Ndugu yangu unaweza ukatofautiana na mtu kimtazamo lakini bado ukamkosoa kwa hoja bila kuingiza masuala ya ugonjwa wa mtu maana Cancer inaweza kumpata mtu yeyote(mimi, wewe na yule) bila hata kufanya dhambi yoyote hakuna anayependa maradhi inatokea tu, sasa wewe unaonyesha kufurahia wenzako kuumwa bila shaka utakuwa unafurahia hata vifo vya wenzako(this is animosity), binafsi najua mateso ya maradhi nilimuuguza baba yangu mzazi mwaka jana alikuwa anasumbuliwa na mapafu, akafariki dunia maumivu yake hayajaisha mpaka leo sasa ningesikia mtu anafurahia kuumwa kwake au kufariki kwake ningejisikia vibaya sana, hivyohivyo nawe pia utajisikia vibaya kama ndugu yako au mzazi wako atapatwa na maradhi au kifo lakini unaona vema wengine kuumwa na hata kufa as if wewe utaishi milele(sitetei maovu ya mtu hapa maana mimi siyo mwanachama wa CCM wala CHADEMA nk wala sijakukosoa kwa sababu labda nimenufaika na Escrow HAPANA simfahamu rais Kikwete zaidi ya kumuona kwenye TV na kwenye kampeni zake za urais lakini kuhusisha kuumwa kwake na siasa siyo utu ndugu yangu wako manabii na mitume waliotikisa ulimwengu kwa nyakati tofauti lakini waliumwa na kufa kwa hiyo kumshambulia Kikwete kwa maradhi yake siyo jambo jema)