Wizara ya Ujenzi sasa ni mufilisi? Ati milioni 10 zatengwa ili kumaliza foleni Dar!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
17,547
Reaction score
28,493
20260224_142840.jpg

Katika miaka ya karibuni , wizara hii ya Ujenzi imekuwa kichwa cha mwenda wazimu.

Kila anyejifunza kunyoa anapelekwa hapo, na nywele anajua anakozipeleka.
Siyo siri ,sasa Wizara , taasisi zake kama TANROADS, ni mufilisi.

Wadau wa ujenzi wanaikimbia wizara ya Ujenzi.
Yote tisa, kumi ni hii habari ya kutengwa Tshs milioni 10 kwa Wanafunzi wa chuo kikuu kutoa wazo la kumaliza foleni Dar!!!

Wizara Ina wahandisi waliobobea katika fani ya barabara, Kuna makampuni ya kihandisi kufanya feasibility studies za Traffic na Highway Engineering na Design.
Kwa watu wabobezi katika fani tungeweza kusema Waziri Ulega amekula maharage ya wapi?
 
Wakati wanajenga mwendokasi phase 2 pale kwenye makutano ya barabara inayotoka SGR station na Bandari/Gerezani road nilisema lazima patakuwa na foleni kubwa asubuhi na jioni. Na ndio kinachotokea sasa hivi foleni asubuhi inafika hadi chuo cha polisi.
Kwanini? Ni hivi ukitoka Bandar/iGerezani road ni two lane road ila ukifika kwenye mataa kuelekea SGR inakuwa njia moja. Hii ina create bottle neck na ndio chanzo cha foleni. Haihitaji uwe engineer au PhD holder kujua hilo. Sasa hawa wahandisi walifikiri nini?
 
Hiyo million 10, ni Kwa vijana wasomi kutoka vyuoni. atakae Toa WAZO/ ideas litakalo saidia kupunguza/kuondoa Foleni Dar es salaam.

Ulega, Yuko sahihi kwenye Sera maendeleo ya 2050 vijana kushirikishwa kwenye shughuli za maendeleo.

anataka mchango wa vijana wasomi. Utumike sambamba kwenye za maendeleo Nchi ✅👍
 
Kuna upungufu mkubwa wa kufikiri katika watu wa Wizara hii ya ujenzi.
Mbaya zaidi sasa uongozi wa wizara unataka wanafunzi wa uhandisi ndio watoe majawabu.
 
Hiyo kazi mbona inaweza kufanyika kwa Artificial Intelligence. Maana hao wanafunzi wa chuo nao wataenda kwenye artificial intelligence ili kuja na wazo
Dar maendeleo yake yoote yanafata barabara kubwa 4 tu ambazo ziliendelezwa n wakoloni kwenda katikat ya jiji.

Barabara hizi nne ndo zinagubikwa n maswali yasiyo n majibu kila siku. N ukiangalia vizur dar ina centered development. Hii inaplekea kuwa na folen jion n asubuhi.

Swali kwa ulega, kwa nn asubuhi n jioni?
 
Hiyo million 10, ni Kwa vijana wasomi kutoka vyuoni. atakae Toa WAZO/ ideas litakalo saidia kupunguza/kuondoa Foleni Dar es salaam.

Ulega, Yuko sahihi kwenye Sera maendeleo ya 2050 vijana kushirikishwa kwenye shughuli za maendeleo.

anataka mchango wa vijana wasomi. Utumike sambamba kwenye za maendeleo Nchi ✅👍
Na wabobezi pale wizarani wanafanya nini, si heri waachie ngazi vijana waingie?
Tumehadithiwa Flyover tano jijini sasa tunajua ni hewa tupu!!
 
Ni kweli, watu wizarani they dont think outside the box, ingawaje wapo tu!
Tatizo hawa watu wamekaa tu ofisini. Hawafanyi hata simple research. Nishafanya uchunguzi ile barabra ya Tanzanite bridge,Obama drive to ocean road hospital. Umeme ukikatika hakuna foleni ila ukiwepo barabara ina foleni. Unajua kwanini? Junction
Ya gymkhana na Obama drive 99% ya magari yanatoka ocean road magari machache sana yanatoka gymkhana. Kukiwa na uneme taa zinazuia magari yanayotoka ocean road sawa na magari machache yanayotoka gymkana matokeoa yake kunakuwa na msongamano kuanzia kwemye taa hapo gymkhana hadi ocean road hospital. Ukizima taa tu foleni Inaisha. Hata pale junction ya tanzanite/toure drive/Zambia road tatizoni hilo hilo magari mengi yanatoka na kuingia tanazanite bridge ila taa zinazuia magari ya Tanzanite muda sawa na hizi njia nyingine ambazo zina less than 10% ya traffic ukiziima taa tu foleni inaisha. Hakuna smart traffic management.
 
Na wabobezi pale wizarani wanafanya nini, si heri waachie ngazi vijana waingie?
Tumehadithiwa Flyover tano jijini sasa tunajua ni hewa tupu!!
Flyover sio solutions ya Foleni Dar es salaam, bali Lilikuwa ni WAZO la kishabiki la kisiasa TU 😂.

Sema waataalamu wanatoa sana ushauri mzuri, ila haufwati, kinacho fuatwa ni maagizo kutoka juu ya kisiasa .
 
View attachment 3548043
Katika miaka ya karibuni , wizara hii ya Ujenzi imekuwa kichwa cha mwenda wazimu.

Kila anyejifunza kunyoa anapelekwa hapo, na nywele anajua anakozipeleka.
Siyo siri ,sasa Wizara , taasisi zake kama TANROADS, ni mufilisi.

Wadau wa ujenzi wanaikimbia wizara ya Ujenzi.
Yote tisa, kumi ni hii habari ya kutengwa Tshs milioni 10 kwa Wanafunzi wa chuo kikuu kutoa wazo la kumaliza foleni Dar!!!

Wizara Ina wahandisi waliobobea katika fani ya barabara, Kuna makampuni ya kihandisi kufanya feasibility studies za Traffic na Highway Engineering na Design.
Kwa watu wabobezi katika fani tungeweza kusema Waziri Ulega amekula maharage ya wapi?
Kama hawana mawazo kuongoza kuanzia diwani wabunge mawaziri na Rais
Kwanini wanalazimisha kubaki si wapishe wenye akili ya kuongoza
 
Back
Top Bottom