Sasa hukugundua sauti ya mama mkwe?Sikutuma kwenye namba yake maana aliomba nimtumie mtu akisema anasubiri akanipa namba na jina la huyo nitakayemtumia. Sikudoubt sana sababu kuna vijana huwa wanamnunulia mizigo yake ya biashara
Kwa nini asifike nao mbali wakati mnaonekana ni mabashite (zero brain)????Yeye katumia akili kuipata hiyo pesa kwangu lakini ni aina moja ya wizi ambao hatafika nao mbali. Maana anachofanya ni kusave namba kwa kufwata mtu uliyeongea nae karibuni kungine anaweza save namba ya mtu ambaye atagundulika mapema.
Nchi bado ina vilaza wengi sana hasa wasukuma.Sas naww ulivotuma hela jina gani lilitokea?la mamamkwe au la nani? Km pia hujui jina la mamamkwe wako basi ni uzembe wako
Wewe ni KILAZA WA KUTUPWAAlisema kuna mtu anasubiri pesa kwa hiyo akanipa namba ya huyo mtu na jina litakalokuja baada ya kutuma pesa...Sio kwamba nilituma kwa namba ya mamamkwe
Habari wanajukwaa,
Kuna aina ya wizi unaendelea mkoani Mwanza unaweza kuwa wa kitambo sana lakini umeshamiri katika wiki hii hivyo naomba muwe makini sana.
Kuna kijana mmoja mtanashati tena ukimwona ana heshima zake anatembelea kwenye maduka ya jumla, rejareja na pia deport za bia na soda kufanya utapeli wake kwa mtandao.Ninasimulia kifupi alivyonipata ili muwe makini nae kama ana wenzie pia.
Jana mida ya asubuhi kijana mmoja alikuja dukani kwangu nauza bia za jumla na pombe kali akauliza bei ya Zanzi kubwa nikamtajia akaomba kupunguziwa sababu hakuwa nayo.
Wakati tunaelewana bei akatoa simu yake akampigia mtu kumjulisha kwamba bei ya Zanzi sio kama waliyotegemea ila simu ikazima kabla hawajaelewana.
Akaniomba dada naazima simu yako nimjulishe mwenzangu nikamjibu sina dakika akasema hata meseji tu nitume nikampa.Akatuma meseji akarudisha simu akaaga ngoja nitoe hela hapo narudi.
Baada ya kama nusu saa simu yangu ikaita namba imeseviwa jina la Mamamkwe wangu nikapokea lakini hatukuelewana simu ikakatika akatuma meseji una laki 5 hapo nikamjibu hapana sina kwa sasa.
Akaniuliza kiwango nilicho nacho nikamjibu nina laki 2 akaomba naomba nitumie 195000 kuna mtu anasubiri na namba akaituma ya kumtumia mtu huyo na jina litakalotokea baada ya kutuma. Sababu mamakwe wangu ni mtu wa biashara hapa Mwanza sikusita nikamtumia akashukuru tukaagana kwa meseji.
Baada ya masaa kama 5 akatuma meseji tena anauliza una shilingi ngapi sasa hivi hapo ndio nikastuka sio kawaida mama aulizie mauzo yangu basi nikampigia mwenzangu amuulize mama ni anakosea meseji anamtumia mfanyakazi wake au ni vipi.
Baada ya hapo ndio tukajua tumetapeliwa ila sikuelewa kivipi namba ninayo kwenye simu na imeseviwa kabisa.
Kumbe anachofanya ukimpa simu anaangalia Call log ile namba uliyowasiliana nayo karibuni anaandika namba yake anaisave kwa jina hilo hilo ndio anatumia kutapeli akijua mtu mpaka ugundue ni ngumu sana.
Jana ametapeli maduka mengi sana maeneo ya Mkuyuni na ataendelea kutapeli kwa hiyo muwe makini nae sana.Ni wizi wa kizamani lakini mtu huwezi jua siku wala saa.
Poleni kwa waraka mrefu najua utawasaidia wakazi wenzangu wa Mwanza kwa mwizi huyu.
Naona umekuja kwa kasi sana ....mwisho wako sio mbali na utaishia pabaya....endelea kutapeli hela za hao "vilaza" ukijona una akili ila za sakafuni.......!!! Nashangaa unavyokazana kilaza kilaza wakati wewe ni mmoja wao umeshakariri kila aliye Mwanza ni msukuma na uahamba wako....Tindiga mhadzabe wewe[emoji57][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]Nchi bado ina vilaza wengi sana hasa wasukuma.
Kazi zao ni kukamata wanaokosoa mamalaka....na makampuni ya simu hayana msaada zaidi anakwambia hela ameshaitoa basi hawana la kufanga....Wacha matapeli wote siku zao zinahesabikaHivi wenye kampuni za simu pamoja na TCRA wao, wanatusaidiaje kwa hili janga, najiuliza usajili wa line za simu kwa vitambulisho ni kwajili ya kuwanasa wanaoikosoa mamlaka tu!? kwanini mbinu hiyohiyo isitumike kuwanasa watu wa aina hiyo!? Kwanini TISS wasianzishe kitengo cha kushughulikia jambo hili, ikumbukwe kuwa watu wanaona serikali haina msaada kwasababu ya kushindwa kubuni mbinu za kukabiliana na wahalifu wanao waharibia shughuli zao za kiuchumi
195,000 imeliwa bila jashoFanya kazi ule hela kwa jasho lamo sio kutapeli hela halafu unajiona una akili kuwaita wenzako "Vilaza" ipo siku yako tapeli while you can
Ukisoma vizuri utaelewa.... Nahisi ukamuelewa jamaaWe wakati unatuma hukuona jina la unayemtumia
Sio wabishi sometimes roho za huruma unakuta mtu ana uhitaji lakini pia katika biashara ni jambo ambalo gumu kuepukikaSasa mwakyembe keshawambia usimpe mtu simu yako tena ukikutwa simu yako haina password unafungwa. Tatizo lenu wabongo wabishi mno.