chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,003
- 20,665
Rais Samia atakuwa na ziara mkoani mwanza mwishoni mwa mwezi January 2024.
Namshauri atoe maelekezo kwamba yaongezwe maeneo ya hifadhi ya mazalia ya samaki ambayo yatakuwa na kinga ya kisheria kwa watu kutofanya uvuvi. Kila mkoa ambao ziwa lipo, kuwe na eneo tengefu la mazalia ya samaki, wavuvi wasiguse huko.
Kwa sasa kisiwa cha Rubondo ndicho kinafanya uhifadhi huo, na mahala hapo, samaki huwa wanalindwa dhidi ya uvuvi. Kwa maneno ya waliofika huko, unaweza kukuta samaki wakubwa sana.
Nashauri ziwa liwekewe maeneo zaidi ya uhifadhi ili kufanya hata vifaa anavyogawa viwe na tija ya muda mrefu.
La pili ni kutenga visiwa kwa ajili ya uwekezaji wa kitalii ndani ya ziwa victoria, kama alivyofanya Rais Mwinyi Zanzibar. Hili lifanyike mapema kabla visiwa havijavamiwq na makazi holela. Baada ya hapo itangazwe tenda kwa wawekezaji ambao watajenga mahoteli ya kisasa na kufanya utalii wa ziwa uongeze pato la taifa.
Mwisho, ni ufugaji wa samaki kwa vizimba, walau yatafutwe maeneo maalum, kwa vibali maalum, ufanyike ufugaji wa vizimba ndani ya ziwa chini ya uangalizi wa Wizara ya Uvuvi.
Ifike muda sasa tuache kufukuzana na samaki ziwani, tuwafuge kwa vizimba na mabwawa.