Wivu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wivu!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Mar 28, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  WIVU!!
  Wivu uko kila mahali...kwenye mapenzi...kati ya marafiki...kati ya wafanyakazi na wanafunzi wenza...ndugu na hata maadui.

  ''Wivu ni kidonda ukizidisha utakonda.'' Ndivyo tulivyokua tukiambiana wakati tunakua...na huo ndio ukweli wenyewe.Maana kama vitu vingine vingi wivu ni mzuri ila ukizidi kipimo unageuka sumu.

  Kwenye mapenzi: Wivu kati ya wawili ndani ya mahusiano unaweza kua kirutubisho au chachu ya mapenzi.Ukionyesha kwa kiasi utamfanya mwenzi wako ahisi kwamba unampenda na kumjali...sisemi kwamba ni kitu pekee kinachofanya hivyo bali ni kichocheo kizuri iwapo hakitazidishwa na kusababisha kero.Wivu unapozidi unaonyesha mapungufu yako kanakwamba hujiamini kitu ambacho kinaweza kupelekea mwenzako nae ahisi kwamba HUMUAMINI.

  Kati ya wanafunzi/wafanyakazi: Unapomuonea wivu mwenzako kwa maendeleo yako ikiwa utaupangilia vizuri itakusukuma wewe kujitahidi kufika alipo yeye au hata zaidi.Ila ukikosea tu ukazidisha kiasi itasababisha chuki dhidi ya mwenzako huyo.Na kama mnavyojua chuki ni sumu.....sumu inayomuumiza aliyenayo na sio anayepelekewa hiyo chuki.Ukiwa na chuki utaishia kuchukia maendeleo ya mwenzako badala ya kujiboresha wewe hivyo hautafaidika.

  Wivu kati ya ndugu na marafiki: Kwanza jiulize kwanini umuonee wivu ndugu au rafiki yako??Kwanini usifurahie mafanikio yake huku ukijaribu kufikia pale alipo yeye???Katika watu ambao unatakiwa ujitahidi kutowaonea wivu ni ndugu au rafiki wa karibu....maana ukizidi unaweza kuzaa chuki.Ikiwa unawaonea utumie kama msukumo wa kuelekea kwenye ubora badala ya kuonyesha udhaifu wako na kupelekea kumchukia mwenzako kwa kua na kitu ambacho huna.

  Wivu dhidi ya adui: Jua kabisa kama humpendi mtu tayari kitendo cha kumuonea wivu kitakuumiza zaidi wewe binafsi zaidi ya kukusaidia.Japo ukiweza kuuendesha wivu wako badala ya wivu kukuendesha unaweza ukafaidika!

  Kwahiyo wivu ni mzuri maana huleta maendeleo na hudumisha mapenzi pale unapotumiwa vizuri.....ila wivu huo huo huweza kugeuka kero au kuzaa chuki ambayo matokeo yake yaweza kua ufitini..umbea..kutojiridhisha/kutojitosheleza...na hata kufikia hatua ya kuumizana.

  Hivyo basi....usiache kumuonyesha mpenzi wako wivu angalau kidogo wala usiache kuwa na wivu wa maendeleo....hayo mengine achana nayo maana maisha mafupi haya usitumie muda wako kuchukia na kuharibu....utumie kukunufaisha wewe na uwapendao.

  Nawatakia jumatatu na wiki njema kwa ujumla.
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Dah! Ndefu sana. Asbh nitaisoma fresh, sahz nahisi usingizi.
   
 3. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mambo my spanish lady leo tumekutana, u mzima ? Lizzy nitakujibu asubuhi hope your ok.
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Najaribu kuacha uchakachuaji alafu nyie mnataka kunirudisha????:angry:Msirudie tena!!:frown:
  Nwyz niko pouwa Uporoto!!Hope you are too!!!
   
 5. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ulichokizungumzia hapo naona ni kama vitu viwili,Neno wivu jinsi ulivyolitumia umelielezea vizuri lakini kila nikijaribu kuangalia hapo kwenye ndugu naona ni kama vile unaongelea husuda,lakini anyway nitarudi tuendeleze mjadala.Hawajambo Unga LTD.
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mmmh PM husuda na chuki sindo vinavyoendana?UngaLTD tupo gado!
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Gmorning Lizzy
  mimi kuna dada namwonea wivu just because ana mtoto mzuri sasa hapo sijui inakuwaje?
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  I hope sio kwa ubaya ila ni kwa uzuri
   
 9. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ha hahaaaaaa

  Lizy umenikumbusha riwaya moja hivi inaitwa "Hiba ya wivu" kama kuna mtu aliisoma basi atakubaliana na wewe 100%
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Goodmorning dear!Hehehe...sio mbaya ila tu usije ukafikia kumchukia dada wa watu na katoto kake usije ukakaharibu sura bure. Maana ukizidi unaweza ukaanza kuona kama huyo dada anaringa kwaajili ya uzuri wa mtoto wake hata kama sio kweli...na njia pekee kumkomoa ni kuchakachua uzuri wa mtoto!
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Susy embu nipe mistari michache kuhusu kitabu maana jina kama nalijua ila sikumbuki kama nilikisoma au lah!
   
