Wizara ya Afya: Mwaka 2022/23 Wajawazito 943 walifariki dunia wakati na baada ya Kujifungua

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Akiwasilisha makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Afya Bungeni, Waziri Ummy Mwalimu amesema kwa mwaka 2022/23 jumla ya Wanawake 2,028,151 (98%) walihudhuria Kliniki kwa mara ya kwanza kulinganisha na Wajawazito Milioni 1.5 wa mwaka 2022.

Pia, amesema kwa upande wa Huduma za Wakati na Baada ya Kujifungua, jumla Wanawake 1,500,404 walijifungulia katika Vituo vya Afya kulinganisha na Wajawazito 1,400,003 waliojifungua mwaka 2022.

Hata hivyo, Ripoti ya CAG ya mwaka 2021/22, ilionesha kulikuwa na ongezeko la Vifo vya Wajawazito zaidi ya Wastani wa Vifo 102 hadi 989 kwa kila Vizazi Hai 100,000 ikiwa ni juu ya lengo la Vifo 100 kwa kila Vizazi Hai 100,000.


 
I943 ni dadi kubwa sana wajitahidi kuboresha huduma ili kupunguza vifo vya mama na mtoto kabla na baada ya kujifungua.
 
Back
Top Bottom