BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Kuna hii Zahanati ya Serikali ipo Mburahati hapa Dar es Salaam, inafahamika zaidi kwa jina la Zahanati ya Mianzini, kiukweli huduma zao ni mbovu sana hasa kwa hawa mama zetu Wajawazito.
Awali nilikuwa nasikia tu taarifa hizo kuhusu madai hayo lakini nimeshuhudia mimi mwenyewe, nilienda kumpeleka mgonjwa katika Zahanati hiyo nikashuhudia Wauguzi hasa wa kike ni wa kali muda wote, wananyanyaswa sana Wajawazito na kuwaambia kama wanataka huduma nzuri waende ‘private’.
Kwa ufupi Wajawazito wanaoenda hapo hawapati huduma stahiki, wahudumu wamekuwa sugu, ukitaka ugomvi nao anza kuhoji chochote tu ambacho unaona hakipo sawa utapata cha moto.
Inamaana Serikali nayo imeridhia taasisi zake za Afya kama hii ya Mianzini kuwadharau wagonjwa kwa kuwa tu wanaoenda hapo ni wa kipato cha chini?
============== =================
UFAFANUZI WA MGANGA MKUU WA DAR
Alipoulizwa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema “Tulielekezwa na Wizara ya Afya kuwa namba za simu za Mganga Mkuu wa Mkoa ziwepo kwenye vituo vya afya vya Serikali, kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali kama kero za aina hiyo.
Pia kama kuna mwananchi ambaye anapata changamoto au kero yoyote kwenye vituo vya Afya afya tunasisitiza kuwasiliana na Mganga Mkuu tena ikiwezekana muda huohuo wakati wa keri ili iwe rahisi kuitatua.
“Kuhusu changamoto hiyo ya wauguzi wa Zahanati ya Mianzini bado sijapata hizo taarifa lakini tutafuatilia na kwa kuwa ni changamoto yenye mwendelezo tunaweza kutuma watu wetu au kupandikiza ili kuona kama kuna changamoto ya aina hiyo.”