 12. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Lizy hii riwaya siikumbuki vizuri ila imeandikwa na mama mmoja anaitwa Zainabu M. Mwanga!!! kina mikasa mingi kuhusu mambo ya wivu wa mapenzi!!! jaribu kitafuta kwenye google ukipata nafasi.
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Haya bwana Lizzy,

  Sina la kuongeza mie. Ila kuna watu wanakuwa na wivu wa kipumbavu. Yaani inafikia mahali anamchukia mtu eti kwa sababu huyo mtu kapiga hatua kujiendeleza...Hilo kwa kweli linanikera sana.

  Halafu kuna jingine niliambiwa na kwamba linafanywa na waTZ alioko ughaibuni...ni Watz tu! Kwamba ukimwambia mambo yako na mipango yako anaweza kwenda kukulipia immigration au kwingineko. Nasikia kuna jamaa alimweleza mtu kwamba baada ya kumaliza MSc anataka kumweka sawa supervisor wake ampe PhD...huyo rafiki nasikia alienda kwa supervisor na kumweleza kuwa mshikaji anataka fanye PhD ili akazamie. Na plan za mshikaji zikaishia hapo!

  DC
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hehehe babu..oh samahani Mzee DC sasa huo ndo wivu unaopelekea/ambatana na chuki...asante kwa mfano hai!Wengi sana wanafanyiana vituko vya aina hiyo..hata sijui hua wanapata faida gani maana wanaweza kujaribu kuharibu alafu mwenzake akafanikiwa zaidi hata ya mwanzo.Ila ukweli unabaki pale pale kama ulivyosema mzee...inakera.
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kweli Lizzy,

  Inakera sana. Haijawaji kunitokea kwa sababu sijaishi majuu lakini nasikia waTz wanakimbiana huko majuu kwa sababu ya hivyo vituko vya kipuuzi wakati nchi nyinvine wanasaidiana!

  Ila naamini dawa ya mtu mwenye wivu ni kumwongezea dozi.. Unazidisha kufanya vizuri yaani ..excel more ili huyo mwenye wivu wa kipumbavu afe kwa BP....Na mtu wa namna hiyo hasitahili kuambiwa R.I.P kwa sababu hastahili!
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hehehehe na kweli dawa yao ni kuwakomoa kwa kuendelea zaidi mzee DC.Ila hata hapa nyumbani yapo bwana...unakuta mtu muda wote ni kusema fulani anavyoringia sijui uzuri wake..anavyojiona na kigari chake...jinsi anavyodhani mkewe ni mtulivu kumbe wapi!Mpaka mtu afikie hatua hiyo unajua kabisa hawezi kukufikia mpaka anachukulia mafanikio yako so personal..na kinachobaki ni yeye kuongea vibaya kukuhusu maana kukunyang'anya hawezi na kukufikia ndo kabisa haamini kama anaweza.
   
 17. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mimi naona siku zote WIVU sio mzuri.. Unaweza chukiwa bure, eti kwa saabu umemshinda rafiki yako class! au umependeza siku ya sikukuu, au kwenu kuna video (Enzi za Mwalimu)
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Lizzy,

  Mtu wa namna hiyo ni looser...Ameshakubali kwaba hawezi kufanya lolote la maana na kwa hiyo anaishia kucheza na mdomo..umbeya mtupu. Shida yetu Watanzania ni kwamba kuna watu wanapenda hizo hadithi za kishenzi na ndio maana watu wanaosema hovyo namna hiyo wanayo hadhira ya kutosha!
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hii Riwaya ni nzuri sana na ina mfunzo
  Asante sana Lizzy kwa hii useful sread
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapana ndugu.. Siyo kila wivu ni mbaya. Mfano, binafsi nina wivu sana na mama watoto. Ila sina wivu wa kijinga. Siwezi kupata BP eti kwa sababu kaenda mjini au yuko safari wiki moja. Nafahamu kwamba akiamua kufanya upuuzi na kugawa msosi wangu atagawa tena zaidi ya njugu. Kwa hiyo pamoja na kuwa na wivu, namwachia mwenyewe aamue la kufanya. Na tayari nimemweleza kuwa nina wivu sana na nikifikiria tu kwamba mtu kaniibia natamani kufa kuliko kuona tukio la namna hiyo. Huo si wivu mbaya. Hakuna binadamu anayependa vitu vyake kuchezewa chezewa!

  Ila wivu wa kishenzi kama hayo tunayojadili hapo juu ndio mbaya sana. Ni zaidi ya ushetani!
   
Loading...