Kwanini wizara ya afya iko hivi?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Kila mara kuna tokea taarifa ambayo pengine haiko sahihi ...inaachwa mda mrefu Sana watu wanaamini na wenye kudhurika Wana dhurika halafu inapita miaka ndo wizara inakuja na tamko....

Mwarobaini...hii imani kuwa mti wa mwarobaini unatibu magonjwa zaidi ya 40 ilienea Kwa miaka kabla ya wizara kuja kutoa tahadhari ya sumu Kwenye mmea huo ...

Mafuta ya ubuyu...hii nayo ilizuka ikawa biashara kuubwa mno ...kabla ya wizara kuja na tahadhari ya kiafya......

Mayai ya kwale... sijui wangapi waletapeliwa na sikumbuki kama wizara hata ilikuja kutoa tamko lolote au ilikufa yenyewe hii biashara....

Juzi wizara inasema kunywa maji mengi nayo sio afya ila ni hatari
Watu tumeaminishwa Kwa miaka kunywa Lita za kutosha kila siku Leo wizara inasema tunywe kiasi maji mengi Yana hatari... seriously?

Matunda mchanganyiko...hii nayo imekuwa biashara kuubwa Hadi kwenye mabaa Hadi maofisini miaka na miaka...Leo wizara ndo inaamka kusema ni hatari Kwa afya??

Why wizara hii inachukulia afya za wananchi poa Sana??
 
Ni kushauri Kitu Kaka!!!Usiamini na kamwe Acha kabisa kuamini maneno ya wanasiasa Haswa hawa wa kwetu hapa utaumiza ndonga bure huwa hawapo siriazi kabisaa na matamshi ya matamko Yao na kamwe usitegemee ya kwamba kuna siku wanakuwa siriazi fanya yako hao wanayafanya Yao Kwa faida zao na maslahi Yao zaidi,, jitahidi uwaelewe au fanya uchunguzi wa kina naamini utawaelewa na naamini pia utaacha na hutawazingatia kamwe na rudia tena kamwe
 
Sio kila mtu anaweza kuidharau..
Wapo wanaoiamini na kufata maelekezo yake...
Watanzania Wengi wanasikiliza wizara na Taasisi za Serikali...
 
Waziri mwenyewe mwenye dhaman ni kihojaa

Matunda mchanganyiko ndo wameniacha hoi zaidi
 
Wanatakiwa wawe wanawasilisha hayo matamko kama nadharia.

Labda kulingana na utafiti

Au kulingana na Ayuverda za wahindi

Au waganga wa kienyeji

Sio kuwasilisha kitu kama vile ndio only known fact kumbw ni kinadharia tu.
 
Back
Top Bottom