Wizi wa kijinga sana unafanyika Mwanza

Wizi wa kijinga sana unafanyika Mwanza

trudie

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
4,546
Reaction score
11,136
Habari wanajukwaa,

Kuna aina ya wizi unaendelea mkoani Mwanza unaweza kuwa wa kitambo sana lakini umeshamiri katika wiki hii hivyo naomba muwe makini sana.

Kuna kijana mmoja mtanashati tena ukimwona ana heshima zake anatembelea kwenye maduka ya jumla, rejareja na pia deport za bia na soda kufanya utapeli wake kwa mtandao.Ninasimulia kifupi alivyonipata ili muwe makini nae kama ana wenzie pia.

Jana mida ya asubuhi kijana mmoja alikuja dukani kwangu nauza bia za jumla na pombe kali akauliza bei ya Zanzi kubwa nikamtajia akaomba kupunguziwa sababu hakuwa nayo.
Wakati tunaelewana bei akatoa simu yake akampigia mtu kumjulisha kwamba bei ya Zanzi sio kama waliyotegemea ila simu ikazima kabla hawajaelewana.

Akaniomba dada naazima simu yako nimjulishe mwenzangu nikamjibu sina dakika akasema hata meseji tu nitume nikampa.Akatuma meseji akarudisha simu akaaga ngoja nitoe hela hapo narudi.

Baada ya kama nusu saa simu yangu ikaita namba imeseviwa jina la Mamamkwe wangu nikapokea lakini hatukuelewana simu ikakatika akatuma meseji una laki 5 hapo nikamjibu hapana sina kwa sasa.
Akaniuliza kiwango nilicho nacho nikamjibu nina laki 2 akaomba naomba nitumie 195000 kuna mtu anasubiri na namba akaituma ya kumtumia mtu huyo na jina litakalotokea baada ya kutuma. Sababu mamakwe wangu ni mtu wa biashara hapa Mwanza sikusita nikamtumia akashukuru tukaagana kwa meseji.

Baada ya masaa kama 5 akatuma meseji tena anauliza una shilingi ngapi sasa hivi hapo ndio nikastuka sio kawaida mama aulizie mauzo yangu basi nikampigia mwenzangu amuulize mama ni anakosea meseji anamtumia mfanyakazi wake au ni vipi.

Baada ya hapo ndio tukajua tumetapeliwa ila sikuelewa kivipi namba ninayo kwenye simu na imeseviwa kabisa.
Kumbe anachofanya ukimpa simu anaangalia Call log ile namba uliyowasiliana nayo karibuni anaandika namba yake anaisave kwa jina hilo hilo ndio anatumia kutapeli akijua mtu mpaka ugundue ni ngumu sana.

Jana ametapeli maduka mengi sana maeneo ya Mkuyuni na ataendelea kutapeli kwa hiyo muwe makini nae sana.Ni wizi wa kizamani lakini mtu huwezi jua siku wala saa.
Poleni kwa waraka mrefu najua utawasaidia wakazi wenzangu wa Mwanza kwa mwizi huyu.
 
Dawa yake ni ndogo sana,ashushwe Busha tu,tuone kama ataweza tena kuwa smart kwa kuvaa hizo modo!
Maana ukienda Voda au Polisi sina hakika kama kuna msaada.!
 
Ahsante sana kwa kutufumbua macho, cha msingi hapa ni kuwa makini na simu zetu, maana wizi wote ni kutokana na access ya simu, hivyo tuwe makini na simu zetu na tusiwe wepesi kutekeleza maagizo yoyote mpaka tujiridhishe, maana matapeli huja na mbinu nyingi na timing pia, mambo ya kujifanya tupo busy hatutatki kuhakiki kabla ya kuamua ndio yanatugharimu.

Mwisho kabisa nakupa pole kwa kutapeliwa jasho lako!
 
Kwanini unasema ni wizi wa "kijinga?" wakati huyo mwizi/tapeli katumia "akili" kupata hiyo hela toka kwako? ingawa wizi/utapeli ni kosa kisheria.
Yeye katumia akili kuipata hiyo pesa kwangu lakini ni aina moja ya wizi ambao hatafika nao mbali. Maana anachofanya ni kusave namba kwa kufwata mtu uliyeongea nae karibuni kungine anaweza save namba ya mtu ambaye atagundulika mapema.
 
Dawa yake ni ndogo sana,ashushwe Busha tu,tuone kama ataweza tena kuwa smart kwa kuvaa hizo modo!
Maana ukienda Voda au Polisi sina hakika kama kuna msaada.!
Mitandao ya simu haiwezi kusaidia sababu ana namba nyingi na akishatapelia haipatikani tena. Polisi nako unaweza poteza muda wako bure
 
Ahsante sana kwa kutufumbua macho, cha msingi hapa ni kuwa makini na simu zetu, maana wizi wote ni kutokana na access ya simu, hivyo tuwe makini na simu zetu na tusiwe wepesi kutekeleza maagizo yoyote mpaka tujiridhishe, maana matapeli huja na mbinu nyingi na timing pia, mambo ya kujifanya tupo busy hatutatki kuhakiki kabla ya kuamua ndio yanatugharimu.

