Wizara yamshukuru Rais Samia Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Profesa Riziki Shemdoe amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha Shilingi Bilioni 266.7 kugharamia ujenzi wa mradi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko mkoani Lindi.

Profesa Shemdoe amesema bandari hiyo ya uvuvi ikikamilika itakuwa msaada mkubwa kwa Watanzania wanaofanya kazi ya uvuvi huku ikitarajiwa kutoa ajira 30,000 kwa vijana wa Kike na wa kiume pamoja na kuongeza usafirishaii wa samaki nje ya nchi na itaongeza tija ya uvuvi Bahari Kuu.

Vilevile, Katibu Mkuu aliainisha faida nyingine kuwa itapunguza changamoto ya upungufu wa samaki ndani ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuongeza mchango wa sekta ya uvuvi kutoka asilimia 1.71 mwaka 2023 hadi kufikia asilimia 3 hadi 5 ifikapo 2026.

Profesa Shemdoe alisema tayari Rais Samia amesharidhia malipo ya awali ya jumla ya Sh bilioni 40 na zimeshalipwa kwa mkandarasi anayejenga bandari hiyo.
 
Back
Top Bottom