Pole sana, watu nao wanauliza maswali yale yale na toka mwanzo maelezo umetoa vizuri sana.Alisema kuna mtu anasubiri pesa kwa hiyo akanipa namba ya huyo mtu na jina litakalokuja baada ya kutuma pesa...Sio kwamba nilituma kwa namba ya mamamkwe
Katumia lugha ambayo imenyoka na ya msisitizo jambo ambalo jinsi unavyomheshimu Mamamkwe lazima utekeleze haraka.Du baada ya kusoma mlivyokuwa mnajibizana imebidi nicheke sana, ila pole sana. Ulimshikia heshima zote kumbe ni mwizi.
Unajua kuna watu wanasema huu wizi ni mrahisi kugundua lakini mimi naona huyo mwizi atakuwa ameshaibia wengi. Kwa hali ya kawaida ya biashara zetu siyo rahisi mtu uchunguze vitu vidogo vidogo. Kwa mfano mimi nina kawaida ya kuandikia msg na rafiki au ndugu zangu kwa mtndo wa.... ''Ee bwanae nimekwama kuna issue nataka kufanya. Hebu rusha laki mbili faster tutaongea baadae.'' Huu mtindo wa kuandika msg namana hii uko sana hasa kwa watu wenye maduka wanapokwenda maduka ya jumla kufanya shopping ya mali ya duka huku wameacha wafanyakazi dukani. Mtu pengine anakuwa yupo kwenye watu wengi anaona kuanza kupiga simu na kutaja nirushie fedha atakuwa taget ya wezi hivyo ngoja aandike msg.Acha kabisa mkuu na ndicho kunachonipa hasira yaani... nimetuma pesa akaniambia nimepata nikamtakia na mchana mwema najua napalilia penzi kwa mamamkwe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Halfu inaonekana huyo mwizi alishafanya research ya kutosha kuhusu wasifu wa wahusika.Katumia lugha ambayo imenyoka na ya msisitizo jambo ambalo jinsi unavyomheshimu Mamamkwe lazima utekeleze haraka.
Pia alisoma na mazingira akaona kuna huduma ya Tigo Pesa ipo karibu na hilo Duka ndio maana akamwambia nenda hapo mbele ukatume hiyo hela Tigo pesa.
Ndio maana ishu kaifanikisha ndani ya nusu saa tu.Halfu inaonekana huyo mwizi alishafanya research ya kutosha kuhusu wasifu wa wahusika.
Ni kweli alifanya research sababu pia alienda na duka la jirani yangu akamkuta dogo huko akaulizia maziwa ya kopo kama alivyofanya kwangu akazima simu akaisave jina la kaka yake ambae ni bodaboda....dogo alivyopata meseji ya kutuma laki 5 akampigia Mwizi naye akamjibu nipo kwenye boda siwezi kukuelewa we tuma pes.Uzuri dogo aliishika namba ya bro wake ndio kilichomwokoaHalfu inaonekana huyo mwizi alishafanya research ya kutosha kuhusu wasifu wa wahusika.
Soma vizuri jibu la swali lako lipo.We wakati unatuma hukuona jina la unayemtumia
Mtu anakupigia hujainasa sauti yake na ulipoona simu imezima kwa nini hukutaka kujua why? Simu kuzima na mawasiliano hayajakamilika?Asante sana watu wanataka hela kwa njia rahisi sana hawataki kufanya kazi. Anaamka asubuhi kapendeza anazunguka kutapeli
Inategemea na mfumo wa mawasiliano na mtu hyo kama mmeshazoea kuwasiliana kwa text huwezi doubt chochote.Sema all in all tuwe makini tuuMtu anakupigia hujainasa sauti yake na ulipoona simu imezima kwa nini hukutaka kujua why? Simu kuzima na mawasiliano hayajakamilika?
Binafsi naona kuna hali ya juu ya uzembe pole ila jifunze kuwa makini
Ni ujinga wake ndiyo ulisababisha atapeliwe, kwani alivyopigiwa kwa mala yakwanza, wakawa hawaelewani, utashindwa kujua sauti ya mama mkwe wako sure mtu unayewasiliana nae hata kama abadilishe namba?Kumuuliza mama mkwe maswali mengi ni ukosefu wa nidhamu ,mfano "mama mkwe mbona jina limetoka Lameck Malulu badala ya Rosemary?"