Wizara ya Habari na Taasisi mnaosimamia maudhui kwenye vyombo vya habari hasa radio & runinga hamlioni hili?

Street Hustler

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
2,146
4,205
Kiukweli Kama Ni mtu ambae unajitambua vizuri utakuwa umeshuhudia Mambo yasiyo na shaha au kusikiliza Mambo yasiyo na staha na ukashindwa kuelewa hv Kuna weledi umetumika vizuri kuanzia chombo husika mpaka wanaowasimamia.

Usiku kwa nimejikuta nikisikiliza radio East Africa radio aisee sikujua napenda kipindi Cha jion Ila Leo nimejikuta naskiliza hii redio mpaka muda yaan n ujinga mtupu inakuwaje mtu anatoa habari za sijui umelogwa njoo uchukue dawa Yan nusu saa nzima mnawalisha watanzania ujinga eti mganga wa jadi kalipia kipindi kuja kutafuta watu wakuwatibu kweli mnakitakia nn hiki kizazi kilichipo na kijacho kwenye Taifa hili?

Sijawahi kusikia kipindi cha kualika watu wanaojishughulisha/waliofanikiwa kwenye kilimo, Ufugaji, Biashara, ufundi hata ubunufu.

Mbaya Zaid utakuta Jana flan kaacha paja, Jana umeachika Mara sijui mpenzi wako Nani Mara sijui ujinga gani jamani?

Hivi hata Kama media zinatafuta pesa kweli waneshindwa kubuni vitu vyenye tija kuwasikilizisha watanzania ili kesho Taifa lipone hv kumbe kulipia airtime ndio unaeza ongea ujinga hv kwenye radio.

Jamii forums naomba muwape taarifa wizara ya habari naamini mnashirikiana nayo vizuri ebu waambini wawasimamie vizuri hv vyombo vya habari mbona Kuna vingi vya kuongea na kuonyesha lakin ujinga wa uganga, maudhui ya ngono sijui nn jamani hata nyie mlioko kwenye media hata Kama hamna watoto he wazazi wenu hawaon au hawasikii mnayoyasema kuwen mfano mwema kwa dunia ya sasa.
 
Back
Top Bottom