Wizi wa kijinga sana unafanyika Mwanza

Wizi wa kijinga sana unafanyika Mwanza

Duh, alafu utakuta laki mbili ndio faida ya siku au hata mbili kama sio tatu.

Pole.
 
Style hiyo ya Wizi imeshatumika sana Dar es salaam. Ni wizi tu wa mtandao kupitia application kwenye Computer Uyo tapeli anafahamu baadhi ya watu wako. So namba anakuwanazo
 
Pole mkuu ila ungeweka na namba zake alizotumia kukutapeli kama ushahidi zaid
 
Wewe ilitakiwa kumpigia mamamkwe siyo text,usikubali kutuma pesa bila kuongea na mhusika mambo ya pesa ni kuwa nayo makini.
 
Habari wanajukwaa,

Kuna aina ya wizi unaendelea mkoani Mwanza unaweza kuwa wa kitambo sana lakini umeshamiri katika wiki hii hivyo naomba muwe makini sana.

Kuna kijana mmoja mtanashati tena ukimwona ana heshima zake anatembelea kwenye maduka ya jumla, rejareja na pia deport za bia na soda kufanya utapeli wake kwa mtandao.Ninasimulia kifupi alivyonipata ili muwe makini nae kama ana wenzie pia.

Jana mida ya asubuhi kijana mmoja alikuja dukani kwangu nauza bia za jumla na pombe kali akauliza bei ya Zanzi kubwa nikamtajia akaomba kupunguziwa sababu hakuwa nayo.
Wakati tunaelewana bei akatoa simu yake akampigia mtu kumjulisha kwamba bei ya Zanzi sio kama waliyotegemea ila simu ikazima kabla hawajaelewana.

Akaniomba dada naazima simu yako nimjulishe mwenzangu nikamjibu sina dakika akasema hata meseji tu nitume nikampa.Akatuma meseji akarudisha simu akaaga ngoja nitoe hela hapo narudi.

Baada ya kama nusu saa simu yangu ikaita namba imeseviwa jina la Mamamkwe wangu nikapokea lakini hatukuelewana simu ikakatika akatuma meseji una laki 5 hapo nikamjibu hapana sina kwa sasa.
Akaniuliza kiwango nilicho nacho nikamjibu nina laki 2 akaomba naomba nitumie 195000 kuna mtu anasubiri na namba akaituma ya kumtumia mtu huyo na jina litakalotokea baada ya kutuma. Sababu mamakwe wangu ni mtu wa biashara hapa Mwanza sikusita nikamtumia akashukuru tukaagana kwa meseji.

Baada ya masaa kama 5 akatuma meseji tena anauliza una shilingi ngapi sasa hivi hapo ndio nikastuka sio kawaida mama aulizie mauzo yangu basi nikampigia mwenzangu amuulize mama ni anakosea meseji anamtumia mfanyakazi wake au ni vipi.

Baada ya hapo ndio tukajua tumetapeliwa ila sikuelewa kivipi namba ninayo kwenye simu na imeseviwa kabisa.
Kumbe anachofanya ukimpa simu anaangalia Call log ile namba uliyowasiliana nayo karibuni anaandika namba yake anaisave kwa jina hilo hilo ndio anatumia kutapeli akijua mtu mpaka ugundue ni ngumu sana.

Jana ametapeli maduka mengi sana maeneo ya Mkuyuni na ataendelea kutapeli kwa hiyo muwe makini nae sana.Ni wizi wa kizamani lakini mtu huwezi jua siku wala saa.
Poleni kwa waraka mrefu najua utawasaidia wakazi wenzangu wa Mwanza kwa mwizi huyu.
Du. Huu wizi ni mkali.
 
pole sana,cha msingi ni kuwa makini muda wote kwani ata mkuu wangu wa kazi alishatapeliwa kwa namna hiyo.Husimpe mtu yoyote chombo chako cha mawasiliano hukiwa humjui au ata unamjua kwani anaweza fanya lolote kupitia simu na badae kuonekana umefanya wewe.
 
Asante sana wezi kama hawa wakomeshwe leo atakuwa kahamia mtaa mwingine ambako hajajulikana.
Waambie POLISI MWZ bila shaka wana kitengo cha IT ni rahisi kutrack kwa Mobl CO na GPS na kundaka kilahini tuu!!
 
Weka hapa namba uliyoitumia
Pole mkuu ila ungeweka na namba zake alizotumia kukutapeli kama ushahidi zaid
Lakini sasa hivi namba zake zote hazipatikani naona anazo nyingi sana akitapelia anazizima
20180424_140438.jpg
 
Wewe ilitakiwa kumpigia mamamkwe siyo text,usikubali kutuma pesa bila kuongea na mhusika mambo ya pesa ni kuwa nayo makini.
nashukuru mkuu nitakuwa makini muda mwingine hata sijajua kwanini sikufikiria kumpigia..
 
Duh, alafu utakuta laki mbili ndio faida ya siku au hata mbili kama sio tatu.

Pole.
Asante sana wanarudisha sana nyuma hawa wezi na matapeli
 
Style hiyo ya Wizi imeshatumika sana Dar es salaam. Ni wizi tu wa mtandao kupitia application kwenye Computer Uyo tapeli anafahamu baadhi ya watu wako. So namba anakuwanazo
Hapana mkuu hakuwa na namba zozote alichofanya alipoomba simu akaenda kwenye call log akasave namba yake kwa jina nililomsave mama mkwe yeye akaongeza kanukta mwishoni. Halafu meseji aliyoomba kutuma aliituma ndio akapata namba yangu so ana namba nyingi au wapo wengi
 
pole sana,cha msingi ni kuwa makini muda wote kwani ata mkuu wangu wa kazi alishatapeliwa kwa namna hiyo.Husimpe mtu yoyote chombo chako cha mawasiliano hukiwa humjui au ata unamjua kwani anaweza fanya lolote kupitia simu na badae kuonekana umefanya wewe.
Asante sana mkuu nakuwa makini kuanzia sasa
 
Waambie POLISI MWZ bila shaka wana kitengo cha IT ni rahisi kutrack kwa Mobl CO na GPS na kundaka kilahini tuu!!
Namba akishaitumia haipatikani tena kama hapo zote 3 hazipatikani kwahiyo inaonekana anazo nyingi sana
 
Back
Top Bottom