Mwisho kabisa nakupa pole kwa kutapeliwa jasho lako!
Ni kweli kabisa tuwe makini sana na simu zetu. Muda mwingine katika biashara unawaza ngoja nimsaidie awasiliane na mwenzake ili nisimpoteze mteja lakini hasara unayopata ni kubwa sana. Tupende kujihakikishia tunapowasiliana na wenzetu kuhusu mambo ya hela usikubali kuwasiliana kwa meseji bora kusikia sauti kabisa.
 
Pole dada. Ila wa Tanzania tubadilike usikubali kumpa/kuruhusu kutumia kifaa chako chochote cha eletroniki mtu yoyote. Bora kama kuna haja ya kumsaidia mtu mwambie akuandikie namba uikague ukiridhika ni sahihi ufanye mawasiliano ww mwenyewe bila ya kuruhusu kumpatia kifaa chako.
Ndio mana kwenye sheria sasa hv mnalazimishwa kuweka password katika vifaa vyote vya kieletroniki.
Jamii itakuona mbaya ila utaepukana na mengi.
 
Habari wanajukwaa,

Kuna aina ya wizi unaendelea mkoani Mwanza unaweza kuwa wa kitambo sana lakini umeshamiri katika wiki hii hivyo naomba muwe makini sana.

Kuna kijana mmoja mtanashati tena ukimwona ana heshima zake anatembelea kwenye maduka ya jumla, rejareja na pia deport za bia na soda kufanya utapeli wake kwa mtandao.Ninasimulia kifupi alivyonipata ili muwe makini nae kama ana wenzie pia.

Jana mida ya asubuhi kijana mmoja alikuja dukani kwangu nauza bia za jumla na pombe kali akauliza bei ya Zanzi kubwa nikamtajia akaomba kupunguziwa sababu hakuwa nayo.
Wakati tunaelewana bei akatoa simu yake akampigia mtu kumjulisha kwamba bei ya Zanzi sio kama waliyotegemea ila simu ikazima kabla hawajaelewana.

Akaniomba dada naazima simu yako nimjulishe mwenzangu nikamjibu sina dakika akasema hata meseji tu nitume nikampa.Akatuma meseji akarudisha simu akaaga ngoja nitoe hela hapo narudi.

Baada ya kama nusu saa simu yangu ikaita namba imeseviwa jina la Mamamkwe wangu nikapokea lakini hatukuelewana simu ikakatika akatuma meseji una laki 5 hapo nikamjibu hapana sina kwa sasa.
Akaniuliza kiwango nilicho nacho nikamjibu nina laki 2 akaomba naomba nitumie 195000 kuna mtu anasubiri na namba akaituma. Sababu mamakwe wangu ni mtu wa biashara hapa Mwanza sikusita nikamtumia akashukuru tukaagana kwa meseji.

Baada ya masaa kama 5 akatuma meseji tena anauliza una shilingi ngapi sasa hivi hapo ndio nikastuka sio kawaida mama aulizie mauzo yangu basi nikampigia mwenzangu amuulize mama ni anakosea meseji anamtumia mfanyakazi wake au ni vipi.

Baada ya hapo ndio tukajua tumetapeliwa ila sikuelewa kivipi namba ninayo kwenye simu na imeseviwa kabisa.
Kumbe anachofanya ukimpa simu anaangalia Call log ile namba uliyowasiliana nayo karibuni anaandika namba yake anaisave kwa jina hilo hilo ndio anatumia kutapeli akijua mtu mpaka ugundue ni ngumu sana.

Jana ametapeli maduka mengi sana maeneo ya Mkuyuni na ataendelea kutapeli kwa hiyo muwe makini nae sana.Ni wizi wa kizamani lakini mtu huwezi jua siku wala saa.
Poleni kwa waraka mrefu najua utawasaidia wakazi wenzangu wa Mwanza kwa mwizi huyu.
Nimeshakujua, kumbe ndio wewe... Pole sana
 
Sas naww ulivotuma hela jina gani lilitokea?la mamamkwe au la nani? Km pia hujui jina la mamamkwe wako basi ni uzembe wako
 
Pole dada. Ila wa Tanzania tubadilike usikubali kumpa/kuruhusu kutumia kifaa chako chochote cha eletroniki mtu yoyote. Bora kama kuna haja ya kumsaidia mtu mwambie akuandikie namba uikague ukiridhika ni sahihi ufanye mawasiliano ww mwenyewe bila ya kuruhusu kumpatia kifaa chako.
Ndio mana kwenye sheria sasa hv mnalazimishwa kuweka password katika vifaa vyote vya kieletroniki.
Jamii itakuona mbaya ila utaepukana na mengi.
Asante sana mkuu tunajifunza kutokana na makosa ndio maana nimewaambia na wenzangu wawe makini nao. Sio kila mteja ana nia njema na wewe
 
Mitandao ya simu haiwezi kusaidia sababu ana namba nyingi na akishatapelia haipatikani tena. Polisi nako unaweza poteza muda wako bure
Awali kabla hajassve hiyo nmba.....kulikuwa kuna hilo jina mama mkWe?
 
Back
Top Bottom