Hawa watu wana akili sana na wanafanya research sana kabla ya kupiga tukio. Wanatarget zaidi biashara ambazo wahudumu ni wanawake. Ngoja niwape wizi mwingine.
Huu uko hasa kwenye Mpesa.
1. Wahusika ni chain na mmoja anakua mathalan Dodoma na Mwingine Mwanza.
2. Wanatarget mpesa iliyo active sana na hasa zinazooperate usiku mfn bar n.k
3. Mechanism.
Anakuja mtu dukani kwako anataka kutoa unamtajia Agent namba. Ile agent namba anamtumia mwenzie aliye mkoa mwingine tena wa mbali. Na huyo ndiye anayeitoa pesa. Kisha mpesa anamfowadia aliyepo hapo dukani.
4. Messaging App
Aliyepo dukani anakua na messaging App ambayo ukifungua msg kuisoma inaonyesha content tu ya msg na sio details za sender Mfn Google messaging App. Hivyo, huyo mwenye hii App, namba(ya huyo mtu aliyetoa hela na kumfowardia msg) anakua ameisave M-PESA
So, wakala hata akiomba simu aione msg ataisoma na sbb ya mazingira ya haraka haraka ataona hakuna tabu. Na atamkabidhi pesa.
Wizi ulipo.
Yule mtoaji halisi (Aliyeko mbali), atawapigia voda kureport ametoa hela kimakosa. Wao voda sbb network ziko tofauti na wakala nfn dom to mwanza. Wanaamini.
-pia voda wanaweza wasiliana na huyo wakala. Kama wakala akisema sio sahihi , wote watapaswa kufika katika ofisi za voda eneo husika kupata ukweli.
Ushindi wa mwizi.
1. Kama yule aliyepokea hela kwa wakala, hakusaini kitabu , basi wakala hatoaminika na hela atarudishiwa mwizi.
2, hata kama amesaini, anaweza shindwa sbb mlalamikaji yuko mbali mno na wakala so anaaminika zaidi yeye..
What to do.
1. Hakika aliyetoa uko naye na uikague uhakika wa msg kuwa ni kweli imetoka voda. Acha zile za kuuliza, jina limetokeaje..
2. Msainishe logbook kwa ID yake halisi.
Tuwe makini