magufuli anamtaka kijana Abdulla Mwinyi mbunge wa Afrika Mashariki?
2. Je, Rais Magufuli anamtaka Job Ndugai?
3. Je, Rais anamtaka Dkt. Tulia Ackson, aliyekua naibu mwanasheria mkuu wa serikali?
Nafasi ya Spika ni nafasi nyeti sana katika utendaji wa serikali na Bunge. Inahitaji mtu ambaye ni mtulivu, mwenye hekima na busara katika kuendesha mambo.
Rais Magufuli anahitaji Spika ambaye hatakua mkorofi wala mpenda sifa kupitiliza. Bali Spika mwenye kufuata weledi na kanuni katika kuongoza bunge.
Rais Magufuli hahitaji mamluki wala kibaraka wa waliokua wasaka Urais. Anahitaji mtu msafi asiye na madoa wala kashfa.
Rais Magufuli hahitaji watu walewale katika serikali na safu ya mihimili ya serikali. Hawa watamsumbua na kuleta ujuaji mwingi.
Rais Magufuli ni mtu wa kazi tu. Anahitaji weledi na sio ubabaishaji.
Spika atatoka upande wa Tanzania bara, kwakua Zanzibar tayari wanalo baraza la wawakilishi. Hivyo ukimtoa Abdulla Mwinyi, wanabaki Job Ndugai mtaalamu wa wanyamapori na Dkt Tulia Ackson mwanasheria msomi wa chuo kikuu cha Dar es salaam.
Ukiniuliza Magufuli anamtaka nani? Nitakuuliza unadhani mtu anaweza kuacha nafasi yake ya mwanasheria mkuu wa serikali ili abahatishe uspika? Unadhani kafanya kwa bahati mbaya?
Nani alitarajia kuwa Magufuli angekua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kama jibu ni hakuna, basi tumtazame vizuri Dr. Tulia Ackson. Hapo ndipo jicho la wenye kuona mbali lilipo.
Twende na Dr. Tulia.
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kumbe nchi hii siyo yetu sote bali ni ya magufuli